Kutoka Dodoma!

Kutoka Dodoma!

Shivji aliwahi kuniambia kitu kimoja, doubt everything! Siamini kama suala la bungeni ni uchawi. Ninaamini kuwa uchawi unatumika kutuzuga tu. Kwa nini sio radioactive materials?

Tufukiri kwa mapana

.......pia inawezekana ...lakini tujiulize..radioactive chemicals zinauwezo wa kuuwa bunge zima ..akiwemo mnyunyizaji na wanamtandao maslahi wenzake...je inawekana!!!???

..lakini pia tutafakari kwa upana ..kama karani au mfanyakazi wa bunge anaweza kufungua mlango wa jengo takatifu lilofungwa ...utaratibu ukoje ..anayeshuhulika na usalama bungeni anawezake kuruhusu...watu kujiingilia..na kama inawezekana tu kuingia kama chooni..nadhani ipo siku MBUNGE MMOJA KWA MAZINGIRA YOYOTE YANAYOFANANA NA YA HAWA...ANAWEZA KUWA AMECHOSHWA NA MAISHA NA KUAMUA KUTEKETEZA BUNGE ZIMA!!..THAT IS POSSIBLE!!

NAFIKIRI TUNAYO KAZI YA KUFANYA HASA KUHUSU USALAMA WA WABUNGE WETU!
 
Quote:
Originally Posted by Bongolander View Post
Ndugu yangu umesema PRC Dodoma, una hakika kama kweli wana uwezo wa kweli kufanya kazi hii? una uhakika kama kweli uchunguzi wao ulikuwa free bila kuwa na influence yoyote. I am sure hata kilichonyunyizwa inawezekana hawakijui. Huenda hata hawakuwa na lab technician hata mmoja!
Spika Sita alisema amewapatia wao vielelezo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wakishirikiana na uwt. Ndo tungoje tuwasikie watasema nini na wakae wakijua kuwa wakileta taarifa za ubabaishaji tu, mzigo utakuwa juu ya vichwa vyao

UJINGA MTUPU, kila mtu anajua ni CHENGE lakini WOTE WANAMUOGOPA hata SPIKA mwenyewe na WAANDISHI WA HABARI, kwanini wasimtaje JINA?
 
UJINGA MTUPU, kila mtu anajua ni CHENGE lakini WOTE WANAMUOGOPA hata SPIKA mwenyewe na WAANDISHI WA HABARI, kwanini wasimtaje JINA?

Sitta anajitetea kwamba picha ya deo imefifia na kwamba watu 2 wanaonekana, na mmoja ni Afisa wa Bunge. Hapo simple logic ni kwamba yeye Six alijuaje kwamba huyo ni Afisa wa Bunge na si mtu wa kutoka nje ya Taasisi hiyo? Kwa hiyo picha imewaonyesha ni watu gani na ndiyo maana wamesema kwa uhakika kwamba ni Mbunge na Afisa wa Bunge. Labda ni kama jinsi ilivyo kwenye swala la kifo kwamba ni Daktari pekee ndiyo mwenye mamlaka ya kuthibitisha kifo na hivyo Six amewaachia polisi na uwt ndiyo watangaze kwamba ni nani alionekana kwenye huo mkanda wa deo.
 
...KUNA JAMBO HAPA KAMA WANASHERIA WAPO NA WANAWEZA KUSAHIHISHA....KAMA CHENGE ALIOMBA RUHUSA KWA MUANGALIZI WA BUNGE ..NA AKARUHUSIWA KUINGIA....KWENDA KUTAFUTA AU KUCHUKUA MZIGO WAKE AU CHOCHOTE ...NI VIGUMU KUMTIA HATIANI.....KWA KUWA LAZIMA ITABIDI MKEMIA WA SERIKALI KWELI ADHIBITISHE TRACES ZA SUMU ...OTHERWISE ITACHUKULIWA TU KUWA ALIINGIA KUTAFUTA ALICHOTAKA!!!

KOSA KUBWA HAPO LITAKUWA LA HUYO AFISA WA BUNGE KUMRUHUSU KAMA UTARATIBU HAURUHUSU......SIMPLY CHENGE ANAWEZA KUWA HANA KESI YA KUJIBU...UNLESS KULIKUWA NA NJAMA NA HUYO AFISA NA KAMA WALIMKWEPA MTUNZAJI WA UKUMBI IKIWA AFISA MUHUSIKA HANA MAMLAKA NA KAMA RUHUSA YA KUINGIA UKUMBINI HAIKUTOLEWA.....

SIMPLY CHENGE AKIULIZWA ATASEMA HIVI...." NI Kweli niliingia bungeni baada ya kuomba ruhusa kwa afisa muhusika na yeye alinisindikiza ili kutafuta nyaraka yangu ambayo naamini ilipotelea bungeni ...".....ataendelea " sikudondosha au kuweka chochote ..kama mnaweza mnaweza kuwaita wataalamu wa chemical wakague..."

baada ya hapo sidhani kama askari atakuwa na kipengele cha kuendelea kumzuia....kwani hata kama ni tambiko ..halitakuwa na udhibitisho kisheria...

NADHANI WABUNGE WAACHE UOGA..HUYU ALIKUWA ANAWATISHA TU KISAIKOLOJIA NA KIMSINGI HAMTAKUWA NA KIGEZO CHA KUMTIA HATIANI....
 
Kuna mambo hayaendi sawa bina sawia, hasa baada ya kusoma posts za watu ambao nina amini kwamba wanatoa maelezo ya kina kuhusu hili sakata.

Kwanza nimeshangazwa na jinsi Bunge kama Taasisi jinsi ambavyo linashughulikia hili swala. Kuna mambo mengi sana ya kujiuliza kuhusiana na watendaji wakuu wa Bunge pamoja na wasaidizi wao na watunza usalama wa hilo jengo.

Iwapo camera za usalama za jengo lote zilikuwa zimezimwa, hiyo picha ya Mbunge na Katibu wa Bunge inayowaonyesha wakipita kwenye viti vya waheshimiwa wakimwaga vitu ilitoka kwenye camera ya chombo gani cha habari?

Kwanini kuna contradictions kwenye maelezo yao? Kwamba camera zilikuwa off, mara camera zilikuwa ON na Chenge haonekani? Hapa ninanusa harufu mbaya sana ya ufisadi uliopea. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba Bunge kama Taasisi ilitumiwa na mafisadi ili kufanya hayo waliyoyafanya kwa faida ya mafisadi lakini wameumbuka baada ya picha kutoka nje camera za usalama kumuonyesha Mbunge na Katibu wa Bunge. Kwa hiyo kuna vigogo wa Bunge walijua nini kinafanyika na walitoa baraka zote, may be Sitta na Mama Makinda na some othe Big Shots hawakujua, lakini kuna watu very senior walikuwa involved. Hili swala linahitaji kuwahoji vigogo wote wa Bunge kuanzia Katibu wa Bunge mpaka wanaolinda.

Kuna uzembe fulani katika kushughulikia hili swala. Kwa kawaida mtu akienda kutoa taarifa za mauaji, wizi, na mengineyo huwa anakuwa makini sana kwamba mtu mwingine asiguse chochote ili ushahidi usije ukapotea ama asije akaharibu uchunguzi utakaofanyika. Mfano kuchukua kisu, kushika kitasa cha mlango ama kushika komeo la mlango au zana yoyote iliyotumika kufanya huo uhalifu. Ni polisi ndiyo wanatakiwa kuja kugusa hivyo vitu tena kwa uangalifu na umakini mkubwa ili wasije wakaharibu uchunguzi wao. Swali kwenye hii sakata ni kwamba, je, baada ya kupewa taarifa kwamba kuna madudu yalifanyika kwenye ukumbi kabla ya kikao, walizuia watu wengine kuingia ndani ili kutoharibu uchunguzi? Ni nani alipeleka taarifa za Sitta ama Uongozi wa Bunge kuhusu hilo tukio na je alipeleka kwa wakati muafaka? Na ni hatua zipi zilichukuliwa ili kuzuia kupoteza ushahidi?

Kudai kwamba siku ya pili kulikuwa unga unga kwenye kiti cha Mh. Mwakyembe ina maana kwamba wafagizi hakufuta kiti chake? Ama ina maana usafi haukufanywa? Kama kulikuwa na tukio kama hilo, kwanini Spika hakuahirisha kwa muda kikao hicho ili kupisha uchunguzi wa polisi ili kama kuna sample yoyote ya kuchukua wachukue na kwenda kuifanyia uchunguzi? Ina maana Spika hawezi kuahirisha kikao for a day ili kupisha uchunguzi wa kina ufanyike?

Jengo lile limejaa serikali na wawakilishi wa wananchi kwa hiyo nilitarajia kwamba Usalama wa Taifa hawalali na hawawezi kuwaamini wana usalama wa hapo na inawezekana wafanyakazi wengi wa Bunge kuanzia walinzi mpaka hao wasaidizi ndani ya ukumbi na hata wafagizi ni waajiriwa wa usalama wa Taifa maana humo ndani kuna PM ambaye anatakiwa kulindwa kwa ukaribu sana na pia Ukumbi wa Bunge ni jengo muhimu sana ambalo UWT wanatakiwa kuwa makini nalo masaa 24. Hili linanipeleka kwenye signal nyingine kwamba UWT imetekwa na mafisadi na inafanya kazi zake kwa maslahi ya mafisadi na ndiyo maana kuna mambo mengi sana ambayo hayaendi sawa kwenye uchunguzi wa hili sakata na sijui kama tutapta kitu cha maana kwa kuwa UWT wanaweza kuwa wanahusika na walifanya kwa mahesabu makubwa na kuhakikisha kwamba ushahidi unakuwa mgumu kupatikana.

Kwa mtazamo wangu, ni wakati muafaka kwa JK kubadilisha na kuisafisha UWT vinginevyo nchi hii itaendelea kuwa mikononi mwa mafisadi na iko siku watakuja kufanya mambo makubwa sana. Tukio la hapo Bungeni ni la kiusalama zaidi kuliko kisiasa na hivyo RO alitakiwa awe responsible kwa tukio hilo, maana ni aibu na kama hayo madudu yalifanyika na yeye hakujua basi kuna walakini mkubwa kwamba Idara imepoteza mwelekeo na iko siku tunaweza kusikia Waziri Mkuu ama Jengo zima wamekufa kwa kuvuta hewa ya sumu humo ndani na bado watakaokuwa responsible ni hao hao UWT. Hawa UWT ni wepesi kupenyeza watu wao kwenye vyama vya siasa ili kuvimaliza lakini nitashangaa kama RO atakuwa hana wafagizi, wahudumu, makatibu wa Bunge na wengineo ambao wanahusika moja kwa moja na shughuli za Bunge kila siku kwenye lile jengo. Kama ikiwa hivyo basi ina maana kwamba RO kashindwa kazi au sasa anafanya kazi kisiasa zaidi na siyo usalama wa taifa tena. Kweli nchi imetekwa!

Naona sasa nilipue:

...Kuna mtu nimezungumza naye ninamuamini asilimia 100, na akisoma JF atanijua ni mimi lakini sasa naamua kumwaga mchele mazungumzo yetu na yeye kuhusu tukio hilo.

Huyo jamaa alikuwapo Dodoma kwa dharura Jumanne wiki hii na kurejea Dar Alhamisi Asubuhi, nikahisi safari yake ina uhusiano na tukio husika nikambana anieleze kilichotokea huko Dodoma na maelezo yake leo hii yalikua kama ifuatavyo:

"Nilikutana na Katibu wa Bunge, Tom Kashilila usiku wa Jumatano, muda mfupi baada ya kukutana na Kaimu Mkuu wa Usalama wa Bunge, aitwaye Magati. Magati alishituka kuona kwamba hakuwa amejulishwa na wakubwa zake kuhusu kitendo cha Chenge kudaiwa kuingia ndani ya Ukumbi wa Bunge. Akiwa Mkuu wa USalama, alipaswa kujua kila kitu. Alichanganyikiwa na kuingia kazini usiku huo. Kwa upande wake, Katibu wa Bunge alisema wanafanya uchunguzi wa kina kuhusiana na suala hilo kwani kwa uzoefu wake wa kimataifa, upo uwezekano wa kuwapo vitu hatari. Aliahidi kutoa taarifa kadiri zitakavyopatikana. Baadaye usiku wa manane akanitumia sms kusema kwamba wametoka kukagua kamera za usalama wameshindwa kuona kitu na kwamba siku itakayofuata wataendelea na kuzipitia tena. Baadaye akaja na maelezo kwamba wameshindwa kuthibitisha lolote kwa kuwa kamera zao zilikua zimezimwa. Alipoulizwa kama wamewahoji Chenge na Sagasii akasema hatuwezi kuwahoji kwa kuwa hakuna ushahidi. Ajabu mashahidi muhimu/wahusika unakataa kuwahoji wakati wao ndio wanatakiwa kuanza kuhojiwa. Baadaye Katibu akaongea na mwandishi wa habari akamwambia kwamba wao kamera zao zinakuwa wazi 24hrs lakini wamekagua hawakupata ushahidi wowote. Sagasii anaulizwa na waandishi anasema hajui lolote kwa kuwa hajaarifiwa wala kuulizwa na yeyote. Watu wa STAR TV wanashangaa wao walikuwapo juu wakati huo wakiandaa vifaa vyao kwa ajili ya Jumanne Oktoba 10 lakini hadi leo hawajaulizwa na yeyote. Huku kuna taarifa polisi na usalama wanafanyia kazi mara wamemhoji Chenge, sasa which is which?" MWISHO WA KUNUKUU NA ATANISAMEHE ALIYETAMKA MANENO HAYA MAANA NAONA NI MUHIMU WATU WAJUE NINI KINACHOENDELEA. Naamini akisoma atajua ni mimi kama hatosoma ataulizwa na wahusika ambao amezungumza ama kufanya nao kazi. ATANISAMEHE KWA MASLAHI YA TAIFA
 
Heshima mbele wakuu, According to the dataz yaliyojiri jana Dodoma, kwenye NEC ni kama ifuatavyo:-

1. The dataz ni kwamba asubuhi na mapema, wabunge wa CCM walituma ombi maalum kwa Mwenyekiti wa CCM Rais wa jamhuri, wakitaka kuwepo na kikao cha dharura na nyeti, kati ya wabunge hao na wajumbe wa NEC tu.

2. Wabunge hawa wa CCM walimueleza Mwenyekiti wao, yaani rais wetu kuwa wana agenda mbili wanazotaka kuziongelea na kuzifikisha kwenye kikako hicho cha siri, nazo ni:-

(a). Agenda ya kwanza:- Wabunge wa CCM wanataka Makamba aondolewe mara moja kwenye nafasi yake ya ukatibu mkuu wa CCM, kwa sababu wana ushahidi wakutosha kuwa anashirkiana na kikundi cha viongozi mafisadi ambao wanaonekana wamepania sana kulihujumu taifa na kulindana.

(b). Agenda ya pili:- Wabunge wa CCM wanataka viongozi wote waliobainika kuwa ni mafisadi, kuanzia Mkapa, Lowassa, Msabaha, Karamagi, Chenge, Rostam, na Meghji na wengineo watakaobainika huko mbele, wafukuzwe rasmi na kuvuliwa uanachama wa CCM.

3. Tha dataz ni kwamba kwa sababu Makamba ndiye mtayarisha kikao kikatiba ya CCM, aliamua kuziondoa hizo agenda za kikao bila ya kuwataarifu wabunge in advance, wabunge walipofika kwenye kikao hicho wakashitushwa kuona agenda zao zimetolewa au hazipoa kama walivyoomba.

4. To add the salt to the injury, the dataz ni kwamba Makamba kwa makusudi mazima, akampanga Rostam kuwa mzungumzaji wa kwanza, as opposed na wish ya wabunge ya kutaka Mbunge Ole Sendeka ndiye awe mjumbe wa kwanza kuongea ...........!

Naomba kukatisha kidogo nitarudi tena kumalizia more dataz kutoka Dodoma!
 
Wakuu Wote ndugu zangu wa JF, heshima mbele in the next 15 minutes tutawamwagia yailiyojiri jana Dodoma na NEC,

Mbunge waetu Shujaa Mwakyembe bado yupo Dar kwa medical check zaidi, na tunamuombea sana kwa Mungu kuwa awe salama na aweze kurudi bungeni sasa maana tunamuhitaji huko sasa as anation kuliko wakati wowote wa uhuru wa taifa hili.

Ashante Wakuu nitarudi in 15 minutes na more Big Dataz kutoka Dodoma!

mkuu twakushukuru kwa madata ya kufa mtu aisee yan watukip up2dated kupita maelezo na mafisadi wetu kiasi kwamba ukitoa statement kama hizo za kuwa utarudi after 15 minutes na big dataz...basi na sie after 15 minutes mwanawane twawasha ma screen yetu kutune to JAmbo forums channel mwanawaneeee sasa hapa nimeshasubiria nusu saa naona kimya museee twakutakia kazi njema huko nawe uwe watembea na kiti chako aiseee maana wakikugundua tu wanaweza wakaku balali wallahi!!!

mwaka huu kweli mwaka wao wa shetani kila kitu kimewapa mgongo!!
 
Wakuu heshima mbele, kikao cha NEC ndio kwanza kimeisha, sasa hivi wajumbe karibu wote wako kwenye tafrija ya Birthday ya Mwenyekiti wa CCM Kilimanjaro, inayoendelea sasa hivi Dodoma Hotel,

Lakini kama tulivyoahidi ni kuwa tunaendelea ku-monitor kwa karibu kabisa kinachoendelea sasa hivi Dodoma, na pindi zitakapopatikana tutaendelea kuhabarishana, na mimi sasa nipate nafasi ya kuisoma hii thread nzima.

Ahsanteni Wakuu! JF mbele always one step ahead na kumkoma nyani yaani mchana kweupee!

LONG LIVE FMES!!
 
Katika hili NINAPATA WASIWASI KUNA Ufisadi BUNGENI na kuna UFISADI katika MEDIA. Nitathibitisha kesho wasipotaja majina
 
aiseeee ni kama movie flani hivi twapigiwa hapa alafu twaji burekisha kwa muda kupata matangazo ya biashara na kisha kurudi kuendelea nayoooo

tupeni mambo aisee wala msichokee!!mtalipwa na Mungu kwa kutufungua macho sie tuliokua tumefungwa na kampeni za uongo na kweli...ohh ntacreate ajira milioni ndani ya miaka miwili ya kwanza na blah blah kibaaaao
 
.
NADHANI WABUNGE WAACHE UOGA..HUYU ALIKUWA ANAWATISHA TU KISAIKOLOJIA NA KIMSINGI HAMTAKUWA NA KIGEZO CHA KUMTIA HATIANI....

Ninavyojua mimi kitisho hutolewa kwa lengo la kumdhuru kisaikolojia mhusika, hivyo ni lazima mhusika aone au watu wake waone. Kama hataona yeyote basi hicho siyo kitisho. sasa Je, Chenge alikusudia kuonekana au alikuwa anafanya kwa kujificha? Kama alikuwa anafanya kwa kujificha, basi alikuwa hatishii, alikuwa na makusudi mengine.
 
FIELD MARSHAL ES ......MKURUGENZI WA UJASUSI WA JF ....[JF CENTRAL INTELLIGENCE -AND NATION RESCUE]...hongera kwa well detailed information ..vitengo vyote vipo kazini kamanda....

halisi hata wakihonga magazeti yote ..wazalendo wa kitengo mpo ...hadi mkulima wa TUNDUMA atajua tu ...tunaikomboa nchi dhidi ya uhuni ndani ya CCM!!!.....AMBAO WANATAKA KILA MWANA CCM ANUKE MAVI!!
 
...KUNA JAMBO HAPA KAMA WANASHERIA WAPO NA WANAWEZA KUSAHIHISHA....KAMA CHENGE ALIOMBA RUHUSA KWA MUANGALIZI WA BUNGE ..NA AKARUHUSIWA KUINGIA....KWENDA KUTAFUTA AU KUCHUKUA MZIGO WAKE AU CHOCHOTE ...NI VIGUMU KUMTIA HATIANI.....KWA KUWA LAZIMA ITABIDI MKEMIA WA SERIKALI KWELI ADHIBITISHE TRACES ZA SUMU ...OTHERWISE ITACHUKULIWA TU KUWA ALIINGIA KUTAFUTA ALICHOTAKA!!!

KOSA KUBWA HAPO LITAKUWA LA HUYO AFISA WA BUNGE KUMRUHUSU KAMA UTARATIBU HAURUHUSU......SIMPLY CHENGE ANAWEZA KUWA HANA KESI YA KUJIBU...UNLESS KULIKUWA NA NJAMA NA HUYO AFISA NA KAMA WALIMKWEPA MTUNZAJI WA UKUMBI IKIWA AFISA MUHUSIKA HANA MAMLAKA NA KAMA RUHUSA YA KUINGIA UKUMBINI HAIKUTOLEWA.....

SIMPLY CHENGE AKIULIZWA ATASEMA HIVI...." NI Kweli niliingia bungeni baada ya kuomba ruhusa kwa afisa muhusika na yeye alinisindikiza ili kutafuta nyaraka yangu ambayo naamini ilipotelea bungeni ...".....ataendelea " sikudondosha au kuweka chochote ..kama mnaweza mnaweza kuwaita wataalamu wa chemical wakague..."

baada ya hapo sidhani kama askari atakuwa na kipengele cha kuendelea kumzuia....kwani hata kama ni tambiko ..halitakuwa na udhibitisho kisheria...

NADHANI WABUNGE WAACHE UOGA..HUYU ALIKUWA ANAWATISHA TU KISAIKOLOJIA NA KIMSINGI HAMTAKUWA NA KIGEZO CHA KUMTIA HATIANI....


Kama kweli ALISAHAU kitu, atakuwa ALISAHAU katika kiti chake. Sasa huko klwenye viti vya wabunge wengine, kikiwamo cha spika alifuata nini?
 
Wabunge 'kususa' kikao cha bajeti kesho, Wahofia yaliyomsibu Dkt. Mwakyembe

Na John Daniel, Dodoma

SIKU chache baada ya kugundulika kwa njama za kuwadhuru Mbunge wa Kyela Dkt. Herrison Mwakyembe, Spika wa Bunge Bw. Samwel Sitta, Naibu wake Bi. Anna Makinda, Mbunge wa Same Bi. Anna Kilango na baadhi ya Wabunge sasa hofu imetanda miongoni mwao na kutaka kufanyika kwa uchuguzi wa kina kwenye viti vyote na maeneo mbalimbali ya ukumbi wa Bunge, kabla ya kuendelea kutumia ukumbi huo kesho.

Sambamba na hilo, Taarifa zilizolifikia Majira Jumapili jana jioni zilisema watuhumiwa wanaodaiwa kutaka kuwadhuru Wabunge wameanza mkakati mahususi kuhakikisha kwamba ushahidi kuhusu uchunguzi wa kuwanasa unakwama kwa lengo la kumzushia Bw. Sitta na vyombo vya habari kwa kusema uwongo.

Taarifa hizo pia zilieleza kwamba tayari maofisa wa usalama na wataalamu wa kuchunguza aina mbalimbali za sumu waliwasili mjini hapa na kufanya ukaguzi wa kutosha katika ukumbi huo usiku wa kuamkia jana ili kuhakikisha kwamba shughuli za Bunge zinaendelea kesho kama kawaida.

Wakizungumza na Majira Jumapili kwa nyakati tofauti mjini hapa jana, Wabunge hao walielezea kutokuwa na imani na usalama wa ukumbi huo na kudai kwamba huenda mtuhumiwa aliyeweka 'uganga' huo alichanganya na sumu maalum ya kuangamiza watu taratibu.

"Mimi binafsi nilikwenda kukaa karibu na Mhe. Mwakyembe siku alipopata matatizo ya kiafya na nilipotoka hapo niliharisha usiku kucha," alisema Mbunge mmoja wa CCM ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

"Sikulala ingawa sasa najisikia vizuri lakini sina hakika kama niko kawaida, nina shaka na ule ukumbi na hata kama nitaenda bungeni, nitabadilisha kiti," alisema Mbunge huyo.

Mbunge mwingine ambaye pia hakutaka kutajwa jina gazetini alisema atamuomba Spika kusitisha kwa muda vikao Bunge Jumatatu kama wataalamu wa sumu hawatafanya uchunguzi wa kina kwenye viti.

Habari kutoka katika vyanzo vyetu zilieleza kwamba watuhumiwa hao wameanza mkakati wa kupoteza ushahidi kwa kushirikiana na baadhi wachunguzi wa suala hilo.

"Mmoja wa Ofisa ambaye anatoka katika chombo nyeti ameanza kutaka kumsaidia mtuhumiwa yule kwa kutuambia kwamba hakuna kitu kama hicho, sasa sisi tunajiuliza yeye amepewa jukumu la kuchunguza suala hili sasa inakuaje anatangaza kwamba si kweli wakati uchunguzi haujakamilika?,"alihoji mmoja wa Wabunge.

Akizungumza na Majira kwa nijia ya simu Kaimu Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila alisema hana taarifa hizo na kwamba anachojua ni kwamba taratibu zote za Bunge zitaendelea kama kawaida.

Alipouliozwa kuhusu taarifa za ukumbi wa Bunge kufanyiwa uchunguzi wa kina juzi usiku na wataalam wa kuchunguza sumu waliokuwa na vifaa vya aina mbalimbali alisema hilo ni suala la kiusalama na si la umma hivyo hawezi kulizungumza.

"Nani amekwambia habari hizo, huenda yeye anayajua zaidi, hilo ni suala la kiusalama si Public, siwezi kulizungumza,"alisema Dkt. Kashilila.

Hata hivyo habari zaidi zilieleza kwamba ukaguzi huo wa kitaalaamu umefanywa hadi kwenye mavazi ya Spika na Naibu wake ili kuhakikisha kwamba havina madhara yoyote.

Habari hizo zilieleza kwamba kutokana na hali hiyo kutakwepo na mabadiliko makubwa ya ukaguzi na udhibiti wa usalama Bungeni kuhakikisha kwamba vitendo vyovyote vinavyoweza kuleta hofu ndani ya ukumbi huo havitokei tena.

Source: Majira
 
Mkuu Kadampinzani, kubeep huku ni balaa..hakuna tofauti na mtu kuonja sumu aone kama itamuua!!
 
FIELD MARSHAL ES ......MKURUGENZI WA UJASUSI WA JF ....[JF CENTRAL INTELLIGENCE -AND NATION RESCUE]...hongera kwa well detailed information ..vitengo vyote vipo kazini kamanda....

halisi hata wakihonga magazeti yote ..wazalendo wa kitengo mpo ...hadi mkulima wa TUNDUMA atajua tu ...tunaikomboa nchi dhidi ya uhuni ndani ya CCM!!!.....AMBAO WANATAKA KILA MWANA CCM ANUKE MAVI!!

......I love JF!!, wawakilishi wetu wanastahili pongezi kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya.....long live JF
 
Whatever aliekamatwa na ngozi ndie mwizi ,mambo ya kuwaaacha wahalifu na wahujumu wa uchumi kundelea kuwepo bungeni haya ndio mavuno yake, kila mtu ambae ni mpenda amani anawashangaa hawa waliojiuzulu toka ngazi kuu ya uongozi bado wanabaki katika nafasi za ubunge ambayo ni moja ya ngazi za serikali kama walijiuzulu kwa ridhaa zao toka ngazi za juu ili kulinda heshima yao kwa nini walibaki hapa na sasa wanaumbuka na kusababisha tafrani na aibu kwa Taifa
Nina wasi wasi dua za Wapemba zimeanza kuisakama serikali ya Kikwete ,pia nina wasi wasi kutokana na dua za Wapemba tokea mauaji makubwa yaliyosababisha wakimbizi wa Kitanzania nje ya Tanzania kuwa serikali hii yeyote ya CCM itakuwa yenye kuumbuka tu kila siku zinavyokwenda wakiziba huku kunatoboka kule na ndio tuonavyo ,kila wakijaribu kulindana jamaa nao wanazidi kuvuruga naona mwisho itakuwa hakuna mswalie mtume.
Huku si kuumbuka kwa Chenge kama ni yeye ila nikuumbuka kwa serikali nzima ya MH.Kikwete na CCM yake imekuwa kama wezi wanaofukuzwa kila wanapojifisha kunatokea linalowaanika na kuwaweka uchi ,sasa wanauliza nani atakaeweza kumfunga jipaka kengele.
 
Samahani kwa kutoka kidogo, now more dataz kutoka Dodoma ni kwamba:-

1. Katika kile kilicho onekana kuwashitua wajumbe wote wa mkutano huo wa siri, Rostam alianza hotuba yake kwa kumfagilia sana Mkapa, kuwa alifanya kazi nzuri na nzito sana kwa taifa hili na aliliacha taifa hili likiwa na utajiri mwingi na mapesa mengi sana katika akiba zake, na kwamba wale wote wanaomshambulia ni wajinga na wasiokuwa na elimu ya kutosha kuhusu hili taifa.

2. Kwa kawaida Rostam anapotoa hotuba za siasa kama hii huanza na kumsifia rais wa sasa, lakini on this one it was not the case, na alipomaliza hotuba yake, wajumbe wote walionekana kuwa na mshangao mkubwa, na Rostam aliiishia kupigiwa makofi na wajumbe kama sita akiwemo Almeir, na Makamba.

3. Muda wote huu rais yaani Mwenyekiti wa CCM, alikuwa akimuangalia huyu mkulu kwa dharau na tabasamu la mamba, na mara baada ya kumalizika kwa hotuba hiyo ya Rostam, rais aliamua kuingilia na kutoa comment ndogo ya kejeli kuwa ".....Rostam you are very intelligent man ndio maana hata ukapewa nafasi ya kuzungumza kwanza....".

4. Wabunge wa CCM, waliokuwa wamepigwa na mshangao mkubwa wa haya yote, wakaomba mkutano uahirishwe hadi leo asubuhi kwa sababu walitaka kupewa nafasi ya kutafakari kwanza yaliyojiri, na leo asubuhi sana kikako kimeanza tena, lakini thia time kwa kishindo kikubwa cha Mbunge Ole Sendeka, kuanza kuongea kwanza, ndio maana tunasema Mungu amrudishe haraka sana kwenye hiki kikao Shujaa Mwakyembe!

5. Toka kikako kianza asubuhi kumekuwa na kurushiana mawe na vijembe huku ikiwa inaonekana wazi kuwa sasa kuna makundi mawili makuwa ya wabunge, moja ni lile linalotaka mabadiliko na kuwakomboa wananchi na kusafisha ufisadi, na kuna kundi la pili ambalo ukweli ni kwamba lina nguvu kubwa sana hasa za ki-financial ambalo nalo linaonekana kuwa limepania sana kusimamia agenda moja tu, nayo ni kutaka wapewe nafasi ya kutuibia wananchi as they wish bila kubughudhiwa na wananchi wala sheria, na kundi hili linaonekana kuwa very serious na nia yao, na cha ajabu zaidi ya yote ni ile dalili zote kuonyesha kuwa Mkapa naye yuko nao kwa jinsi alivyokuwa akitabasabu sana watu wa kundi hili lenye nia mbaya na taifa wanapopewa nafasi ya kuongea!

Wakuuu ahsanteni sana, so far tumeweza ku-monitor dataz mpaka kufikia hapa, sasa wajumbe wako break na hakuna uhakika kama watarudi tena kwenye kikako, lakini mengi zaidi tutaendelea kuhabarishana as soon as tukiyapata, lakini dataz mpya zaidi itakuwa ni kesho!

JF mbele always, one step ahead, straight ahead .....na kumkoma nyani mchana! Oooh I Love it!

Ahsante Wakuu!
 
Back
Top Bottom