Kutoka Dodoma!

Apr 27, 2006
12,621
1,241
Wakuu wangu heshima mbele kama kawa, ninaomba kuweka mpya kutoka Dodoma:-

1. Leo asubuhi Mbunge Chenge, alichukuliwa na polisi na kuepelekwa kituo cha polisi Dodoma mjini, kwa mahojiano ya muda wa karibu masaaa matatu kuhusiana na kitendo alichokifanya majuzi cha kujaribu kuweka "Uchawi" kwa baadhi ya wabunge wenziwe ndani ya bunge, kitendo ambacho kilikamatwa na vinasa picha vya jengo vilivyomo ndani ya jengo la bunge, Dodoma.

2. Mheshimiwa Mkapa, kwa mara ya kwanza leo amehudhuria kikao cha siri cha NEC, kinachoendelea toka jana usiku, mjini Dodoma, ameonekana akiwa hoi na amechoka sana, wachunguzi wa siasa hawaelewi ni kwa nini baada ya Mkapa kukataa kwa makusudi kuhudhuria vikao mbali mbali vya cc na NEC vilivyopita, safari hii ametokea bila ya taaarifa kuhudhuria kikao hiki, ambacho kimeitwa ghafla sana.

3. Gavana wa Benki kuuu Bwana Ndulu, kwa mara nyingine aliiitwa mbele ya kikao hiki kutoa maelezo mazito sana, kuhusiana na ishu za EPA, na zingine za ufisadi, according to the dataz ni kwamba alishambuliwa sana kwa maswali ya wajumbe huko ndani.

4. Hali ya Mbunge Shujaaa Mwakyembe, sio mbaya sana lakini sio nzuri pia, sasa hvii ninapooandika yumo njiani kuepelekwa Dar, kwenda kuangaliwa zaidi kiafya na wataaalamu wa juu wa afya nchini, inasemekana kuwa chanzo ni sangoma ya Chenge.

5. Kwa niaba ya wananchi wengi hapa, tumewasiliana na Mbunge Kimaro, ili aweze kuja na kutupa yanayojiri kulingana na haitma yake kiuongozi na all the ishus za siasa za taifa kwa ujumla, tunategmea kupata jibu rasmi baadaye kuhusu kupatikana kwake na siku, then tutawasilaina na wakulu wengine hapa na hasa mkulu MMMJ.

Ahsante Wakuu, na Mods naomba ikisha expire iepelekwe popote, ni kuhabarishana tu kinachoendelea kwenye siasa za taifa letu!!
 
mkuu asante kwa taarifa hizi. tunazifuatilia kwa ukaribu sana kwani naona sasa mwisho wa mafisadi ndio unakaribia. yaani huu ndio mwanzo wa mwisho.
 
mkuu asante sana kwa news

la kuvunda halina ubani. mwaka huu mambo yote lazima yawe namba nane kama ilivyo namba ya mwaka huu
 
Mzee mwenzangu.. siyo usangoma....na kilichohusishwa siyo ulozi wa kiafrika mzee.. hakuna uchawi wa kiafrika hapo isipokuwa wa kizungu. Tangu nimeandika na kusema futeni ushirikina... na jaribu kuweka ushirikina wa kisayansi.... mtaelewa jambo hili na uzito wake. Kuna mtu atavuliwa uanachama muda si mrefu.....!
 
Mkuu FMES

Heshima mbele hapa sasa ni kumkoma nyani tu hadi giladi, Mzee Mwanakijiji aliposema vinasa picha vya TV mojawapo kuna waliomdhihaki na kusema ni udaku; wako wapi waje kuomba simile?

Hadi kieleweke maana Taifa liko njia panda na yote haya yasingeweza kutokea kama huyu Chenge angeadhibiwa na bunge kwanza kwa kulidanganya kuhusu yeye kuweka sahihi ughaibuni kwa maslahi yake binafsi. Pili kwa kusababisha bunge kuonekana ni kichekesho na kuwa kama vituko vya Pwagu na Pwaguzi.

Je, ni kwa nini hakuwekewa kolokoloni ili ijulikane anakula na nani? Che-nkapa maji yako shingoni ni jiwe moja tu linatakiwa avutwe na kuzama.


Bravo JF members ambao tumekuwa nao bega kwa bega katika kulitetea taifa na Utanzania.
 
Mzee mwenzangu.. siyo usangoma....na kilichohusishwa siyo ulozi wa kiafrika mzee.. hakuna uchawi wa kiafrika hapo isipokuwa wa kizungu. Tangu nimeandika na kusema futeni ushirikina... na jaribu kuweka ushirikina wa kisayansi.... mtaelewa jambo hili na uzito wake. Kuna mtu atavuliwa uanachama muda si mrefu.....!

Hivi nani analeta polunium 210 Tanzania? (Chenge & co.?) Inabebwa vipi? Serikali na bunge ni lazima kuchukua hatua haraka sana kwa sababu wengi wataathirika na sio waliowekewa kwenye viti tu. JF doctors waje hapa na kutuhabarisha.
 
Huyo Mkapa anadhani kwa kuhudhuria kikao hicho ndiyo jamaa wataogopa kumchukulia hatua dhidi ya ufisadi wake? Arie tu!!! Tamaa yake imemponza.

Posted Date::6/13/2008
Mbunge anaswa akifanya tambiko bungeni Dodoma
*Alisindikizwa na kigogo wa Bunge
*Spika akiri kupokea taarifa hizo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mwananchi

MBUNGE na Afisa mmoja Mwandamizi wa Bunge wamekutwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakifanya vitu vinavyodhaniwa kuwa ni vya kishirikina.

Taarifa zilizopatikana mwanzoni mwa wiki hii na kuthibitishwa na ofisi za Bunge, inadaiwa mbunge huyo alifanya tambiko hilo Jumatatu, kabla ya mkutano wa Bunge la Bajeti kuanza Jumanne wiki hii.

Shuhuda aliieleza Mwananchi kwamba, mbunge huyo aliingia kwenye ukumbi huo akiwa ameongozana na katibu mmoja wa bunge (jina tunalo) na kuanza kupita kila kiti cha mbunge na hatimaye aliishia kiti cha Spika.

Aliongeza kuwa, watu hao wakiwa wamefuatana walikuwa wakipita kila kiti huku mbunge huyo akinyunyiza vitu vinavyohisiwa kuwa dawa za kienyeji katika viti vya wabunge.

"Alipofika kwenye kiti cha Spika, alisimama muda mrefu akiwa ananyunyizia vitu fulani, lakini sikujua ni nini na wao waliamini kamera zote zilikuwa zimefungwa," alidai shuhuda huyo.

Shuhuda huyo alidai kuwa, mbunge huyo na mtumishi wa bunge walifanya shughuli yao bila kufahamu iwapo walikuwa wakionekana, bila kujua kuwa kulikuwa kuna watu wanafanya majaribio ya kunasa sauti na picha za ukumbini.

"Walianza kwa kusimama nje kwa muda mrefu wakiwa na wabunge wengine, baada ya wabunge kuondoka, mbunge huyo alibaki na katibu na kuingia ukumbini na kuanza kufanya kazi zao," alidai.

Alipoulizwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, iwapo ana taarifa hizo jana, alisema amezipata na kueleza kushangazwa kwake iwapo bado kuna watu wanaoamini mambo ya ushirikina.

"Taarifa ninazo ila siamini, isipokuwa inashangaza kuona kama bado kuna watu wanaamini mambo hayo kwenye dunia ya leo," alisema Sitta.

Sitta alisema baada ya kupata taarifa hizo, Katibu wa Bunge ameanzisha uchunguzi wa suala hilo. Hata hivyo alisema ushirikina hauwezi kusimama badala ya ukweli na haki.

Wakati huo huo, jana alasiri uvumi ulienea mjini hapa kuwa Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe alikuwa amefariki dunia.

Dk Mwakyembe ambaye juzi hali ilibadilika ghafla akiwa bungeni, alieleza Mwananchi kuwa afya yake ilikuwa imeimarika na kushangaa lengo la watu wanaoeneza uvumi huo.

Baada ya Dk Mwakyembe kukimbizwa kliniki juzi, baadhi ya wabunge walianza kuhusisha tukio hilo na 'tambiko' hilo lililofanyika Jumatatu, huku wengine wakiapa kutokubali hali hiyo kuendelea.

"Hawa watu na washindwe kwa Jina la Yesu. Wanataka kutuulia mtu bure na matambiko yao, Mungu yupo atasimama kati, ukweli utashinda," alisema mbunge mmoja wa Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Mbunge huyo ndiye aliyeoongoza Kamati ya Bunge ya Kuchunguza Mchakato waUshindi wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura kwa Kampuni ya Richmond Development.

Watu mbalimbali nchini walikuwa wakipiga simu mjini Dodoma kuuliza ukweli wa taarifa hizo, lakini wote walikuwa wakijibiwa kwamba hakuna kitu cha aina hiyo.

Kaimu Katibu wa Bunge alikanusha kuhusiana na uvumi wa kifo cha mbunge huyo na akasema Dk Mwakyembe ana afya njema na kwamba jana alizungumza naye akiwa na pamoja Spika wa Bunge Samuel Sitta ambaye aliwaaga jana kwenda safarini Dar es Salaam.

Alisema kuwa ni kweli walipata taarifa za kuzidiwa kiafya hali iliyomfanya akimbizwe kituo cha afya cha karibu ambako alipumzishwa kwa muda kabla ya kuruhusiwa siku hiyo hiyo.

Alisema kuwa hivi sasa afya ya mbunge huyo ni njeama na haina mashaka ya aina yoyote yaliyosababisha watu kadhaa kupata hofu.
 
Shukrani Mkuu FMES kwa datazz na yaliyojiri huko Dodoma. Swali....hivi ni kwanini tunawaachia kikundi cha maharamia wachache...RA, AC, EL, YM na wengineo wasio na mapenzi ya dhati na nchi yetu...kuendelea kufanya 'madudu' ya ajabu na nchi yetu tukufu....kama viongozi na serikali yao....hawatawadhibiti...then sitashangaa...'wenyenchi' wakichukua sheria mkononi!
 
[SIZE="

1. Leo asubuhi Mbunge Chenge, alichukuliwa na polisi na kuepelekwa kituo cha polisi Dodoma mjini, kwa mahojiano ya muda wa karibu masaaa matatu kuhusiana na kitendo alichokifanya majuzi cha kujaribu kuweka [COLOR="Red"]"Uchawi" [/COLOR]kwa baadhi ya wabunge wenziwe ndani ya bunge, kitendo ambacho kilikamatwa na vinasa picha vya jengo vilivyomo ndani ya jengo la bunge, Dodoma.
[/SIZE]
kuna uhakika gani kuwa ni uchawi?hizi ni blah blah
 
Kwa mwendo huu kuwe na Ceasefire na Mafisadi, mmmh I don't think so. Bunge linatakiwa kuweka kila kitu nje nje. Waache tabia ya kufichaficha mambo ingawa JF Always inawaumbua.
 
Takataka zote zinazokuwa zinafanyika huko zikiwekwa wazi na nje nje, waheshimiwa watakuwa wanaogopa kuendelea kufanya ujinga wao na kuwajibika sawasawa. Lakini wakishaleta mambo ya kulindana basi wataendeleza tabia hizo chafu.
 
Mbona waiba kuku mitaani hawakamatwi baada ya masaa 24 ingawa huko mitaani hamna camera za kuwakamata wakifanya vitendo hivyo? Imekuwaje jeshi la polisi lipate kigugumizi mpaka baada ya masaa 24 baada ya tukio hilo kukamatwa "live" na camera, na wao kupata taarifa hiyo? Ama mapolisi nao wameambukizwa na kigugumizi cha "Mkuu" katika utekelezaji wa kazi yao ya "usalama wa raia"?
 
Upupu wao ukiwekwa nje nje especially kupitia magazeti, luninga siamini kama itakuwa ni aibu either kwa serikali au Bunge. Kwa hii issue ya Chenge hakuna cha aibu kwa Bunge au Serikali. Itakuwa aibu kwa Chenge pamoja na wananchi wa Bariadi. Wananchi hao watakuwa wameaibishwa kwa sababu hawajamtuma huyo mbunge wao kufanya hayo madudu huko. Hivyo itakuwa ni wajibu wa wao pamoja na sheria nyingine kumuadhibisha mbunge huyo.
 
Mzee mwenzangu.. siyo usangoma....na kilichohusishwa siyo ulozi wa kiafrika mzee.. hakuna uchawi wa kiafrika hapo isipokuwa wa kizungu. Tangu nimeandika na kusema futeni ushirikina... na jaribu kuweka ushirikina wa kisayansi.... mtaelewa jambo hili na uzito wake. Kuna mtu atavuliwa uanachama muda si mrefu.....!

MKJJ...This is serious!! Tanzania inaelekea wapi?? HAWA NDO VIONGOZI WETU......
 
Upupu wao ukiwekwa nje nje especially kupitia magazeti, luninga siamini kama itakuwa ni aibu either kwa serikali au Bunge. Kwa hii issue ya Chenge hakuna cha aibu kwa Bunge au Serikali. Itakuwa aibu kwa Chenge pamoja na wananchi wa Bariadi. Wananchi hao watakuwa wameaibishwa kwa sababu hawajamtuma huyo mbunge wao kufanya hayo madudu huko. Hivyo itakuwa ni wajibu wa wao pamoja na sheria nyingine kumuadhibisha mbunge huyo.

Tumuadhibu kwa lipi?jamani kwani chenge kakamatwa na uchawi!evidence ziko wapi?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom