Kutoka Dodoma!

Kutoka Dodoma!

Ama kweli Mungu si athumani wala juma ... hamfichi mnafiki waumbuke wote
 
Hahahah mimi hainiingii akilini na kuteteana kwao kwa kitoto namna hii....najuaa walioko madarakani wanajua sana kuteteana...kila jambo huwa lina jibu lake la kisanii......
 
Mr Tom,
Mkuu penigne unaifahamu CCM lakini humfahamu Kikwete! ...
Hivi sasa Kikwete hana ubavu kabisa na analindwa na serikali kama rais lakini chama hakina uwezo wa kukemea mabaya... hakina! kwa sababu wahusika wakubwa ni wale wenye kuendesha chama chenyewe...
Mtu yeyote mwenye ubavu hawezi kuweka suluhisho kati yake na wahalifu yaaania ana shake hands na enemy wake...
Labda useme tu kuwa hawa watu hawawezi kuingamiza CCM kama chama lakini kulingana na mtaji uliopo labda tokee Nabii Mussa mwingine... CCM ipo hatarini sana kupoteza heshima yake kwa wananchi kama KANU. Ni swala la muda tu hivi sasa..

'Samaki huanza kuozea kichwani!'

kwa mtazamo wangu, CCM imeanza kupoteza nguvu ya mwenyekiti wake kichama tangu Nyerere afariki!

...ili kujinusuru, wangebadili hili la mwenyekiti wa Chama pia kuwa Rais wa nchi. Angalau wakati wa Mzee Malecela kama makamu mwenyekiti kulikuwa na kauoga kidogo,

Pressure imekuwa kubwa mno, naamini sio kila Raisi anaweza kumudu hizo kofia mbili. Mzee Mwinyi alijitahidi, Mkapa ndio hivyo tena, authoritarian style angalau siku zilikwenda, huyu M'kiti wa sasa na participative style yake, mkondo umeuzidi uwezo mashua!... chama kinayumba!
Accountability ipo wapi?

Wapinzani wakitumia nyufa hizi vizuri, 2010 hadithi itakuwa nyingine.

Naamini tutashinda tu tena muda si mrefu ila ukombozi wa kweli na endelevu itakuwa mbali but we will get there. Usishangae hata yakaandaliwa maandamano ya kupongezana baada ya kumtia huyuu lakini nae anasoma alama za nyakati ndo maana hata habanduki na ndipo mchezo unaponoga. Tuelimishana bila kuchoka kunahitika kwani kasumba hii Mkuu FMES ipo na tatizo ni historia, wavivu kufikiri, ubinafsi wa kupindukia na wenye kuamini mungu pesa ambazo watakula leo na kesho tu.

Daima mbele nyuma mwiko.....
 
Mzee Kitila,

Mimi nakuaminia kama mtu makini sana... mbona inaonyesha kama ulikuwa unajua yanayoendelea upande... mmoja na hivyo hizi habari zingine unaziona si za Kweli?

Kwa data zilizotolewa na the so called ... "Wenye Dataz" na hizi za Katibu Mwenezi wa CCM...

Mimi naona zote zina-logic fulani... tofauti tu ni kwamba za wale wa the Dataz... hawana full access.. kama za Katibu Mwenezi wa CCM...

Hivyo... sidhani kama tumefanyiwa usainii... inawezekana "wenye dataz" ndio walikuwa wanaota... ndoto za mchana...

"KWA BINADAMU ALIYEPEWA KICHWA NA UBONGO KUFIKIRI NA HAFIKIRI, UTI WA MGONGO UNGEMTOSHA"
Omutwale Production 2008
 
CCM yayumba

na Mwandishi Wetu, Dodoma

HALI ya mambo si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Kapteni John Chiligati, alikiri kuwa ufisadi umekiyumbisha chama hicho.

Wakati Chiligati akikiri hivyo, tofauti za wazi na za moja kwa moja baina ya makada mahiri wa chama hicho nazo zimeanza kujionyesha dhahiri, huku baadhi ya wanachama wakimpinga wazi wazi Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba, na kutaka aondolewe katika wadhifa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao maalumu kilichowakutanisha wabunge na wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, Chiligati alikiri kuyumba kwa CCM katika siku za hivi karibuni kutokana na kashfa kadhaa.

Alisema kashfa zilizokiyumbisha chama hicho ni pamoja na ile inayohusiana na mchakato wa kandarasi ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.

Aliitaja kashfa nyingine kuwa ni ile ya wizi wa mabilioni ya fedha kutoka katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) na Benki Kuu (BoT).

Chiligati alikiri kuwa, kikao kilichofanyika jana kilibaini kuwa kashfa hizo, na nyingine kadhaa, zimepunguza kwa kiasi kikubwa imani ya wananchi juu wa chama hicho.

Alisema kilichokitikisa chama hicho ni kuhusishwa kwa viongozi kadhaa na makada wa chama hicho, ambao walikuwa pia viongozi wa serikali.

Hata hivyo, alisema chama hicho kimeweza kuidhibiti hali hiyo, sasa kinajipanga upya ili kurejesha imani ya wananchi kwa chama hicho, tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Chiligati alisema kuwa kikao hicho kimekubaliana kuwa wanachama wote ambao watabainika kuhusika katika kashfa za Richmond na EPA, wachukuliwe hatua stahiki, ikiwamo ya kufukuzwa kwenye chama na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Alisema kinachosubiriwa hivi sasa ni ripoti ya utekelezaji wa mapendekezo ya kamati ya Bunge kuhusiana na sakata la Richmond, ambayo imefanyiwa kazi na timu maalumu iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Alisema pia kuwa chama hicho kinasubiri ripoti itakayotolewa na timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, kuchunguza sakata la EPA, kabla ya kuchukua hatua kwa watakaoonekana kuhusika.

"Kama ilivyo kwenye mchezo wa mpira, kunakuwa na matukio mengi, hivi sasa tupo kwenye half time (kipindi cha mapumziko)… lakini tupo kwenye mwelekeo mzuri," alisema Chiligati.

Hata hivyo, alipotakiwa kuwataja wanachama ambao wapo hatarini kufukuzwa, Chiligati alikataa kufanya hivyo, kwa maelezo kuwa taarifa kamili juu ya suala hilo itatolewa baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchunguzi unaoendelea kuhusiana na masuala hayo mawili.

Sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Richmond, lililochunguzwa na kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela-CCM), ndilo lililosababisha kujiuzulu kwa aliyewahi kuwa waziri mkuu, Edward Lowassa na kusababisha kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri Februari mwaka huu.

Aidha, pamoja na Lowassa, ripoti ya kamati hiyo ilisababisha pia aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na waziri wa Afrika Mashairki, Dk. Ibrahim Msabaha, nao kujiuzulu baada ya kutajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine na mchakato wa kuipatia kampuni hiyo kandarasi katika mazingira ya kutatanisha.

Akimzungumzia Lowassa, baada ya kuulizwa na waandishi kuwa ni mmoja wa viongozi walio hatarini kufukuzwa, Chiligati alisema kuwa hata katika ripoti hiyo hakumuona akiwa anahusika moja kwa moja, na ndiyo maana ilipendekeza yeye mwenyewe apime uzito wa suala hilo na kuchukua hatua zinazofaa.

Alisema wengi walioonekana kuhusika moja kwa moja na Richmond ni wasaidizi wa aliyekuwa waziri mkuu huyo, ingawa yeye mwenyewe aliamua kujiuzulu kutokana na kuwajibika kwa makosa yaliyofanywa na watu aliokuwa anapaswa kusimamia utendaji wao.

Chiligati alisema kuwa wajumbe wa NEC waliwamwagia sifa viongozi kadhaa walioachia ngazi kutokana na kashfa, kwani kitendo hicho kimekipa heshima chama hicho.

Kwa upande mwingine, habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa baadhi ya wajumbe walikuja juu, na wakaeleza wazi wazi kutokuwa na imani na Makamba, na kupendekeza aondolewe kwenye wadhifa huo mara moja.

Wajumbe hao walisema kuwa Makamba amekuwa mbabe mno katika utendaji wake na wakati mwingine anatumia lugha ambazo zinakigawa zaidi chama kuliko kukijenga.

Walisema hali hiyo inahatarisha umoja wa chama na ukichanganya na hali ya kisiasa nchini hivi sasa, kuna hatari chama hicho kikapata wakati mgumu kurejesha imani ya wananchi juu yake.

Walitaka aondolewe kwenye nafasi hiyo wakidai kuwa, licha ya kuwagawa wanachama ndani ya chama, kauli za Makamba wakati mwingine zinafanya kazi ya kukisafisha chama kilichochafuliwa kwa tuhuma za ufisadi kuwa ngumu.

Inadaiwa kuwa kikao hicho ni matunda ya mbinyo wa baadhi ya wabunge, ambao walifikisha ujumbe kwa mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete, wakiomba kuitishwa kwa kikao kitakachojadili masuala mazito yanayokikabili chama hivi sasa, lakini yamekuwa yakipigwa danadana.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho, zilieleza kuwa baadhi ya makada walijitoa wazi wazi kueleza kusikitishwa kwao na jinsi ambavyo baadhi ya watuhumiwa wamekuwa wakilindwa ndani ya chama.

Wabunge hao, ambao kwa sasa hatutayataja majina yao, walieleza kuwa uamuzi wa kuendelea kuwakingia kifua wanachama hao wenye kashfa, ambao baadhi yao walishaondolewa au kujiondoa kutoka serikalini, unakichafua chama hicho na kukipa wakati mgumu kutetea masuala yake kwa wananchi, wakati huu ambapo vita dhidi ya ufisadi imegeuka kuwa ajenda ya kila mtu nchini.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa mikakati ya wabunge hao ilianza juzi, ambapo waliomba kikao hicho kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, na kumfikishia Makamba ajenda kadhaa.

Mbili kati ya ajenda hizo zilikuwa zinamgusa Makamba. Ajenda moja inadaiwa kumgusa moja kwa moja, kwa kuwa ilikuwa inataka aondolewe kwenye wadhifa huo kutokana na tuhuma kadhaa ambazo kwa sababu hatujazithibitisha hatuwezi kuzitaja kwa sasa.

Aidha, ajenda nyingine ilihusiana na kujadiliwa, kwa lengo la kufukuzwa kutoka katika chama, wanachama wote ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakitazamwa na jamii kwa jicho lisilopendeza, kutokana na tuhuma za ufisadi dhidi yao.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza zaidi kuwa yaliibuka mabishano makali kutokana na mjadala wa hoja ya Richmond, baada ya Lowassa kusimama na kujitetea kuwa alishatoa ushauri mara mbili mkataba huo uvunjwe lakini alikataliwa.

Baada ya mabishano makali, inadaiwa kuwa Rais Kikwete alilazimika kusimama na kutoa ufafanuzi na kueleza kuwa Lowassa alikuwa na nafasi ya kutoa maelezo na kutojiuzulu nafasi yake, lakini mwenye aliona kujiuzulu ndio uamuzi wa busara.

Kikwete aliwaonya wajumbe kuwa makini wanapojadili suala la giza na umeme na kuwataka iwapo wanataka kufahamu madhara ya kukosa umeme na kuwa gizani, wawaulize watu kutoka Zanzibar.

Alipotoa kauli hiyo, karibu wajumbe wote wa NEC kutoka Zanzibar walisimama, ingawa haikuweza kufahamika mara moja hatua hiyo ililenga nini.

Mjadala huo ulizua pande mbili zinazopingana, ikiwamo kambi inayowatetea kina Lowassa na viongozi wengine waliolazimika kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo, na kambi nyingine ikitaka wachukuliwe hatua kali zaidi kwa kukichafua chama kutokana na kuhusika kwao kwenye kashfa hizo.

juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 5 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)

Soma hii aya "Hata hivyo, alisema chama hicho kimeweza kuidhibiti hali hiyo, sasa kinajipanga upya ili kurejesha imani ya wananchi kwa chama hicho, tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010".

Watanzania msilale. hii ni kauli ya Bw Chilligati. sasa wanapanga kuiba tena! Mungu wangu. Pamoja na ufisadi mkubwa ambao bado wahusika hawajaadhibiwa. Sasa wahusika walele wanapanga kuiba 2010. kazi ya CCm ni uchaguzi tuuuuuuuuu

na Mkeli hamisi, Tbr, TZ, - 16.06.08 @ 09:01 | #16729

kama kweli ccm wamedhamilia kuwafukuza kazi waliokua viongozi waliohusishwa na ufisadi basi wafanye ivyo na sio kubaki kupiga kelele tu,chiligati anasema wanachama wao watakaothibitika kushiriki katika ufisadi wa richmond na epa watachukuliwa hatua stahiki,kwa hiyo anataka kusema mpaka sasa ccm haiwajui wanachama wao walioshiriki katika hizo kashfa, na kikwete anaposema tuwaulize watu wa znz kero za kukaa gizani,ana mana watu wa bara hawajui adha ya kukaa kizani,au anataka kuonyesha kua richmond iliwahi na kutuokoa kukaa kizani,kwa maana nyingine kuonyesha kua swala zima la richmond kwake ni sawa tu,sidhani kama kuna lolote ccm watafanya bali ni porojo tu.

na mstari wa mbele, calif/usa, - 16.06.08 @ 09:04 | #16732

Hawa CCM waache kufanya watu wengine kama akili hamnazo. Mtu hawezi kuwa ***** halafu yeye mwenyewe aseme mimi ni *****. Lowasa ni fisadi tena 'maafisa' sasa kumpa nafasi ajieleze ni kudanganya walala hoi.

Halafu kingine Kikwete hawezi kumuondoa Lowasa, hao ndo walimueka madarakani. Na huyu Makamba, aliletwa na Kikwete, lakini siwezi kushangaa Makamba kwa sababu hata hiyo kazi yenu ya ukatibu mkuu hana hata sifa.

na chaloo heri, Dar, TZ, - 16.06.08 @ 09:36 | #16737

HAKIKA CCM MNATUSHANGAZA BAADALA YA KUZUNGUMZIA UTEKELEZAJI WA ILANI ZA CHAMA CHENU KABLA YA 2010 MNAAZA KUZUNGUMZIA KUJIPANGA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU!!!!!KWELI AKILI HANAZO.ZUNGUZIENI HALU YA UCHUMI WA NCHI YETU NA SIO KUANZA KUJIPANGA JINSI YA KUTUIBIA TENA. ANGALIA BEI ZA MAFUTA NA VYAKULA ZILIVYO JUU,MAISHA YMEKUWA MAGUMU KUPITA KIASI WAKATI KIKUNDI KIDOGO KIKIENDELEA KUNEEMEKA. INATIA UCHUNGU. IKO SIKU WA TZ WATAWATAFUNA SIJUI MTAKIMBILIA WAPI.

na MPENDA HAKI, DSM, - 16.06.08 @ 10:00 | #16744

Kikwete leo umenitonesha kidonda! Unamtetea Lowassa!! Pia unaishabikia kashfa ya Richmond!! Rais wetu Tz?? Hii inaonyesha wazi kuna mkono wa JK ktk UFISADI uliofanyika hapo. Lowasa ni bonge la Fisadi, iweje wewe kama Rais umtetee? Kumbe ndo maana hata mafisadi hawawajibishwi!? Haya sasa angalia hao mafisadi wameanza kushika NDUMBA zao kwa lengo la kuwadhuru wabunge wema!! Hatuponi kwa kuwa Rais wa TZ anawalea mafisadi.

na RichmondEPA, Tanzaniabara, - 16.06.08 @ 10:07 | #16746

Source: Tanzania Daima

Hoja: Hatua za kuwaadhibu wanaCCM waliohusika na ufisadi zinachukulia baada ya 'half time kuisha' (Chiligati, 2008). Hatua hizo zitategemea ripoti ya kamati iliyoundwa na Pinda na ile ya EPA. Je hizi kamati zinanguvu ya kumfunga paka kengere? Hivi ripoti ya kamati ya Mwakyembe na ile ya ukaguzi wa EPA hazitoshi kutoa adhabu?
 
“Kama ilivyo kwenye mchezo wa mpira, kunakuwa na matukio mengi, hivi sasa tupo kwenye half time (kipindi cha mapumziko)… lakini tupo kwenye mwelekeo mzuri,” alisema Chiligati.

Hili ndo tatizo la kuwa na ubia kwenye urais, hakutakuwa na jipya toka kwa huyu zero wetu
 
Jamni tunaomba FMES utupdate news nn kina jili saizi hapo DOM....
 
Labda hii ni update

Aliyeingia bungeni usiku atajwa

na Martin Malera, Dodoma

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kapteni John Chiligati, jana alimtaja mbele ya waandishi wa habari mbunge ambaye aliingia katika ukumbi wa Bunge jioni ya Jumatatu.

Tukio hilo linahusishwa na ushirikina kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi, ambazo zimekuwa zikisambaa kwa muda wa siku tatu zilizopita.

Ingawa hakumtaja kwa jina, Chiligati alisema kuwa mbunge huyo alikuwa waziri lakini sasa hana tena wadhifa huo.

Akifafanua, Chiligati alikiri kuwa mbunge huyo aliomba na kupewa ruhusa kuingia ndani ya ukumbi huo wa Bunge, ili kukagua na kuangalia nafasi atakayokuwa anaketi.

Alisema kuwa mbunge huyo alilazimika kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na kiti maalumu cha kukalia ndani ya Bunge kutokana na kuondoka kwake kutoka katika wadhifa wa uwaziri.

Chiligati alisema kwamba, kwa kuwa Bunge lilikuwa linaanza vikao vyake siku inayofuata, mbunge huyo aliona ni busara kutafuta mahali pa kukaa jioni hiyo, ili asisumbuke asubuhi.

Alikiri kuwa ni kweli aliingia ndani ya ukumbi wa Bunge na kupita katika kila kiti, akiangalia majina kwa lengo la kutafuta kiti kilichokuwa wazi.

Alisema wakati akifanya hivyo, hakuweka uchawi wowote kama ambavyo inadaiwa na watu hivi sasa.

Kwa taratibu za Bunge, kila kundi ndani ya Bunge hilo lina mahali pake maalumu pa kukaa kwa mpangilio unaoeleweka. Makundi hayo ni pamoja na mawaziri, ambao huketi upande wa kuume kwa Spika, wapinzani, ambao huketi upande wa kushoto wa Spika na wabunge wengine ambao hukaa katika nafasi zilizosalia.

Chini ya utaratibu huo, mpangilio wa kukaa hupangwa mwanzoni mwa Bunge, ambapo kila mbunge hupangiwa kiti chake cha kukaa. Hata hivyo, wabunge wanaruhusiwa kuhama kwa muda kwenda eneo jingine na wanapomaliza dharura hiyo hurejea kwenye viti vyao.

Spika Samuel Sitta, naye alishathibitisha kuwa, zipo picha zinazomuonyesha mbunge huyo akiwa ameandamana na mtumishi mmoja wa Bunge, akipita katika viti kadhaa ndani ya ukumbi huo wakati ukiwa umefungwa.

Ingawa Sitta na Chiligati waliepuka kumtaja mbunge huyo kwa jina, lakini kiongozi ambaye alikuwa waziri na kujiuzulu katika siku za hivi karibuni ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.

Chenge alijiuzulu kutokana na kuhusishwa kwake kwenye uchunguzi unaoendeshwa na Taasisi ya Kuchunguza makosa ya rushwa ya Uingereza (SFO).

Makachero wa SFO walivutika kumchunguza Chenge katika uchunguzi wao dhidi ya Kampuni ya Bae Systems ya Uingereza iliyoiuzia Tanzania rada kwa bei ya juu.

Licha ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati mkataba wa mauzo hayo unafikiwa, makachero wa SFO walimkuta Chenge akiwa na akiba ya takriban dola za Marekani milioni moja kwenye akaunti iliyo katika benki moja katika visiwa vya Jersey.

Tangu ajiuzulu nafasi hiyo, Chenge hajawahi kuhudhuria vikao vya Bunge, na ni kweli hivi sasa anawajibika kutafuta nafasi ya kukaa kwa kuwa hataweza tena kukaa katika nafasi ya mawaziri aliyokuwa akikaa zamani.

Tukio hilo limewaweka wabunge roho juu, hasa baada ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, kuugua ghafla katikati ya wiki iliyopita na kulazimika kukimbizwa katika kliniki ya Bunge ili kupata huduma za kiafya.

Wabunge kadhaa sasa wanaonekana kuogopa kuusogelea ukumbi wa Bunge, kutokana na taarifa hizo za kuwepo kwa vitendo vya kishirikina.

“Hili tukio limetutia hofu, tunadhani kuna kila sababu ya kukamilisha uchunguzi wa tukio hili mapema. Spika ameeleza kuwa tukio hili linachunguzwa, tunaomba lichunguzwe kweli, tena kwa haraka, ili kutuondolea hofu tuliyonayo sasa,” alisema mmoja wa wabunge kutoka Mkoa wa Mwanza.

Mbunge mwingine ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alilieleza gazeti hili kuwa Spika anapaswa kutoa taarifa ya tukio hili bungeni na kulitolea ufafanuzi badala ya kuendelea kulizungumza kwenye vyombo vya habari.

“Hizi taarifa zipo, wabunge wengi wanazijua, lakini Spika analizungumzia kwenye vyombo vya habari. Mimi nadhani suala hili linagusa maisha yetu, ni bora akalieleza Bunge nini kilitokea,” alisema mbunge huyo.

Akizungumza na waandishi juzi, Sitta alisema kuwa, ofisi yake imekabidhi picha za video zilizomnasa mbunge huyo akiwa ameambatana na Ofisa Mwandamizi wa Bunge kwa siri, waliokuwa wakiweka vitu vinavyoaminika kuwa vya kishirikina au aina fulani ya sumu kwenye kila kiti cha mbunge.

Kwa mujibu wa Sitta, picha za mkanda huo zilizonaswa na kamera za usalama zilizomo ndani ya jengo hilo la kisasa, zimefifia kiasi cha kushindwa kubaini kwa haraka watu wanaoonekana ndani ya mkanda huo.

Kutokana na hali hiyo, Sitta alisema ofisi yake imeamua kuukabidhi mkanda wa picha hizo kwa maofisa usalama wa taifa na kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi zaidi
 
Wakuu heshima mbele, JF one step ahead we are back on the track wakati wowote tutamwaga news au new Dataz, za kutoka Dodoma stay tuned!

Nafikiri ndugu zangu mtakuwa mmeshaelewa kuwa tusipkuwa one step ahead kuna hatari wasiziseme kabisaaa yaani za ndani!

Ahsante Wakuu! Baadaye!
 
Karibu Mkuu,
Lete mambo! Macho yangu kwenye screen, vidole kwenye cursor, pointer kwenye refresh button kuzisubiri habari toka kwa FMES
 
Wakuu heshima mbele, JF one step ahead we are back on the track wakati wowote tutamwaga news au new Dataz, za kutoka Dodoma stay tuned!

Nafikiri ndugu zangu mtakuwa mmeshaelewa kuwa tusipkuwa one step ahead kuna hatari wasiziseme kabisaaa yaani za ndani!

Ahsante Wakuu! Baadaye!

Mkuu Wangu,

Udumu Daima.Ni kazi nzito kwa taifa hili na nakupa salute kwa kuwa pamoja always kwa ishuz za Taifa.

Madataz mengine unaibuka nayo ni kama ule mtambo uliodondoshwa Hiroshima.

Wakuu Wengine humu ndani,

Mimi bado niko na Huyu member wa Hapa anayejiita "MTU WA PWANI" ,huyu mkuu alimzushia ZITTO kwamba inasemekana ni yeye aliyeonekana ndani ya ukumbi wa BUNGE,Nilimuonya na wakulu wengine humu jamvini pia wakamuonya,still aka-insist kuwa Ni ZITTO.

Sasa ilipokuja kuthibitika kuwa si Zitto,nikamshauri huyu mkuu aje aombe radhi hapa Jamvini kwani Amedhalilisha kijiwe hiki ili tuonekane wote humu ndani ni wadaku,watoto nk. kwa kuwachafulia watu majina.Sasa bado namshauri huyu mkuu arudi hapa kuomba msamaha maanake si uungwana wala heri kumkashifu mbunge wa watu halafu members na Mods hapa tuone halafu tukae kimya kwani at last itakua ni mazoea.

Jana aliniomba ushahidi,kwa bahati mzuri MAMA akampatia maanake alinitaka nilete ushahidi la sivyo mimi nimtake radhi,sasa nilimpatia na amepotea.

Btw: Komandoo ES,bado nakusubiri kwa hamu mkuu na na hilo li-B29
 
Mie jamani naomba kujua huyo chiligati sijui nani sijamwelewa
Hivi wabunge viti bungeni wanajitafutia wao wenyewe nafasi ipo wapi wakae au wanawekewa na watumishi wa bunge?
2. Kama wanajitafutia wenyewe sasa hayo majina kwenye viti yalitoka wapi?kiasi jamaa awe anaangalia jina lake?
3. Na kama kulikuwa na majina kumbe iliwezekana kabisa kuoneshwa kiti chake wakati ule ule rasmi wa kuingia bungeni
4. Kwa mtizamo reasonable kabisa hata mie nikienda pale bungeni leo sitatafuta kiti najua nitaoneshwa tu na makarani wa bunge sembuse mtu aliyekuwa waziri na inajulikana kabisa anarudi kuwa back bencher?
5. Kwa taarifa zilizopo ule ukumbi wa bunge una idadi ya viti kubwa kuliko wabunge waliopo,je kulikuwa na haja ya kutafuta kiti mapema?
6. kwani bunge wakati linaanza ile siku ya kwanza alikaa wapi?mpaka atafute kwa kukaa awamu ya pili ambako kungesomwa bajeti?au hata kama alikuwepo kwanini atafute kiti siku ambayo sio official kwa wabunge kuingia kwenye debate hall?
7. Kwa spika ama naibu spika nako ni back bencher?mbona alishawapta hata mawaziri au alitaka kuongoza bunge siku hiyo?
Maswali haya na mengine mengi yanazua circumstantial evidence kuwa huenda basi amehusika,na kwa wale waliosoma sheria ya ushahidi najua wamo wana sheria humu,kuna vitu kama res gestae kwenye ushahidi na pia section 3-20 ya sheria ya ushahidiTanzania ambapo kuna mambo ya ushahidi wa kusikia au kudhani yanaruhusiwa ili mradi yawe supported na other set of facts(yaani corroborated) hivi hamuoni kama chenge anatia shaka?

Asante mkuu... kwa kuongezea ni kwamba... hakuwa mgeni bungeni..maana toka akiwa AG anaingia bungeni... huo ugeni na mchecheto wa kutafuta kiti baada ya saa za kazi unatoka wapi?????
ushers wa bunge kwani kazi yao nini??
hata mwanafunzi mgeni wa darasa la kwanza hatangulii shule siku moja kabla shule kufunguliwa kwenda kujitafutia pa kukaa...
 
Huyo ni mwanga tu,kwanini asingetoa taarifa na akatafutiwa?

Mtu wa Pwani bado pia nakususubiri uje kuonyesha uunwana
 
ama kweli mapinduzi daima.
niliondoka hapa wiki tu .....nimerudi chenge keshakuwa mental unstable!!!
chenge anaweza kujivuwa hili kwa kuplead temporary insane kwa kufichuliwa vijisenti vyake
 
Huyo ni mwanga tu,kwanini asingetoa taarifa na akatafutiwa?

Mtu wa Pwani bado pia nakususubiri uje kuonyesha uunwana

Kubali yaishe tu..kuomba msamaha yataka moyo..ila usione vibaya maana this is a safe space hatukuoni unavyoona aibu!
 
'Samaki huanza kuozea kichwani!'

kwa mtazamo wangu, CCM imeanza kupoteza nguvu ya mwenyekiti wake kichama tangu Nyerere afariki!

...ili kujinusuru, wangebadili hili la mwenyekiti wa Chama pia kuwa Rais wa nchi. Angalau wakati wa Mzee Malecela kama makamu mwenyekiti kulikuwa na kauoga kidogo,

Pressure imekuwa kubwa mno, naamini sio kila Raisi anaweza kumudu hizo kofia mbili. Mzee Mwinyi alijitahidi, Mkapa ndio hivyo tena, authoritarian style angalau siku zilikwenda, huyu M'kiti wa sasa na participative style yake, mkondo umeuzidi uwezo mashua!... chama kinayumba!
Accountability ipo wapi?

Wapinzani wakitumia nyufa hizi vizuri, 2010 hadithi itakuwa nyingine.

Huu ni mtazamo wako Mkuu, lakini kuna wengi kama shy na kibunango ambao wanaona bado CCM bado wako katika mstari. Na halafu kuhusu upinzani naona bado kabisa na kama Wtz watawakubali bas ni kwa makosa ya CCM na sio kuwa wapinzani wana dira inayojulikana ya kuiendeleza nchi hii.
 
[/B][/COLOR]

Kubali yaishe tu..kuomba msamaha yataka moyo..ila usione vibaya maana this is a safe space hatukuoni unavyoona aibu!

Kweli kabisa mkuu,Amekwepa na ameenda kuanzisha thread nyingine.But,wakuu huyu ni mfano wa wachache wanaowapa sababu Jeshi la Polisi na maofisa usalama kuja kutuharibia malengo yetu mbele ya Jamii.

Mtu kama huyu mkuu anaweza siku moja kuja kufanya mambo yote makubwa ambayo hii forum imewafanyia watanzania yayeyuke hata ukisema wewe ni memba wa hapa watu waanze kuturushia mawe.Hatutakubali hilo litokee.

Mkuu,Mtu wa Pwani,plz come back uweke mambo sawa na ulinde hadhi ya hili jamvi.

Btw: Mkuu ES bado niko na wewe kwenye kusubiria Dataz na nondoz nzito nzito.Salute kwako Komandoo!
 
Back
Top Bottom