Mkuu najua kuo sasa hivi uko Dodoma, ninasema hivi ukisoma kwa makini historia za Empire nyingi sana za zamani huko Europe, ni kwamba almost siku zote wafalme au viongozi wao wa hizo Empire, walikuwa wako vitani, lakini kuna wakati walikuwa wakishinda vita na kutawala kwa muda wa miaka kama kumi mpaka 30,
Mkuu historia yao iko very clear kuwa wakisha shinda vita, walikuwa na tabia ya kuwapiga risasi au kuwa-eliminate wale wote waliowasaidia katika kushinda vita, kwa sababu inapswa kuwa very clear kwa kiongozi yoyote yule duniani kuwa wasaidizi wa vita, sio watawala, kwa hiyo dawa ni kuachana nao mara tu power ikipatikana, ukisoma kitabu cha Jerry Ralwings, yuko very clear on hilo, walipofanikiwa kupindua nchi tu, basi mshikaji wake wa karibu General Oqnqwipa alikimbia mwenyewe kabla Ralwings hajawakamata washikaji wake wote waliomsaidia na kuwaua kwa risasi, anasema ndio maana aliweza kutawala mpaka alipoamua ku-retire!
Mkuu wangu I am revolutionist wa vitendo sio maneno matupu, Muuungwana alipaswa kuachana na hawa washikaji the minute aliposhinda tu, kwa sababu sasa hivi asipoaangalia wataiushia kumpumzisha yeye, maana sasa wana nguvu nzito sana ya Mkapa nyuma yao!
Mkuu,kwanza ni kwamba bado sijatua Dodoma.Nimehitimu shahada yangu mwezi uliopita.Kwasasa bado nabeba maboxi kwa muda hapa kwa Mzee Bush nikichanga nauli ya kurudia nyumbani Tanzania.Panapo majariwa ya Mwenyezi Mungu, nitakuwa Dodoma wiki ya kwanza ya mwezi wa nane.
Nafurahi kusikia kwamba wewe ni mwanamapinduzi wa kweli.Kimsingi,hata mimi napenda watu wa aina yako.
Mkuu nimekuelewa juu ya hizo historia.Ni kweli unayoyasema.Likini historia hiyohiyo inathibitisha wazi kuwa sio wote waliowaangamiza wasaidizi wao walikuwa na nia njema ya kufanya hivyo.Wengine walikuwa wakifanya hivyo kwa hofu ya kugeukwa na wale waliowasaidia kushinda vita.Ni hii ilitokea sana kwa wale waliokuwa wakiwafahamu vema nje na ndani na hivyo kuhatarisha uhai wa tawala zao.Umetoa mfano wa huyu rais wa zamani wa Ghana, Jerry Ralwings.Sasa huyu bwana ni mmoja wa hao watawala waliowaua wasaidizi wao kwa hulka zao za kidikteta tu na wala sio kwa nia njema.Nimesoma na waghana wengi sana hapa Marekani.Kwa kweli namna wanavyozungumzia utawala wa kidikteta wa Jerry na idadi ya wanasiasa aliowaua katika kipindi cha utawala wake,hutatamani hata kutumia rejea yoyoye toka kwake.Jerry alikuwa ni mshenzi na myama.Kuna mghana mmoja nimesoma naye darasa moja ambaye mjomba wake alikuwa ni mmoja wa wahanga wa utawala wake.Akikusimulia vitendo viovu vya utawala wa Jerry, utasikitika sana.
Kwa hiyo mkuu ninachotaka kusema ni kwamba, sio watawala wote waliwateketeza wasaidizi wao kama njia bora ya kujiwekea mazingira mazuri ya kutawala.Bali wengine walifanya hivyo kutokana na hulka zao za kifashsti na kutopenda mawazo mbadala.Maana mtu kama Jerry, sio tu kwamba aliwaua wale waliomsaidia tu,bali aliendelea kufanya hivyo katika kipindi chote cha utawala wake kwa wale wote walioonekana kuwa mwiba kwenye utawala wake.Sasa siamnini mkuu kama unaweza kuufagilia utawala wa watu aina ya kina Jerry.
Sasa nikirudi kwa muungwana, kuna mambo ya kuyaangalia kabla ya kumlaumu kuwa kwanini asiwatose waliomsaidia muda mfupi baada ya kushinda.
Jambo la kwanza ni la kibinadamu kabisa.Wahenga walisema "akufaae kwa dhiki ndiye rafiki".Sasa mkuu hili halina ubishi kabisa kwamba,katika hali ya kawaida kwa binadamu mwenye akili timamu,huwezi kuacha kumfikiria kwanza kumkumbuka mtu aliyechangia mafanikoa yako ya aina yoyote ile katika maisha.Sasa hii si hulka ya kibinadamu tu bali ni ya kiMungu pia.Najua wewe ni msomaji wa biblia.Unajua habari ya msamaria mwema,kuwatembelea wafungwa,wagonjwa,na kuwasaidia wenye njaa.Na kuna mahali biblia imezungumza kabisa umuhimu wa kuwasaidia kwanza watu wa nyumbani kwako .Ninachotaka kukazia hapa ni kwamba,suala la kuwakumbuka kwanza waliokusaidia katika mahitaji yako ni la kawaida na la kiungwana zaidi,ukiachilia mbali mifano ya madikteta wachache kama kina Jerry.Na hili lipo mahali pote katika ulimwengu wa siasa.Kwa hiyo muungwana hakufanya jambo jipya.Na tumbuke kuwa sio wote waliomsaidia muungwana ni tatizo katika utawala wake.Wako wanamtandao wengine wanachapa kazi vizuri kabisa bila shaka yoyote.
Sasa ni bahati mbaya sana kwamba,vinara wa mtandao ndio walioharibu.Na bahati mbaya sana kwamba vinara hao wamekuwa watu wa karibu na muungwana kwa kipindi kirefu.Sasa hapa ni pagumu sana kwa kweli.Nasema hivyo kwa kuwa nafahamu fika kuwa kuna mambo ya siri yaliyokuwa yanafanywa na vinara hawa na muungwana alikuwa hajui lolote.Hapa nazungumzia tabia binafsi za vigogo wa mtandao.Mkuu naomba uelewe kuwa wewe unaweza kuwa mtu wangu wa karibu kwa muda mrefu, lakini usijue mambo ninayoyafanya sirini.Kwa hiyo,ninachotaka kusema ni kwamba, si muungwana tu aliyewaamini na kujiridhisha na watu wake.Watanzania wengi tu tuliwaamini makada hawa.Ndio maana kama utakumbuka wakati jina la el linasomwa na spika bungeni kuwa pm,bunge zima lilipuka kwa vifijo(ingawa wengi pia walitegemea hivyo).Zikapigwa kura za kumthibitisha bungeni.Akaungwa mkono wa wabunge wote wakiwemo kina Zito,Slaa na wabunge wa upinzani wengine.Sasa,hii maana yake nini? Maana yake ni kwamba kabla ya zogo la Richmond, hakuna aliyekuwa na shaka yoyote juu maadili ya uongozi ya el na wenzie.
Kwa hiyo mkuu muhimu kwa sasa ni kwa muungwana kuwa makini na watu anaowaamini ili wasimharibie.Ahakikishe anajiridisha sana na watu anaowapa majukumu ya kumsaidia.Najua ameliona hilo na amejipanga vizuri.
Mkuu suala la hawa jamaa kuwa na nguvu kubwa kwa sasa wakisaidiwa na Mkapa,mimi sidhani kama wanaweza tatizo kwa muungwana na CCM kwa ujumla.Mkuu mimi naijua CCM vizuri sana.Kwa mtizamo wa haraka haraka na wa nje,unaweza kudhani nguvu ya hawa watu ni kubwa na yenye athari kwa chama.Lakini nakuhakikishia kwa namna ninavyokijua chama,muungwana wala hawa hofu kwa sababu, kwa muundo na mfumo wa chama, muungwna sasa hivi ndiye mwenye nguvu,rasilimali na uwezo wa kufanya chochote kuliko mtu wala kikundi chochote ndani ya chama na serikali.Hata hao watu wanalijua vema hilo.Ni kweli kwa ujinga wao,wanaweza kutumia pesa na ushawishi mwingine wakafanikiwa kulata vurugu kidogo.Lakini mwisho wa siku wao ndio wataumia zaidi.Ni suala la muungwana kuamua tu.Akiamua wote hao watakufa kisiasa ndani ya dk chache sana.Kwa tunaomjua muungwana sio wa mchezo hata kidogo.Na wao wanalifahamu hilo.Wachokoze wakione cha moto!