Wakuu,
Habari hii nzito sana na naikubali....
Ama kweli tumefikia mahala ambapo sasa Utamaduni wa sayansi ya mwafrika inachukua nafasi kubwa ya maisha yetu. Uchawi ni sayansi hiyo hiyo mnayoizungumzia isipokuwa haina vipimo vya maabala zetu isipokuwa hizo za makati za ufundi..
Hata huyo Moses alikuwa na nyanga zote kuweza kukabiliana na manyanga ya Pharaoh ambaye kama sii uchawi asingeweza kubadilisha mkongojo wake kuwa nyoka. Tukumbuke tu ndani ya uchawi hutanguliwa na mkulu fulani iwe Mungu ama Nyamuhanga au RA the Egyptian Sun God...kifupi wote wanatumia magical substances ambazo leo tunazipa majina ya kisayansi kutokana na powerful supernatural substances iwe zinatokana na mizizi, miti, madini ama ritually miili ya viumbe kama binadamu na kadhalika.
Sasa mchawi akichukua embryo stem cell na kuzifanyia kazi watu tunaona maajabu lakini madaktari wa Ulaya wakichukua vitu hivyo hivyo ili kuponya ugonjwa tunawaona wao ndoo wakweli hali Wamasai wameshaufanyia kazi karne na karne..
Kifupi tunao wanasayansi kwa sababu kuna vitu na magonjwa ya ajabu ambayo yanatakiwa wataalan na pia kuna waganga wa kienyeji kwa sababu kuna Uchawi.. Hili swala la imani lipo iwe ktk imani ya kizungu ama kiafrika kwa sababu kama huamini magonjwa kama HIV ambayo kwa lugha ya kiafrika ni uchawi tu tusingekuwa na waganga wa maabara. Na kifupi HIV hata waganga wa kizungu huko Bagamoyo kwao wameshindwa!
Haya huku nimeenda mbali sana na kile kilichotokea Dodoma lakini nachojaribu kusema ni kwamba wapo wanaudhulika.. iwe sumu iliyotokana na nyongo ya nyoka ama binadamu na imetengenezwa kienyeji haina maana haiwezi kuleta madhara!...maadam, ktk maisha yetu tutaendelea kuwa na contact na hizi ritual paraphernalia madhara lazima yatakuwepo...Na gharama yake sio kubwa kama sumu ya mzungu ambayo ina complication kibao ktk kuzipata.. results ni zile zile kumwondoa mtu!..
wameondoka kina Malima, Kolimba, AC, Balali oooops! tena ktk mahospital makubwa na sababu mlizopewa hazina hata kichwa bado mnataka ushahidi gani kuwa uchawi upo na imani pekee haiwezi kusaidia isipokuwa nawe unatakiwa uwe na zana haswa! Kama ni Biblia au Kuran sio tu kuibeba mkononi na kuamini Yesu au Mungu laaah! unatakiwa uzijue aya zinazoweza kupambana na uchawi uliorushwa! Kinga haiwezi kuwepo kama hujaweka ngao yako kule kunakotokea mashambulizi...
je, naamini uchawi?... ooooh YES! kwa sababu uchawi ni sayansi kama sayansi nyinginezo na dawa ya sumu ya nyoka ni lazima uwe na antivenom.
Mkandara
sisi wenda hua si wagunduzi kwa sababu kitu tukikiona cha staajabisha tunakita imani.
UCHAWI si imani Ni sayansi ambayo bado tafiti zake hazijatoa majibu hii ni kutokana na Techonojia tuliyonayo hajikomaa ila theory zipo za kutosha,Ni kama vile theory za fibre optics zilikuwepo karne nyingi ila implementation ilikua ngumu kutokana na technolojia wakati huo haijakomaa.
kifupi.
electrons hua zinaishi kwenye valency band ktk maada yoyote lakini hiyo maada ukiipa energy mfano mwanga,moto,chemical(uchawi,kemia) hua electorn inaruka na kwenda kwenye condunction band,sasa basi electorn ikipoteza hiyo energy inaanguka kutoka conduction hadi valency band na nguvu iliyopotea inapaa hewani kama photons.
Na kwa vile electrons hua zinatofautiana energy vivyo hivyo photons hewani zitatofautiana energy na hii energy ndio ina characterize masafa (frequency) yake ,sasa basi hili bando la photons lililo na energy tofautitofauti huitwa spectrums,Na photon zenye energy kubwa ndizo zina frequency kubwa kumbe basi spectrum sio continuous bali discrete.
Sasa basi ktk bando hili la photons(spectrum) wanasansi ambacho wameshaona ni-
1.Radio wave 0.3-3KHz ambazo ndio masikio ya mtu yanaweza sikia,hivyo electron yoyote iliyo ktk masafa hayo masikio ya mtu yanausikia mwendo huo.
2.microwave 3-300kHz electrons iliyo ktk masafa hayo inaweza kuchemsha maji .hapa watu wengi hujiuliza kwanini ukiweka chakula kwenye microwave ni chakula tu ndio kina pata joto walakini chombo hakipati joto.kumbuka michrowave inachemsha maji tu kumbe chakula kinachemka kwa sababu kina majimaji.
3.Light 3-30GHz electrons ktk masafa hayo inatoa mwanga ambao macho ya binadamu unaweza kuyaona.
4.infrared
5.ultraviolet
6.x-ray 30-300PHz hii inaweza penyeza kwenye nyama na ndio elecrons zilizo ktk mwendo huo hua zinatumika kule hospitali kupiga x ray
7.gamma ray 30-300 EHz
Sasa basi Wataalamu wa jadi hua wanatumia chemical means (kuchanganya miti,nyama ya mtu,ubongo wa mtu)kuzirusha electrons ambazo hua zinapaa ktk spectrums with very specific frequency ambazo hazipo hapo juu Na
zinakua ktk makundi mawili 1. kuyahadaa macho na akili ya binadamu yani hizi photons zikigonga akili na macho kinafanyika modulation yani signal inahamisha frequency iliyozoa macho ama akili ndio maana badala ya mtu unaweza ona mbuzi badala ya karatasi unaweza ona fedha(mazingaombwe) mfano mtu akikupiga ngumi vizuri ktk macho unaweza ona shimo refu sehemu iliyotambalale,kumbe hii ni energy aliyo apply ktk macho ni sawasawa tu na energy ya electrons ila tofauti ziko ktk form tofauti ya energy moja ni mechanical nyingine ni electromagenet.
2.Ni hiyo ya kudhuru ambayo unaiua cell za binadamu kama ilivyo tu neuclear,x-ray ama gamma-ray.
Na kumbuka kila kitu cha moto kinatoa (emmit) microwave ndio maana upo unajotojoto na kila mwili unakua ktk resonance frequency fulani sasa mtaalamu(mchawi) anaweza kukutrace sehemu yoyote ulipo yani anachukua band yote ya microwave anaifanyia kitu kinaitwa filtering anaipeleka kwenye kitu kinaitwa matched filter anakupata.Hii matched filter kazi yake na kucompare signal inayoingia na reference aliyo nayo.
Hii reference signal anakua nayo anakua ameichukua mapema physically kutoka kwako ndio maana kuna kamsemo wanasema mlozi hawezi loga mtu asiye mjua maana anakua hana reference signal.Hii technologia nadhani hata akina bush wanatumia kuwatafuta akina Ossama.
Hizi ni theory zangu risechi sijaiweza maana wachawi hawataki kutoa ushirikiano.
Samahani kwa kuvamia maada.