Kutoka Dodoma!

Kutoka Dodoma!

angekua huo uchawi wake kaufanyia nyumbani mwake kwa mkewe na wanawa,sidhani kama tungeieven fungua thread kudiscuss mambo yake,ukumbuke uchawi huo kaufanya ndani ya bunge ambapo wawakilishi wetu sie wa tz wanago ku discuss mambo ambayo ni kwa manufaa yetu dats why yatubidi tudiscuss as its among our bnez n we shud b concerned abt them...

holllo if ur not chenge mwenyewe,his wife,mwanawe au punga lake kama sio huyo mganga wake (i doubt it if wanatumiaga internet),plz u better sometimes not bisha hata mambo yasiyofaa kubisha maana inafikia stage yakera kupita maelezo ila we hujui tu weye waona raha!!
Unajua hajui tunavyokereka hapa sijui anafanya makusudi sijui haelewi? ningekuwa na uwezo ningem ignore nisione post zake.....any way ana uhuru wa kusema.
 
Unajua hajui tunavyokereka hapa sijui anafanya makusudi sijui haelewi? ningekuwa na uwezo ningem ignore nisione post zake.....any way ana uhuru wa kusema.
Mnataka watu wote wawe Against Chenge?yaani kila mtu aamini Chenge mchawi?poleni kwa kukereka ila ukweli ndo huo!Chenge siyo mchawi!
Ukweli unauma!poleni sana
Asanteni
Hollo
 
Masatu,
Unachokisema ni sawa na kusema eti kwa sababu ni muda wa chai, basi tuhangaike kuinywa hiyo chai ingawa kikombe ndani ni kichafu. Siye tunasema kwamba hiyo chai na iachwe hadi kikombe kiwe kisafi na maji ya kuosha yawepo na si leo tu ila kwa muda mrefu ujao. Waafrica tumekuwa na macho ya chatu. Heri ya chatu anasikia kishindo kwa mbalii. Inabidi tujiweke chini na tusafishe kila kitu na kuweka mikakati ili huko mbeleni upupu upungue. Hata ukikaa na kuijadili bajeti, unafikiri utabadilisha kitu? Peter Tosh aliimba kuwa "kila mtu ataka kwenda mbinguni ila hakuna anayetaka kufa". Kwa hiyo ili tufike mbinguni inabdi TUFE kwanza. Hapa hatujali bajeti wala Uchawi. Siye leo ni UFISADI kwanza na kila inapopatikana mwanya basi tutaingiaMO wote na kukoromboaMO humo ndaniNI hadi kieleweke. Lengo hapa ni moja MAFISADI WAANGAMIZWE ili iwe fundisho kuwa wee iba tu ila siku moja ...... Wimbo huo wa Tosh unaongezea kuwa ".... I don't want piece, i don't want freedom, I'M JUST CRYING FOR JUSTICE ..." Bila "Equal right and justice walau 40% kwa wanyonge" basi ujue siku zote Wanyonge watafungwa 666 kwa 13. Nafikiri wajua FISADI ni 666 na 13 ni gundu (Wadanganyika).

Hii safi sana!
JF Fikra mpya na mawazo mapya tunaviona!
Members wapya wapya kwakweli wanaleta changamoto!
Sikonge tunaomba pia uendelee kueneza habari njema za JAMII FORUMS popote pale ulipo na kwa namna yote ile unayoweza..Hii ni pamoja na members wengine wapya na watazamaji.

NB:Mkuu Sikonge...Only kwenye wadanganyika ni 12 letters na si 13.Tuendelee kuomba Mungu huku tukichukua hatua sahihi ikiwa ni pamoja na kumuondoa JK madarakani.
 
Mnataka watu wote wawe Against Chenge?yaani kila mtu aamini Chenge mchawi?poleni kwa kukereka ila ukweli ndo huo!Chenge siyo mchawi!
Ukweli unauma!poleni sana
Asanteni
Hollo
Hollo uliniuliza kama nilipotea toka wakati wa Ballali.
Hapo naona unapoteza memory na sasa una spin!
Wewe ndiye uliyepotea toka wakati wa rumours za kifo cha Chenge! Remember?
 
na hili litamalizika hivi hivi kama masihara. tutaambiwa alikuwa anatafuta kiti, na habari imeisha. tanzania hasa naipenda!
 
sasa yeye Chenge ameulizwa na waandishi kuhusu suala hili au ndio wote wanagwaya wakimdhani "kigagula"?

Mkjj, Nani ana ubavu wa kumsogelea 'Mzee wa vihirizi' ili amhoji? Ukimsogelea ili umhoji anaweza kukurushia vya kukurushia halafu ukapotea duniani...🙂
 
na hili litamalizika hivi hivi kama masihara. tutaambiwa alikuwa anatafuta kiti, na habari imeisha. tanzania hasa naipenda!
Aaah we unasubiri 'tuambiwe' wakati 'tushaambiwa' na habari ndiyo 'imeshazikwa'. Kilichobaki ni watu kuendelea na issues nyingine.

Proof haitatafutwa zaidi ya hiyo na nikwambie tu, hakuna utafiti zaidi ya huo!
 
Mnataka watu wote wawe Against Chenge?yaani kila mtu aamini Chenge mchawi?poleni kwa kukereka ila ukweli ndo huo!Chenge siyo mchawi!
Ukweli unauma!poleni sana
Asanteni
Hollo

Holo kaza buti ndugu yangu!!! my signature below should give you energy to continue telling us the truth!!! usiogope makelele ya watu ambao hata Tanzania hawajaiona kwa miaka 10 iliyopita!
 
Je sehemu anayokaa spika na naibu spika alifuata nini huko? Kama ni mbunge angetafuta kiti chake sehemu wanayokaa wabunge wa ccm na yeye siyo mgeni ndani ya jengo la bunge kiasi cha kutokujuwa wapiga ngojera wenzake wa ccm wanakaa wapi. Lazima kieleweke !!!
 
Wakati Munajadili haya mkumbuke... huyu mtuhumiwa ni mtanzania mwenzetu,,, mwenye haki ya kusikilizwa, kutendewa haki!!! sasa mambo tusioyajua tunapolazimisha as if tulikuwepo huko sio sawa hata kidogo!!!

Kuna wakati munastahili kuwa waumini wa dini kidogo!!! kwa kuwa mzee wa watu hana uwezo wa kuja hapa kwenye jukwaa!!! isiwe sababu ya kumpiga mawe kiasi hicho ebo???
 
Don't worry; hili nalo litapita in the next few days, tutaanza na lingine madamu madhira yote haya ya CCM tutayasahau!
 
Wakuu woote hongereni sana kwa mjadala huu wa kusisimua.

NB: Mtu wa Pwani naona umehama kabisa hata thread.

Mkuu,Tshala nashukuru sana kwa wewe kuwa Muungwana na kusema ukweli.Sasa Huyu Mtu wa Pwani atakoma kuropoka ovyo
 
Aaah we unasubiri 'tuambiwe' wakati 'tushaambiwa' na habari ndiyo 'imeshazikwa'. Kilichobaki ni watu kuendelea na issues nyingine.

Proof haitatafutwa zaidi ya hiyo na nikwambie tu, hakuna utafiti zaidi ya huo!

Ndio maana sasa ni wakati wa kujiandaa na mbinu mbadala ya kumuondolea Kikwete mbali kabisa ifikapo 2010.
Na hao wana CCM wanaojidai ni wazalendo...Huu ndio wakakti wa kubwaga manyanga na kuamua uamuzi mmoja...You are either with wazalendo or with FISADIS..Absolutely NO NEUTRAL GROUND na pia muanze kuwa makini la sivyo na nyie tutawajumuisha na Kikwete na Makamba,Mkapa,Mgonja,Chenge,Lowassa,Ballali,Mramba,Karamagi,RA,Nimrod Mkono na mafisadi wengine siku ya kiama cha ufedhuli wao itakapowadia...Ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno.
 
Kuna vijana wengi ama member wengi wapya tu wa kuwapa shukrani ambao bado tutaendelea kuwahitaji kwenye mijadala mingine..Kama kina Sikonge,Shapu,Tshala.Womenfosubtanc,Kokolo,Interested Observer,Mchukia Ufisadi,Jobo na wengineo wengi..Sasa kuna mjadalamwingine..Haya tuendelee sasa kujadili mkombozi wetu atakayemuondoa Kikwete madarakani na Taifa kuzaliwa upya.
 
Aaah we unasubiri 'tuambiwe' wakati 'tushaambiwa' na habari ndiyo 'imeshazikwa'. Kilichobaki ni watu kuendelea na issues nyingine.

Proof haitatafutwa zaidi ya hiyo na nikwambie tu, hakuna utafiti zaidi ya huo!

Tusionekane kuwa tumeshindwa hasa wana JF...mjue hii forum wakuu wengi wanaisoma na ndio wanachukulia kama opinion poll ya nchi...kwa hiyo tukianza kulegea tu wao ndio furaha yao....tusiwape mwanya.....ALUTA CONTINUA.

Naona umuhimu wa sasa nguvu zetu na nia yetu iwe ni kukitoa tu hiki chama cha mafisadi, ingawaje ni mwanangu na nilimwaminia sana kisura lakini kwangu mimi UTAIFA ndio mosi.
 
Bila kuwasahau..Yo Yo, Omutwale, Mambo, Kilizanzibar,Kwetu ni Kwetu, Mchelea Mwana, Kigoma,Nikifufuka mmekwisha...
 
WAKUU ONA MANENO YA MHE. SITTA YANAVYOJICHANG'ANYA, LEO KASEMA CAMERA ZA USALAMA ZILIKUWA ON SIYO OFF KAMA ALIVYOSEMA JANA.

Ndumba Bungeni: Wabunge wahofia viti vyao

2008-06-16 18:15:03
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Ikiwa leo ni siku ya kwanza kwa wabunge kuingia tena ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya kuwapo kwa uvumi wa kunyunyizwa vitu vinavyodhaniwa kuwa ni vya kichawi kwenye viti vyao, baadhi ya wabunge wameonekana leo asubuhi wakiwa bado wanahofia siti zao na hivyo kulazimika kuangalia na wengine kuvipangusa na leso zaidi ya mara moja kabla ya kuketi.

Tukio hilo la wabunge kudaiwa kuwekewa vitu vya kichawi kwenye siti zao, limedaiwa kutokea katikati ya wiki iliyopita na kuzua hofu kubwa, hivyo kuilazimu ofisi ya Bunge, kupitia kwa Kaimu Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilillah kutoa taarifa kuwa ukumbi uko shwari na hakuna tishio lolote la usalama kwa waheshimiwa wabunge.

Hata hivyo, licha ya kuhakikishiwa kuwa hakuna hofu yoyote bungeni humo, bado baadhi ya wabunge walionekana wakiwa na hofu na kuchunguza sana viti vyao kabla ya kukaa.

Hata hivyo, hofu ya wabunge hao waliokuwa bado wamejawa na hisia kuwa pengine wamefanyiwa kitu mbaya kwa kuwekewa vitu vya kudhuru, iliondolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Samwel Sitta, ambaye alitoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na sakata lenyewe kabla ya kuwataka wasiwe na hofu na badala yake waendelee na majukumu yao bungeni humo kama kawaida kwani ukumbi ni salama.

Akizungumza wakati wa kikao cha asubuhi ya leo, Spika Sitta amesema vyombo vya usalama, ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa, vimefanya uchunguzi ukumbini humo na kumhakikishia kuwa hauna hatari yoyote.

Akizungumzia sakata lenyewe, Spika Sitta akasema lilianza kwa kuonekana watu wawili wakitangatanga bungeni humo siku ya Jumanne iliyopita, mishale ya saa 2:00 usiku.

Akasema taarifa za kuwapo kwa tukio hilo, alizipata siku ya Alhamisi baada ya kuambiwa na Katibu wa Bunge kuwa kamera za usalama ndani ya ukumbi wa Bunge, zimenasa watu wawili wakitangatanga Bungeni.

Akasema picha hizo zikamuonyesha mtu mmoja kati yao akiwa na vitu mkononi ambavyo alikuwa akivinyunyiza sehemu mbalimbali.

Spika Sitta akasema siku hiyo baada ya kupewa taarifa wakati kikao cha Bunge kikiendelea, akatumiwa kimemo na Mbunge Victor Mwambalaswa, akimjulisha kuwa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa ameugua ghafla ndani ya ukumbi huo.

Akasema alipohusianisha matukio hayo, alihisi huwenda vitu vilivyoonekaka vikirushwa na mtu aliyenaswa na kamera za usalama ilikuwa ni sumu ya kisasa.

Akasema hapo ndipo akachukua hatua ya kulikabidhi suala hilo kwa Polisi na Usalama wa Taifa ili kulifanyia uchunguzi wa kina.

Akasema Jumamosi ya juzi, Polisi na maofisa wa Usalama wa Taifa walimpatia ripoti ya uchunguzi, wakimhakikishia kuwa ukumbi huo ni salama.

Akasema hata hivyo, suala la kuwabaini watu walionaswa na kamera wakitangatanga ndani ya ukumbi wa bunge, bado linaendelea kuchunguzwa na kuwa litachukua muda mrefu kidogo.

Akasema kuwa suala hilo linahitaji muda kwa vile uchunguzi wake unahitaji kurejea kwenye matukio ya nyuma kwa zaidi ya saa 72 ili kujua kilichotokea siku hiyo.

Baada ya ufafanuzi huo, Bunge liliendelea na kikao chake kama kawaida, ambapo mjadala kuhusu bajeti ulianza na hadi tukienda mitamboni, wabunge 56 walishajiorodhesha kwa ajili ya kuchangia mjadala huo.

* SOURCE: Alasiri
 
Wakati Munajadili haya mkumbuke... huyu mtuhumiwa ni mtanzania mwenzetu,,, mwenye haki ya kusikilizwa, kutendewa haki!!! sasa mambo tusioyajua tunapolazimisha as if tulikuwepo huko sio sawa hata kidogo!!!

Kuna wakati munastahili kuwa waumini wa dini kidogo!!! kwa kuwa mzee wa watu hana uwezo wa kuja hapa kwenye jukwaa!!! isiwe sababu ya kumpiga mawe kiasi hicho ebo???

Haki ya Mtanzania ilishapindwa doggy style...Na kubakwa. Haki hiyo sasa imekuwa ni...Victims..
Ni victims wa sexual harassment ya kifikra baada ya ubakwaji wa haki hiyo...Mjadala wa kina Chenge kuwekeana sumu si kitu...Wao waendelee na yao na siye tunaendelea na yetu..Kuna member mmoja alishaweka wazi hapa kuwa tutatobozana katikati.
Hao wana CCM wazalendo wameshaonyeshwa kuwa ni either wajiunge na wazalendo sasa ama wabakie humo humo CCM ambako sasa hata ofisi zake zinavamiwa na majambazi kwasababu wameshajua ndio kwenye pesa!
Msije mkapiga kelele mkawalaghai wananchi na huku mkiwa hamuwezi kufanya lolote kwasababu ya Mwenyekiti Kikwete na katibu wake Makamba wakisaidiana na mafisadi wengine!
 
Back
Top Bottom