Mh. Madam President ana haki kabisa kumchagua msaidizi wake. Ila alifanya kosa kwa kumchagua Dr P. Mpango. Sababu kuu ni kuwa ametoka wizara nyeti ya Fedha.
Wizara hii aliiongoza kwa miaka 5 na zaidi na ndio inayoongoza kwa kashfa za ubambikaji wa kodi, kushuka kwa thamani ya shilingi, wizi uliokithiri, unyang'anyi wa pesa za watu kwenye mabenki n.k. Ripoti ya CAG ilifichua baadhi ya madudu lakini ilibidi ifiche mambo mengi ili kumlinda Makamu wa Rais.
Kwa kuwa demokrasia ndio inaanza kurudi na sera za Madam President zinavutia wengi ndani na nje ya nchi ningemshauri Dr Mpango ajiuzulu ili CAG na wahusika wengineo wawe huru kutoa taarifa mbalimbali za ubadhirifu. Ukiyagusa madudu ya benki kuu tayari umemgusa Mh Vice President, hata ubadhirifu, uonevu uliokuwa unafanywa wazi wazi na wizara zingine moja kwa moja unamgusa VP.
Ili Madam President aendelee kuheshimika na mabilioni yaliyopotea hasa benki kuu itakuwa busara sana kwa VP kuresign, kulinda heshima yake.
Wapo watakaopinga lakini ndio demokrasia yenyewe.