Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amekutana na Rais Samia Ikulu ya Chamwino katika shughuli ya kupokea hundi ya msaada wa waathirika wa mafuriko ya Hanang ambayo mpaka sasa yamepelekea vifo vya watu 85.
Ukimya wa Dkt. Mpango takriban mwezi mmoja ulizua sintofahamu katika mitandao ya kijamii huku wengi wakidai ni mgonjwa anapatiwa matibabu nje ya nchi na wengine wakihitimisha kuwa hatuko naye duniani.
Kabla ya kukutana na Rais, Dkt Mpango alishiriki ibada ya misa Dodoma Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska, Jumapili leo Desemba 10, 2023. Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.
Akitoa hotuba fupi kanisani, Dkt. Mpango amesema kuwa alikuwa nje ya nchi mwezi mzima kwa kazi maalum. Amesema kuwa yeye ni mzima kabisa wa afya na hajapungua hata kidogo.
Ameendelea kusema kuwa yamesemwa mengi, na wengine bado wanasema mimi ni mzuka. Amesema kuwa mitandao ni mizuri ila baadhi ya watu wanaitumia visivyo. Inaumiza watu wengi . Wapo wengi ambao wameumizwa na maneno ambayo hayana msingi, kwa hiyo tujitahidi kutumia mitandao ipasavyo kwa kumuogopa Mungu.
Kwa hiyo wale waliokuwa wanatuma picha yangu na mshumaa pembeni, wengine wanasema mzee amekata moto, bado kabisa, kazi ambayo Mungu alinituma kufanya bado sijaimaliza.