Kumchagua Dkt. Mpango kuwa Makamu wa Rais ni kosa kwa kuwa kashfa nyingi zipo Wizara ya Fedha

Mars 12

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
221
349
Mh. Madam President ana haki kabisa kumchagua msaidizi wake. Ila alifanya kosa kwa kumchagua Dr P. Mpango. Sababu kuu ni kuwa ametoka wizara nyeti ya Fedha.

Wizara hii aliiongoza kwa miaka 5 na zaidi na ndio inayoongoza kwa kashfa za ubambikaji wa kodi, kushuka kwa thamani ya shilingi, wizi uliokithiri, unyang'anyi wa pesa za watu kwenye mabenki n.k. Ripoti ya CAG ilifichua baadhi ya madudu lakini ilibidi ifiche mambo mengi ili kumlinda Makamu wa Rais.

Kwa kuwa demokrasia ndio inaanza kurudi na sera za Madam President zinavutia wengi ndani na nje ya nchi ningemshauri Dr Mpango ajiuzulu ili CAG na wahusika wengineo wawe huru kutoa taarifa mbalimbali za ubadhirifu. Ukiyagusa madudu ya benki kuu tayari umemgusa Mh Vice President, hata ubadhirifu, uonevu uliokuwa unafanywa wazi wazi na wizara zingine moja kwa moja unamgusa VP.

Ili Madam President aendelee kuheshimika na mabilioni yaliyopotea hasa benki kuu itakuwa busara sana kwa VP kuresign, kulinda heshima yake.

Wapo watakaopinga lakini ndio demokrasia yenyewe.
 
Mnaomtia kiburi SSH, sijui mama anaupiga sijui upuuzi Gani ndo mnazidi kumchimbia kaburi.

Hivi unajua yeye ndio mwenye Mamlaka ya mwisho? Sisi tunamlaumu Mpango KWA kutomshauri Yeye SSH vizuri lakini yeye ndio mwenye maamuzi na haya yanayoendelea Yana haraka zake zote
 
Yani dr mpango pia anahusika na hii tozo mpya ya mitandao ya simu sio?
 
Vivyo hivyo yangetokea kwa Jk Bilal angekuwa nahodha mkuu
 
Mpango aliishi vizuri na rais na Makamu wake SSH. Ndiyo maana ameaminiwa,sasa kama kuna matumizi mabaya hiyo wizara aliyeongoza na ilikuwa ni maelekezo kutoka juu, kosa lake mr Mpango ni lipi? Unakumbuka hotuaba moja anasema mhe. Rais ulitunyoosha sana. Ina maana alikuwa jahazi moja na mhe.

Mpango, tena mpaka anasema tulikuwa tukipigiana simu, tunalalamika mbona mambo ya Rais wetu magumu. SSH na Mpango ni ndege wa manyoya ya aina moja kwa hiyo wataruka pamoja.

Siri za Baraza la mawaziri wanajua waliomo tu ,na hata ukitolewa mle kiapo kinakubana usizitoe . Katiba yetu Rais ndiye kila kitu wengine wote ni washauri tu na Rais halazimiki kupokea ushauri wa mtu yeyote. Huo ndio uelewa wangu mdogo
 
Obvious, maandalizi ya bajeti yalianza akiwa wizara hiyo
Acha hizo wewe zile bilioni walizojilipa kuanzia March hadi may mpango hakuwa waziri wa fedha wakasema kazi maalum ndo hii sasa mnayopokea saa hivi na bado
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom