Dkt. Mpango amtabiria mtoto kukalia kiti cha Makamu wa Rais

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amemtabiria mtoto wa kwanza kuzaliwa katika kituo cha afya Ketumbeine kuja kuwa Makamu wa Rais miaka ijayo.

Dkt. Mpango ametoa utabiri huo leo Februari 10, 2024 kwa mtoto aliyezaliwa na kupewa jina la Philipo baada ya msichana, Nengai Nairowa (17) kutembelewa na makamu huyo wa Rais katika wodi ya wajawazito wakati wa uzinduzi wa kituo cha afya Kitumbaine kilichoko wilaya ya Longido mkoani Arusha.

“Mtoto huyu ni bahati yangu na amepewa jina langu kwa sababu amezaliwa baada tu ya kumtembelea wodini na sasa Mtanzania huyu mpya aliyekuja na kilo 2.8 atakuja kuwa Makamu wa Rais wa nchi hii, yaani mrithi wangu nimempata mapema,” amesema Dk Mpango.

“Na nitaenda kumtembelea kumsalimia ili kumjua mrithi wangu baada ya hotuba hapa,” amesema.

Mpango ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa za kuzaliwa mtoto huyo, akiwa jukwaani akihutubia wananchi wa Longido baada ya uzinduzi wa kituo hicho cha afya Kitumbaine.

Katika hatua nyingine, Dk Mpango amewapongeza wananchi wa Longido kwa kutoa mifugo yao kuchangia zaidi ya Sh300 milioni katika kituo hicho kilichogharimu zaidi ya Sh1.32 bilioni, huku Serikali kuu ikitoka Sh800 milioni na Shirika la World Vision wakichangia Sh215 milioni.

Source - Mwananchi
 
Sijawahi kumuelewa huyu bwana Mipango.
Watu dizaini hii Mtikila alikuwa anawaita babu jinga. BTW badala ya ku-wish mtoto awe mwanasayansi mkubwa duniani yeye anawaza mambo ya vyeo tu. Anyways, Mpango simchukii kwani hana tifutifu kama wanasiasa wengine na pengine akipewa urais anaweza kufanya vizuri kwa sababu anaonekana kama hana tamaa.
 
Wanasiasa waongo nyie
Wanaweza kuwa waongo lakini sema tu tofauti ya umri itamfanya isiwezekane. Wanasiasa hutengenezwa. Ndio maana unaona watoto wa viongozi ni wabunge na wengine mawaziri. Ni kwa sababu wako karibu na wazazi wao, kubebwa hata baada ya wazazi wa kufariki n.k. Mpango kasema hayo akiwepo, lakini baadaye yanasahaulika.
 
Watu dizaini hii Mtikila alikuwa anawaita babu jinga. BTW badala ya ku-wish mtoto awe mwanasayansi mkubwa duniani yeye anawaza mambo ya vyeo tu. Anyways, Mpango simchukii kwani hana tifutifu kama wanasiasa wengine na pengine akipewa urais anaweza kufanya vizuri kwa sababu anaonekana kama hana tamaa.
Ukishamaliza Umakamu wa Rais hakuna tena Safari ya kuelekea Urais, nimekukumbusha tu
 
Pengine hujaelewa nilichoandika? Na pia hakuna sheria inayosema makamu hawezi kuwa rais...
Hujanielewa na hutokujakunielewa km hujanielewa hata hapo Ila ujue hivyo ndivyo ilivyo ukishamaliza umakamu Safari ya kuelekea urais haipo,
 
Kwaiyo mzeee ametangulia longido mapema sana ivo alaf na breaking news alitangaza akiwa huko huko longido ?
 
Angesema atamsomesha hafi chuo kikuu ....aje kuwa VP na kumsaidia sio kusema na kumuachoa hewani angewakabidhi JWTZ awe mtoto wa Srrikaki kama kweli ana nia...dhati wangemlea milele....
 
Back
Top Bottom