Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Mengi yatafuata. Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)

Hapo ndio penye uongo
 
km kweli chanzo cha kufeli huku kwa 60% kumesababishwa na sababu ulizo zianisha,Je shule za private pia zina uhaba wa walim??je zina maslahi duni kwa walim??je hazina maabara na vifaa vya kufundishia vya kutosha?je walim wa shule za private pia wana mgogoro na serikali???

Nimeuliza hivyo ni kwasababu tumeshuhudia pia anguko la kutisha kwenye shule za private ambapo miaka yote huishia divishen 3 lkn mwaka jana shule hizo zimetoa zero za kutosha!!...mfano Jitegemee sec wana ziro 410 hali ambayo haijawah kutokea tangu shule ianzishwe!

Nakushauri pia kapitie mitaala ya kufundishia pamoja na quality ya walimu tulionao hapa Tanzania, halafu rudi tujadili vizuri. Sababu ziko nyingi ila nilizotaja hapo ni kidogo sana. Ninachokikataa na kukiona cha kipuuzi zaidi ni suala la kusema wana-standardize matokeo, hapa wanafanya standardization kwa faida ya nani? Kujifariji kuwa waliofaulu ni wengi wakati ukweli unajulikana? Huoni kuwa kwa kufanya hivyo tuna haribu quality ya wasomi wajao?
 
Kama kweli wata standardize matokeo basi tutegemee baada ya miaka miwili ijayo kutakuwa na matokeo machafu ya form 6
 
ni bora PROF NA DR NDALICHAKO WALINDE HESHIMA YAO prof mukandala ni msomi mzuri ila ana tabia ya kuyumbishwa na wanasiasa na kama atalisimamia msimamo wake basi itakuwa ushindi ata kwa wanafunzi wa UDSM pia Dr JOYCE NDALICHAKO bingwa wa mathematics mwenye msimamo na asiyeyumbishwa ata kidogo anaweza akajiuzulu kama serikali itaendelea na msimamo wao cha msingi WAWE NA MSIMAMO MOJA ILA NAMWOFIA PROF ANAWEZA AKALEGEZA MSIMAMO.

Prof. Msomi tena mzuri?alafu anayumbishwa na wanasiasa?Sasa hapo maana ya usomi ni nini?Kweli watanzania huwa siwaelewi mnavyomtambua msomi!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hii model inaweza kujaribu kudescribe Tanzania.
real-life-vs-politics_jpg_550.jpg
 
Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Mengi yatafuata. Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)

Kama akifanya hivyo basi atakuwa amerudia kuwa Prof maana alishauvua muda sasa. Prof. Must be strong. Ready to die like CHACHAGE. Namuunga mkono mia kwa mia. Elimu si kitu cha kuingiza siasa.
 
You are unbelievably Stupid!! Yaani ili watoto "wenu" wasome unaona bora kuwadanganya wamepata C kumbe actually ni F!!! Bora waende wenye F wakijijua ili wakaze msuli, Stupid!

Habari za udaku hizi unaziweka hapa JF? kapeleke huko vijiweni kwa wala ugoro!

Suala la kuboresha matokeo haliwezi kupuuzwa katika kipindi hiki cha mpito.

Ni lazima matokeo yaboreshwe ili vijana wetu waweze kuendelea na masomo.

Lakini, katika kulitekeleza hilo, wanafunzi wanaopaswa kufaidika na mpango huu ni wale tu wenye div 4 ya point 26-28.

Kundi ili ni wale wenye walau alama C moja mpaka mbili, kwa hali kama hiyo matokeo yakiboreshwa, hawa wataweza kuendelea na masomo.

Lengo kuu la serikali katika ili sio zima moto, la hasha, ila katika kuendeleza juhudi za serikali kuboresha elimu, huu mpango utatumika mwaka huu tu ili kukabiliana na janga la wanafunzi kukosa shule kidato cha 5 na 6.

Kwa wale wote wapenda taifa lao na wanaojali maendeleo ya elimu, wataupa ECKO mpango huu wa serikali.
 
Anakataa kwa sheria ipi?

Sheria yetu (mbovu) ndio inayompa mamlaka waziri kutoa maagizo (hata ya kisiasa kwenye mambo ya taaluma) kwa baraza la mitihani na kwa mujibu wa sheria hiyo (s 20, Necta Act 1973) baraza linalazimika kutekeleza maagizo hayo!

Which minister specifically, or just any minister. The directive was from the PM and this guy doesn't deal with education (in its specificity).
 
Hivi huyu Lukuvi yeye alienda shule ya Ukweli au ni ngumbaru tu
 
Akiachia ngazi Ndalichako itakuwa sawa na Kuvuja kwa Pakacha. Huyu mama amelalamikiwa sana, hata kama ni mtendaji mzuri lakini lawama zikizidi ni bora kutafuta ustaarabu mwingine. Mbona elimu yake ni nzuri tu aachane na hiyo kazi ya NECTA ni kama imemshinda vile. Sifa ya kiongozi mzuri ni pamoja na ku_manage Public Relations

wanaomlalamikia ni wale ambao wanataka njia za mkato kwenye elimu. amewazibia hivyo lazima wamlaumu.
 
Katika hili la elimu, serikali imeona kichaka cha kujifichia ni kulitupia NECTA mzigo. Sasa kama wakina Ndali na Muka wanajiheshimu ni bora wakang'atuka na wakaweka mambo hadharani tofauti na hapo nao ni sehemu ya uchafu wa serikali wa kuangamiza kizazi cha taifa hili.
 
Kama ni kweli wanapaswa kusimamia jambo hili maana matokeo yalikuwa na baraka za serikali.
 
Hi ndo Tz watu na matukio

Wanajiandaa na 2015 kama walivyofanya free kuvuka kidato cha pili baadae walipomaliza uchaguzi wakarudisha, sishangai wakiyafuta

Hapo ni siasa kwanza elimu baadae.... alfu bila woga wanasaidi mikataba mingi tu ya East Africa Community
 
He is professional,hawez kukubali huu -----,coz kusahihishwa upya ni sawa sawa tu na kuwabeba!kuliko waitumie kipumbavu kodi yetu bora waamue tu waliopata zero na 4 wapewe 3 kama ndo wameamua huo -----!kiukweli somewhere someone messed up ndo mana haya yote yanatokea!the way forward ni wahusika wajulikane,wastep down,wawajibishwe!ila tukifanya mchezo ndo itakuwa hivi hivi!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Watanzania bwana ni wagumu kweli, kweli. Sidhai yaliyoandikwa hapa yanaweza kusimamiwa na mkandara. Lakini kama alihusika kutoa matokeo yale kama nilivyo yaona na serikali ikamuuliza na kuweza kupata majibu ambayo yeye hakuyatafuta, basi hana budi kuachia ngazi watu wenye uwezo wa kuyaona na kutoa majibu sahii wakachukua nafasi.
 
Back
Top Bottom