Kisbo imepitwa hapa mapema tu!

Kisbo imepitwa hapa mapema tu!

Kisbo ni hatari. Jana nilienda Dodoma na basi za kwanza kukutana nazo zilikuwa Kisbo ya mwanza na nyuma yake Kisbo ya Kahama. Nilikuja kukutana na basi zingine baada ya kilometa 10 which means distance between the buses ilishakua zaidi ya km 20 na hapo Kisbo ilikuwa imemaliza eneo la spidi 50 na zile zingine bado hazijaingia ambapo ina maana itabidi zipoze wakati mwenzao anakandamiza.
 
Mie nimepanda Kisesa gari lisilo na haraka ila naamini nitatoboa tu japo kama kisbo ipo inawezekana inapita Moro saizi maana sijawaona kabisa barabarani leo.

mtatoboa kweli!
 
Hiyo lugha ya kusanda ni kisukuma ? Ndio nini? Maana waswahili wa usiku mani wana vilugha vya hivyo hatari. Mfano kuniga ni kukaba
Kumbe kusanda ipo na kwenye lugha ya kisukuma?akhsante kwa kunijuza,sie moro tunaitumia tukimaanisha mtu 'kuweka mpira kwapani!'
 
Kisbo hiyo ni ndege ya chini, hailali njiani hiyo inatoboa Dar siku zote. Subiri utasikia utumbo wako unatembea humo
 
Kuna mambo ya kishirikina wanafanya gari haitapigwa tochi wala kusumbuliwa njia nzima...
 
Wote hatunufaiki na utawala huu kama wewe.

Hapo kwenye tax 30,000 weka 400 daladala ,chakula 30,000 weka 5000 , gesti 30,000 weka 10,000 .

Mwisho ndege tunaogopa viberiti vyetu vya moyo.

Acha waswahili tufurahie ligi ya mabus njiani ,ndo raha yake ya kututolea stress ,mtasema ajali hata ndege zinapata ajali au unaweza fika airport ukapanda tax yako na mkapata ajali vile vile .

Vipi route ya Dar to Mbeya bado Newforce wanakimbiza?
Newforce ya Tunduma ni hatari
 
baada ya singida hakuna aliyekatisha, wale waliotupita shy tulibambana singida walikuwa wanaenda arusha. nadhan huko mbele yetu kuna kidia one, katagi sijajua anaenda wapi make naye alipopita hajaonekana tena.
Hapo mlipobambana singida basi la Asante Rabi la kwenda Arusha halikuwepo kweli, manake nalo ni balaa
 
Nilishapanda Kisbo ya kutoka kahama mara kama Tatu hv, raha yake utaionea mkitoka Moro Chalinze aisee kama unaroho ndogo unaweza faint kabisa jamaa wanazichomoa hzo ikifika usiku balaa
 
Route ya dar arusha ndio imekua ya kibwege hakuna gari linalokimbia tena...

Daima tutazikumbuka

Buffalo
Ngorika macedonia
Chakito longway
Meridian express
Hujakutana na dar express (DFR) Dar-Nairobi... Moto wakuotea mbali
 
Back
Top Bottom