Kisbo ya Dar- Kahama mmetuchoka abiria wenu?

Kisbo ya Dar- Kahama mmetuchoka abiria wenu?

Mzee

Platinum Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
13,620
Reaction score
5,868
Habari za hapa WanaJukwaa.

Leo niko safarini toka Dat kwenda Kahama. Nilinunua tiketi ktk gari ya Kisbo...

#1. Kwa mujibu wa ratiba ilikuwa tuondoke saa 12 kamili..... Hadi saa moja bado hatuoni muelekeo wa safari.

#2. Baadae wakatuambia gari ni bovu.... Saa 2 hivi wakatuletea gari linaitwa Fahari..

>>Hili gari ni bovu kweli kweli.

>>Tumefika Mbezi nalo likaharibika... Ndio tumetoka hapa muda huu.

Angalizo:

1. Kisbo mnatakiwa kutumia akili mnapofaulisha abiria... Mnapaswa kuzingatia Muda pamoja na Ubora wa gari mnalofaulisha.

2. Kama nitafika salama hii ni safari yangu ya mwisho kupanda hizi gari...

Nitahamasisha yeyote ninayemjua aachane na hizi gari.

Sijui nitafika lini Kahama.

WanaJF wa Kahama naomba mnipokee

Mzee!
 
Duh Pole Sana, utafika Salama tu, sometimes kuna mambo yanatokea ili kutuepushia majanga! Au kuna Riziki utashushiwa hapo, Ukifika Kahama niko Ushirombo

Gari limezingua tena hapa Mlandizi..

Nimeamini kweli Biashara za Kibongo ni za hovyo hovyo sana.

Nimeacha Red Belt nikijua Kisbo wanaakili kumbe nao ni hovyo kabisa.
 
Kisbo ndege za ardhini

Kisbo wametuchoka abiri wao.

Leo walichotufanyia sio Uungwana kabisa..

Fahari hili litafika keshokutwa!
 
Habari za hapa WanaJukwaa.

Leo niko safarini toka Dat kwenda Kahama. Nilinunua tiketi ktk gari ya Kisbo...

#1. Kwa mujibu wa ratiba ilikuwa tuondoke saa 12 kamili..... Hadi saa moja bado hatuoni muelekeo wa safari.

#2. Baadae wakatuambia gari ni bovu.... Saa 2 hivi wakatuletea gari linaitwa Fahari..

>>Hili gari ni bovu kweli kweli.

>>Tumefika Mbezi nalo likaharibika... Ndio tumetoka hapa muda huu.

Angalizo:

1. Kisbo mnatakiwa kutumia akili mnapofaulisha abiria... Mnapaswa kuzingatia Muda pamoja na Ubora wa gari mnalofaulisha.

2. Kama nitafika salama hii ni safari yangu ya mwisho kupanda hizi gari...

Nitahamasisha yeyote ninayemjua aachane na hizi gari.

Sijui nitafika lini Kahama.

WanaJF wa Kahama naomba mnipokee

Mzee!
Panda kitu SHABIBY LINE, utaunganisha na basi lingine vituo vya mbele.
 
Acha kupiga kelele kabla hujafika. Usiwe mshamba wa safari. Shit happens. Huwezi jui labda mungu anakuepusha na janga kubwa zaidi. ALWAYS STAY POSITIVE.
 
Kisbo ndege za ardhini
Hamna kitu, gari la kutoka mwanza kuja dar mara kadhaa naliona saa saba mchana ndio linaingia dar na lilitoka mwanza jana. Mashine Osaka ile scania ya 'double diff'.
 
Kisbo wametuchoka abiri wao.

Leo walichotufanyia sio Uungwana kabisa..

Fahari hili litafika keshokutwa!
Tupia Picha tulione hilo fahari
Dai nauli yako kimya kimya
 
hzo safar huwa zinachukiza,japokuwa kuna wakat huwa kuna mpango wa mungu au shetan pia,so better to pray
 
Inaumaga sana, tatizo watanzania wengi hawajielewi maan unaweza kukazana peke yako kupigania haki zako wao wanakuangalia tu kama misanamu. Pole sana mkuu, Muombe Mungu utafika salama
 
Inaumaga sana, tatizo watanzania wengi hawajielewi maan unaweza kukazana peke yako kupigania haki zako wao wanakuangalia tu kama misanamu. Pole sana mkuu, Muombe Mungu utafika salama

Ndio maana Tanzania tunaogopa soko la Afrika Mashariki.

Biashara za Tanzania zinaendeshwa Kisanii sanii...

Hawa Kisbo wangekuwa wanajielewa wasingetupandisha ktk gari hivyo namna hii...
 
Back
Top Bottom