Kisbo imepitwa hapa mapema tu!

Kisbo imepitwa hapa mapema tu!

khaa! kuna gari inaitwa katagi nayo imetupita hapa hatujafika hata missungwi
Katagi inaenda zake mbeya.Ila jua mnyama kisbo atakuwa mbele tu. Alafu utatupa mrejesho. Kwa mbeya katagi ndo wao
 
Nauli kutoka Mwanza hadi dar Kwa basi ni elfu 60, Chakula njiani 20, tax kufika standi 10, ( masaa 14hrs road) ukishuka ubungo either ulale gest 30000 au uchukue tax elf 30, kama kuna ndugu Wa kukupokea (hasara na usumbufu Wa kukufuata stand tumpe naye elf 30) haya uchofu Wa safari utakupasa upumzike ambapo hasara ya kulala siku nzima inayofuata elf 30 n.k let's say imekucost laki mbili kupanda bus,
Ungefanya mipango ya FASTJET 150000 /= AU Ungefanya mpango Wa precision Air 360000/= Ungefika chap na Kwa haraka ukaendeleza majukumu yako ya kuingiza Pesa nyingine ;
Mi ninafikiri siku nyingine panda ndege kupunguza gharama ( Note; gharama zingine hazionekani direct)
SAFARI ZA BUS MASAFA MALEFU IFIKE MAHALI TUACHANE NAZO zimepitwa na wakati ( Tutumie bus safar fupi fupi)
==========================
NI SAWA NA KUNUNUA KIWANJA KWENYE KILIMA AU BONDENI 2MIL HALAFU MSINGI WA NYUMBA IKAKUCOST 15MIL pamoja risk za Maji na bomoabomoa! Wakati kuna viwanja flat saafi vinauzwa 8mil na mzingi only 3mil na ni sehemu salama
Kwa hyo wenye mabasi wayaapaki au
 
Huu ndio uzi wa wiki, kifurushi kimekata namwagiza dogo kwa Mangi fastaaa! Sexer kama huna bando niambie dogo alete na vocha yako kabisa maana hii mida no kuchimba dawa no kununua vocha!

mkuu ni full data, network maeneo mengine inakata
 
Umenikumbusha ligi ya Tawaqal na Kiswele enzi hizo Dar to Songea, huku kuna giriki kule yuko Yogi palikuwa hapatoshi!
We tunaendana umri.Miaka ya 1992 mpaka 95 wamasai wa Ruvu walikuwa wanaulizana "Kiswele napita?" Haya toa ng'ombe.

Maana Kiswele iliwahi gonga ng'ombe 10 halafu ikatambaa.

Those days bus zilikuwa na bull bars.Na kulikuwa hakuna camera.

Basi zilikuwa zinakimbia balaa.
 
Jamani nilishauriwa humuhumu JF ili nifike Dar kutoka Mwanza kwa siku moja nipande basi la Kisbo, wanaJF wakasisitiza hakuna basi linalokimbia kama Kisbo, nami kweli nikakata tiketi ya hilo basi.

Sasa ajabu leo tumetoka Nyegezi stand tumevuka tu Buhongwa Kisbo ikapitwa basi fulani linaitwa Master, sasa nimeanza kupata wasiwasi kama kweli nitafika leo manake uongo umeanza kudhihirika.
Kama mkipata ajali msilalamikie mwendo kasi ilhali mnaupenda kwa kiwango hiki. Pokeeni maumivu na mateso yake kwa namna hii hii mpendayo mwendokasi.

The Quill.
 
Back
Top Bottom