Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Insurgent ninapenda theory zako,, unasema Mallya alimhamisha Wangwe, wakati mzee anasema yeye ndiye aliyemfungua Wangwe akiwa amefunga mkanda, sasa hapa nani anasema ukweli kati ya wewe na huyu mzee?

Halafu mkuu unafikiri hii ajali imesababishwa na nini mvua, jua kali, upepo, au ni kawaida tu? Halafu hebu rudia tena la mtaalamu, kwa sababu familia ilimleta justi in time kabla ya mazishi, maana tumeona kesi maiti imekwenda kufukuliwa sasa hapa wala haijazikwa tatizo lilikuwa ni nini mkuu?

nitarudi baadaye mkuu with more! lakini so far I like this! yaani utetezi wako kwa serikali na Mallya.

Mimi sio mtetezi wa serikali wala Mallya naangalia kote.

- Kama mzee alimfungua mkanda akiwa kiti cha abiria then Mallya alikuwa anaendesha.

- Kama mzee alimfungua mkanda akiwa kiti cha dereva then inawezekana Mallya alimwamishia pale baada ya ajali kwani alikuwa mgonjwa na asingeweza kuendesha.

Kama ni ya kwanza, alilaza kiti hivyo kuuzuia mkanda kufanya kazi yake ipasavyo.

Mkuu FMES mimi kutoa hii theory hakumaanishi naitetea serikali hii ni theory bado hatujui ukweli.
 
Mkuu Insurgent,

Kwanza karibu tena baada ya kupotea sana,

1. Sasa back to the ishu mzee aliyekuwa wa kwanza kwenye ajali anasema alimfungua mkanda marehemu Wangwe, wewe unasema hakufunga vipi hiyo nayo imekaaje mkuu?

2. Mtu mwingine aliyekuwemo kwenye gari, kwanza ulisema alitoboa baada tu ya ajali, sasa unasema ilikuwa ni theory tu?

3. Mallya alikuwa anamuendesha marehemu akiwa nyuma, sio mbele tena? hii nayo vipi ilikuwa ni theory tu au?

4. Mallya akaishia kutoka akiwa mzima salimini kwa sababu tu alifunga mkanda? Hivi umeyaona mazishi ya usoni mwake hapo anapopelekwa Hospitali?

5. Serikali haikutaka mtaalamu wa kuangalia maiti anayekubalika na Familia ya marehemu, lakini ikaridhika na mtaalamu aliyefanya hiyo kazi, unafikiri ni kwa nini?

6. Serikali iliyotuambia kuwa Balali amefia Boston, wakati ukweli sasa uko wazi kuwa alifia DC, sasa wewe na Mtanzania, mnataka tuiamini serikali kuwa this time inasema ukweli?

Wakuu naomba kusema hivi, kuna watu kama mimi binafsi, siamini tena kwa 100%, kuwa hii ajali ya Wangwe ilikuwa ni ajali ya kawaida au mkono wa Mungu, ninarudia tena kwua siamini, na ninaahidi kwua nitautafuta ukweli mpaka niupate na nintauweka hapa hapa JF, kwa wale wanaohusika naomba mjitokeze mapema, maana when the time comes asije akalia mtu hapa! Siwezi kuahidi time lakini ninaahidi kuiwa nita-get ot the bottom of this na ukweli nitauweka hapa wazi!

Mimi ninarudia tena kua siamini kabisaa, kama ni kuvunja sheria kutoamini kwangu so be it!

Mkuu FMES,

Najua wewe ni katika watu wenye uzoefu na magari na unaendesha masafa marefu. Kwenye gari kuna mambo chungu nzima yanayoweza kusababisha ajali.

Lengo hapa ni kuelemishana kwa hoja na kukubaliana, wakati mwingine kukubali kutokukubaliana. Hakuna ambaye theory yake ni msahafu juu ya hili. Anayejua ukweli kamili ni Mallya na mungu wake.

Binafsi simlaumu mtu akiamini tofauti na mimi na nitaheshimu huo msimamo wake.

Tatizo linakuja pale watu wanapoacha kujadili hoja iliyombele yetu na wanakimbilia kumtwanga risasi messenger.
 
Haya Maneno yako Mkuu,"Tutayakumbuka".Wala haihitaji Intelligenjia kubwa kujua kwamba kuna mchezo mchafu unachezwa hapa..Mallya amekwishafikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na atakwenda huko (Mahakamani) tena 24/08.Katika siku yake ya mwanzo Mallya ameshitakiwa kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendo kasi bila kuwa na Leseni..Angalia kosa hilo Waungwana,Huyu Mallya alitakiwa kushtakiwa kwa kutoa maelezo ya Uongo kwa vyombo vya Dola,Lakini pia amesababisha kifo cha Mbunge,na kama hiyo haitoshi pia alikutwa na Kitambulisho kisichokuwa chake...Mbona haya hayasemwi? Mara tuanaambiwa kuwa Mallya ni mfanyabiashara Jijini Dar.Ni biashara gani anazofanya huyu Muungwana?

Wale wenye Kumbumbuku kumbukeni kesi ya Mohammed Enterprises ya kuingiza chakula kibovu...Ilirushwa rushwa na tukaanza kusikia kifo cha Mkemia Mkuu wa serikali na baadaye Jaji naye alifariki..Ile kesi iliishia wapi?Sasa hali ile itatokea kwenye kesi hii ya Mallya,kwa sababu kama ilivyokuwa kwenye kesi ya Mohammed Enterprises ninaamini kuna makubwa nyuma ya pazia kuliko haya tunayoyaona...

Na aliyehusika na hiki chakula kibovu hivi sasa ni mbunge wa CCM , kweki ama si kweli....
 
Uchunguzi wa kina unahitajika. niliposikia kifo cha wangwe na kwamba kijana huyu amenusurika, nikajua lazima kuna mkono wa mtu. suala la ajali ni la kawaida, na hakuna mtu anayeweza kukwepa, hata kama dereva hana leseni. hizo ni traffick case ambazo zimejaa kila mahali. iweje yeye adai kwamba hajawahi kuendesha gari tangu avunjike mkono wakati akijifunza jijini nairobi 2004 wakati mtoto wa marehemu anashuhudia kwamba ndiye aliyekuwa akiendesha muda wote na akamuonya kwa mwendo kasi? alikuwa anajaribu kuficha nini? na iweje achomoe memory card ya simu yake na kuitupa? ilikuwa na nini? nadhani vyombo vya usalama vijaribu kutrace kwenye mitandao yote ya simu mawasiliano yote yaliyofanywa kwa simu za marehemu na huyo mallya. assumption sometimes leads to truth. alikutwa na vitambulisho vya ajabu ajabu, akakutwa na bastola, ndivyo tunavyoambiwa, ichunguzwe hiyo bastola pia ilikuwa ya nani au kama anaimiliki kihalali, kama ni kweli alikutwa nayo. kauli zake nazo zichunguzwe kwa makini, kwamba alikuwa nyuma, amelala, amesikia kishindo akajua magurudumu yamepasuka, alijuaye na alikuwa amelala hata kama amezinduka usingizini? anasema alipoteza fahamu, lakini anasema yeye ndiye aliyesaidia kuchukua simu za marehemu na pesa, na ndiye aliyepiga simu kwa spika, inawezekanaje kama alikuwa amepoteza fahamu? huyu jamaa kama ni jasusi, basi ni yule anayejifunza, maana hajui hata kudanganya.

Good analysis and questions, THE QUESTION IS IF Govnmt. did it then they will say nothing.Kindly we have to think of independent agencies as other arleady suggested,say Scotland yard.To cook any believable story or repot regarding this matter is very easy.

Waberoya
 
View attachment 1930

Angalieni mkono wa kushoto wa Malya na ulizeni Maswali...

Mzee Mwkjj..., 'Deus Francis Mallya' anaonekana ameshikilia funguo, 'simu ya mkononi' na bahasha/karatasi nyeupe ilokunjwa...

au unazungumzia hao jamaa kushoto kwake?
 
Kukimbizwa kwenye mazishi ni jambo la kawaida hasa mtu husika anaposhukiwa
Shinyanga na mwanza wakikushukia huwa wanaenda wanakukamata wanaenda KUKUTEMYA yani wanakuchukua maili kadhaa polini na kukuulia mbali ndege na wanyama wanafanya kitoeo wala ndugu zako hawataona sehemu wala kabuli lako.

Wakikukosa ama ukatoroka kijiji huwa wanakuwinda na kuvamia nyumba na kukatakata mapanga.
Yote haya hufanyika bila ya MEDIA wala chombo chochote cha habari kuwaandaa wananchi hawa ,wala hua hawafanyi hivyo kwa makusudi ya siasa.

Mkama,
Ni kweli unayosema. Ila mwisho wa siku huwa hakuna mtu anasema kuwa NI MKAMA huyu kamuuwa marehemu au kaagiza watu wauwe. Kibaya hapa ni pale mtu anaposema ni CCM au CHADEMA ndiyo wameuwa. Naona wewe muda wote unataka watu waseme NI CHADEMA. Mie hadi sasa sielewi na naona huu mjadala kweli umekosa mwelekeo. Ntasubiri. FMES ukipata habari kamali baada ya uchunguzi, please anzisha thread mpya maana hizi zimekuwa ndefu sana. Heri niangalie CHUCK NORRIS.
 
hivi kweli mnategemea hata kama kuna kitu kibaya kimefanyika, au kuna watu nyuma ya kifo hicho hivi kweli mnaamini kuna chombo kinachoweza kuchunguza kwa uhuru? Subirini iundwe Kamati Ya Jaji Mkuu kuchunguza jambo hili!
 
lazima mtambue mantiki ya uhusika wa ROSTAM hapa sio tu kuwageuzia kibao WASEMA MAFISADI bali pia kuhakikisha kuwa ifikapo 2010 kina MWAKYEMBE na wenziwe wapatao 70 ndani ya bunge hawana upenyo wa kutokea CCM wakihsalimwa vichwa kama ilivyokuwa kwa wakina KITINE 2005. Wanaamini kuwa endapo hakutakuwa na chama mbadala cha kukimbilia wakati huo ambao utakuwa mchache kwa kuanzisha chama kipya na kujijenga basi ni wazi "USHUJAA" wao utakwisha na kelele dhidi ya UFISADI itapungua kama sio kwisha kabisa....

Kwa mimi niliyekuwepo TARIME kuanzia mwili ulipoingia hadi siku ya kuzikwa nashukuru wengi wenu hapa jinsi mnavyochemsha kwani mnaniwezesha kujielimisha mambo mengi ikiwemo hili suala la kujenga imani kwa misingi ya hisia zilizokosa chembe ya ujuvi......

Tanzanianjema
 
Kwangu mimi mwanakijiji hana haki yoyote ya kutafuta uthibitisho... kwa kuwa hao anawasema kila siku mafisadi hana uthibitisho wa namna yoyote... hili analisemea tu kwa kuwa ana maslahi binafsi ndani yake...

Kuna mambo mengi tu ambayo mwanakijiji ameyatunga akiwa marekani akalazimisha watu kuamini hapa...

Mnanichanganya wakuu, kumbe kuna uongo humu ndani?? Kasheshe naomba habari moja tu ya kutunga aliyowahi kutoa humu ndani ya JF ndani hutaniona tena humu ndani ya JF please, narudia sema habari ya kuzushi aliyowahi kuitoa MMKJJ.USIPITOA utakuwa unaconfirm kinyume chake kuwa wewe ndio mzushi.

NASUBIRI JIBU NA NINAKUANDIKIA KWENYE PM YAKO PIA

WABEROYA.
 
Halisi,

Mwanasiasa ukiogopa kifo kwenye kutetea ukweli, hutakiwi kuwa mwanasiasa.

Wewe utasema Bhutto yuko wapi? Huenda yale aliyokuwa anayaamini yanatekelezeka zaidi baada ya kufa kuliko alivyokuwa hai.

Huoni Nyerere amakuwa mungu mtu kwa TZ baada ya kufa?

Pia kama hakukuwa na umuhimu wa yeye kuwepo Tarime, kwanini akatishe ziara yake yote mpaka akafike Tarime? Naona hapo kuna kujichanganya kidogo.

Naona sasa lawama zimeanza kuhamia TLP/NCCR? Si walisema wanaungana na kuweka mgombea mmoja?

Tanzania kuna mafisi ya siasa, yakiona mnofu, yale makubaliano ya kufaidi nyama pamoja yanapotea na kila mtu anataka ashibe peke yake.

Hili ni lipicha lile lile tulilolizoea ila wachezaji ndio wamebadilika, ubinafsi badala ya maslahi ya taifa.

sasa mabodyguard wa nini kwa wanasiasa?
 
View attachment 1930



Mzee Mwkjj..., 'Deus Francis Mallya' anaonekana ameshikilia funguo, 'simu ya mkononi' na bahasha/karatasi nyeupe ilokunjwa...

au unazungumzia hao jamaa kushoto kwake?

Mkono wa Mallya wa Kushoto ambako kama marehemu alikuwa amekaa kiti cha abiria cha mbele wakati ajali inatokea(kwa mujibu wa Mzee George) angechafuka kutokana na Damu za Marehemu. Nilitegemea mkono wa kushoto kuwa na Damu zaidi.
 
lazima mtambue mantiki ya uhusika wa ROSTAM hapa sio tu kuwageuzia kibao WASEMA MAFISADI bali pia kuhakikisha kuwa ifikapo 2010 kina MWAKYEMBE na wenziwe wapatao 70 ndani ya bunge hawana upenyo wa kutokea CCM wakihsalimwa vichwa kama ilivyokuwa kwa wakina KITINE 2005. Wanaamini kuwa endapo hakutakuwa na chama mbadala cha kukimbilia wakati huo ambao utakuwa mchache kwa kuanzisha chama kipya na kujijenga basi ni wazi "USHUJAA" wao utakwisha na kelele dhidi ya UFISADI itapungua kama sio kwisha kabisa....

Kwa mimi niliyekuwepo TARIME kuanzia mwili ulipoingia hadi siku ya kuzikwa nashukuru wengi wenu hapa jinsi mnavyochemsha kwani mnaniwezesha kujielimisha mambo mengi ikiwemo hili suala la kujenga imani kwa misingi ya hisia zilizokosa chembe ya ujuvi......

Tanzanianjema
 
Mkama,
Ni kweli unayosema. Ila mwisho wa siku huwa hakuna mtu anasema kuwa NI MKAMA huyu kamuuwa marehemu au kaagiza watu wauwe. Kibaya hapa ni pale mtu anaposema ni CCM au CHADEMA ndiyo wameuwa. Naona wewe muda wote unataka watu waseme NI CHADEMA. Mie hadi sasa sielewi na naona huu mjadala kweli umekosa mwelekeo. Ntasubiri. FMES ukipata habari kamali baada ya uchunguzi, please anzisha thread mpya maana hizi zimekuwa ndefu sana. Heri niangalie CHUCK NORRIS.

Mimi sisemi kama Chacha kauliwa na chadema ,Ila ajali ndio imemuua kama wataalamu wetu walivyothibitisha,Mimi nilisema kama Chacha angekua hakufa kwa ajali basi maeneo yote shukiwa yangelichunguzwa na kuanzia na CHADEMA ,CCM then RA.

Mimi nachosema hapa Kutolewa Bunduki ktk misiba wakikushuku ni jambo la kawaida wala hakuna mkono wa mtu ,Hayo magazeti siku zote ndio staili yao ya kuandika ili wauze wale wako ktk biashara.

Kanda ya ziwa hasa shinyanga na mwanza bibi aki apear ktk msiba ametoka kupuliza moto wa magunzi ya mahindi amechapa chafya nyingi na macho makundu pia akaongeza ugolo wake puani na macho yakakolea kua mekundu ,kijana mmoja tu akianzisha yawezekana ni haka ka bibi angalia kalivyo na macho mekundu hakachelewi hako kabibi kukatwa mapanga.SEBUSE mtu ambaye walikua wanakwaluzana harafu mda mfupi jamaa akafa??

Jamaa kama alitolewa bunduki akubali tu wala hakuna cha RA wala CCM ila ni wenyewe ndiyo waliona iwe hivyo.
Kutolewa Bunduki haina maana jamaa alihusika.VIBIBI shinyanga 100% hua havina hatia ila ni kwasababu miaka 70 yote vimekua vikupuriza moto ambao kuni zake ni magunzi ya mahandi nakuvipelekea kua na macho mekundu.

Kwani navyo hua hua ni njama ya kuharibu chama cha siasa?
 
View attachment 1930



Mzee Mwkjj..., 'Deus Francis Mallya' anaonekana ameshikilia funguo, 'simu ya mkononi' na bahasha/karatasi nyeupe ilokunjwa...

au unazungumzia hao jamaa kushoto kwake?

Ndiyo hiyo au angalia na hapa:


Malya.JPG.jpg


Angalie hizo picha mbili na hivyo alivyovishika na anza kuunda maswali.
 
Ni muhim kwa Matukio au Ajali au Vifo vya Utata vifanyie Uchunguzi...Tuwe na Hii culture.

1. Vyama 3 vya Upinzani kutoa matamshi yao hayo si ya kupuuzwa, na kama wamekosea, basi wakaliwe Kooni kama Yanga Sports walivyofanya, mtu akimtuhumu mtu, basi Taasisi Husika zifanye uchunguzi ili Haki iweze kupatikana. Mfano kama uchunguzi utafanyika ikaonekana sio, basi vyama 3 vya Upinzani vitahitajika kuwaomba radhi Jamii ya watanzania kwa kuropoka kwao, na kama kweli, basi ita strenghen security iliyopo. LISIWE JAMBO JEPESI LA MTU KUKAA KIJIWENI AU KTK PRESS THEN AKAMTUHUMU MWINGINE, UTAKUWA MCHEZO MCHAFU.

2. Ni kweli Tunatakiwa tuamini kuwa kila Jambo limepangwa na M/Mungu. Kifo ni mojawapo. lkn kufanya uchunguzi ktk vifo pia ni muhim. Kwani sheria za M/Mungu mtu alie uwa nae auwawe au Ndugu wa Marehemu wamsamehe. pia ikitokea ajali wakati unamuendesha Baba Mzazi, unaweza usirithi mali.,....itakavyokuwa Uchunguzi ni kitu muhim kufanyika, ili isiwe jambo jepesi mtu kusababisha Ajali, basi za wengine zikashindikana kupatikana.

3. Sijui kwanini Chadema hawakuwa ktk Jopo la vyama vya Upinzani, inawezekana for good, lkn kwa Wapinzani wao itaonekana wao kuwa wapo Kinyume

4. Kwanini Vyama vya Upinzani, vikaongea na aliekuwa Mke wa Wangwe, hapa JF yaliletwa madai kuwa Wangwe yupo mbali na mkewe, na wapo waliodiriki kusema kuwa kuna sintofahamu, sijui hili tunaweza kulijadili vp

5. CCM wao kama Wapinzani wa Chadema, kitendo cha wao kutoweka Msisitizo juu ya Uchunguzi Huru, unatia Mashaka!!!!
 
Hiyo picha moja kwa moja inaonyesha kuwa Kijana Deus alikuwa Dereva No doubt..........kwa jinsi nilivyoliona lile gari most likely mtu aliyekuwa anaendesha anaweza kupona............well............tuendelee kutoa tafsiri zetu............
 
Je hili gari lilipoacha njia lilibingirita?

Kwa mtizamo wangu, kama lingebiringita roof ingebondeka kuelekea ndani, (mfano wa chapati), hebu itazame picha ya gari tena, utaona paa limetuna kama kawaida, halafu tazama upande mmoja wa gari, haukuumia kama upande mwingine, lingebiringita lazima na upande mwingine ungeumia kwa kiwango kikubwa , sasa je liligonga gari jingine ubavuni wakati linataka kuovertake?,au liligongwa na gari jingine ubavuni kisha gari hilo likatokomea?.

kama tunavyoona katika picha ya hiyo gari, je dereva alikwishaona ajali haikwepeki na ili kuokoa roho yake akaamua kuligongesha gari upande wa abiria?(si ndivyo madereva wengi walivyo? ,akiona ajali analengesha kwa abiria?)
 
Je hili gari lilipoacha njia lilibingirita?

Malya.JPG.jpg


Angalie hizo picha mbili na hivyo alivyovishika na anza kuunda maswali.

...kunusurika katika ajali mbaya kama ile na kuweza kukumbuka wapi simu na 'nyaraka muhimu' kunaweza zua utata mwingi,

...'mwonekano' na inavyodaiwa, gari lilibiringika mara tano, japo Mallya mwenyewe anasema alisikia kishindo tu na vumbi!

...Mkuu wewe umeona nini, 'when a picture is worth a thousand words'?.
 
Je ina maana Kijana Mallya.........alifundishwa kijitoa mhanga?......maana ajali kama ile hata iwe umekaa vipi.........na hat akama tuseme alitumwa ili kuua ........basi na yeye alikuwa tayari kufa.....kwani hata kwake lolote lingeweza kutokea.

Kitakachomfunga Deus ni kudanganya (ofcourse na kuendesha bila ya kuwa na leseni) kuwa hakuwa anaendesha wakti anajua fika kuwa alikuwa anaendesha......kwani mazingira yote yanaonyesha hivyo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom