Kitila,
Msimamo wangu mimi ni kuwatumia wabunge kuendesha mambo ya CHADEMA. Kuwapa ukurugenzi watu ambao wako nje ya bunge nafikiri ni makosa labda kwa vyama ambavyo havina wabunge wa kutosha.
Kwenye hili wangeanza na Dr. Slaa toka mwanzoni, au Zitto na mpaka mwisho.
Ukisoma kule kwenye ile thread nyingi ya Mnyika akutana na Bille na Rostam, utaelewa nina maana gani.
Hivi Mnyika alitumwa na chama hata kutuma sms kwa RA? Inabidi chama au kampuni kuwe na protocol ya aina fulani hivi inavyokuja kwenye mawasiliano na mtu/vyombo vya nje ya chama/shirika.
Swali lingine ninalojiuliza, kwanini Mbowe alikubali ushauri wa polisi kwamba asihudhurie mazishi ya Wangwe? Ile ilikuwa sio amri, ulikuwa ushauri, kama hakukuwa na hatari kabisa hata kwake, kwanini akubaliane na ushauri wa namna hiyo? Tumeona mara chungu nzima wanasiasa wakikataa ushauri kuhusu maisha yao kuwa hatarini, wengine wanakubali wengine wanakataa. Hata Bhutto alishauriwa asirudi Pakistan shauri ya usalama wake, lakini akaenda na kufa. Mbowe angweza kwenda kwenye mazishi na kumaliza kilimilimi cha waliosema kafukuzwa. Lakini pia angeweza kwenda na kufukuzwa na ingelikuwa mbaya zaidi kwake.
Mtanzania una point, lakini kumbuka hata katika uandishi wa habari, wanasema, "hakuna story yenye thamani ya maisha yako" na katika siasa, hakuna siasa yenye thamani ya maisha ya kiongozi, na umejijibu kwa Bhutto kukataa ushauri na kufa, sasa siasa atazifanyia kaburini na hakuna alichofanikisha kwa maana ya malengo ya kuwakomboa aliowakusudia kuwakomboa. Kwa Mbowe ina maana zaidi kwani siasa za Tanzania haziko Tarime pekee na hata za Tarime haziko katika msiba pekee na katika msiba si lazima Mbowe pekee anayeweza kufanya siasa kwa niaba ya Chadema. Alikuwapo Zitto hadi ktika posmoterm na wapo viongozi wa wilaya na mkoa ambao wanaendelea na kampeni. TLP na NCCR Mageuzi walifika na kumrubuni kaka yake Wangwe ajiunge nao agombee ubunge, lakini hakuna dalili na sasa siasa zinapamba moto huko Tarime, bila ya kuwapo Mbowe
Mkuu, nadhani ungejitahidi kuwa unafuatilia mambo. Hakuna makosa kwani Msemaji wa Chadema ni Katibu Mkuu wa chama hicho kwa maana ya taasisi ya UKATIBU MKUU kutoka ofisi za chama hicho zilizopo Dar es Salaam na si kokote na si Dk. Slaa, Zitto, Mnyika au yeyote. Kwa mantiki hiyo kama utakumbuka wakati wote Dk. Slaa akiwa Dodoma ama nje ya Dar es Salaam, kunakua na msemaji ama Zitto, Mnyika, Antony Komu, Erasto Tumbo au yeyote seniour aliyeko ofisi za Dar es Salaam. Chama hicho hakijalishi umri wala umaarufu wa mtu na kwa mara ya mwisho, Mnyika ndiye aliyeandika barua kwenda kwa IGP na ndiye aliyekwenda TBC kutoa taarifa, sasa hapa sioni jambo la kushangaza. CCM pia kuna wakati wanafanya hivyo kwa wakati nakumbuka Makamba akiwa hayupo alikua akizungumza aliyekua Naibu Katibu Mkuu, Kapteni Jaka MWambi (Amekuwa balozi) na wakati mwingine KAtibu Mwenezi na kuna wakati hata Salum Msabaha Mbaruku na hivi karibuni tumemsikia Tambwe Hiza
Gari la Wangwe limepindukia kwenye eneo maarufu kwa kilimo cha karanga, huwezi lima karanga kwenye ardhi yenye miamba ya mawe chini ambayo inatakiwa kuwepo kwenye ardhi ili gari la Wangwe liumie kama lilivyoumia, au?
Halisi,
Mwanasiasa ukiogopa kifo kwenye kutetea ukweli, hutakiwi kuwa mwanasiasa.
Mallya na mtu mwingine (aliyetoka baruti baada ya ajali) walikuwa mbele na wengi wa mbele hufunga mikanda.
Huyu Mallya hana hata vumbi!....
Kwamba wewe unataka kuwaambia watu kuwa Mbowe hakuwa kwenye wakati mgumu, na wala hakuondolewa pale akisindikizwa na askali. Mimi nilikuwepo jana na hivi niko Mwanza yaliyoandikwa ni kweli ndivyo ilivyo kuwa na kama hamuamini muone kama siku ya mazishi Mbowe atakuwepo. Halafu kuhusu habari kufanana hiyo siyo ajabu inategemeana na chanzo cha habari