CCM na siasa za marehemu

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Asalaam za siku nyingi wana JF.

Nilipotea kwa muda mrefu humu jamvini hii ni kutokana na shughuli za ujenzi wa taifa.

Leo napenda kuzungumzia kwa kifupi kuhusu mwenendo wa siasa zetu za hapa bongo. Hatua tuliyofikia kisiasa ni mbaya sana hatuna tofauti na wanyama, tunafanya siasa za uhasama, siasa za kulipiza kisasi, siasa za kudharau utu wetu wenyewe, imefikia hatua ya kuwatumia marehemu waliotangulia mbele za haki.

Ukweli ulio wazi, baadhi ya ndugu zetu wa CCM wamejivua utu hawawaheshimu ndugu zao waliotangulia kana kwamba wao hawaelekei huko. Juzi nilimsikia kada mmoja wa chama kipya cha ACT kupitia Star TV akisema, "ana uhakika Chacha Wangwe RIP aliuawa na Chadema", nikajiuliza polisi wako wapi na yeye alikuwa wapi kupeleka ushahidi huo mahakamani wakati wa kesi hadi kupelekea Deusi Mallya kufungwa kwa zaidi ya miaka mitatu. Leo tena nimesikia Antony Diallo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza anataka kumtumia Mallya huyo huyo aliyefungwa kwa kesi ile ile kuendelea kumtumia marehemu Wangwe.

Hizi siasa za kutumia marehemu zimetoka wapi? nani mwanzilishi wake? na zinatupeleka wapi.

Naomba kuwaasa wana CCM wanapoanza kufukua makaburi wasije kujilaumu hapo baadaye wakati makaburi ya ndugu zao yatapoanza kufufuliwa.

Niwakumbushe tu kama CCM wako tayari kutuambia nani alisababisha kifo cha Kolimba, nani alimuua Sokoine, kina nani wako nyuma ya kifo cha Imran Kombe. Kwani Karume Sr. aliuawa na nani? Tukiachilia mbali vifo vyenye utata kama vya (RIP) Malima, Prof Shaba, Dr. Mvungi, Prof. Harub Othman, Prof. Chachage, na wengine wengi, CCM wanaweza kututhibitishia baba wa taifa alikufa tarehe ngapi? Ni maswali mengi ya kujiuliza lakini ukiangalia kwa undani hayana msingi wowote. Tuache kutonesha vidonda.

CCM kama chama au mtu yeyote anayefanya siasa za marehemu aache mara moja kuwatumia marehemu ndugu zetu wapendwa kwenye siasa zao chafu. Kama kuna mtu anapenda sana kutumia marehemu basi awatumie wazazi wake au ndugu zake waliotangulia mbele ya haki. Inasikitisha.

Naomba kuwasilisha.

Katibu Mkuu wa CCM Imrani Kombe aliuliwa na Polisi kwa kupigwa risasi,miezi michache baada ya kusema CCM imepoteza Dira!!

Kumekuwepo na propaganda za kipumb@vu sana kwenye media ya kiongozi wa CCM kutumia makada waliofukuzwa CHADEMA kutumiwa na CCM inayoendesha serikali kusambaza tuhuma za mauaji ya kisiasa!!

Wachunguzi na wafuatiliaji wa kisiasa wanajua kuwa kila awamu ya CCM iliyokaa madarakani ilifanya mauaji ya mtu mmoja mmoja na hata kwa makundi ya watu!!!

Awamu iliyopo madarakani haiwezi kujinasua na mauaji,rejea kupelekwa kwa jeshi mkoani Mtwara na kufanyika uvunjifu wa haki kwa kutumia silaha za moto,ulipuaji wa mabomu kwenye mikutano ya kisiasa na sasa kwenye nyumba za Ibada,Mauaji ya Mwangosi,watesaji wa Kibanda na Mwangosi,kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda,kupigwa na kukamatwa viongozi wa uamsho ambao kimsingi wanapinga serikali 2 na sasa wameshughulikiwa na ugaidi,"ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya"!!

Awamu ya Mkapa ilikubuhu zaidi kwa mauaji hadi kufikia hatua ya kuzalisha wakimbizi,rejea mauaji ya Zanzibar 2001,rejea mauaji ya Mwembe Chai ndani ya msikiti na nje,rejea ufukiwaji wa wachimbaji wadogo wadogo kwenye migodi kisa kupisha makaburu kutekeleza sera ya uwekezaji na ubinafsishaji,kutangazwa CUF ni Chama cha Kigaidi na IGP Omary Mahita kuratibu makontena fake ya visu na majambia ya CUF ambapo hadi sasa vinauzwa!!

CCM na vibaraka wake waache kuhatarisha amani kwa kufanya propaganda za kishenzi,

RockSpider 01:11 Today

Diallo, Mchange, Deus Malya et al wanazidi kujidhalilisha! Autopsy iliyofanyika chini ya Prof. Wangwe ilikuwaje? Kwanini Prof. Wangwe na Baadhi ya Ndugu waliwekwa sawa na CCM? Ilikuwaje Makamba Sr akakutwa na Laptop ya Marehemu 15 baada ya ajali? Ilikuwaje Sitta aliipoteza hoja ya Marehemu kuhusiana na Mgodi wa North Mara? Kwanini Sitta alichanganyikiwa sana baada ya ajali? huku akiihusisha na ile hoja yake binafsi kuhusiana na mgodi wa North Mara?

Yule Witness aliekuwepo pale Pandambili yuko wapi sasa hivi? Mkanganyiko kuwa Marehemu alikuwa anaendesha, Mara Malya ndo alikuwa anaendesha ilitatuliwa vipi? Ilikuwaje Marehemu alikuwa kwenye kiti cha nyuma? Ilikuwaje Malya akatoka clean kama bwana harusi kwenye ajali kubwa kama ile? ... Kwanini tusiamini ile theory kuwa Marehemu aliuawa mapema na alisafirishwa hadi eneo la tukio, wakaweka natisha accelerator gari likawa katika mwendokasi na kusababisha ajali ionekane halisi!!! Kuthibitisha hilo; tayari laptop ya Marehemu alikwisha kabidhiwa Katibu Mkuu wa CCM Makamba Sr!!! ...

CCM na wajinga wajinga wengine wote wajue kuwa wanatonesha vidonda vingi sana, watambue kuwa ndugu na Jamaa zetu waliowaua tunajua! Uvumilivu wetu usichukuliwe kama sisi ni Mbumbu sana hatujui kilicho wakumba akina Sokoine, Imran Kombe, Karume, Malima, Kolimba, Nyerere, Mwangosi, Mbwambo, Prof Shaba, Prof. Chachage, Prof. Harub Othman, Dr. Mvungi et al ... RIP Wapendwa wetu... Kibanda na Dr. Ulimboka ni mashuhuda wazuri sana: Mshaurini Diallo awape airtime kama kweli ana mbupuma aka balls ...
 
Magamba wana spin ili watengeneze katiba ya chama chao
Hata kama ni spinning watafute mbinu nyingine kama ile ya kikombe cha babu lakini si kwa kuwatumia marehemu, wawaache marehemu wapumzike kwa amani.
 
Hizi ni siasa za maji taka sana hazifai kwa jamii iliyostaarabika.
 
Napenda mtu kama huyu anatoa mada na vielelezo sio propaganda za watu wakunuliwa
We unaamini ugoro huo?
Prof Chachage na Prof H Othman died of natural cause, Prof Shaba yuko Marekani kwa mwanawe.
Tatizo you people can be led by the nose to believe anything.
 
Imrani Kombe alikuwa Katibu Mkuu wa CCM?! Alikufaje??!! Waliomuua wako wapi??!!

Serikali ilishitakiwa na kuamriwa kulipa fidia ya 500mln,kwa nini??!!

Id yako inafahamika kwa kutetea ushenzi unaoharibu ustawi wa jamii na Taifa,nitajadiliana na wewe ukijibu hoja kwa mtiririko!!
 
CCM inacheza na siasa za mauaji ikidhani inakikomoa Chadema lakini mwisho wa siasa hizi ni wao kusaga meno.

Chuki kama hizi za kupotosha na kupandikiza ndio chanzo cha mauaji ya halaiki kama sio vita!!

CCM wenyewe haswa na watoto wao hawaendi publicly kueneza upotofu huu kwa kuwa wapo kwenye gorofa la vioo hawawezi kurusha mawe,wanawanunua maskini wenzetu wenye umalaya wa kisiasa na mamluki kadhaa kufanya kazi hii ya kishenzi kwa malipo ya shekeli,rejea madiwani wa CHADEMA walionunuliwa na CCM Shinyanga na kina Masele,Mwigulu & co kwa uratibu wa Mchange wakarudi CHADEMA baada ya kupewa pesa bandia
 
Imrani Kombe alikuwa Katibu Mkuu wa CCM?! Alikufaje??!! Waliomuua wako wapi??!!

Serikali ilishitakiwa na kuamriwa kulipa fidia ya 500mln,kwa nini??!!

Id yako inafahamika kwa kutetea ushenzi unaoharibu ustawi wa jamii na Taifa,nitajadiliana na wewe ukijibu hoja kwa mtiririko!!
Kama ni suala la kuua au kuuwawa mbona linatoka mbali.
Unamfahamu Mwamwindi?
Naye aliua!!
Ushenzi mkubwa zaidi ni kufikiri wote wanaouwawa ni kwa sababu za kisiasa.
Kwa taarifa yako Prof Chachage namfahamu vizuri sana pengine toka wakati wewe unatoka kamasi.

Ukikubali kurubuniwa na kurubunika ni kama mwanamke aliyejirahisi, the rest ni uroda tu.
 
Hakuna unachojibu zaidi ya nyatu nyatu,kama ufahamu wako mkubwa ndio huu tangu nikiwa mdogo basi sina cha kukusaidia kwani kuna misamiati mingi inayoakisi watu na matukio,kubwa jinga ukiwemo!!

The last bars I think ni meseji kwa Mchange anayechangwa kama karata na kuwekwa mezani watu wacheze,bahati mbaya sio kisu wala kopa,ni garasa la mavi!!!
 
Kama ni suala la kuua au kuuwawa mbona linatoka mbali.
Unamfahamu Mwamwindi?
Naye aliua!!
Ushenzi mkubwa zaidi ni kufikiri wote wanaouwawa ni kwa sababu za kisiasa.
Kwa taarifa yako Prof Chachage namfahamu vizuri sana pengine toka wakati wewe unatoka kamasi.

Ukikubali kurubuniwa na kurubunika ni kama mwanamke aliyejirahisi, the rest ni uroda tu.
Kama wewe si mfuatiliaji wa mambo ya siasa unaweza kuona hivyo vifo ni vya kawaida.

CCM regime si chama cha kwanza kuua mahasimu wake hasa inapoona maslahi yake au ya watawala yako hatarini, kama unakumbuka hata Robert Ouko alifanywa hivyo hivyo na serikali ya Kenya.
 
Mwandishi umenikumbusha uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki baada ya Mkapa kumwaga mboga ndipo Vicent Nyerere akamwaga ugali na kumfanya Mkapa na CCM yake kukaa kimya. Hii ni baada ya Mkapa kupanda jukwaani na kuwaambia wana Arumeru kuwa Vicent sio mtoto wala mwanafamilia wa Nyerere, kuona hivyo Vicent akaamua kufunguka na kutoa siri kwa kusema "Mwambieni Mkapa awaambie ukweli nani na nini kilimuua baba wa Taifa" na kuivua nguo serikali kabla mama Maria Nyerere kuingilia saga hili. Sasa safari hii wamekuja na Mchange, na uhakika CCM mtaumbuka zaidi ya Arumeru.
 
Katibu Mkuu wa CCM Imrani Kombe aliuliwa na Polisi kwa kupigwa risasi,miezi michache baada ya kusema CCM imepoteza Dira!!

...

No thank you! Big No! Ukweli hauna budi kusemwa kama ulivyo.

Hapo kwenye red: haijawahi kutokea!
Hapo kwenye underline: ni kweli
Hapo kwenye green: hayo maneno hayakuwahi kutamkwa na anayetajwa kwenye red!

Therefore, logically, F AND T AND F = F; maelezo yako yote yamekuwa uwongo hivyo yamepoteza maana.
 
Mwandishi umenikumbusha uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki baada ya Mkapa kumwaga mboga ndipo Vicent Nyerere akamwaga ugali na kumfanya Mkapa na CCM yake kukaa kimya. Hii ni baada ya Mkapa kupanda jukwaani na kuwaambia wana Arumeru kuwa Vicent sio mtoto wala mwanafamilia wa Nyerere, kuona hivyo Vicent akaamua kufunguka na kutoa siri kwa kusema "Mwambieni Mkapa awaambie ukweli nani na nini kilimuua baba wa Taifa" na kuivua nguo serikali kabla mama Maria Nyerere kuingilia saga hili. Sasa safari hii wamekuja na Mchange, na uhakika CCM mtaumbuka zaidi ya Arumeru.
Ni kweli mkuu nakumbuka wakati ule Mkapa alilianzisha Vincent akamalizia wakabaki kulialia,

ndiyo maana nimewaambia wanapoanza kufukua makaburi ya wenzao wasilalamike makaburi ya wapenzi wao yatakapoanza kufukuliwa.
 
Back
Top Bottom