Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Hayo yalikuwa makosa ya kiuandishi tu...Lakini ni wazi kuwa Mhariri wa Gazeti hilo atakuja front kutoa masahihisho ya habari hiyo.
 
nyerere aliwahi kuiita dsm kuwa rumorville, kwamba tunapenda mno uvumi, tutakapogundua kuwa tumepoteza muda mwingi kujadili kifo cha kawaida cha mbunge chacha wangwe, mafisadi watakuwa wameshakomba hazina yote kwa ajili ya kujipanga kwa uchaguzi wa 2010
 
kwanini hadi leo Chadema haijaitisha uchunguzi huru kama wa Scotland Yard na badala yake wameng'ang'ania kuwataka Polisi wafanye kazi hiyo wakati kimsingi ingekuwa na Polisi wenyewe wahojiwe na mtu aliye huru? Nani alitoa habari kwa Polisi kwanza; Polisi gani walifika pale mapema? n.k

Katika hili Polisi wetu wangekaa pembeni.

No wonder kuna wanaoamini kuwa watu wanaoishi sana nje ya nchi ni hatari kwa usalama wa nchi yetu. Huu ung'ang'anizi wa SCOTLAND YARD unachefua. Kesho utadai serikali ya Uingereza kusaidia kutuongoza. Badala ya kufocus na jinsi ya kuboresha vyombo vyetu tunadhani solution ni hao majasusi wa nje.....Wakiwadharau mnakuja juu....

Tanzanianjema
 
it looks like a rat, it smells like a rat, lakini naambiwa no no no sio panya huyo ni nguchiro.....i'm confused,,,,,what kind of coincidence is this???
 
Insurgent,

Nakubaliana na theory yako. Naamini Mallya alikuwa anaendesha gari na Wangwe alikuwa kiti cha nyuma na most likely hakufunga mkanda. Atakuwa alichoka na kuamua kujipumzisha.
Kuumia alikoumia ni dalili ya mtu ambaye hakufunga mkanda. Ukifunga mkanda ni ngumu sana kupasuka kichwa labda ugonge mwamba au mti.

Duniani kote, wanaosababisha ajali husingizia waliokufa. Siamini kwamba kulikuwa na mtu wa tatu.


Mtanzania, huyu ni Malya akiingia hospitali baada tu ya ajali

Malya.JPG.jpg


Gari lilipopelekwa Gereji:


KIFO cha Mbunge wa Tarime Chacha Wangwe, kimezidi kugubikwa na giza nene baada ya fundi magari katika gereji iliyoko eneo la Sido mjini hapa kusema kwamba, mtu anayedaiwa kuwa dereva wa gari iliyopata ajali na kuumua mbunge huyo, Deus Mallya, ndiye aliyeendesha gari la marehemu hadi gereji kabla ya safari siku ya ajali.

Maelezo hayo ya fundi huyo Israel Remen, ambayo yanashabihiana na ya watoto wa marehemu, yanapingana na kauli ya Mallya ambaye alikuwa katika gari moja na marehemu Wangwe, lakini (Mallya) anadai kwamba hajui kuendesha gari.

Akizungumza na gazeti hili katika gereji hiyo iliyopo karibu na ofisi za Shirika la Sido, Remen alisema, awali marehemu alipita na Mallya na kusema gari lingerudishwa na rafiki yake huyo kutengenezwa.

Alizidi kusimulia kwamba, baadaye Mallya alilifikisha gari hilo gereji hapo akiwa analiendesha na likafanyiwa matengenezo mbalimbali Remen alitaja matengenezo hayo kuwa ni pamoja na kumwaga mafuta machafu (oil) na matengenezo mengine madogodogo. (Gari lilipelekwa hapo mara mbili; ya kwanza na Malya, na ya pili angalia hapa chini).


Hata hivyo, alisema baadaye mnamo saa 12.00, Mallya alirudi tena safari hiyo akiwa na marehemu na kutakiwa kukaza sukrubu za tairi la kulia la nyuma.

"Alivyokuja, alikuwa na mheshimiwa (marehemu) ambaye alikaa kiti cha mbele akiwa amekilaza, mimi nikamwambia mheshimiwa usipate tabu kushuka kaa hapo hapo, basi nikakaza kisha wakaondoka Mallya akiwa anaendesha," alisisitiza.

Fundi huyo alipoulizwa kwamba aliwahi kumwona Mallya akimwendesha marehemu kabla, alijibu: "Si mara moja, nilimwona sana, hapa mjini ndiye alikuwa akimwendesha, hata siku chache zilizopita niliwakuta mjini na wakanipungia mkono."

Kwa mujibu wa Remen, tayari yeye amehojiwa na polisi na alipelekwa hospitali mkoani hapa kwa ajili ya kumtambua Mallya, na kuongeza kwamba alithibitishia polisi kwamba ndiye aliyefika na gari hiyo akiwa anaendesha.
"Nashangaa anaposema hajui kuendesha gari, alikuja hapa na gari akiwa ndiye anaendesha, na si mara ya kwanza, hata mjini alikuwa akimwendesha mheshimiwa," alifichua siri.

Kauli hii ya fundi gereji huyo inazidi kuibua mjadala na utata kuhusu mazingira ya kifo cha Wangwe ambaye alikufa Jumatatu usiku, eneo la Pandambili, Wilayani Kongwa akiwa safarini kwenda Dar es Salaam kuwahi mazishi ya mbunge wa kwanza wa Tarime, Bhoke Munanka.

My Take:

Pale lilipoletwa gari mara ya kwanza na Malya peke yake ni muhimu kweli kujua ni matengenezo gani yalifanyika na kwanini suala la kukaza screws za tairi la nyuma hakukufanywa wakati huo hadi baadaye na yeyote aneyejua magari anajua wazi kuwa kukaza sukurubu za tairi unless hauna zile spana huitaji kwenda gereji.

Ina maana tangia mwanzo wa safari Wangwe alikuwa amejilaza chali... drugged? Kwa sababu ningependa kujua huyo fundi alipomwambia Mheshimiwa kaa tuu hapo hapo, Wangwe alionesha ishara ya kujibu au kuitika?
 
NInachoshangaa ni jinsi ambavyo hakuna mmoja wao kati ya akana Mrema, Lipumba na Mbata na waandishi wa habari aliyeelezea jinsi ambavyo mabango yalikuwa yanaelezea kuwa kifo cha Wangwe kimetokana na jinsi anavyoshupalia Ufisadi. Jadilini pia mabango yaliyoandikwa WIZI WA MADINI umekufikishia mauti mpambanaji wetu.

Mbona hakukuwa na bango lolote dhidi ya Mbowe na CHADEMA. Sasa mnataka tutoke kwenye real picture ambayo ninyi media wenyewe mlituletea (including TBC1)

I so doubt the force behind this discussions. MAFISADI again facilitating this.
 
And then Mallya akatoka akiwa mzima salimini..... na huyo mtu mwingine......., isipokuwa Wangwe tu,

ulikuwa umeanza maneno yako vizuri sana mpaka ulipofikia hapa tu mkuu!

Again mtu wa tatu ilikuwa theory, lakini naamimini kama, Marehemu Wangwe alikuwa anaumwa na akaamua kulala nyuma basi hakufunga mkanda. Suala la Wangwe kuumwa liko confirmed na mtoto wake.

Just for the record...recall ajali ya rally kule Zanzibar. Mtoto wa Bakhressa alipasuka kichwa (mind you alivaa helmet na gari ilikuwa na rolling cage) na navigator alitoka bila scratch...Je huyu navigator alitumwa kumuua? Tufungue thread ya kuuliza "Mtoto wa Bakhressa aliuawa?"

Another record, mmoja kati ya mabodyguard wa Mbowe alikuwa askari wa TPDF na ni well trained...sasa huyu naye ni jasusi? CHADEMA kina watu wengi ambao wamewahi kuwa part of system either directly or indirectly...

Samahani siwezi kulog mara nyingi hapa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu.

Adios!
 
Mkuu Insurgent,

Kwanza karibu tena baada ya kupotea sana,

1. Sasa back to the ishu mzee aliyekuwa wa kwanza kwenye ajali anasema alimfungua mkanda marehemu Wangwe, wewe unasema hakufunga vipi hiyo nayo imekaaje mkuu?

2. Mtu mwingine aliyekuwemo kwenye gari, kwanza ulisema alitoboa baada tu ya ajali, sasa unasema ilikuwa ni theory tu?

3. Mallya alikuwa anamuendesha marehemu akiwa nyuma, sio mbele tena? hii nayo vipi ilikuwa ni theory tu au?

4. Mallya akaishia kutoka akiwa mzima salimini kwa sababu tu alifunga mkanda? Hivi umeyaona mazishi ya usoni mwake hapo anapopelekwa Hospitali?

5. Serikali haikutaka mtaalamu wa kuangalia maiti anayekubalika na Familia ya marehemu, lakini ikaridhika na mtaalamu aliyefanya hiyo kazi, unafikiri ni kwa nini?

6. Serikali iliyotuambia kuwa Balali amefia Boston, wakati ukweli sasa uko wazi kuwa alifia DC, sasa wewe na Mtanzania, mnataka tuiamini serikali kuwa this time inasema ukweli?

Wakuu naomba kusema hivi, kuna watu kama mimi binafsi, siamini tena kwa 100%, kuwa hii ajali ya Wangwe ilikuwa ni ajali ya kawaida au mkono wa Mungu, ninarudia tena kwua siamini, na ninaahidi kwua nitautafuta ukweli mpaka niupate na nintauweka hapa hapa JF, kwa wale wanaohusika naomba mjitokeze mapema, maana when the time comes asije akalia mtu hapa! Siwezi kuahidi time lakini ninaahidi kuiwa nita-get ot the bottom of this na ukweli nitauweka hapa wazi!

Mimi ninarudia tena kua siamini kabisaa, kama ni kuvunja sheria kutoamini kwangu so be it!
 
My Take:

Pale lilipoletwa gari mara ya kwanza na Malya peke yake ni muhimu kweli kujua ni matengenezo gani yalifanyika na kwanini suala la kukaza screws za tairi la nyuma hakukufanywa wakati huo hadi baadaye na yeyote aneyejua magari anajua wazi kuwa kukaza sukurubu za tairi unless hauna zile spana huitaji kwenda gereji.

Ina maana tangia mwanzo wa safari Wangwe alikuwa amejilaza chali... drugged? Kwa sababu ningependa kujua huyo fundi alipomwambia Mheshimiwa kaa tuu hapo hapo, Wangwe alionesha ishara ya kujibu au kuitika?

Nakubaliana nawe asilimia 100 hapo juu kuhusu matengenezo yaliyofanyika wakati huo Mallya akiwa pekee na mafundi....Ni muhimu sana kupata ukweli wa hilo. Sio hivyo tu, ni muhimu kujua mara ya pili waliondoka hapo hotelini exactly muda gani na kuunganisha muda wa ajali ilipotokea na umbali wa walipoanzia safari na sehemu ya ajali....Hii itasaidi kujua kama kuna muda ulitokea kwa mengine tofauti na kuendeshwa kwa gari yalitokea njiani....

Wanaohoji kuwa iweje Mallya atoke na maumivu machache hivi hawajaona kuwa upande wa dereva wa lile gari haukuwa umeumia sana kama sehemu zingine. Hivi inahitaji nini kung'amua kuwa kama Mallya alifunga mkanda kuna uwezekano wa yeye kutoumia sana tofauti na alikuwa amekaa nyumba na kuwa na uwezekano wa kuwa alikuwa amejilaza bila kufunga mkanda ama amejifunga mkanda lakini amelaza kiti hivyo mknda kuwa loose zaidi ya itakiwavyo?

Hili la ku-drugged nadhani ni jitihada za kulazimisha hoja/hisia zako kuwa kuna assasination ilifanyika. Sababu hata mtoto wake Zakayo alitoa ushuhuda kuhusu hali aliyondoka nayo Baba yake pale nyumbani....hata maji ya dawa yalikuwa ya kunyweshwa....Na si kuna uthibitisho wa hospital kuwa Marehemu alikuwa anaumwa Malaria?

Tanzanianjema
 
Mimi naomba tuwe wabunifu kidogo na tuone kama tunaweza kujibu maswali muhimu kadhaa:

1. Kama kuna mkono wa mtu kwenye hiki kifo, kwa nini Mhe. Chacha Wangwe ?
2. Je kama kingetokea kwa kiongozi mwingine kwenye upinzani na hasa CHADEMA, tungetarajia nini ?
3. Kwa nini ilitokea kwa muda uliotokea ?
4. Watu ambao wanapata ahueni kutokana na tukio hili ni akina nani na wana nyadhifa zipi ?
5. Baada ya tukio hili tutarajie hali itakuwaje mbele ya safari ?

Majibu kwa mengine ni rahisi na wazi na kwa mengine kuna utata kidogo. Mimi mag3, majibu yangu ni haya - (kumbuka mimi ni binadamu)

1. Kwa kuangalia mazingira ya tukio hakuna kiongozi yeyote mwingine aliyetoa opportunity kwa aliyetaka kuchafua hali ya hewa nchini kama Mhe. Wangwe. Matamshi na matendo yake yalitoa nafasi nzuri kwa huyo mtu(watu) kufanikisha lengo lake la kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Kifo cha Mhe. Wangwe kimedhoofisha upinzani kwa kiwango fulani lakini kwa kiongozi yeyote mwingine, kingeupa nguvu upinzani.
2. Muda ulikuwa muafaka hasa baada yeye kufanya maamuzi ama kwa kushinikizwa ama kwa kuwa compromised na hivyo akajisahau. Kumbuka kama angeweza kutoa mada yake bungeni, hangeweza kuondoka usiku ule na mpaka sasa hatujui word for word alilotaka kulisema. Ni nani angependa anyamaze milele ?
3. Watu wa kwanza kushukiwa na kwa sababu tofauti kabisa hawakuwa nchini -RA na Mbowe - na wote kwa sababu tofauti ilibidi wavunje safari zao na kurudi. Mimi nasema huenda kuendelea kuwashuku wao peke yao ni mbinu za kupoteza lengo. Wanaopata ahueni kutokana na tukio ni muhimu sana na tusiliangalie hili jambo kwa juu juu. Ni watu tunaoweza kuwatambua vizuri kwa vile walivyoweza kushupalia hili tukio na kuanza kuleta hisia za ajabu ajabu kama ya risasi kichwani. Vibaraka walitia kambi Tarime kwa nia ya kuhakikisha habari zinapotoshwa.
4. Chadema hivi sasa hawana mbunge Tarime na inabidi wafanye kazi ya ziada kukanusha kuhusika kwao wakati EPA, Richmond, Dowans etc zitakaa pembeni na MAFISADI watazidi kupeta. Hakuna jimbo ambalo wananchi wake wameamka na kuelewa kinachotendeka nchini na walioonja machungu ya UFISADI kuliko Tarime na hivyo kuwa target yao - kumbuka Kigoma na Kabourou.
5. Upinzani uliogawanyika utakimbilia kugombania Tarime na CCM na vyombo vyake vya dola na habari vitahamia Tarime. MAFISADI watatumia hii nafasi kuchonganisha wananchi kwa lengo la kuliteka tena jimbo la Tarime na huu utakuwa mwanzo wa wapinzani kukata tamaa. Kuna watakaopatwa na woga na kusema bora yaishe na kansa yao itaenea kwa kasi na mwishowe kitadumu Chama Cha Mafisadi.

Wazalendo tumeonywa na mwenye masikio na asikie. Forewarned is forearmed. Je tutaruhusu? A luta continua.....
 
LYatoga /Lipumba wamedata,JK fisadi,Mbatia mzushi,Vyombo vyote vya habari bomu

Ni Mbowe tu ndio safi na gazati lake la Tanzania daima.Interesting sana

Hizi picha nzuri sana kwa kumkoma nyani giladi.Ila nitazijadili hizi picha nitakapomuona Mbowe naye anakunywa maji ka Lyatoga,Mimi simjui Mbowe naomba mnielekeze ktk picha kuanzia moja ama mbili ni wangapi kutoka kulia ama kushuto.
 
Unajua this forum siku zote ina vichwa na tuna mazumbukuku pia, Mkuu Triplets kula tano mwanangu, ujumbe wako hapo juu ni saafi sana!
 
No wonder kuna wanaoamini kuwa watu wanaoishi sana nje ya nchi ni hatari kwa usalama wa nchi yetu. Huu ung'ang'anizi wa SCOTLAND YARD unachefua. Kesho utadai serikali ya Uingereza kusaidia kutuongoza. Badala ya kufocus na jinsi ya kuboresha vyombo vyetu tunadhani solution ni hao majasusi wa nje.....Wakiwadharau mnakuja juu....

Tanzanianjema

umesoma hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi Julai?
 
Mkuu Insurgent,

Kwanza karibu tena baada ya kupotea sana,

ASANTE SANA MKUU!

1. Sasa back to the ishu mzee aliyekuwa wa kwanza kwenye ajali anasema alimfungua mkanda marehemu Wangwe, wewe unasema hakufunga vipi hiyo nayo imekaaje mkuu?


2. Mtu mwingine aliyekuwemo kwenye gari, kwanza ulisema alitoboa baada tu ya ajali, sasa unasema ilikuwa ni theory tu?

Najibu 1 and 2 hapa:

- Kuhusu namba 1, kama Mallya alikuwa hana leseni na alijua amesababisha kifo, inawezekana kabisa alijaribu kumweka Wangwe mbele baada ya ajali ili aepuke kifungo. Sheria yetu ya traffic ilibadilishwa ili kutoa adhabu kali kwa madereva wazembe. Kwa sasa ukisababisha kifo katika ajali kifungo ni miaka miwili, hakuna FINE.

- Ni kweli nilitoa theory ya kwamba kama Wangwe alikuwa nyuma then inawezekana kulikuwa na mtu wa tatu. Baadaye nilitoa counter argument ya mtu wa tatu based on his sickness. Na sasa nakuuliza, tuseme alikuwa mbele na alifunga mkanda. Kama alilaza kiti mkanda ungemsaidia?!


3. Mallya alikuwa anamuendesha marehemu akiwa nyuma, sio mbele tena? hii nayo vipi ilikuwa ni theory tu au?

- Hakuna sehemu nimesema Mallya alikuwa nyuma, stick to my theory.

4. Mallya akaishia kutoka akiwa mzima salimini kwa sababu tu alifunga mkanda? Hivi umeyaona mazishi ya usoni mwake hapo anapopelekwa Hospitali?

- Rudi kwa watu wengine ambao wamewahi kutoka bila mikwaruzo (example Bakhressa son navigator)

5. Serikali haikutaka mtaalamu wa kuangalia maiti anayekubalika na Familia ya marehemu, lakini ikaridhika na mtaalamu aliyefanya hiyo kazi, unafikiri ni kwa nini?

- Familia iliomba kuleta mtaalamu wao baadaye na sio immediately after accident. Naamini ni baada ya mabingwa wa spin kuwavuta masikio.

6. Serikali iliyotuambia kuwa Balali amefia Boston, wakati ukweli sasa uko wazi kuwa alifia DC, sasa wewe na Mtanzania, mnataka tuiamini serikali kuwa this time inasema ukweli?

- Out of topic. Two different things.

Wakuu naomba kusema hivi, kuna watu kama mimi binafsi, siamini tena kwa 100%, kuwa hii ajali ya Wangwe ilikuwa ni ajali ya kawaida au mkono wa Mungu, ninarudia tena kwua siamini, na ninaahidi kwua nitautafuta ukweli mpaka niupate na nintauweka hapa hapa JF, kwa wale wanaohusika naomba mjitokeze mapema, maana when the time comes asije akalia mtu hapa! Siwezi kuahidi time lakini ninaahidi kuiwa nita-get ot the bottom of this na ukweli nitauweka hapa wazi!

- Kuamini na kutoamini ni haki ya kila binadamu...

Mimi ninarudia tena kua siamini kabisaa, kama ni kuvunja sheria kutoamini kwangu so be it!

Asante Mkuu FMES.
 
Kwa kweli debate ya mapanga kama yalikuwepo au hapana inashusha hadhi ya siasa za taifa letu bure, kwa sababu what is there to be gained politically na this kind of debate? Nani atakaye profit kutokana na hii debate?

tumeambiwa mara ngapi hapa kuwa Lipumba ni babu kubwa sana, sasa leo Professor mzima anaenda kuongelea mapanga, niliwaambieni kuwa alinunuliwa kwa shillingi millioni 70 kutoka Oman, baada ya kuzikataa millioni 50 za CCM,

Sasa ameshachukuwa hela nyingi sana za UN, kwa ajili ya kazi aliyoyakuwa kuifanya Geneva na baadye kuhamia NY, sasa hela za watu ameshachukua hakuna cha kazi wala ripoti huyo anadunda na ishu za mapanga, kesho na keshokutwa wabongo tukinyimwa kazi UN mtasema tunaonewa,

Mkuu wangu Kitila umemuona rafiki yako huyu? Mimi nilisema kuwa huyu ni tapeli wa kutupwa umekubali sasa au?
 
Insurgent, katika theory yako what caused the accident?

Primary cause: HIGH SPEED.

Secondary causes: The tire, driver profiency in handling hazards at high speeds.

The car might have had some problems. Kumbuka waliipeleka gereji. Kwenye tairi kuna vitu viwili, wheel nuts and wheel bolts. Inawezekana kabisa hawa walireplace wheel bolts na gereji iliwapiga mchanga wa macho na kuwawekea "fake" au fundi aliyekaza hakuwa makini.
 
Insurgent ninapenda theory zako,, unasema Mallya alimhamisha Wangwe, wakati mzee anasema yeye ndiye aliyemfungua Wangwe akiwa amefunga mkanda, sasa hapa nani anasema ukweli kati ya wewe na huyu mzee?

Halafu mkuu unafikiri hii ajali imesababishwa na nini mvua, jua kali, upepo, au ni kawaida tu? Halafu hebu rudia tena la mtaalamu, kwa sababu familia ilimleta justi in time kabla ya mazishi, maana tumeona kesi maiti imekwenda kufukuliwa sasa hapa wala haijazikwa tatizo lilikuwa ni nini mkuu?

nitarudi baadaye mkuu with more! lakini so far I like this! yaani utetezi wako kwa serikali na Mallya.
 
Suala la Mpanga,sime,mishale lilikuwa la kupangwa na kwa kuwa halikuweza kutokea ilikuwa tayari habari imeshaandikwa na kusambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa hicho kinaweza kutokea.

Kumbukeni kifo cha Salome Mbatia kuna kiongozi mmoja alipiga simu news room na kuwaambia kuwa wasubiri big news ,........connect the dots.

Pili kulikuwa na mpango huo na ulifanyika kuanzia Dodoma kwa baadhi ya viongozi na hata Mawaziri kuwafuata watu kuwataka wamzuie Mbowe kwenda ili baad ya siku waseme kuwa si mnaona kuwa ameshindwa kuja kumzika?then waunganishe......connect the dots.....

Kuna haja ya nkuendelea kufuatilia mjadala huu kwa umakini na kujua nini kilikuwa kimepangwa na hata kuvifanya vyombo husika vitangaze vile.

Je?ni mkakati wa muda mrefu kuwa Mbowe asiende huko kufanya Kampeni kwa kisingizio kuwa hilo litasababisha uvunjifu wa aman?

Je?nani anahusika na mpango huu wa kidahalimu na wa kutaka kuliangamiza Taifa hili?

Kuna nini kilichotokea mpaka Wangwe akapata ajali na kufa nani anahusika kwenye hili?

TAnzania tumefikia huko?ni kwa nini?

Naamini kuwa siku ipo na ukweli utakuwa hadharani kama ilivyotokea kule Kenya kwa Robert Ouko , yalisemwa na baadae yalibainika kuwa nani alihusika.


Kukimbizwa kwenye mazishi ni jambo la kawaida hasa mtu husika anaposhukiwa
Shinyanga na mwanza wakikushukia huwa wanaenda wanakukamata wanaenda KUKUTEMYA yani wanakuchukua maili kadhaa polini na kukuulia mbali ndege na wanyama wanafanya kitoeo wala ndugu zako hawataona sehemu wala kabuli lako.

Wakikukosa ama ukatoroka kijiji huwa wanakuwinda na kuvamia nyumba na kukatakata mapanga.
Yote haya hufanyika bila ya MEDIA wala chombo chochote cha habari kuwaandaa wananchi hawa ,wala hua hawafanyi hivyo kwa makusudi ya siasa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom