Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Just to make things clear waungwana, Deus Mallya is not me:-
 
Kama huyu kijana ndiye alikuwa anaendesha gari, hana leseni, na kwa mwendo kasi; kwanini ameshtakiwa kwa makosa ya kutokuwa na leseni na kuendesha gari kasi bila kushtakiwa kwa kosa la kusababisha kifo? Akili mukichwa. Tukubali tu ilikuwa ni ajali ya kawaida (kwamba mtu asiye ne leseni, anaenda kasi, anamuendesha Mbunge wa Bunge la Muungano - ni kawaida tu)?

Do we have intellignt intelligence personell in this country to give us the truth? Sidhani kama akina Lipumba wamekurupuk tu kama ambavyo che Mkapa angesema. There is something seriously uncertain kumhusu huyu Malya! Anayejua ukweli atuambie basi.
 
nimetokea kumfahamu deus kwa muda sasa na mpaka haya yote yanatokea nilikuwa namdai hela kubwa, sijui naweza kumfuata huko dodoma ALIPO?
katika maongezi yangu na deus, aliwahi kuniambia kuwa anaukaribu na Ghadafi, rais wa libya, kusema ukweli maelezo yake yanaonyesha kama alijifunza ujasusi, lakini ana milolongo mirefu sana ya kufahamiana na baadhi ya viongozi, enzi hizo alikuja mitaa ya mwenge akiwa anauza kibandani. ukiongea naye kwa karibu inaonyesha kama sio mtu wa kawaida. waweza fikiri ni zoba fulani au anakitu anaficha.
ameishi mwenge kwa muda na anakijiofisi chake mitaa ya kinondoni na ktik maongezi ni kama anaukaribu sana na CHADEMA nzima. simu yake haikuwa hewani wiki mpoja kabla ya ajali japo aliniambia kwamba alielekea morogoro na baadaye dodoma na angerudi da alhamisi ya wiki iliyopita kabla ya ajali ili anilipe deni langu.
sasa sijui naweza kumfuata dodoma kumdai au natonekana mwenzake?
 
Kubalini tu yaishe; na msije kushtuka kijana akipata ugonjwa wa ghafla n.k au kesi ikaenda weeee na baada ya muda akatuaga dunia. Na ikitokea msiulize kubalini tu ni mapenzi ya Mungu.
 
Kubalini tu yaishe; na msije kushtuka kijana akipata ugonjwa wa ghafla n.k au kesi ikaenda weeee na baada ya muda akatuaga dunia. Na ikitokea msiulize kubalini tu ni mapenzi ya Mungu.

Tatizo lako ni kwamba umezidi kuwa mkweli. Yetu macho!
 
Kubalini tu yaishe; na msije kushtuka kijana akipata ugonjwa wa ghafla n.k au kesi ikaenda weeee na baada ya muda akatuaga dunia. Na ikitokea msiulize kubalini tu ni mapenzi ya Mungu.
..What do u' mean?? anaweza kubalaliwa????? Kwi!! kwi!! kwikwikwi!!!!!!!!
 
mrema anaumwa na kirusi cha ukosefu wa ruzuku chamani. anadhani jibu ni ifo cha wangwe kuwa ataibuka mtu katika ukoo wa wangwe halafu ajiunge na TLp, ili waendelee kupata ruzuku waliyopoteza baada ya mahakama kutengua ubunge wa mbunge pekee wa tlp, phares kabuye
 
Kubalini tu yaishe; na msije kushtuka kijana akipata ugonjwa wa ghafla n.k au kesi ikaenda weeee na baada ya muda akatuaga dunia. Na ikitokea msiulize kubalini tu ni mapenzi ya Mungu.

Haya Maneno yako Mkuu,"Tutayakumbuka".Wala haihitaji Intelligenjia kubwa kujua kwamba kuna mchezo mchafu unachezwa hapa..Mallya amekwishafikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na atakwenda huko (Mahakamani) tena 24/08.Katika siku yake ya mwanzo Mallya ameshitakiwa kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendo kasi bila kuwa na Leseni..Angalia kosa hilo Waungwana,Huyu Mallya alitakiwa kushtakiwa kwa kutoa maelezo ya Uongo kwa vyombo vya Dola,Lakini pia amesababisha kifo cha Mbunge,na kama hiyo haitoshi pia alikutwa na Kitambulisho kisichokuwa chake...Mbona haya hayasemwi? Mara tuanaambiwa kuwa Mallya ni mfanyabiashara Jijini Dar.Ni biashara gani anazofanya huyu Muungwana?

Wale wenye Kumbumbuku kumbukeni kesi ya Mohammed Enterprises ya kuingiza chakula kibovu...Ilirushwa rushwa na tukaanza kusikia kifo cha Mkemia Mkuu wa serikali na baadaye Jaji naye alifariki..Ile kesi iliishia wapi?Sasa hali ile itatokea kwenye kesi hii ya Mallya,kwa sababu kama ilivyokuwa kwenye kesi ya Mohammed Enterprises ninaamini kuna makubwa nyuma ya pazia kuliko haya tunayoyaona...
 
...........kwanini ameshtakiwa kwa makosa ya kutokuwa na leseni na kuendesha gari kasi bila kushtakiwa kwa kosa la kusababisha kifo? Akili mukichwa.

😱 mmmmmmmmmmmmmmmh akili Kunkichwa? Uhusiano na merehemu ulikuwa mwema na Ulianzaje? more questions than Answers
 
Kwa hiyo ushahidi wa mzee aliyemfungua mkanda Marehemu umeshaamua kuutupilia mbali?

Mzeeba,

Kwenye ajali kama hizo usije ukasikiliza ushahidi wa mtu mmoja. Anaweza akawa alimfungua lakini pia inawezekana hakumfungua. Ukiamini yote aliyosema huyo mzee lazima pia uamini kwamba kulikuwa na mtu wa tatu.

Kule kuumia sio kwa mtu aliyefunga mkanda, unless kama kuna mti au mwamba ulimgonga.

Sisemi niko 100% lakini kwa uzoefu wa kuangalia ajali mbalimbali, kupasuliwa kichwa kisogoni sio rahisi kutokea ukiwa umefunga mkanda.
 
Too many questions arise. Kama ni kweli yeye ni jasusi;

1. Who is he working for? The party, outside the party, special(Classified) department in the party?

2. Any connections with the death of Late Hon. Wangwe, if there was any Project going on, is he part of it?

Please tell me more about this guy!.........
kama ni jasusi anatumiwa narostam aziz na mafisadi wenzake kufanya alichofanya ili ku-divert minds za watanzania wasimzungumzie yeye fisadi bali chadema na wangwe
 
Suala la Mpanga,sime,mishale lilikuwa la kupangwa na kwa kuwa halikuweza kutokea ilikuwa tayari habari imeshaandikwa na kusambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa hicho kinaweza kutokea.

Kumbukeni kifo cha Salome Mbatia kuna kiongozi mmoja alipiga simu news room na kuwaambia kuwa wasubiri big news ,........connect the dots.

Pili kulikuwa na mpango huo na ulifanyika kuanzia Dodoma kwa baadhi ya viongozi na hata Mawaziri kuwafuata watu kuwataka wamzuie Mbowe kwenda ili baad ya siku waseme kuwa si mnaona kuwa ameshindwa kuja kumzika?then waunganishe......connect the dots.....

Kuna haja ya nkuendelea kufuatilia mjadala huu kwa umakini na kujua nini kilikuwa kimepangwa na hata kuvifanya vyombo husika vitangaze vile.

Je?ni mkakati wa muda mrefu kuwa Mbowe asiende huko kufanya Kampeni kwa kisingizio kuwa hilo litasababisha uvunjifu wa aman?

Je?nani anahusika na mpango huu wa kidahalimu na wa kutaka kuliangamiza Taifa hili?

Kuna nini kilichotokea mpaka Wangwe akapata ajali na kufa nani anahusika kwenye hili?

TAnzania tumefikia huko?ni kwa nini?

Naamini kuwa siku ipo na ukweli utakuwa hadharani kama ilivyotokea kule Kenya kwa Robert Ouko , yalisemwa na baadae yalibainika kuwa nani alihusika.
 
Polisi wanayo passport ya Bwana Mallya, kwa hiyo ninachoeleza ni kwa mujibu wa habari toka vyanzo vyao. Ni vyema Mbatia akahojiwa kwa kina aseme anachokifahamu cha ziada ili aisaidie polisi katika uchunguzi

PM

Aseme nini zaidi ya uchochezi tuu
It is too low kwa viongozi wa siasa kumpandisha chati huyo dereva asiye na leseni
La msingi tujiulize ni kigezo gani marehemu aliamua kumpa gari aendeshe bila kuona leseni yake au ndiyo hiyo Cost saving
 
kwanini hadi leo Chadema haijaitisha uchunguzi huru kama wa Scotland Yard na badala yake wameng'ang'ania kuwataka Polisi wafanye kazi hiyo wakati kimsingi ingekuwa na Polisi wenyewe wahojiwe na mtu aliye huru? Nani alitoa habari kwa Polisi kwanza; Polisi gani walifika pale mapema? n.k

Katika hili Polisi wetu wangekaa pembeni.
 
Kifo cha Wangwe: Vigogo BP juu!

2008-08-04 16:01:41
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Mazingira tata ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, Mhe. Chacha Wangwe (CHADEMA), yamewafanya baadhi ya vigogo kuingiwa na hofu kubwa ya maisha yao na sasa wengine wamedai kuwa wana data ambazo hata kuzianika hadharani wanaogopa kwa sababu za kiusalama.

``Uchunguzi umethibitisha wazi kuwa Wangwe hakuuawa kwa risasi... lakini pamoja na ukweli huo, bado baadhi ya vigogo katika siasa, hasa wale wa upinzani, wamekuwa na hofu kutokana na mazingira tata ya ajali yenyewe na kile kilichomtokea (Wangwe) hadi kufa,`` kimesema chanzo chetu kimoja kilicho jirani na vigogo maarufu wa upinzani nchini.

``Hivi sasa kuna data nyingi zilizopatikana na kuibua maswali mengi kuhusiana na kile kilichotokea. Kijana aliyekuwa na Wangwe wakati wa ajali ndiye anayeelekezewa kidole zaidi kutokana na maelezo yake kila alipohojiwa... hili limeongeza hofu zaidi kwa vigogo hao, wakiamini kuwa wao wako hatarini na taifa pia liko hatarini,`` kimeongeza chanzo hicho.

Taarifa hizo za kuwepo kwa hofu miongoni mwa baadhi ya vigogo zimetiwa nguvu na yale yaliyosemwa jana Wenyeviti wa Umoja wa Vyama vinne vya upinzani nchini jana na kunukuliwa na vyombo vya habari leo asubuhi, kuhusiana na shaka iliyopo katika ajali iliyomuua Mheshimiwa Wangwe.

Wakizungumza hiyo jana, wenyeviti wa vyama hivyo vya CUF, CHADEMA, TLP na NCCR, wamesema wanazo taarifa zinazoibua maswali mengi kuhusiana na kifo cha Wangwe, hasa juu ya kijana anayedaiwa kuwa naye ndani ya gari, Bw. Deus Mallya.

Wakasema maelezo ya kijana huyo juu ya tukio hilo, namna Wangwe alivyopata majeraha yaliyomuua na ziada ya taarifa walizopata toka kwa watu wanaomfahamu kijana huyo (Mallya), ni baadhi ya mambo yanayowafanya wawe na hofu kuwa kuna ujasusi umefanyika.

Wakasema viongozi hao ambao ni Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF, Augustino Mrema (TLP) na James Mbatia (CHADEMA), kuwa kwa taarifa walizo nazo, wanaamini vilevile kuwa upo mtandao hatari unaotishia usalama wa taifa.

Akizungumzia hofu hiyo, Prof. Lipumba akasema waliyemuona Mallya kabla ya tukio, wanasema alikuwa ni mtaalam wa kompyuta, alikuwa na vitambulisho vingi na vingine vimeandikwa kiarabu na pia, wanahisi kuwa amepata mafunzo ya kijasusi nchini Libya.

``Imekuwaje akawa karibu na marehemu kwa muda mfupi?`` Akahoji Profesa Lipumba wakati wakizungumza na waandishi wa habari.

Akautaja utata mmojawapo juu ya kifo cha Wangwe kuwa ni kuonekana kuwa kichwa cha marehemu kimepondeka na hakuna maelezo dhahiri ya suala hilo.

``...mle ndani ya gari hakuna hakukuwa na vyuma wala mabati yaliyopondeka. Kweli hakufa kwa kupigwa risasi... lakini ile ajali ilitokeaje mpaka lochwa kikapondeka?`` akasema Prof. Lipumba.

Aidha, Mbatia naye akasema.
Aidha, Mbatia naye akasema kutokana na utata mwingi juu ya kifo hicho ikiwa ni pamoja na maelezo ya kujikanyaga ya kijana Mallya, wao wameamua kumuona IGP Said Mwema ili wampe taarifa za siri kuhusiana na ukweli wa kifo hicho, kwa maslahi ya taifa.

``Inaonekana kuna mtandao unaohatarisha usalama wa nchi.... kijana huyo (Mallya) ana mafunzo ya Kimafia,`` akasema Mbatia.

SOURCE: Alasiri

http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/08/04/119907.html
 
  • Key Challenge ya kwanza ya Taifa ni kuzama kwenye KUFUFUA uchumi.
  • Key Challenge ya Vyama vya Siasa ni ku-Clean their House.

I would therefore not advise neither CHADEMA no CUF, etc etc. to investigate something which will not add value, it is simple that we have already lost late Hon. Chacha Z. Wangwe.

Ni wakati wetu na sisi tujiandae kwa kutenda mema huku duniani kwa kuwa na sisi si muda mrefu... majority of us less than 50 years to come... tutaenda huko alikoenda Chacha Wangwe.
 
Kifo cha Wangwe: Vigogo BP juu!

2008-08-04 16:01:41
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Mazingira tata ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, Mhe. Chacha Wangwe (CHADEMA), yamewafanya baadhi ya vigogo kuingiwa na hofu kubwa ya maisha yao na sasa wengine wamedai kuwa wana data ambazo hata kuzianika hadharani wanaogopa kwa sababu za kiusalama.

``Uchunguzi umethibitisha wazi kuwa Wangwe hakuuawa kwa risasi... lakini pamoja na ukweli huo, bado baadhi ya vigogo katika siasa, hasa wale wa upinzani, wamekuwa na hofu kutokana na mazingira tata ya ajali yenyewe na kile kilichomtokea (Wangwe) hadi kufa,`` kimesema chanzo chetu kimoja kilicho jirani na vigogo maarufu wa upinzani nchini.

``Hivi sasa kuna data nyingi zilizopatikana na kuibua maswali mengi kuhusiana na kile kilichotokea. Kijana aliyekuwa na Wangwe wakati wa ajali ndiye anayeelekezewa kidole zaidi kutokana na maelezo yake kila alipohojiwa... hili limeongeza hofu zaidi kwa vigogo hao, wakiamini kuwa wao wako hatarini na taifa pia liko hatarini,`` kimeongeza chanzo hicho.

Taarifa hizo za kuwepo kwa hofu miongoni mwa baadhi ya vigogo zimetiwa nguvu na yale yaliyosemwa jana Wenyeviti wa Umoja wa Vyama vinne vya upinzani nchini jana na kunukuliwa na vyombo vya habari leo asubuhi, kuhusiana na shaka iliyopo katika ajali iliyomuua Mheshimiwa Wangwe.

Wakizungumza hiyo jana, wenyeviti wa vyama hivyo vya CUF, CHADEMA, TLP na NCCR, wamesema wanazo taarifa zinazoibua maswali mengi kuhusiana na kifo cha Wangwe, hasa juu ya kijana anayedaiwa kuwa naye ndani ya gari, Bw. Deus Mallya.

Wakasema maelezo ya kijana huyo juu ya tukio hilo, namna Wangwe alivyopata majeraha yaliyomuua na ziada ya taarifa walizopata toka kwa watu wanaomfahamu kijana huyo (Mallya), ni baadhi ya mambo yanayowafanya wawe na hofu kuwa kuna ujasusi umefanyika.

Wakasema viongozi hao ambao ni Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF, Augustino Mrema (TLP) na James Mbatia (CHADEMA), kuwa kwa taarifa walizo nazo, wanaamini vilevile kuwa upo mtandao hatari unaotishia usalama wa taifa.

Akizungumzia hofu hiyo, Prof. Lipumba akasema waliyemuona Mallya kabla ya tukio, wanasema alikuwa ni mtaalam wa kompyuta, alikuwa na vitambulisho vingi na vingine vimeandikwa kiarabu na pia, wanahisi kuwa amepata mafunzo ya kijasusi nchini Libya.

``Imekuwaje akawa karibu na marehemu kwa muda mfupi?`` Akahoji Profesa Lipumba wakati wakizungumza na waandishi wa habari.

Akautaja utata mmojawapo juu ya kifo cha Wangwe kuwa ni kuonekana kuwa kichwa cha marehemu kimepondeka na hakuna maelezo dhahiri ya suala hilo.

``...mle ndani ya gari hakuna hakukuwa na vyuma wala mabati yaliyopondeka. Kweli hakufa kwa kupigwa risasi... lakini ile ajali ilitokeaje mpaka lochwa kikapondeka?`` akasema Prof. Lipumba.

Aidha, Mbatia naye akasema.
Aidha, Mbatia naye akasema kutokana na utata mwingi juu ya kifo hicho ikiwa ni pamoja na maelezo ya kujikanyaga ya kijana Mallya, wao wameamua kumuona IGP Said Mwema ili wampe taarifa za siri kuhusiana na ukweli wa kifo hicho, kwa maslahi ya taifa.

``Inaonekana kuna mtandao unaohatarisha usalama wa nchi.... kijana huyo (Mallya) ana mafunzo ya Kimafia,`` akasema Mbatia.

SOURCE: Alasiri

http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/08/04/119907.html

Yamekuwa haya tena!!

Na kama siyo kweli, itabidi jukwaa la wahariri liunde tume/kamati nyingine kulichunguza gazeti hili kama limepotosha au la!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom