Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kama kweli kwa karne hii kuna watu wataamini au kuaminishwa kuwa Mh Winfred Lwakatare ndio katoa video hii ni hatari sana kwa Taifa la Tanzania kwani kuna watu watakuja kuwanunua then mkauzwa then wajanja wakala pesa zao kwa ulaini,Hivi Bongo kuna wasomi kweli??

Hii video jamani imetengenezwa na ni rahisi sana kutengeneza ni mambo ya Computer hayo wananchi msipumbazwe kama ni kweli mlikona wapi muuji au wauaji wakapangaa ujinga kama huu hadharani tena kweupe kabisa kama ionyeshavyo hii video Lol kama na Police wamemkamata kwa hii video kweli hapo hakuna Police kuna Policeuniform na mijikanda kuzunguka mwli mzima lakini hakuna wataalamu teh teh teh.

Kina Riziwani Kikwete na Nape Nnauye walisema wanafahamu watu waliomfanyia Kibanda so swali hawa nao walikamatwa kwa kuhojiwa na kama hawajakamatwa wakati wanawafahamu watesaji hapo kweli kuna Police??

Mwaka jana CCM kupitia kwa kina Mwigulu,Wasira Steven walisema kuwa CHADEMA mwisho wake ni mwaka huu sasa hii ndio propoganda hiyo lol siasa za Bongo ni uchwara kweli kweli kama alivyosema Rostam Aziz.

Mwaka jana Mwingulu alisema ana video ya mpango wa mauaji ya CHADEMA na wakaambiwa waipeleke Police ili kama ni kweli wahusika wakamatwe,waliambiwa na viongozi wa CHADEMA lakibni hawajaipeleka kwa maana hiyo walikuwa hawajaimaliza sasa CCM walishamtesa na kutaka kumuuwa Kibanda ndio wanatoa video hii ya kuchonga hivi kwa miaka hii watu wenye akili zao wanaweza kutoa hii movie?

Jamani Watanzania tukae mamcho naa hawa jamaa wa CCM wametumia njia nyingi sana kuikandamiza CHADEMA lakini wameshindwa sasa wamekuja na upuuzi huu watakaowaamini watakuwa wanakasoro za akili.

CCM wameona maji yako shingoni ndio wanacheza movie za kina Jack Chein za kuruka kwenye ukuta na watoto wanaamini ni kweli so wataoiamini hii video nawasikitikia sana sana wako nyuma sana na Dunia hii ya Technologia
 
na Lwakatare akija kukuri hadharani ni yeye utakimbilia wapi? acha kuwa msemaji wake tumsubiri mwenyewe aje atuambie kisa cha kupanga mikakati ya kujeruhi watanzania wasio na hatia ni nini?
Bado tutamwambia kuwa video chip ile ni ya kugushi kwa sababu tunao ushahidi wa kisayansi. Atakuwa na kosa la kugushi! Itabidi pia akiri juu ya utengenezaji wake kuwa haikuwa picha iliyopigwa moja kwa moja bali ilikuwa picha ya kulishwa maneno kiteknolojia! Watu wa IT tunao ushahidi hata wa software zinazotumika kutengenezea picha hizo!
 
kweli usalama wa taifa imekaliwa na vilaza hasa RO,mauaji mengi yamehusisha polisi leo wanatengeneza filamu ya kizushi,watz tuko makini hebu watoe uchizi wao,lwakatare wanamdharirisha,aibu serikali ya mr dhaifu
 
Mkuu KIRUMO kama una kaweledi kidogo juu ya hili, waweza tengeneza nyingine hata kama ya dakika moja ukamlisha mtu 'potential' maneno kadhaa live na ukairusha kuonyesha kwamba hiyo tekinolojia ipo? Naamini hiyo yaweza kuwa muarobaini tosha wa huu upuuzi!
Mkuu, kuna mtu kaweka uzi hapa JF wa Jinsi Teknolojia hiyo ilivyotumika kumlisha Obama maneno. Fuatilizia.
 
Siri za mauaji zinafanywa hadharani utadhani wanauziana nyanya.......

Kwenye clip hiyo mpaka watu wanasalimiana na watu wengine... Wanapiga story hadharani... Hata ukitaka kumuwinda swala lazima ujiweke mahali pa siri... Sasa wao wapo hadharani eti wanapanga mauaji
 
Mkuu KIRUMO kama una kaweledi kidogo juu ya hili, waweza tengeneza nyingine hata kama ya dakika moja ukamlisha mtu 'potential' maneno kadhaa live na ukairusha kuonyesha kwamba hiyo tekinolojia ipo? Naamini hiyo yaweza kuwa muarobaini tosha wa huu upuuzi!
Bila shaka ushaipata maana ipo hapahapa ktk uzi huu1
 
Hii video itawatesa sana naona mnajaribu kufanya cover up lakini ukweli huu wa vitendo vya utesaji ambao umekua ukifanywa na kitengo cha ulinzi na usalama ndani ya chadema utaishi muda mrefu sana.

Kwasababu ya serikali dhaifu ya chama dhaifu yenye viongozi dhaifu na propaganda uchwara, 2015 bye bye magambaz. Vipimo vinaonesha kuwa uwezo wenu wa kunyambua hoja umeporomoka, mmeanza kufanya propaganda kama wale 60% wa kawambwa. Mmeishiwa uwezo wa kufikiri na kuamua. Pumziko la milele linakuja. Kama KANU huko kenya sasa hivi umaarufu wake unalingana na SAU ya tanzania, na ccm ndo inaelekea huko. Siku si nyingio mtakuwa kama CCK. Believe on not, the day is just close to the doors of Lumumba.
 
kila mtu ni kuhangaika
tu au huelewi? sisi cdm tunahangaika na video ya lwakatare kama
unavyosema sawasawa tu na jinsi ninyi ccm mnavyohangaika na cdm




wanajanvi tunakwenda wapi? kama hii CLIP niyakweli tuliachie jeshi la police lifanye kazi yake, kama kunamwanajanvi ambaye anaushaidi zaidi ni bora akalisaidie jeshi la police kitaalam zaidi kuliko kuongea zaidi. shuzi limepata mjambaji.
 
Mkuu BOCHO,CCM ina wasomi wengi mno,masters za kumwaga maprofesa nao lukuki,hilo wala halina ubishi,je wamelifanyia nini taifa hili miaka 50 matatizo kibao hata Rwanda inatushinda.Kuwa na elimu ni suala moja lakini kuwajibika ni suala jingine tofauti,na ndio maana pamoja na mawazili wote wa JK ni Mwakyembe na Magufuli tu ndio wanaowajibika wengine wanahangaikia matumbo yao.kuitetea CCM ni lazima upate msaada wa mawazo toka kwa watu wanaoishi sayari ya mars ni mahiri sana kujenga hoja.

Tatizo la Tanzania sio CCM tu ni watanzania wote kwa nafasi zetu mbali mbali tulizokuwa nazo.

Hebu niambie:

1) CCM itajuaje kama mimi nikiwa mtumishi wa TRA nimeshirikiana na wafanyabiashara katika kukwepa kodi (Collusion)?

2) CCM itajuaje kama nyara za serikali zimetoroshwa nje ya nchi ikiwa watanzania waliopewa nafasi kwenye maeneo hayo watashirikiana na maharamia kutosha nyara za serikali (collussion)?

3) CCM itajuaje kama kuna watumishi wa umma wanaoongeza bei katika manunuzi kwa kushirikiana na wauzaji na hivyo kupandisha gharama za manunuzi ya serikali (procurement frauds)?

4) Zile overtime mnazopewa wakati muda wa kawaida mnautumia kukesha JF na kucheza karata. Unafikiri ni CCM pia?

Tatizo sio CCM pekee na serikali, ni sisi watazania kwanza inabidi tubadilike kuwa na moyo wa uzalendo ndipo mambo yatakapobadilika for good katika nchi yetu.

Bila kuwajibika, si CHADEMA wala chama chochote cha upinzani kitakachoweza kuleta the so called mabadiliko ya kweli Tanzania.

Amka usidanganywe badilika wewe kwanza na umwambie mwenzako abadilike.

Pamoja tunaweza.
 
Tanzania inaharibiwa na watanzania wenyewe...Chokonoeni sana vita mtaipata tu kwa uroho wa madaraka
 
Hizi ndio aina ya software zinazotumika kutengenezea upuuzi wa aina hizi mojawapo ni hii inayoitwa crazytalk_Master6 iliyotengenezwa na company ya macrovision corporation file version: 12.0.0.58855 inauwezo mkubwa sana hasa ikimpata mtu mwenye uwezo wakuitumia tofauti na hao mamburula wa CCM walivyojichanganya kuitumia hadi Pinnacle version 11 kwenye kurekebisha sauti. kifupi ni dalili njema kwa Chadema maana CCM hawajui kua wanachangia kukipandisha chat CDM kwenye masikio ya watanzania huku wao CCM wakiendelea kufutika kwenye mioyo ya wazalendo wa kweli .

Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu viva Chadema .
 
tatizo la kutojiamini hiyo ni inferiority complex jadilini issue at hand.
Au mnatafuta sympathy ya upuuzi wa akina Ilunga?

HUjafuatilia huu mjadala ulikotokea, usingesema ulichosema coz' kwa makusudi watu walikuwa wanahusisha hili na suala la hao hao akina Ilunga unaowasema!!
 
NasDaz, rejea hoja yangu, nadhan huku katikati tumeanza kugawana njia, hatetewi mtu, nilieleza wasiwasi wangu na mambo yote yaliyocenter around the whole issue na nkaiweka hiyo clip ili at least kushed light kuwa ipo technologia ya kulishana maneno kwenye hii planet earth, Na nikaelezea kuwa asbh ya jana watu walikita urguments zao kuwa mtu anawezaje kulishwa maneno??? Ndio nikaweka hiyo kutoa mwanga kwa wale wote wasiofahamu hii maneno. Bado tunamsubiri muhusika/mahakama kutueleza ukweli, hili sio jukwaa la kuhukumu au kukanusha tuhuma. Ila tu ni vyema tukawa na mtazamo mpana zaid katika ujengaji wa hoja zetu.

I like honesty answers!! Labda nikuambie kitu kimoja....binafsi nina taabu na wale ambao moja kwa moja wanapinga simply because kuna video manipulation technology huku wakiwa hawatuoneshi wapi the video under question imekuwa manipulated!

On the other hand, mimi najihisi ni mtu wa ajabu kidogo! Unajua nini? Mkuu wangu Patriote sifahamu nafasi yako ktk CHADEMA ipo vipi....i mean, ikiwa nawe ni viongozi wa CHADEMA, wala sitaona taabu nikikuona unakanusha kwamba hii video ni fake....kama kiongozi, una wajibu huo coz' that's how politics work unless kama cha kukanusha chenyewe kipo wazi; kukanusha itakuwa uendawazimu!! Hivyo basi, nikuone wewe(kama upo kwenye CDM Team), Mwita Maranya, Molemo au wengine sawa na hao wakikanusha, wala sitakuwa na tatizo coz' nafahamu mnatekeleza wajibu wenu....DAMAGE CONTROL. Lakini vilevile uungwana una-suggest kwamba, ukiona nakupinga, na wewe unafahamu kabisa ninachosimamia ni sahihi, basi usinione mjinga....fahamu tu kwamba, nimegoma kununua political lie/propaganda!

Tatizo lililopo kwa baadhi ya mashabiki wa CHADEMA(am certain, u're not one of them) ni kwamba, sie wote ambao tunaamini kwamba the video ni genuine; we're fool na hatujui lolote abt video manipulation technology as if any video siku hizi lazima itakuwa manipulated!! Hapa, ndipo linapoanza tatizo!
 
Hii video ya "Rwakatare" inanikumbusha miaka ya 2000 ( nadhani 2004 au 2005) ZANU PF walitengeneza VIDEO kama hii ikimuonyesha Morgan Tsvangirai akipanga mipango ya kupindua nchi kwa kushirikiana na majasusi fulani. Baada ya video kuwa scrutinized Tsvangirai alishinda kesi.

Video ya Rwakatare ni ya kiwango cha chini sana kulinganisha na iliyokuwa ya Tsvangirai. Uliona mipango ya kuua inafanyika sehemu ambayo movement kibao. Nadhani ni baa/grocery fulani hivi, maana inaonekana kama wahudumu wanaenda jikoni kutoa order ya wateja. Tena hiiyo baa ipo karibu sana na barabara.
 
Back
Top Bottom