Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kama siasa chafu hii imeenda shule iwe kweli au uongo.....nchi inaelekea kubaya
Computer ni kitu cha ajabu kwa mtu anayejua kuitumia. Waweza kuchukua picha ukawekea maneno mengine na background scene na sauti tofauti kabisa kiasi mtu asiyejua IT akadhani ni picha halisi. Ni mchezo mdogo sana wa IT. Najua hii imetengenezwa kuwa confuse wengi lakini mtu anayejua hiyo michezo ya IT anajua kwa hakika kuwa kuwa hiyo sio picha na maneno halisi. Maelezo mengi yametolewa kuhusu hilo na sipendi kuyarudia ila tu- NI PICHA YA KUGUSHI!
 
Hao jamaa wamechemsha ile mbaya,hozo pesa wanazotumia kuandaa huo ujinga kwanini wasipeleke kwa watu wenye mahitaji kuliko kujidharirisha kwa kuandaa vitu vilivyokosa quality kabisa.
 
shukrani sana.
wenye akili timamu haituingii akilini.
 
Hakuna haja ya kuhangaika na nadharia za upungufu au uhalisia wa video. Kwa vile Lwakatare mwenyewe ni mtu anayeexist na sio fictional character, ni vema aje yeye mwenyewe atuelezee ni lini video hiyo ilipigwa, wapi, na nani na walikuwa wanajadili nini. Hili hakuna sababu ya mtu yeyote kumuwakilisha Lwakatare na the longer anakaa kimya the more inaonekana ana makosa.

Point mkuu but...
 
Wana mapinduzi wanaamini kuwa ukiona mambo kama haya tambua kuwa ukombozi upo karibu. Uhuru na Ruto walifanya kama haya na sasa wameingia ikulu, aibu kwa ICC na mafia wao. Nadhani ni muda wa kushangilia ushindi na mapinduzi ya kweli, watanzania wenye akili, na hasa hawa wanaotumia mitandao ya kijamii na forum makini kama JF watatumia akili zao kuchambua hili. Maana mengi yamesemwa kuhusu CHADEMA yameshindwa....walianza na ukanda ukashindwa, wakaja na dini wakashindwa, wakaja na kadi ya dokta Slaa wakashindwa, sasa wemeibuka na mauaji...hakika MUNGU ni yule yule jana, leo na hata milele, ataendelea kutupigania wana CHADEMA.

Tualianza na MUNGU, tunaendelea na MUNGU, tutamaliza na MUNGU
Ikiwa MUNGU, yupo upande wetu, nani atanyanyuka kinyume chetu?

nakukumbusha usiende kinyume na mtazamo wa Chama chako kuwa Odinga Kaibiwa kura! So jipangaeni kwa Maandamano kabambe katika jiji la Nairobi hakuna kulala mpaka kieleweke!
 
Kufuatia suala la Lwakatare kushika kasi humu jamvini, zimetokea hisia na mawazo tofauti sana baina ya wachangiaji mbalimbali juu ya mada hii ya kurecordiwa Lwakatare kupanga kumdhuru mwandishi. Wengi tulihoji sana uwezekano wa hii ishu kama ni halisi/si halisi. Kutokana na kuwa gizani kitechnologia, wengi hadi ninavyoongea hivi bado huwezi kuwabadilisha mawazo kuwa technolojia inaweza ikahusika katika kufake ile clip. Na kutokana na suala hili kugubikwa na propaganda za kisiasa, watu wamesahau hata technologia rahiti tu ya kuifanya midomo ya Cartoon icheze kulingana na maneno yanayotamkwa na cartoon/robot.

Kuweka kumbukumbu vizuri tarehe za mwanzon kabisa za mwaka huu mpya Mwigulu Nchemba alitueleza kuwa alikuwa na mkanda unaoonyesha viongoz (wengi) wa chadema kupanga mauaji. Mkanda umetoka tumeona kiongozi mmoja tu ndo anayepanga mauaji, kupungua kwa washiriki kutoka kwa viongoz hadi kiongozi, inahusishwa na ugumu uliopo wa kuinvolve watu wengi kwenye kufake/kulisha maneno watu wengi kwenye clip moja.

Aidha, baada ya tukio la utekwaji wa kibanda, wameibuka Nape na Ridhiwani hadharani na kuongea wakiwa na confinence ya 100% kuwa ''hawa wenzetu wa upinzani''/na ''safari hii pia mseme kuwa Ikulu/Rama/Magogoni ndio wanaohusika, kazi iliyopaswa kufanywa na vyombo vya dola. Siku chache baadaye Single ya Lwakatale ikatambulishwa rasmi kupitia Youtube na immediately ikatua jamvini na hata Polisi kuipata habari hii via Jamvini/Youtube na sio kwa Mwigulu. Sasa ukiconnect dots.......unaruhusiwa kabisa kufikiri kuwa tayari wenzetu wa upande wa pili walisha preview hii clip waliyoshiriki kuiandaa na ndo mana walikuwa na uhakika kuwa kwa level yetu ta technology, ni rahisi sana kushawishika kwa hii clip kuwa ni halisi.

Tulishasikia pia Wassira akitamka kuwa CDM lazima ife 2013, wengi hatukuelewa na hadi sasa hatujaelewa alikuwa anamaana gani kutamka maneno kama yale mtu wa makamo yulo. Sasa kauli za hivi za kumtamkia kifo mwenzio zinasignal kuwepo kwa mkakati wa maksudi wa kumuua mwenzio??Aidha, CCM katika vikao vyao vya CC/NEC, ccm walijadili kwa kina namna ya kudeal/kuisambaratisha CDM badala ya namna ya kutumikia umma wa watanzania waliowaweka madarakani. Hapa pia panazaa jambo.

Baada ya utanguliz huu naomba niimwage kwenu faked clip ya Barack Obama ili at least tujue tu kuwa suala la kulishwa maneno linawezekana. BOFYA A Bad Lip Reading of Barack Obama's Inauguration (Legendado PT-BR) - YouTube. Aidha, clip hii isikuzuie kuendelea kuamini unachokiamini, mimi nimeonelea tu niwafahamishe wale wote wenzangu ambao asubuh ya leo tulihisi sio kitu kinachowezekana hapa duniani.
 
Computer ni kitu cha ajabu kwa mtu anayejua kuitumia. Waweza kuchukua picha ukawekea maneno mengine na background scene na sauti tofauti kabisa kiasi mtu asiyejua IT akadhani ni picha halisi. Ni mchezo mdogo sana wa IT. Najua hii imetengenezwa kuwa confuse wengi lakini mtu anayejua hiyo michezo ya IT anajua kwa hakika kuwa kuwa hiyo sio picha na maneno halisi. Maelezo mengi yametolewa kuhusu hilo na sipendi kuyarudia ila tu- NI PICHA YA KUGUSHI!

Mkuu KIRUMO kama una kaweledi kidogo juu ya hili, waweza tengeneza nyingine hata kama ya dakika moja ukamlisha mtu 'potential' maneno kadhaa live na ukairusha kuonyesha kwamba hiyo tekinolojia ipo? Naamini hiyo yaweza kuwa muarobaini tosha wa huu upuuzi!
 
Kama nilivyochangia katika thread inayohusu video ya Lwakatare
1.Anayerekodi anamuongoza mzungumzaji kwa kumwambia maneno "niweke? mmh hapoo? haya" . pia anamuelekeza arudie maneno.

2.Imerekodiwa bar, watu wanapitapita wanasalimia na kutaja majina yao. Kwa watu makini hawawezipanga mpango hatari kwenye eneo la wazi hivyo.

3.Sura ya muongeaji si halisi na tone yake si halisi.

4.Anayerekodi anachomeka jina la Zitto kuhalalisha mpango.
JIPANGENI UPYA KUHARIRI VIZURI NA ALIYEHARIRI AMECHEMKA

Chekini hii video mtaelewa walichofanya
 
Last edited by a moderator:
Kama nilivyochangia katika thread inayohusu video ya Lwakatare
1.Anayerekodi anamuongoza mzungumzaji kwa kumwambia maneno "niweke? mmh hapoo? haya" . pia anamuelekeza arudie maneno.

2.Imerekodiwa bar, watu wanapitapita wanasalimia na kutaja majina yao. Kwa watu makini hawawezipanga mpango hatari kwenye eneo la wazi hivyo.

3.Sura ya muongeaji si halisi na tone yake si halisi.

4.Anayerekodi anachomeka jina la Zitto kuhalalisha mpango.
JIPANGENI UPYA KUHARIRI VIZURI NA ALIYEHARIRI AMECHEMKA
Ya nini kutapatapa wandugu?! Kwani Lwakatare mwenyewe atashindwa ku-prove beyond reasonable doubt kwamba ile video ni fabricated material?! Mbona wana-CDM wameshawahi kukumbwa na kesi mara kadhaa, so wht's so special kwenye hili la Lwakatare?! Waingereza wana msemo, A Black Cat May Be A Bad Lucky Only If You Are A Mouse! Wewe kama si panya, ya nini kumuhofia a black cat?! Unajua mnavyojitokeza hapa na kufungua nyuzi mpya mpya kuonesha kwamba video ni fabricated material, hapo ndipo mnapo-raise doubts kwa watu!! Mmesahau Uhuru Kenyatta pale alipojipeleka mwenyewe ICC?! Kenyatta alifahamu kwamba he's not a Mouse, so hakuwa na sababu za kumwogopa a Black Cat ICC!!!
 
Mkuu KIRUMO kama una kaweledi kidogo juu ya hili, waweza tengeneza nyingine hata kama ya dakika moja ukamlisha mtu 'potential' maneno kadhaa live na ukairusha kuonyesha kwamba hiyo tekinolojia ipo? Naamini hiyo yaweza kuwa muarobaini tosha wa huu upuuzi!

Hapana, aibadilishe ile ile ya Lwakatare iwe Nchemba!!
 
Tunachezeana michezo ya kitoto sana na ndo maana unaona kundi kubwa la wanaccm walijifanya Manabii wa kutabiri anguko la cdm, kumbe walishaidhinisha uandaliwaji wa hii movie, kumbuka kuwa wanawatu wao nje wanaoweza kuwajulisha hali ya technologia huko nje na hivyo kutumia utaratibu kama huu kuchafua hali ya kisiasa nchini. 2015 tutaelewana tu.
 
Ukiwa mnafiki uwe na kumbukumbu, na wewe umetumia teknolojia gani kumlisha maneno Riz wan na Nape kuwa wamesema Chadema wanahusika, Wengi wetu tulipitia Wall paper ya Ridh na Nape hakuna neno Chadema walipotaja, Alama za Mtu mnafiki ni 3 na moja wapo ni Uongo.Lwakatare kesha nasa kwenye mtego hateguliwi kwa manati mtazid kumuumiza! Yeye ndo atathibitisha sio kukimbilia kwenye Google Engine kutafuta namna ya kumtoa!
 
All in all..., hii nchi tumefika ambapo sipo.., watu waanze kutupwa ndani na tuache utani kwenye mambo serious.., uchunguzi ufanyike, ikigundulika kwamba watu walipanga mauaji, waliua au walisingizia wenzao (kugushi) basi wawekwe ndani huu sasa ushakuwa zaidi ya upuuzi (siasa mpaka kwenye maisha ya watu)
 
Mkuu wangu Patriote,
Waingereza wana msemo wao kwamba "A BLACK CAT MAY BE A BAD LUCKY ONLY IF YOU ARE MOUSE!" Chambilecho wewe sio panya, yanini kuingiwa taharuki pindi umwonapo paka?! Naona wapwa mmekazana sana kulikanusha hili jambo....pamoja na post kadhaa za kukanusha, bado hivi sasa kuna new threads za kukanusha...!! Hofu ya nini? I believe Lwakatare is smart enough ku-prove beyond reasonable doubt kwamba ile video is just a fabricated material; sasa nyie hofu yenu nini mkuu wangu Patriote? Mnatutia mashaka sie wengine; a black cat may be a bad luck only if you're mouse! Wewe majani, hofu yako nini kuingizwa kwenye banda la mbwa wakati unafahamu mbwa hali majani?! Unakumbuka pale Uhuru Kenyatta alipojipeleka mwenyewe ICC? Kenyatta alifahamu he's not a mouse so he'd no reason to get scared of a balck cat ICC!! Wewe kama ni majani, pigana kufa na kupona, ikibidi kanusha kwa nguvu zote kwamba wewe si majani ikiwa umegundua unataka kupelekwa zizi la mbuzi, lakini kwenye banda la mbwa; aaaargh, hofu ya nini!!!
 
Hivi hawa kina Mwigulu hawana hata aibu ya kutoa video kama hizo Lol ati wasomi vitu hivi i mean video kama hizi hutolewa na macomedia lkn sio wasomi ati wanajiita wana first DG of Economy aibu kweli kweli
 
nilikuwa nataka kuja na hoja kama yako, angalia midomo ya rwakatare wakati anaongea, jamani hapa hakuna uhalisia kabisa, ni kama maneno anafaanya kuyafwatisha kwa kumung'unya ila hayatoki kwa midogo yake!! alafu huyu mtu anayeelekezwa inakuwaje mwanzo mwisho yeye ni ehe ehe ehe hana hata la kuchangia??
 
Mkuu wangu Patriote,
Waingereza wana msemo wao kwamba "A BLACK CAT MAY BE A BAD LUCKY ONLY IF YOU ARE MOUSE!" Chambilecho wewe sio panya, yanini kuingiwa taharuki pindi umwonapo paka?! Naona wapwa mmekazana sana kulikanusha hili jambo....pamoja na post kadhaa za kukanusha, bado hivi sasa kuna new threads za kukanusha...!! Hofu ya nini? I believe Lwakatare is smart enough ku-prove beyond reasonable doubt kwamba ile video is just a fabricated material; sasa nyie hofu yenu nini mkuu wangu Patriote? Mnatutia mashaka sie wengine; a black cat may be a bad luck only if you're mouse! Wewe majani, hofu yako nini kuingizwa kwenye banda la mbwa wakati unafahamu mbwa hali majani?! Unakumbuka pale Uhuru Kenyatta alipojipeleka mwenyewe ICC? Kenyatta alifahamu he's not a mouse so he'd no reason to get scared of a balck cat ICC!! Wewe kama ni majani, pigana kufa na kupona, ikibidi kanusha kwa nguvu zote kwamba wewe si majani ikiwa umegundua unataka kupelekwa zizi la mbuzi, lakini kwenye banda la mbwa; aaaargh, hofu ya nini!!!

Kwenye bold: Naona mzigo unaelemea kwenu....propaganda skills show imefika pazuri!
 
Back
Top Bottom