Nadhani wenye maamuzi ya mwisho ni polisi, pamoja na kwamba mtuhumiwa ametokea upinzani, nitawaomba polisi wetu wasitumie upinzani kama kigezo cha kumhukumu mtuhumiwa. Lwakatare apewe haki yake kama Lwakatare na kama raia mwingine yeyote wa nchi hii.. Nadhani aliyeweka hii video alikuwa na mawazo hasi na upinzani ndiyo maana anawauliza wa "CHADEMA, hapa Lwakatare anamaanisha nini?.. Kwa uelewa wangu huyu mtu hana dhamira njama kwa Nchi yetu ya Tanzania, anaweza kuwa mtu hatari sana katika mipango na mikakati yote ilyokwisha ripotiwa ya mauaji, utekaji na uumizwaji wa raia, waandishi na wanaharakati mbalimbali hapa Tanzania. Nadhani Polisi wangeanza na huyu mtu angeweza kuwasaidia sana katika utekelezaji na upelelezi wa makosa yanayofanana na haya. Nachoona hapa ni hiki,.
- Mweka video alishiriki katika kuiandaa clip hii kikamilifu.
- Anatumiwa na watu wasiyoitakia mema Nchi yetu ya Tanzania,
- Ana mtandao ambao huratibu uchafu wote unaofanywa na hawa magaidi ndiyo maana anahisisha mambo ya utekaji yanayoendelea hapa nchini na vyama vya upinzani hususani CDM.
- Anaweza kuwa ni mtu wa system mwenye dhamana ndiyo maana hakupeleka hii clip sehemu husika kama kituo cha polisi akiogopa atatoa ushirikiano ambao utamfanya ajulikane..
- Anaweza akawa anajua ukweli wa mambo mengi sana maovu yanayotokea hapa nchini ya kihalifu na kigaidi, na kama ni mwandishi wa habari, anafaa zaidi katka upelelezi.
Rai yangu njema, nawaaomba polisi wamsake huyu mtu atawasaidia sana katika kubaini njama mbalimbali za uovu zinazoendelea hapa nchini.. Kama ni mtu mwenye nia njema atajitokeza ili awasaidie polisi katika kufahamu mambo yafuatayo.
- Hizo video nyingine za mikakati ya mauaji
- Sehemu ilitumika katika kurekodia video hizi,
- Mtu/taasisi iliyo nyuma yao katika kufadhili mpango huu,
- mbinu nyingine chafu ambazo wameshafanikisha na ambazo ziko kwenye pipeline.
Nawasilisha...