Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Mimi namshangaa sana Mwanakijiji, yeye ndiye alikuwa mstari wa mbele kumtetea Zitto akidai "mnaotaka Zitto aseme je aseme nini" na utetezi usio na kichwa wala miguu lakini walio na macho waliona sina haja ya kurudia ( rejea thread ya wakubwa na marupurupu) Ironically wazazi wa marehemu time and again wanasisitiza mapenzi wa mungu yamepita na hakuna foul play, cha kushangaza huyu Mwanakijiji analazimisha ( though by implication) kila mtu hapa akubali kuwa Nchimbi ndiye anahusika moja kwa moja na kifo cha AC. Hii ni hatari sana kwa ustawi wa familia na jamii kwa ujumla, sumu anayoeneza mwanakijiji ni mbaya sana. Mara ooh Scotland yard mara ugonjwa Waziri Kayombo kuna mkono wa Nchimbi na upuuzi kibao, bro watch out unapanda mbegu mbaya sana.
Amina kafia hospitali na sio kwa mganga wa kienyeji, standard procedure kunakuwa na postmortem na results watakuwa nazo ndugu wa marehemu ambao wanasema point blank kuwa hakuna foul play. Watu wana question mpaka uwezo wa muumba kuchukua mja wake eti haiwezekani 26 yrs old akafa kwa sukari! sijui mnapata wapi hiyo wanakufa watoto wadogo kwa sukari sembuse 26 yrs old. Mnalundika ma conspiracy theories kibao, mara genge wa wauza dawa za kulevya, mara karogwa, mara Nchimbi which is which sasa? spinning tu.
Hii tabia ya kutafuta ujiko kutoka kwa marehemu haifai jamani, kwani ule mradi wa Ukraine umeishia wapi? there is alot ujiko there, what abt petition Msolla ajiuzuru? mwacheni Amina apumzike.
Mnataka kumtumia Amina mpaka ktk umauti wake kwa manufaa yenu ya kisiasa its really sad.
JIBU LANGU KWA MASATU NA WENZAKE
Masatu kati ya watu wote wewe usijitahidi kuwa mtetezi wa Amina na kuja na madai ya kujifanya kuwa hili suala ni "so private" kwamba halistahili kuzungumzwa na ya kwamba watu hawatakiwi kuulizia habari au kutoa maoni yao. Wakati sisi wengine tumezungumza tangu dei wani kuhusu binti huyu na msimamo wote haujabadilika na kutaka haki yake iheshimiwe na uhuru wake kulindwa wewe Masatu ulikuwa wapi? Tuliposema kuwa kuna mambo ambayo ni private na hili la vijana hawa (sikumchagua Zitto peke yake kama mnavyofanya nyinyi) ni jambo la aibu na wajibu wao (kama walichodaiwa kufanya ni kweli) kwanza kabisa ni kwa familia zao na familia zao siyo wana JF! Nenda usome maandiko yangu tena ya utetezi wa Amina na Zitto nikawaambia mapema kabisa hili suala tuache kama Zitto anataka kuja kusema atakuja kusema, mkasema najaribu kuwanyamazisha watu kwamba kuna mtu ambaye ni mkubwa kuliko hii forum. Kwa ujasiri na pasipo kigugumizi mkajitokeza "kutetea heshima ya forum hii".
Ni wewe uliyekuja na kusema
Ingawa lengo lako lilikuwa ni zuri hata hivyo ulijikuta kuwa umesahau kile mlichokisimamia. Kwamba hakuna kitu ambacho ni private. Tatizo ni kuwa leo mmegundua kuwa mtu akifa kumbe anastahili heshima fulani na kuna mambo fulani ambayo ni private. Tatizo ni kuwa ni nyinyi mliovunja kanuni ya mambo binafsi na kwa uthabiti wa maneno yenu wenyewe mkadai kwa ujasiri kama kejeli kwa kauli mbiu yangu kuwa "yote yanazungumzika na kama tumewazungumza so and so basi tutazungumza mambo haya ya Zitto". Hivi kweli mnafikiri kama ni Zitto ndiyo angekuwa amekufa mngedai heshima hiyo?"chonde chonde jamani, tusiwaseme marehemu nawaomba sana".
Wakati tarehe 8 mwezi Mei niliposema hali ya Amina ni mbaya, na tukaanzisha na zile tsheti na tukasema mwacheni aseme. Kama hataki kusema asilazimishwe na kama anataka kusema asinyamazishwe wewe ulikuwa wapi? Niliposema, wamemnyang'anya simu na mawasiliano yoyote yale, na nikasema uhuru wake wa kikatiba umeingiliwa wewe ulikuwa upande gani? Au umesahau. Mshirika wa upande wako ajiitaye "Mtanzania" akaja na kusema hivi bila hata ya kufikiri ili kuniumbua kuwa mimi nasema uongo
Ni kweli unaweza kufikiri natafuta ujiko, ujiko wa nini, silipwi, sigombei Ubunge, Amina siyo ndugu yangu, vijana wa Ukraine siyo wanangu, yule mama ambaye alifiwa na kijana wa kitanzania kule Zambia nikamsaidia atafute familia yake Handeni simjui mimi… binti aliyebakwa Dar na mbakaji kuachiliwa hadi nilipoingilia kati (of course u didn't know that) ni ujiko gani ninaupata mimi? Katika haya yote wewe ulikuwa wapi?"Mwanakijiji,
Amina mbona yuko bungeni, je kazuiwa na nani? Ukitaka namba yake omba
na wana JF watakupatia. Huenda namba uliyokuwa nayo kabadilisha kwasababu hataki muendelee kumsumbua. wabunge wengi wanabadlisha namba zao kila mwezi." Angalia Ukurasa wa 58 kwenye "Kashfa ya Zitto & Chifupa" Leo Amina yuko wapi?
Kada Mpinzani akajenga hoja kunionesha kuwa mada yangu "silencing of an MP" haikuwa na msingi wowote na kusema hivi kwa mbwembwe zote za ajuaye
Nikamjibu Kada Mpinzani kwa hekima ya mvi zangu:"halafu hiyo sidhani kabisa kama ndio ishu yenyewe, yaani kumnyamazisha, kama kweli wangetaka kumnyamazisha sidhani hata kama huo ubunge angeukwaa, mie nadhani anasubiri moto uliowaka upoe na atoke upya lakini hilo la kusema amenyamazishwa nalipinga, umeenda mbali mno kufananisha na anna nicole smith ( kama alivyosema glenn beck mwenyewe ) kama ni hivyo, basi kila kitu tunaweza kufananisha na marehemu anna nicole smith, both kwa wanawake na wanaume !
chifupa atatoka tu upya nani aliyekwambia kanyamazishwa na kama ikitokea hiyo uliyosema yote ni kazi ya mola kwani mimi na wewe pia vile vile wakati wetu ukiwadia tutarudisha namba !!"
Angalia Ukurasa wa 57 wa "Kashfa""Kadampinzani... haya mimi nimeshanyanyua bendera ya tahadhari. Anachofanyiwa Amina kimuudhi Mtanzania yeyote yule na kutaka kama ni mgonjwa aruhusiwe kumuona daktari, kama anataka kukutana na mtu yeyote au kuzungumza na mtu yeyote awe huru kufanya hivyo. Na kama hataki kuzungumza basi aachwe aendelee na mambo yake, mimi siko kwenye watu watakao'mlazimisha azungumzie kilichojiri" kwani kashema hadharani kwamba hakukuwa na kitu hicho na ninaamini. Hilo jingine la njama za kiongozi wa CCM hilo akitaka kulizungumzia basi aachwe asipotaka basi aachwe aseme kabadili mawazo. Lakini kitendo cha kumuwekea minders, kuingilia mawasiliano yake binafsi ni kitendo kisichokubalika kabisa."
Leo nadaiwa kutenda dhambi kwa kusaidia mwili wa kijana wa kitanzania kurudishwa nyumbani baada ya kuuawa Brazili, linashikiliwa hilo kwenye shingo yangu kama nira, ati naambiwa ni kosa la milele nililolifanya kwa vile huyo kijana wanadai alikuwa ni muuza madawa. Nakubali kuwajibika kwa hilo. Ninawapenda watanzania wenzangu na sitawahukumu kiurahisi hivyo. Nikuambie mapema, leo Nchimbi akipatikana na madhara yoyote tutapiga kelele ukweli ujulikane kwani hatuko hapa kwa kutafuta kisasi. Soma makala yangu J'tatu ambapo nimemtetea Nchimbi. Wakati wewe na wenzako mnaangalia kila jambo nisemalo kwa mwanga wa "Uchadema na UCCM" mimi hilo sina, kwani maslahi pekee ni ya Tanzania na kiapo pekee nilichowahi kula ni cha kulinda Katiba ya Tanzania! Leo mtanzania yeyote akipata matatizo mahali popote duniani NITATUMIA uwezo wangu wote kumsaidia, nikishindwa nitatafuta watu wengine wasaidie! Hata watu tunaobishana hapa, sina kinyongo na mtu hata mmoja na wakitaka msaada wangu nitawapa 100% licha ya kwamba wengine watasema kwanini umsaidie yule?
Masatu, mmevunja principle moja kubwa na hiyo principle imeanza kuwavunja. Nakumbuka nilivyowasihi sana kwamba jamani tukubaliane kuna mambo private na mengine tuyaache hivyo. Na nikawahakikishia kuwa mkikubali kwamba hakuna mambo private kitakuja kuwageuka hamkuelewa ninazungumzia nini… Leo mmegeuka kama makamanda wa Privacy.. kwamba kwa vile sasa ndugu yetu ni marehemu basi kisisemwe kitu chochote, kwamba wakati sisi wengine tunapigia kelele tukaonekana wehu na watuwa kutafuta misifa leo mmejipanga mistari "kumtetea" Amina! Mambo mengine yanastahili kuwa na haya ngaa kidogo. Msimamo wangu wa kumtetea Amina tangu akiwa hai haujabadilika, haya ya kutunza usiri wa mambo ninayoyajua bado ipo, na kwamba kama Zitto anataka kusema jambo anayo haki hiyo na asipotaka nitaitetea haki hiyo mpaka kifo. Isipokuwa alazimishwe na mahakama vinginevyo hakuna cha kumlazimisha mtu kusema. Chombo pekee ambacho raia wanauwezo na haki ya kukilazimisha kufanya ni serikali yao.
Watu wanadai ati natafuta ujiko. Ujiko wa nini kwenye kifo cha mtoto wa watu? Furaha gani mimi ninapata baada ya kupiga kelele zote hizi? Ungejua jinsi moyo wangu ulivyoumia, ungejua jinsi undumbula gwangu ulivyochubuka, ungejuwa motema wane ulivyobubujika machozi, ungejua umtima wanene ulivyojisikia majonzi ungeelewa. Machozi yangu hayana ujiko! Naelewa mmezoea viongozi wababaishaji wanaofanya jambo ili wanufaike kwa namna fulani, naelewa mmezoea kupigwa porojo na ni vigumu kumpata mtu ambaye "what is you see is what you get". Najua watanzania tumezoea mazingaombwe na viini macho.... friends, what you see with me is what you get... what I'm saying online, is what I say in real life! Of course, I have my shortcomings and udhaifu...and believe me I have plenty.. ila kutafuta haki, usawa, kuwajibika viongozi nitasimama hata kama nitasimama peke yangu na kuwa kituko!
Masatu na wenzako, Mmevunja principle ya mambo binafsi baada ya kuhakikisha mmeshusha ile alama ya heshima na mambo binafsi chini mno, na kufikia kufikia kuwaita watu wazinzi, wezi wa wake za watu, wakatajwa mama zao hapa kwa kashfa n.k na nakumbuka nilikuuliza Masatu unafikiri vipi kuhusu mama wa Zitto kuletwa hapa na kuvuliwa nguo hadharani na mmoja wa mashabiki wako ukajibu "no comment"! Leo hii una ujasiri wa kuja kunishambulia hadharani hivi ati umegeuka kuwa mtetezi wa Amina na privacy! Give me a break! Watetezi wa Amina wapo na wanajulikana na hawahitaji sifa za mtu. Na jumatatu, tutaanza moja na tutaendelea jumanne. Kama kwa maneno yenu na kutumia msiba kuwa mtatunyamazisha hapa, ati kwa vile leo mko wengi, na ya kwamba mmeleta balance of power mmekosea. Hatunyamazi.
Nimewakalia kimya kwa sababu najua watu ni wasahaulifu, lakini mashambulizi yako hapo juu sikuweza kuyanyamazia, na you picked on a wrong dude… siogopi, sihofii, siabudu sanamu ya mwanadamu yeyote, sipendelei, sipendi.. na simama kwa upande wa wale wanaohitaji sauti. Kama unafikiri mkinifanya mimi kuwa mada itanifanya kwa namna fulani nipatwe na kigugumizi, wrong! never been scared, not today.. not ever! What is the worst that can happen to me? ABSOLUTELY NOTHING.
I'M OUT.. MEET ME MONDAY FOR THE FIRST DOSE OF REALITY