Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,960
2,000
Kada, niwie radhi na nimesahihisha pale. I was a little bit fired up kutokana na post ya Masatu...no hard feelings.
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,156
2,000
kuna tuhuma kuwa mh zitto hakuenda kuuaga mwili wa marehemu mh chifupa

hali mabayo inaibua masuali mengi, na kuuliza huo ukaribu ambao yeye amejisifia kuwa alikuwa nao.pia inatoa maswali kuwa zitto si rafiki wa kweli maana kwenye shida yeye hazuki.

yule ambaye anatuhumiwa na hata yeye mwenyewe marehemu mh nchimbi ameshiriki kikamilifu.

nnaomba wanaojua hili suali watukwekee bayana au ndio protokoli imemzuia???????
 

Mr. Clean

Senior Member
Aug 7, 2006
195
225
kuna tuhuma kuwa mh zitto hakuenda kuuaga mwili wa marehemu mh chifupa

hali mabayo inaibua masuali mengi, na kuuliza huo ukaribu ambao yeye amejisifia kuwa alikuwa nao.pia inatoa maswali kuwa zitto si rafiki wa kweli maana kwenye shida yeye hazuki.

yule ambaye anatuhumiwa na hata yeye mwenyewe marehemu mh nchimbi ameshiriki kikamilifu.

nnaomba wanaojua hili suali watukwekee bayana au ndio protokoli imemzuia???????

Mtumwitu,

Sio kwamba namtetea Zitto, ila yaonesha swala hili lajieleza toka bungeni:-
Spika alitangaza majina ya wabunge walioteuliwa kuliwakilisha bunge, na jina la Nchimbi likiwemo, isitoshe yeye ndo alikuwa mwenyekiti wamarehemu AC.

Jina la Zitto halikuwemo, kwa upande wa wawakilishi wapinzani. Hivyo kwenda kuaga mwili,angekuwa ametoroka bungeni. KOSA!.
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,448
2,000
Mtumwitu,

Swali lako linaweza kuwa na majibu mengi sana ambayo yote yanaweza kuwa sahihi. Jibu jepesi ni kuwa Zitto hakuwa amechaguliwa na spika kuwa mmoja wa wawakilishi wa bunge kwenye msiba ule, wakati huyu Nchimbi alikuwa ameteuliwa.

Unaweza kuuliza tena kuwa kwa nini asingelazimisha awe mmoja wao au kwa nini hakuja kama mwombolezaji binafsi. Jibu la swali hilo linategemea na taratibu za bunge kama inawezekana mbunge kughaili maagizo ya spika, na vile vile huenda kiungwana pia isiwe vizuri kujionyesha kwa mme wa Marehemu Amina ambaye alikuwa ameshamtuhumu Zitto kutembea na mke wake ambaye ndiye aliyefariki na walikuwa hawjamaliza tofauti hizo; siyo vizuri kuongeza chumvi juu ya jeraha. Kumbuka kuomboleza siyo lazima mtu ajionyeshe msibani; kuna wanoajionyesha lakini siyo waombolezaji halisi.
 

omarilyas

JF-Expert Member
Jan 24, 2007
2,130
1,195
Ni amina pekee ndiye anayejua nani alikuwa rafiki wa kweli.....kama kwenda msibani hata wale waliomkebehi/kumtisha siku ile aliposimama kuongelea madawa kuwa anarusha mawe akiwa ndani ya nyumba ya vioo walikwenda kumuaga.....
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,282
1,195
Mwanakijiji,

Unashangaza na majibu yako yanayojichanganya na yenye jazba nyingi.

U have tried ( in vain ) so hard to manupulate the whole saga. Kule kwenye thread ya marupurupu umekuwa mtetezi wa "mambo binafsi" in favour of Zitto. Huku ( kwenye tanzia ya Amina)umemhukumu na kumtia hatiani Nchimbi kwamba anahusika na kifo cha Amina. Familia ya marehemu wanasema hakuna foul play. Cha kushangaza wewe mtetezi wa "mambo binafsi" unabadilisha joho na kushikia bango waitwe Scotland yard. Tazama ugeu geu wako hapa unataka taarifa gani zaidi ya wazazi wa marehemu ambao ndio wenye postmortem report? kwanini unashinikiza uchunguzi zaidi? je sasa ufuasi wako wa "mambo binafsi" ushauacha? Tazama u flip flop wako chini hapa;

Mwanakijiji
Zitto, hili suala la binafsi kama utalizungumzia utalizungumzia on your own personal terms siyo kwa kufurahisha JF au watu wachache wanaotaka kuridhisha udadisi wao tu. NI kweli jambo hili lilivuta hisia za watu wengi na mambo ya kitaifa n.k. Kama tulivyosema awali kama CCM na wahusika upande huo hawataki kuzungumzia kwanini tukulazimishe wewe ulizungumzie ilimradi tu tujue "nini kilitokea".
Leo unadai kuwa ulikuwa mtetezi wa Amina since day one, unasahau huko nyuma ni wewe uliesema kuwa katika masuala ambayo huyapi umuhimu ni hili la Zitto na Amina!

Mwanakijiji
Zitto akiamua kuzungumzia sasa hivi sina tatizo ni uamuzi wake, akitaka kuzungumzia mwezi ujao sawa sina tatizo, akigoma kulizungumzia kabisa sina tatizo...ni uamuzi wake! kati ya vitu vilivyoko mawazoni mwangu suala la Amina na Zitto liko mbali kweli!

Mwanakijiji unadai mimi nimevunja principle ya utetezi wa mambo binafsi, si kweli, ninachotetea hapa ni upotoshaji na ushabiki unaouleta kupitia mgongo wa marehemu, wahusika wanasema hakuna mkono wa mtu kwenye msiba ule wewe na genge lako mnang'ang'ania Nchimbi anahusika. Hicho ndicho ninachokipinga inavyoonyesha una ajenda yako ya siri. Kule kwenye marurupu umekuwa ukidai forcefully kuwa hakuna majibu atakayotoa Zitto yatatosheleza bila ya kuongeza maswali mengine, well sasa huku familia ishatupa majibu na inavyoelekea hakutakuwa na majibu yatakayo kutosheleza!

Mwanakijiji
Nilishasema tangu mwanzo hakuna jibu litakaloridhisha na hakuna swali litakaloachwa kuulizwa! Mmemuuliza Zitto kawajibu. Haitoshi. Mmeyaleta ya mama yake haitoshi. Hamuwezi kukubali jibu lolote isipokuwa "ndiyo mimi na Amina tulikuwa na uhusiano wa kimapenzi na ulikuwa mzuri kweli". Akijibu hivyo haina maana itakuwa mwisho maswali yatakuja "kwanini uvunje ndoa ya watu, wewe kama kiongozi.. tukuamini vipi na wake zetu? vipi mabinti zetu na dada zetu, unawezaje kukaa Bungeni ilhali hivi na vile".
Well, yaonyesha pia hakutakuwa na majibu ya kukutosholeza Mwanakijiji


Umedai umeandika makala ya kumtetea Nchimbi itatoka J3. Hiki ni kiroja kingine wakati huo huo unadai kuna mkono wa Nchimbi kwenye ugonjwa wa Kayombo.

KLH News! Kayombo apelekwa India kwa Matibabu!
Bila ya shaka wote mmesikia kuwa Mbunge wa CCM na Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji alikuwa amelazwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Habari ambazo zimenifikia ni kuwa Mheshimiwa huyo amesafirishwa kupelekwa India kwa matibabu zaidi. Bw. Kayombo kwa wale wanaokumbuka alipata nafasi ya kuzungumza nami kuhusu kukataa kwa serikali kuleta mikataba Bungeni. Katika uchaguzi ujao wa NEC Bw. Kayombo anagombea kuingia NEC kupitia mkoa wa Ruvuma. Nafasi hiyo ya NEC inagombewa pia na Naibu Waziri wa Michezo na Utamaduni Bw. Emmanuel Nchimbi.
Ukazidi kumsakama

Mwanakijiji
Mbunge mmoja kijana wa CCM aliyekuwa uwanja wa ndege kumsindikiza Marehemu alisikika akizungumzia taarifa za kupelekwa Kayombo India akisema "heri yangu mimi sigombei UNEC wowote".
Mwanakijiji
Mtanzania, ningekuwa sijatenda haki kama nisingejaribu kuonesha huo uhusiano hasa wakati CCM inaelekea kwenye uchaguzi.
Unadai utakuwa hujatenda "haki" yaani kumzushia mtu ni kutenda haki!

Ninachotaka kusisitiza hapa sio kufunga mjadala wa Amina bali ni kuheshimu maamuzi wa wana familia. Inaelekea wewe Mwanakijiji ndio una uchungu sana na Amina kuliko baba yake sio? Kwanini hutaki kuheshimu maamuzi ya wanandugu?

Mwanakijiji unataka kuburuza watu wote tuamini kuwa kifo cha Amina kuna mkono wa mtu, sorry hilo wengine hatukubaliani nalo.
 

barabaraya18

Senior Member
Sep 18, 2006
106
0
mie nilimshangaa huyu mwanakijiji kujidai anamjua sana AMINA halafu information ndogo kama dhehebu la AMINA alikuwa hajui.Japo ni mahiri wa kuandika lakini kama yuko careless na data zake inamaana kuwa work done nzima yake ni ZERO! Utamiss vipi important info kama hiyo?
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,065
2,000
Basi sasa imetosha. Kama wanafamilia ya Amina wameridhika na matokeo ya autoposy sisi wengine hatuna budi kuacha kung'ang'ania uchunguzi zaidi hata kama hatuamini au hatujaridhishwa na sababu iliyotolewa/ zilizotolewa ya/za kifo chake. Tumwache marehemu apumzike na familia yake ipate muda wa kuombeleza na hatimaye kurudia hali yao ya kawaida. Nasisitiza tena: familia yake ndio yenye uamuzi wa mwisho na ni vyema uamuzi wao ukaheshimiwa.
 

Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,232
1,225
Mwanakijiji,

Nafikiri huna haja ya kujibu further, level of mis-understanding the hoja is quite high here...........you know what i mean!!?
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,065
2,000
Hebu acha kujifanya una akili kupita wengine humu...ebo!!! Eti level of misunderstanding the hoja is quite high....misunderstanding my .....(excuse my french)....where is the misunderstanding....pinpoint it for me, please.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,960
2,000
Nyani, familia ya yule kijana aliyepigwa risasi na Dito ilisema ni mapenzi ya Mungu... kwanini Dito na kesi ya kujibu?
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,448
2,000
mie nilimshangaa huyu mwanakijiji kujidai anamjua sana AMINA halafu information ndogo kama dhehebu la AMINA alikuwa hajui.
Katika misingi tuliyokulia ya utaifa hapa Tanzania, huwa hatutafuti details za madhehebu, makabila au koo za watu. Kwa hiyo kumjua mtu siyo lazima ujue dhehebu lake, unaweza ukajua kuwa ni mkristo au ni mwislamu lakini usijue zaidi ya hapo. Vile vile unaweza kujua kuwa anatoka mkoa wa Mbeya lakini usijue details zaidi ya hapo.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,065
2,000
Nyani, familia ya yule kijana aliyepigwa risasi na Dito ilisema ni mapenzi ya Mungu... kwanini Dito na kesi ya kujibu?
Duh...ebwana eeh!!! unasema kweli walisema kijana wao kutwangwa risasi at point blank range ni mapenzi ya mungu? Ni nani aliyetoa kauli hiyo...? Kwa kweli hiyo sikumbuki...

Lakini hata kama walisema hivyo...sidhani kama walimaanisha Ditto asichukuliwe hatua...kwa sababu tendo alilofanya Ditto kwa kweli halina ubishi wowote.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,960
2,000
I give up... haya "mapenzi ya Mungu" yatatuletea matatizo kweli. Ni bora watu wote wanakufa kuanzia sasa TAnzania wazazi waliofiwa waseme ni "mapenzi ya Mungu" polisi wasichunguze, watu wasiulize, tuzike na yaishe!
 

omarilyas

JF-Expert Member
Jan 24, 2007
2,130
1,195
Katika misingi tuliyokulia ya utaifa hapa Tanzania, huwa hatutafuti details za madhehebu, makabila au koo za watu. Kwa hiyo kumjua mtu siyo lazima ujue dhehebu lake, unaweza ukajua kuwa ni mkristo au ni mwislamu lakini usijue zaidi ya hapo. Vile vile unaweza kujua kuwa anatoka mkoa wa Mbeya lakini usijue details zaidi ya hapo.
Unfortunately misingi ya utaifa huo tumeshaivunjavunja kitambo kidogo na sasa sio tu huwa tunapendelea kutafuta details kisirisiri lakini tumefikia kuyatafuta na kuyajadili hayo kwa uwazi kabisa bila hata aibu..


Tanzanianjema
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom