Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,185
2,000
Tanzania Njema.

Hata mtililiko wa mada umevurugwa heading inasema Kashfa Nzito kwa Chifupa na Zito. jee Zitto kafanya kitendo cha kashfa na maiti au marehemu? kichwa cha habari hakimvutii mtu mgeni JF kuisoma. pili itampa taabu msomaji mgeni kuelewa somo lilivyounganishwa.

Adm.

Naona umevurunda sana. kichwa cha habari hakiko sawa na kuna maneno mtu unaweza kuyasema akiwa hai na mara akifa huwezi kuyasema. mtoto wa Amina au kaka yake au mdogo wake apite JF katika kipindi hiki akute kichwa cha habari hapo juu " Kashfa nzito Amina na Zito" watajisikiaje? hatuwatendei haki ndugu wa Amina, marafiki na wapenzi.

Naomba irudishwe kama mwanzo au ifungwe, heading yake haiuwiani na maudhui ya michango ya huku mbeleni. sisi sote tutakufa si vizuri kuwabeza maiti.

Nakubaliana nawe kabisa kuwa thread hii sasa ifungwe. Thread hii ilianza wakati Amina akiwa hai; baadhi ya yaliyoandikwa wakati huo hayastahili kusomeka tena wakati huu baada ya kifo chake. Kama kuna mtu anayetaka kuendelea na mjadala kuhusu vipengele fulani vilivyoko kwenye thread hii, basi ifunguliwe thread nyingine mpya kabisa katika mazingira ya sasa ambapo tunajua kuwa Amina keshafariki.
 
B

Brutus

Guest
Guys!
We njoo umnyofoe roho mtoto wangu uone kama hiyo propaganda ya mapenzi ya Mungu itafanya kazi!
Yaani lazima nikunyonyoe!

Huyu mdingi naona ana-play dirty game na roho ya mwanae... "pensheni ya uzeeni'!
Sounds like mwanae alikuwa mtaji wake kisiasa!
Atashinda uchaguzi NEC, atabaki Headquarter ya CCM kama kigogo.. mafao na marupurupu ya kumwaga!
 

mtalii

JF-Expert Member
Dec 14, 2006
286
0
Mtalii,

Unajua hizi njama za Mafia yenu haziwezi kufanya kazi kwangu. Niko hatua moja mbele yenu na hiyo issue ya Zitto hainisumbui kabisa!.... Chadema imewakalia kooni sana mjomba...kiasi kwamba mnashindwa hata kufikiri.

Nitakwambia kitu kimoja uncle matusi yote mnayomrushia Zitto yanazidi kumsumbua marehemu kwa sababu tamko lenu lina mhukumu zaidi marehemu.

Nitakubali maneno yenu ikiwa mtakuwa wazi na kusema Marehemu alikuwa mzinifu na ndio kumemponza!...hapa sintatafuta jibu zaidi.
Mkandara.

Huwezi kuwa na beef na maiti, na kuitumia maiti kama mtaji wa kisiasa. wapi nimemtukana Zitto? umewataja Nchimbi na Mpakanjia kwenye kadhia hii lazima na Zitto atajwe. hao watatu ndio wanajua undani wa suala la marehemu, huwezi kumnyofoa Zito kama unavyotaka na wenzako.

kumuita Amina maneno hayo uliyosema juu kuwa yamemponza ni unyama na ukosefu wa adabu. huwezi kubishana na maiti. mtu akifa kama una beef nae unaziacha.

wewe umemchachamalia binti wa watu. alikokwenda AMINA kila mtu atakwenda usizuzuke na JF kiasi cha kusahau ubinadamu. huo uzinifu wa Amina uliushuhudia?

jamani tuwafanyie heshima maiti. mafundisho ya vitabu yanasema anapozikwa maiti basi huku nyuma yasemwe mema yake.
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,185
2,000
Barabaraya18 alipoulizwa na Mwanakijiji kwa mara ya kwanza maana ya neno "Wagalla" kama halikuwa na maana ya grupu la watu wenye dini tofauti na ya barabaraya18, yeye mwenyewe alijibu kuwa ni "Wagalla" ni viongozi wa CCM na serikali. Sasa anapomsema Mkandara (kwa vile ndiye anyebishiwa na Mtalii) kuwa ni Mgalla wakati akijua fika kuwa huyu siyo kiongozi wa CCM na serikali, kweli inaashiria kuwa maana ya "Wagalla" aliyotuambia huko nyuma ilikuwa ni uwongo, na ninaanza kuamini hisia za mwanakijiji kuwa huyu jamaa ana ubaguzi wa kidini.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,588
2,000
Labda amepanua maana ya neno na sasa linajumuisha pia wapinzani na viongozi wao...

Kwani ule msamiati wa Ungunge una maana ya vibosile wa chama tawala tu?
 

barabaraya18

Senior Member
Sep 18, 2006
106
0
Barabaraya18 alipoulizwa na Mwanakijiji kwa mara ya kwanza maana ya neno "Wagalla" kama halikuwa na maana ya grupu la watu wenye dini tofauti na ya barabaraya18, yeye mwenyewe alijibu kuwa ni "Wagalla" ni viongozi wa CCM na serikali. Sasa anapomsema Mkandara (kwa vile ndiye anyebishiwa na Mtalii) kuwa ni Mgalla wakati akijua fika kuwa huyu siyo kiongozi wa CCM na serikali, kweli inaashiria kuwa maana ya "Wagalla" aliyotuambia huko nyuma ilikuwa ni uwongo, na ninaanza kuamini hisia za mwanakijiji kuwa huyu jamaa ana ubaguzi wa kidini.

HEBU NAOMBA UILETE TAFSIRI NILIYOMPA MWANAKIJIJI kisha tuendelee, in other words lete hiyo post niliyomjibu MWANAKIJIJI
 

mtalii

JF-Expert Member
Dec 14, 2006
286
0
my dear masatu, tukikubali principle kuwa "wazazi wakisema mapenzi ya Mungu basi yote yaishe" tutakuwa kwenye matatizo makubwa kweli. Kuna wakati ambapo Mapenzi ya Mungu na ya mwanadamu yanakuwa yameingiliana kweli kiasi cha kwamba kuyatofautisha inakuwa kazi kidogo. Nikiri hapa kuwa endapo uchunguzi huru utafanyika na pasipo shaka matokeo yakasema hakukuwa na jambo lolote la kisayansi linaloelezea kifo chake au any criminial negligence or acts... NITAKUWA wa kwanza kutaka tukubali uamuzi huo na hapo Mapenzi ya Mungu yatakuwa vindicated.

Naomba nirudie kusema kuwa sisemi kuwa Amina amekufa kutokana na njama za watu fulani, nasema kuna minong'ono na tetesi nyingi mtaani ambazo hadi majina ya watu yanatajwa. Hili si haki kwa mtu yule atajwaye na pia kutokuyapa uzito unaostahili hasa pale kiongozi wa kitaifa anapokufa katika usiri na utata, ni kuchochea minong'ono hiyo.
Mwanakijiji.

Tetesi nyingi mtaani na minong'ono Mkuu usiishi kwa tetesi. hadi Marekani kuna tetesi mitaani?
 

barabaraya18

Senior Member
Sep 18, 2006
106
0
MTALII


Huyo Mwanakijiji nilimshusha HADHi pale alipojidai kutaka kuingilia kujua waislam wanazikana vipi.Sasa nilitegemea mtu kama huyu angekaa pembeni kisha asome ili aelimike lakini wapi! Jamaa anapenda ATTENTION kuliko hata huyo PARIS HILTON. Hakukuwa na sababu ya yeye kuja kuniambia kuwa nimekuwa mdini kwa kuposti picha za masista kwenye msiba wa Amina.

Halafu mbaya zaidi huyu Mwanakijiji kwa jinsi alivyokuwa na moyo wa kumsaidia AMINA CHIFUPA na ile FREE AMINA campaign at least ungefikiria angeweza kufanya research akajua kama amina HAKUWA MKE wa MEDI MPAKANJI kiislam, na mbaya zaidi MWANAKIJIJI aliboa zaidi liposhindwa hata kujua kuwa AMINA alikuwa dhehebu gani, sasa najiuliza hivi hizo pesa zote anazolipwa kashindwa kuajiri RESEARCHER kwa kumfanyia background info ya MINA CHIFUPA?

Mimi based on those na mengineyo siku za nyuma nina suspect kuwa Mwanakiji atakuwa na ATTENTION DEFICIT DISORDER na ni bora anyamaze kwa asiyo yajua kuliko KUPAYUKA na kujiharibia hadhi yake
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,185
2,000
KWA NINI TUANDIKIE MATE WAKATI WINO UPO? LETE HIYO POST NILIYOMJIBU MWANAKIJIJI
Barabaraya18,

Kumbe wewe kigeugeu kweli aisee; hivi kweli unapoandika huwa unajua unachoandika? Tulianzia kwenye talaka tatu ukasema upewe reference, tukakupa ukakimbia. Sasa unakataa kukubali uliyoandika mwenyewe eti hadi tukupe reference. Siyo wewe ulieandika hivi?
waGALA ni watu wa CCM na serikali ambao wanacontol BAKWATA na SHEKHE MKUU
halafu leo unadai hivi:

WAGALLA = ni watu viongozi wa serikali na baadhi ya viongozi upinzania ambao wanacontrol serikali
Huoni kabisa kuwa unatudanganya hapa. Kama una maana yako nyingine moyoni iwe njema au mbaya sina haja ya kuijua lakini usitufanye kama watoto wadogo hapa.

Nimeongezea sehemu hii makusudi: Swala la kujua dhehebu la mtu siyo muhimu kabisa katika jamii yetu. Tunaweza kujua kuwa ni mwislamu au mkiristo lakini hatuna haja ya kujua dhehebu ndani ya uislamu au ukristo wa mtu. Ni kama ambavyo huwa hatuhitaji kujua makabila ya watu.
 

The Invincible

JF-Expert Member
May 6, 2006
5,736
2,000
MTALII

Mimi based on those na mengineyo siku za nyuma nina suspect kuwa Mwanakiji atakuwa na ATTENTION DEFICIT DISORDER na ni bora anyamaze kwa asiyo yajua kuliko KUPAYUKA na kujiharibia hadhi yake
Well,
Labda Mwanakijiji anajiharibia hadhi kwako. kwa upande wangu (na labda wengine) Mzee Mwanakijiji is quite somebody (his contributions).
 

mtalii

JF-Expert Member
Dec 14, 2006
286
0
Barabaraya18 alipoulizwa na Mwanakijiji kwa mara ya kwanza maana ya neno "Wagalla" kama halikuwa na maana ya grupu la watu wenye dini tofauti na ya barabaraya18, yeye mwenyewe alijibu kuwa ni "Wagalla" ni viongozi wa CCM na serikali. Sasa anapomsema Mkandara (kwa vile ndiye anyebishiwa na Mtalii) kuwa ni Mgalla wakati akijua fika kuwa huyu siyo kiongozi wa CCM na serikali, kweli inaashiria kuwa maana ya "Wagalla" aliyotuambia huko nyuma ilikuwa ni uwongo, na ninaanza kuamini hisia za mwanakijiji kuwa huyu jamaa ana ubaguzi wa kidini.
Ubaguzi wa kidini unakujaje hapa? kuna makundi mawili hapa. la kwanza kuna Mpakanjia-muislam na Nchimbi-mkristu. halafu kundi la pili yuko Zitto Kabwe-muislam. wapo wana jf kila upande issue ya udini iko wapi hapa? au Zitto anaonewa kwa dini yake kwa vile yuko peke yake.
 

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,748
0
invinsibo hukutakiwa kuingilia huu mjadala ilihali wewe ndio ( cheo chako humu JF ) ! dont choose sides, wee fuata tu flow ya watu. mie nadhani kila mtu na michango yao naipa kipaumbele.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom