Mugongo Mugongo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2006
- 223
- 8

Jana gazeti la Majira limeripoti kwamba Bwana Mohammed Mpakanjia, mkazi wa Dar es Salaam, amemuandikia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mh. Samuel Sitta, kumuarifu kwamba amemtaliki mkewe, Mhe. Amina Mpakanjia, kwasababu ya kufanya mapenzi nje ya ndoa (ugoni) na Mhe. Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini. Katika barua hiyo, ambayo imenakiliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Bwana Mpakanjia amemuomba Spika Sitta amuonye Mhe. Kabwe kwa kitendo chake hicho.
Gazeti la leo la Tanzania Daima linaripoti kwamba Mhe. Amina Chifupa atafanya mkutano na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo kufafanua hili jambo ingawa amethibitisha kwamba ni kweli mumewe amemtaliki toka tarehe 3 Mei mwaka huu. Hata hivyo, Mhe. Chifupa na Mhe. Kabwe wote wanadai hizi ni njama za wana-CCM. Mhe. Kabwe anadai yeye ana uhusiano mzuri wa "kikazi" na Amina Chifupa na kwamba anamheshimu kama "mtu makini". These are his quotes.
Sasa, Sitta atachukua hatua gani? Je, atalipeleka kwenye Kamati ya Maadili kama ambavyo alipekela malalamiko ya Bwana Mengi? Makamba atachukua hatua gani? Je, the Zitto myth ndio inaanza kuporomoka? Je, kama ukila uroda mke wa mtu na ukakamatwa una haki ya kusingizia ni njama za maadui wako wa kisiasa? Je, maadui zako wa kisiasa wakiona udhaifu wako ni kupenda uroda (hasa kwa wake za watu), je wanaruhusiwa kuu-expose? Some of these are hypothetical questions.