Ndoto ya Amina Chifupa ilivyoyeyuka

Ndoto ya Amina Chifupa ilivyoyeyuka

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,069
Reaction score
34,839
1780593686800.png

Mwezi huu wa Juni, Tanzania inatimiza miaka 19 tangu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM, Amina Chifupa Mpakanjia, aliyefariki tarehe 26 Juni 2007 akiwa na umri wa miaka 26. Kila mwaka ifikapo tarehe 26 Juni, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya, siku ambayo pia huwakumbusha Watanzania wengi juu ya maisha, harakati na kifo cha mwanasiasa huyu kijana aliyepaza sauti dhidi ya janga la mihadarati.

KAMWE hakuna binadamu atakayeishi duniani milele. Kila nafsi lazima ionje mauti kwa wakati wake. Aliyekuwa mwanamuziki mahiri nchini, marehemu Ramadhan Ongala maarufu kama Dr. Remmy, aliwahi kutunga wimbo maarufu uitwao Siku ya Kufa. Ndani ya wimbo huo aliimba, "Siku ya kufa wandugu kwaheri, siku ya kufa nyama yote ya udongo, siku ya kufa ujana wote unakwisha, siku ya kufa akili yote inapotea." Maneno hayo yanaonesha ukweli mchungu wa maisha ya mwanadamu hapa duniani.

Jumanne ya tarehe 26 Juni 2007, Tanzania iligubikwa na simanzi kubwa baada ya kutangazwa kifo cha Amina Chifupa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam. Ilikuwa ni huzuni kila kona ya nchi. Wengi walishindwa kuamini kuwa yule mwanadada shupavu aliyekuwa akisimama kidete kupinga biashara ya dawa za kulevya alikuwa ameondoka duniani akiwa na umri wa miaka 26 pekee.

Amina Chifupa alizaliwa tarehe 20 Mei 1981 jijini Dar es Salaam. Elimu yake ya msingi aliipata katika Shule ya Msingi Ushindi kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu. Baadaye alihamia Shule ya Sekondari Makongo ambako alihitimu elimu ya kidato cha sita mwaka 2001. Baada ya hapo alijiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari cha Royal na kufuzu Diploma ya Uandishi wa Habari.

Kabla hata hajamaliza masomo yake, Amina alianza kujijengea jina kubwa kupitia tasnia ya habari. Mwaka 1999 alianza kazi ya utangazaji katika kituo cha Clouds FM. Sauti yake nyororo, uchangamfu wake na uwezo wake mkubwa wa kuwasiliana na vijana ulimfanya kuwa mmoja wa watangazaji waliopendwa zaidi nchini. Umaarufu wake uliongezeka kwa kasi na jina lake likaanza kujulikana kila kona ya Tanzania.

Mbali na utangazaji, Amina alikuwa mwanachama mahiri wa CCM. Alishika nafasi mbalimbali ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Aliwahi kuwa Kamanda wa UVCCM katika Tawi la Mikocheni A, Katibu wa Kamati ya Uchumi ya UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Mama Mlezi wa UVCCM na UWT katika matawi mbalimbali.

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Amina aliteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia kundi la vijana wa CCM. Akiwa Bungeni, alijitofautisha na wabunge wengi kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja na kuzisimamia bila woga. Ingawa alikuwa mdogo kwa umri kuliko wengi wa wenzake, hakusita kuzungumza mambo aliyoyaamini kuwa ni muhimu kwa taifa.

Jambo lililompa umaarufu mkubwa zaidi lilikuwa ni vita yake dhidi ya biashara ya dawa za kulevya. Katika kipindi ambacho wengi waliogopa kuzungumzia suala hilo hadharani, Amina alisimama kidete na kutangaza kuwa alikuwa na taarifa kuhusu baadhi ya watu waliokuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu. Alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa hata kama mtu wa karibu naye angehusika katika biashara hiyo, asingesita kumtaja hadharani.

Amina hakumung'unya maneno. Alijitokeza mara nyingi hadharani kuzungumzia athari za mihadarati kwa vijana na kusisitiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya wanaohusika. Harakati zake zilimfanya kuwa mmoja wa viongozi vijana waliovutia mjadala mkubwa nchini katika kipindi hicho.

Mwaka 2007 hali yake ya afya ilianza kuzorota. Kwa mara ya kwanza taarifa za kuugua kwake zilitangazwa Bungeni na Spika wa wakati huo, Samuel Sitta, ambaye aliwaomba wabunge na Watanzania kwa ujumla kumuombea apone. Wakati huo kulikuwa na taarifa nyingi zilizokuwa zikisambaa kuhusu maisha yake binafsi na hali yake ya kiafya, jambo lililozua mijadala mbalimbali ndani na nje ya Bunge.
Kadiri siku zilivyopita hali yake iliendelea kuwa mbaya zaidi hadi ilipofika tarehe 26 Juni 2007, taifa likapokea habari iliyowashtua wengi kuwa Amina Chifupa amefariki dunia katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Kifo chake kilizua mjadala mkubwa nchini. Wapo waliokihusisha na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikimkabili, huku wengine wakisisitiza taarifa rasmi za kitabibu zilizotolewa wakati huo. Hata hivyo, jambo ambalo halina ubishi ni kwamba kifo chake kiliacha pengo kubwa katika siasa za Tanzania na miongoni mwa vijana waliokuwa wakimuona kama mfano wa ujasiri.

Siku iliyofuata baada ya kifo chake, maelfu ya wananchi wa Dar es Salaam walifurika pembezoni mwa barabara kuu za jiji kuuaga mwili wake. Viongozi wa serikali, wanasiasa wa vyama mbalimbali na wananchi wa kawaida walijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanamke huyo kijana aliyegusa maisha ya wengi.

Tarehe 28 Juni 2007, Amina Chifupa Mpakanjia alizikwa katika kijiji cha Lupembe, wilayani Njombe, ambako maelfu ya waombolezaji walikusanyika kwa ajili ya safari yake ya mwisho. Mazishi yake yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa pamoja na wananchi wa kawaida waliokuja kutoa heshima zao.

Miaka 19 baada ya kifo chake, jina la Amina Chifupa bado linaendelea kutajwa kila ifikapo mwezi wa Juni. Wengi humkumbuka kama mwanasiasa kijana aliyethubutu kusema kile ambacho wengine waliogopa kukisema. Alikuwa na ndoto ya kuona Tanzania isiyoathiriwa na dawa za kulevya na aliamini kuwa vijana wanapaswa kulindwa dhidi ya janga hilo.

Aliishi miaka michache duniani, lakini aliacha alama kubwa kuliko umri wake. Ujasiri wake, kujiamini kwake na utayari wake wa kusimamia kile alichokiamini vinaendelea kuwa sehemu ya historia ya kizazi chake.

Pumzika kwa amani Amina Chifupa Mpakanjia (20 Mei 1981 – 26 Juni 2007). Historia itaendelea kukukumbuka. Chanzo. Kanyamala Media
 
Kwanini utumie picha ya uwepo wa marehemu na mheshimiwa naibu sijui wanini vile wakati bado wa kuwa mtoto wa mama.! 🤒
 
Such is life, Those who cling to death, live and Those who cling to life, die...
 
Biashara ya mihadarati ni biashara inayolipa zaidi kuliko biashara yeyote duniani ukitoa mafuta na madini, biashara hii imeshikiliwa na vigogo duniani,wakijikita katika kunyamazisha sauti zinazolenga kudhoofisha biashara hiyo, na bila shaka yeyote kama kweli alikuwa mstari wa mbele kupambana na hii biashara haramu basi aliondoshwa. Walaaniwe wote walioinyamazisha sauti imara.
 
Biashara za madawa zinaendeshwa na majambazi hasa. Hayafikirii mara mbili kuamua kumuua mtu.

Ukiangalia MOVIE kama Narcos unaweza jionea umafia wa watu hawa.
 
Huyu demu alikuwa anapigana na kivuli chake bila kujua 🤭

Haki dunia inataka backup
 
Amina wa mpaka njia aka mama Rahnino kitambo Sana hata bongo sitalajii kuijua nipo zangu Rock City tuna kula con kwa salima coni mtaaa wa Kisha mapanda jilani na Toto African club
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom