Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 58,147
- 130,760
Wanabodi,
Angalizo la Nyuzi Ndefu
JF ni user generated forum, ina members wa aina zote na kazi yake ni kuhabarishana, kuelimishana na kuburudishana, na kati ya members hao, kila mmoja anashughuli zake za kumuingizia kipato kuendesha maisha yake, hivyo wao wanaandika jf kama past time tuu, mimi fani yangu ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea, hivyo kuandika ndio shughuli yangu, ndio kazi yangu, ndio maisha yangu. Nyuzi zangu sio nyuzi za kuhabarisha, ni nyuzi za kuelimisha, nyuzi hizi ni somo, ni darasa na ni miswada ya makala za magazetini kila wiki natoa makala mbili kwenye magazeti tofauti, kila makala ina maneno, 1,000, hivyo pole kwa nyuzi ndefu.
Ila kupitia ujio wa AI, kuanzia leo, nyuzi hii, nitakuwa natoa versions mbili, short form ya kuhabarisha na long form ya nyuzi darasa ya kufundishia.
Version 1- Short Form
Hoja hii inatoka kwenye mjadala ulioanzishwa na Pascal Mayalla kwenye mtandao wa JamiiForums, ikimzungumzia mwanasiasa Simai Mohammed Said (Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na aliyekuwa Waziri wa SMZ) baada ya kutoa kauli bungeni inayohusisha mfano wa "Yuda". [1]
Uchambuzi wa hoja kuu za ujumbe huu unajumuisha mambo yafuatayo:
[1] https://www.jamiiforums.com
[2] https://www.jamiiforums.com
Inawezekana kabisa, mtu wewe ukamuona kama ni malaika kabisa, kumbe pia sii malaika, hivyo ufafanuzi wa Mhe Simai, utatusaidia sana kututhibitishia huo u Yuda wa mtu wetu, hivyo tumpe Mhe. Simai the benefits of doubt kuwa he is right, huyu mtu ni Yuda, ila hata kama itatokea, kweli akawa ni Yuda kweli, sio kila Yuda ni Yuda Iskariote, pia kuna Yuda Tadei!. Sisi watu tunaomkubali, tunaujua uwezo wake wa kiuongozi ambao utatufaa kwa jambo letu la 2030, sio kila Yuda ni mpango wa shetani, kuna wakati Mungu anamtumia Yuda kufanikisha ajenda zake za Kimungu kama nilivyo eleza hapa. The Role of Yuda Eskarioti Kwenye Ukombozi wa Dunia: Je, Yuda alaumiwe, alaaniwe au apongezwe?!
Naomba kuikatia hapa, itaendelea baada ya kumpata Mhe. Simai kwa mahojiano na ufafanuzi wa Yuda wake!.
Paskali
Angalizo la Nyuzi Ndefu
JF ni user generated forum, ina members wa aina zote na kazi yake ni kuhabarishana, kuelimishana na kuburudishana, na kati ya members hao, kila mmoja anashughuli zake za kumuingizia kipato kuendesha maisha yake, hivyo wao wanaandika jf kama past time tuu, mimi fani yangu ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea, hivyo kuandika ndio shughuli yangu, ndio kazi yangu, ndio maisha yangu. Nyuzi zangu sio nyuzi za kuhabarisha, ni nyuzi za kuelimisha, nyuzi hizi ni somo, ni darasa na ni miswada ya makala za magazetini kila wiki natoa makala mbili kwenye magazeti tofauti, kila makala ina maneno, 1,000, hivyo pole kwa nyuzi ndefu.
Ila kupitia ujio wa AI, kuanzia leo, nyuzi hii, nitakuwa natoa versions mbili, short form ya kuhabarisha na long form ya nyuzi darasa ya kufundishia.
Version 1- Short Form
Hoja hii inatoka kwenye mjadala ulioanzishwa na Pascal Mayalla kwenye mtandao wa JamiiForums, ikimzungumzia mwanasiasa Simai Mohammed Said (Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na aliyekuwa Waziri wa SMZ) baada ya kutoa kauli bungeni inayohusisha mfano wa "Yuda". [1]
Uchambuzi wa hoja kuu za ujumbe huu unajumuisha mambo yafuatayo:
Uhuru wa Mawazo na Kuvumiliana
- Kuheshimu maoni mbadala: Jamii inatakiwa kujenga utamaduni wa kusikiliza na kuheshimu mitazamo ya watu wengine, hata kama maoni hayo hayakubaliki au yanapingana na mtazamo wa wengi. [2]
- Kuepuka kubeza: Badala ya kumshambulia au kumdharau mtoa hoja, kuna umuhimu wa kumpa nafasi ili afafanue kwa kina mantiki ya kile alichokimaanisha. [2]
Ujasiri na Ushujaa wa Simai
- Kusema ukweli: Mheshimiwa Simai anaonekana kama kiongozi jasiri asiyeogopa kuibua hoja nzito au zenye kuleta taharuki, bila kujali kama zitawafurahisha au kuwakasirisha viongozi wengine. [1]
- Kutikisa ulingo wa siasa: Kauli yake bungeni imezua mjadala mkubwa (ku-trend) na kuamsha hisia tofauti, jambo linalotajwa kama sifa ya viongozi wenye ushawishi. [1]
Mantiki ya "Hoja ya Yuda"
- Hoja ya msingi: Matumizi ya mfano au jina la "Yuda" (ambaye kihistoria anajulikana kwa usaliti) yanaashiria uwepo wa ujumbe mzito wa kiashiria, ama kuhusu uaminifu, usaliti, au migogoro ya ndani ya mifumo ya kisiasa. [2]
- Haja ya ufafanuzi: Mwandishi anasisitiza kuwa hoja hiyo isichukuliwe juu juu tu kama tusi au kashfa, bali itazamwe kama jambo linalohitaji uchunguzi na usikilizaji wa kina ili kuelewa kiini chake. [2]
[1] https://www.jamiiforums.com
[2] https://www.jamiiforums.com
Leo nimapata tena fursa kuwaletea PNA ya Kauli ya Mhe. Simai, kuhusu hoja yake ya Yuda!.
PMA ya leo ni kuhusu Watanzania tujenge tabia ya kuheshimu mawazo ya wengine hata kama hukubaliani nayo!, tujenge utamaduni wa kujadili hoja na sio kujadili watu, hoja ya Mhe. Simai kuhusu Yuda, ni hoja ya msingi, hapa jina la Yuda tamathali za semi kuhusu usaliti, kitendo ambacho sio kitendo kizuri, mtu anayefanya usaliti, sio mtu mwema, , mkiwa vitani kwenye mstari wa mbele, akitokea mtu akafanya usaliti, akigundulika hushughulikiwa hapo hapo bila kucheleweshwa, hivyo kama ni kweli kuna viongozi wasaliti, wasionewe aibu, watajwe kwa majina yao sio majina ya kificho, na usaliti wao, utawekwa hadharani, tuujue, ukithibitishwa, hawatufai!. Hivyo Mhe. Simai ni mtu jasiri, kweli kweli, kule nyuma aliwahi kuwa shujaa wangu, na kitendo cha kuliambia Bunge wazi wazi kuwa kuna usaliti na kumtaja Yuda, huu ni ujasiri, na hoja yake hiyo ya usaliti ni hoja ya msingi, asibezwe, asikilizwe apewe muda aifafanue na kuufafanua huo usaliti ili huyo Yuda ashughulikiwe!.
Safari ya Kuelekea 2030 na hoja za Usaliti, Udini, Zisinyamaziwe.
Hoja hizi hazikuanza leo.
Moja kati ya sifa kubwa za watu mashujaa, ni kitu kinachoitwa ujasiri, majasiri hawa, huwa wanaongea ukweli bila kujali ukweli huo, utamfurahisha nani au utamuudhi nani, au kiongozi akiharibu, bila ya kujali kiongozi huyo ni nani, majasiri hawa watampaka!.
- Alianza kiongozi mmoja kutangaza kuwa kuna watu wanakaa vikao vya siri kupanga kumdhuru, na kudai yeye hatishiki, ameisha pambana na wanyawa wakali simba na chui wakati akichunga mbuzi hivyo hawaogopi- ila hakuwataja hao wanaokaa vikao vya siri wala kusema wanakutania wapi.
- Akaja waziri mmoja akauzungumzia kumhujumu Rais Samia kwa kuwazia 2030, akina sisi wa kuhoji tukahoji na kuuliza, Makonda, Kumbe kuna Watu wanapanga Njama za Kuharibu na Kudhoofisha jitihada za Rais Samia katika uongozi wake kwa Ndoto za 2030? Ni kina nani hao?
- Tukauliza Urais 2030: Kuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yeyote Kuwa na Ndoto ya Urais? Mkwala Huu kwa Ndoto ya Urais, Inaweza Kuwa ni Ule Uchawa wa "Atake Asitake"?!
- Tukauliza Tena Urais 2030: Je Wajua, Kumpiga Mtu Zengwe Asigombee Urais ni Ukiukwaji wa Katiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
- Mimi nika declare interest kuwa Trends Reading: Japo Rais wa 2030 Namjua, Simtaji ili Kumlinda!. Be The First to Know Good News Kawe-2030, MB.ni Mwanamke!, Kawe Itapaa kwa Maendeleo!
- Kiongozi mmoja mkubwa akaibuka na hoja ya vibaraka wapumbavu lakini hakuwataja majina PNA: Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba ni Mkweli Kama Nyerere, Namuunga Mkono Kauli ya Vibaraka Wapumbavu, Tusiishie Kuwasema Tuu, Je Tuwataje Tuwajue Au?
- Kwenye hoja hiyo ya vibaraka wapumbavu, kiongozi huyo akalitaja kanisa fulani, juzi kwenye mazishi ya Mama yake JPM, SMS ya JPM ikasomwa hadharani, ikawaogopesha sana watu na kuwatetemesha kuhusu mtu kukubalika na JPM. Ndipo Mhe. Simai, akaibuka na Yuda!.
Kwa vile Mhe. Simai alikuwa mjumbe wa BLW na waziri wa SMZ, hakuna wakati jina lake limewahi kuvuma kama safari hii, alipomzungumzia Yuda Bungeni, ametisha, ametikisa, ametetemesha, ametingisha, ame trend, ila pia ameogopesha!.
Mimi nimetokea kufahamiana nae, kwa kutambulishwa na ndugu yangu fulani, tukajikuta tunafana fanana kidogo kwenye eneo la ujasiri na pia akija bara, tunakutana viwanja vyetu fulani, hivyo kuna kitendo cha kishujaa alikifanya Zanzibar, nikamuandikia makala kumpongeza.
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Nipashe
![]()
Tanzania tuko hapa tulipo kwenye lindi la umasikini uliotopea kutokana na kukosekana viongozi wa kutosha wenye boldness ya kuchukua maamuzi magumu!. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, John Pombe Magufuli, na huyu dogo Paul Makonda, ni miongoni wa watu wenye boldness ninayoizungumzia hapa!
Ikitokea umelalamikia kuhusu kukosekana kwa boldness kwa viongozi wetu, kwenye issues za uwajibikaji Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba...
- Pascal Mayalla
![]()
- anastahili kujiuzulu mkubwa mkuu nyerere pongezi ushujaa uwaziri uwaziri mkuu
- Replies: 53
- Forum: Jukwaa la Siasa
Ushujaa huo wa Simai, ni kama ushujaa wa Balozi Humphrey Polepole ambao pia niliuandikia makala GE2025 - Polepole: Shujaa, Mzalendo wa Kweli Kama Nyerere, Kang'atuka Kama Nyerere!, Amesema Ukweli Nusu!, Je Atoe Mguu Nje Aseme Ukweli Wote, Apewe Maua Yake?
Ushujaa mkubwa zaidi ni huu alioufanya Bungeni kumtamka mtu fulani mkubwa kuwa ni Yuda!.
Hebu kwanza msikilize,
View: https://youtu.be/GvWM9i_8dC4?si=0N65PKhSXU8zFFu_
Kisha Transcript yake na maoni yangu
SMS - Simai Mohamed Said
PM: Pascal Mayalla
SMS:Mheshimiwa naibu spika, mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu naongoza serikali yake pamoja na Watanzania kwa upendo na mshikamano, lakini kufanikiwa kwetu wakati mwingine kuna watu wanamtendea kinyume, na hapa nataka nimnukuu aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu Mheshimiwa Dotto Biteko aliwahi kusema binadamu ni wale wale.
SMS: Lakini niwaambie ndugu zangu, hawa wale wale leo nambatiza mmoja aliyekuwemo ndani ya serikali, basi ni Yuda.
SMS:Nasema hivyo kwa nini, sisi tunataka maendeleo ya nchi yetu, kosa la mama ni wapi?,kwa sababu ya kumwamini mtu kumbe ni Yuda. –
PM:Hapa Simai anamaanisha kuna jambo rais kalifanya linaonekana kama ni kosa!, je kosa hilo ni kosa gani?, Simai apewe fursa ya kulizungumza!
SMS:Yuda huyu amesaliti ndugu zake hata ile familia ambayo ilimlea kisiasa, hawataki kumuona huyu Yuda.
PM: Ni familia gani ilimlea kisiasa, ambayo hawataki kumuona?.
SMS:Hata huko nyuma amewahi kutajwa ni mzigo, lakini leo mzigo huu tunao ndani ya serikali
PM : Japo ni kweli, kuna mawaziri fulani wa JK waliwahi kutajwa kuwa ni mawaziri mizigo, huyu hakuwemo!, hivyo Mhe. Simai apewe fursa ya kutataja ni lini huyu alikuwa waziri mzigo?
SMS:.Na hapa niseme pia ameshawaumiza watu wengi, Yuda wengine walikuwa mbele sasa tunao huko nyuma bench wenzetu Rais Samia mwanzo , baada ya Yuda kuingia, akawaumiza
PM: Hii maana yake kuna wabunge walikuwa mawaziri, wanakaa mbele, sasa Yuda akawaumiza, wakaachwa sasa wanakaa back bench . Hawa ni mawaziri wepi hao walioumizwa na Yuda?, bila kuwataja, kauli hii itamaanisha kila waziri aliyekuwa na Samia mwanzo, sasa ameachwa ni huyu Yuda?
SMS:Wako wafanyabiashara watendaji ndani ya serikali wengine ambao walikuwa na safari nzuri ya kisiasa wamekatwa katwa wameathirika wako nje na wana msongo wa mawazo
PM: Wengi wangapi kina nani?.
SMS:Lakini Yuda tumeanza kumuona anaibuka katika nyumba za ibada kutafuta huruma za wananchi na watu mbalimbali.
PM: Ameibuka katika nyumba zipi kutafuta huruma za nini za wananchi na watu mbalimbali?
SMS:Lakini nataka niseme waheshimiwa wabunge wenzangu na serikali mliokuwepo hapa, tuamkeni tuamkeni
PM: Hii maana yake kuna mambo fulani yanaendelea chini chini, serika na wabunge wamelala hawajui, hivyo sasa Mhe. Simai, anawaamsha, waamke!, ni mambo yepi hayo?.
SMS:Leo anapita akitaka kutuaminisha sisi kwamba Rais Magufuli alimpenda sana yeyeYuda.
PM: Kwani uongo?, si SMS ya JPM aliisoma yote?.
SMS: Kama alimpenda kweli Kwa nini bwana alimrusha huko nje ya Dunia huko alitupwa Yuda, Huko alitupwa Waliompenda rais Magufuli tunawajua Mwenyewe akiwa aliwapenda tulikuwa tunaona wengine wamo walio humu ndani.Kwa hiyo tumwache Rais Magufuli alifanya kazi kubwa sana Mwenyezi Mung amjalie apumzike kwa amani.
SMS: Lakini Yuda awache Kumtumia majina ya watu.Tuamkeni Wabunge na tusiogope.
SMS: Mimi siwezi kutia ulimi wangu puani
PM: Hii maana yake huyu ni mbunge shujaa anaye nyoosha maneno, hajiumi umi ulimi, au kumumunya maneno anasema wazi.
PNA
Huu ushujaa wa Mhe. Simai ni kuweza kusema lolote linalomkera bila kujali wadhifa wa mhusika ni hazina kubwa kwa Bunge hili la chama kimoja, wabunge kama hawa wenye boldness ya aina hii, ndio wabunge watakaoweza kulisaidia Bunge kuisimamia serikali.
Wakati ule mimi nilipojaza fomu kuomba kuteuliwa, nilisema udhaifu mkubwa wa Bunge letu, nikasema kuna watu wenye boldness fulani, wanakosekana kule, bungeni, kutokana na kukosekana huko, Bunge letu tukufu likawa linapitisha madudu ya ajabu bila kuhojiwa na yeyote!.
Mfano yale madudu ya ile IGA ya DPW na bandari zetu, madudu ya bunge kukutungia sheria batili ya uchaguzi, yenye ubatili kinyume na katiba, ulioshabatilishwa, Bunge kutunga sheria batili ya INEC ambayo haipo kwenye katiba, katiba bado ina NEC!, hivyo watu bold wa type hii, watalisaidia sana taifa.
Hivyo wakati mjadala huu wa huyu Yuda wa Mhe Simai ukiendelea, salama pekee ya Mhe Simai, ni kuhojiwa kufafanua huo uyuda, na kufuatia moto aliouwasha kuwa ni mkubwa sana, Mhe. Simai atashauriwa, kuwa maadam hajataja jina la mtu yeyote, na mbunge ana kinga ya kibunge, kutohojiwa na mamlaka yoyote, hivyo anaweza kuamua kunyamaza kimya, asijibu chochote!, kwa vile mimi huyu bado ni shujaa wangu na ni jasiri, nitamfungia safari kumtembelea hapo Dodoma ajibu kiu yangu.
Ila wakati tukisubiria majibu ya Mhe Simai, kwa vile imetokea mimi kumjua huyo mtu Mhe. Simai aliyemuita Yuda,
Mimi namfahamu kwa sifa njema tuu kama hizi
- PNA: Pongezi Makamu wa Rais Bal. Dr Mchimbi Kuusema Ukweli Kuhusu Ujinga Huu wa Watu Kugombana Kwasababu ya Vyama!. Watanzania Tuukatae Ujinga Huu!
- View attachment 3600577
- Pongezi Makamu Rais Balozi Dr Nchimbi Kumeza Kidonge Kichungu cha Rais wa TLS, Wakili Mwabukusi kwa Viongozi Wabwatukaji wa Mambo ya October 29!
- View attachment 3600580
- BigUP Balozi Dkt. Nchimbi kukubali hoja za Rais wa TLS, Wakili Mwabukusi, kuhusu yaliyopita Oktoba 29 si ndwele, tugange yajayo ya Tume ya Uchunguzi
- Pongezi Makamu Rais Balozi Dr Nchimbi Kumeza Kidonge Kichungu cha Rais wa TLS, Wakili Mwabukusi kwa Viongozi Wabwatukaji wa Mambo ya October 29!
- View attachment 3600584
- Kumweleza Ukweli, Mtu Anayedanganywa ni Kumsaidia!, Asante Balozi Dr. Nchimbi Kuwaambia Ukweli CHADEMA
- PNA: Makamo wa Rais Dr Nchimbi, atamsaidia sana Rais Samia na Taifa, Ni Mkweli Anayeweza Kumweleza Rais Ukweli!. Ili Kumsaidia Aomba Rais Aombewe!
- Wito kwa Watanzania, Wazalendo wa Kweli wa Nchi Yao, na Wenye Mapenzi Mema na Taifa Lao, Tumuombe Rais Samia!, Tuliombee Taifa Letu!
- View attachment 3600592
- Hoja ya Rais Kuombewa: Je, Rais anapaswa kuombewa na viongozi wa dini tuu pekee au na Watanzania wote wenye mapenzi mema na taifa lao?
Inawezekana kabisa, mtu wewe ukamuona kama ni malaika kabisa, kumbe pia sii malaika, hivyo ufafanuzi wa Mhe Simai, utatusaidia sana kututhibitishia huo u Yuda wa mtu wetu, hivyo tumpe Mhe. Simai the benefits of doubt kuwa he is right, huyu mtu ni Yuda, ila hata kama itatokea, kweli akawa ni Yuda kweli, sio kila Yuda ni Yuda Iskariote, pia kuna Yuda Tadei!. Sisi watu tunaomkubali, tunaujua uwezo wake wa kiuongozi ambao utatufaa kwa jambo letu la 2030, sio kila Yuda ni mpango wa shetani, kuna wakati Mungu anamtumia Yuda kufanikisha ajenda zake za Kimungu kama nilivyo eleza hapa. The Role of Yuda Eskarioti Kwenye Ukombozi wa Dunia: Je, Yuda alaumiwe, alaaniwe au apongezwe?!
Naomba kuikatia hapa, itaendelea baada ya kumpata Mhe. Simai kwa mahojiano na ufafanuzi wa Yuda wake!.
Paskali
