Ndivyo Ilivyo
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 243
- 4
Kuhani,
Mkuu Kuhani na wengine wote, kwanza tulitazame swala hili kama lilivyowakilishwa Bungeni. Swala hili limeanza toka miaka 10 na upuuzi uliopita, Zanzibar walipotaka kujiunga..
Kikatiba haikuwezekana kwa sababu Zanzibar sio nchi na swala hili lilikuwa la Muungano hivyo ilibidi uamuzi utolewe ktk bunge la Muungano mahala ambapo limekutana na Utata mkubwa.
Kwa hiyo, hoja bado haijabadilika zaidi isipokuwa ni sisi wananchi tumeshindwa kuelewa swali, kama tanzania inaweza kujiunga na OIC kwa sababu ya kikatiba ambayo inaikataza Zanzibar kujiunga kama nchi.
Kama utakumbuka hata mimi nilipinga vikali Zanzibar kujiunga na OIC kama nchi na hivyo kuwataka swala hili lifikishwe bunge la Muungano ambalo kusema kweli yawezekana Katiba haijitoshelezi.
Ni katiba hiyo hiyo tumeshindwa kutambua kwamba WaZanzibar ni distinct society ambayo imeingia ktk ndoa hii ya Muungano wakiwa na culture zao. Ni katiba hiyo hiyo imeshindwa kutambua kwamba Zanzibar ni sovereign country wakati Tanganyika isingekuwa Tanzania bila Muungano huo. Tanganyika iliondokewa nchi kama Rwanda na Burundi lakini bado tulibakia Tanganyika kwa sababu ile ilikuwa kama mikoa tu, hivyo hata leo tunaweza kuvunja mikoa lakini bado Tanzania ikasimamisha jina lake lakini sivyo kama Zanzibar itaondoka...
Nilichokuwa nikitazama mimi ni haki ya kimsingi ya waislaam ambao wanatengeneza asilimia 99 ya wananchi wa Zanzibar. Hii ndio chulture waliyokuja nayo (Uislaam) ktk Muungano wetu na hatuwezi kuipuuza kwa sababu tu sisi bara tuna dini nyingi na tofauti.
Ndio maana nikatumia mifano mingi ya ndoa kama nchi mbili na hata ndugu kama kigezo cha wananchi wa pande hizi mbili ili kutoa mawazo yangu kwa sababu Muungano wetu ni sawa na ndoa ama udugu wa kaka na dada.
Kuna watu humu wanafikiria kwamba mimi nazungumza kama Muislaam ama natoa hoja zangu kwa sababu ni muislaam, wanafanya makosa ya wazi kabisa kwani hata kama ningekuwa mkristu ningependekeza Tanzania kujiunga na OIC kwa sababu ya Zanzibar.
Hata kama Zanzibar ingekuwa na asilimia 99 ya Wakristu na wakataka kujiunga na baraza lolote la Kikristu ningeunga mkono isipokuwa tu kama wangetaka kutoa maamuzi wao wenyewe bila kuihusisha Bara wakati wanatumia bendera ya Taifa ningepinga. Kwa hiyo utaona kwamba sina upande, lakini waulize wengi humu maswali hayo watakuwa na majibu tofauti..
Tatizo jingine lililojitokeza ni pale tunapotaka kuziangalia faida za Tanzania kujiunga na OIC.. wakuu wangu hili sio swala letu, kama mimi Muislaam nimefunga ndoa na Mkristu inabidi nikubali yanayokuja na Ukristu.. isipokuwa hoja yoyote inayohusu nyumba yetu ni lazima nihusishwe kama mume ktk maamuzi..
Kwa hiyo wakuu, swala bado lipo pale pale na pengine tunajichanganya sisi wenyewe kufikiria kwamba swala hili ni la Bara maadam limekuja ktk bunge la Muungano..!..Zaidi ya yote hayo kuna mambo mengi sana Bara tunawaburuza Zanzibar tukitumia jina na bendera ya Taifa bila wao kuhusishwa wala kupata hata mapato ya Ubalozi tuliotumia..
Kwa hiyo jamani kuwanyima waislaam ama niseme Zanzibar haki yao ya kimsingi ambayo ni moja ya culture yao waliyoingia nayo ktk Muungano kusema kweli tutafanya Udikteta. Na sasa hivi kuna hatari kubwa sana maadui wa Muungano na pengine hao fundamentalist wakaitumia hoja kama hii kubomoa kile mwalimu alikijenga kwa miaka 20 na upuuzi..bahati mbaya ni kuwa fundamentalist toka upande wa pili (Ukristu) ndio wanaoendesha hoja hii ktk Upinzani hali Zanzibar leo wameweza kufungua hata mipaka yao wa Wakristu kufungua makanisa ndani ya nchi yao.
Mwisho, mimi Mkandara pamoja na kuwa Muislaam sintakubali OIC kujenga sheria za Bara ama serikali nzima ya Muungano. Na sidhani kama inawezekana kwa sababu zipo nchi kibao zilizoungana zina toifauti kama zetu na wameweza kuishi kwa amni maadam unafahamu mipaka ya sheria hizo..
Kwa hiyo waungwana swali hapa halijapinda wala kugeuzwa kuwa swala la Tanzania nzima (nilivyoelewa mimi) isipokuwa majibu yake yatatoka kwa mawasilino ya sehemu zote mbili (bungeni) na muhimu zaidi ni sisi kutazama kujiunga huko kutaleta madhara gani Bara!.. Hizo faida wakuu wangu sio kazi yetu hata kidogo, unless tuna hakika kuwa Mwanamke/ mwanaume huyu anataka ku cheat!..
Ahsante sana Mheshimiwa Mukandara. Naona umeeleza kabisa yanayojiri. Pamoja na hayo kwa kujalizia tu. OIC wanaihitaji Zanzibar hivi sasa kujiendeleza kiuchumi. Kuna investments kutoka Vyombo (mabenki) yanayofungamana na OIC na Investors wanaofungamana na vyombo hivyo amabayo hayawezi ku-materialise bila ya Zanzibar kujiunga na OIC. Nayo basi kwa sababu ya Muungano haiwezi kujiunga ila ipitie kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Enyi ndugu zetu wa Bara- Please do the needfull- Wacha Jamhuri iingie kuiwezesha Zanzibar kunufaika. Zanzibar imeyakubalia mangapi yenye maslahi na Tanganyika yafanyike kwa Jina na nguvu za Jamhuri ya Muungano. Nasema tena Thank you Mheshimiwa Mukandara for the post.