Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,592
- 23,952
Asilimia kubwa ya nchi hii ni Waislam, yani Tanzania Bara na Visiwani kwa hio obviously Birth Rate ya Waislam itakuwa higher ukiweka na factors zingine kama Uislamu unavyoruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja....maximum ni wanne.
Yale yale ya Field Marshal Idi Amin Dada, conqueror of the British Empire and man-eater. Mmmh ! Hapa dawa ni kuzaa kwa ari, kasi na nguvu mpya ili kuongezeka na kutapakaa kila kona ya Tanzania halafu njia ya kuingia OIC itakuwa nyeupee!! Tujiepushe tu na ukimwi.
Halafu pia hivi sasa tuna watu wengi ambao wanasilimu na kuukubali Uislamu kuliko wakati wowote kwenye historia yetu(Source: islamic propagation centre).
Source !! Lo makubwa haya - bravo bila shaka siyo muda mrefu hao makafiri, mapagani na wote waliopotea njia mwisho wao hauko mbali. Lakini kwanza hawa wenye mioyo migumu wapewe muda kusilimu na wasipofanya hivyo.. ..............
Ni uwongo kwamba sisi tunataka kujiunga na OIC kwa ajili ya maslahi yetu, je ni maslahi gani hayo? yaweke wazi ili na sisi tujue! Nchi za Sudan, Somalia na Djibouti ziko kwenye vita kwa ajili ya ukabila na sio udini...kwa nini unahoji uwezo wa OIC kuzisaidia nchi hizi na uihoji Umoja wa Mataifa(UN), au nchi hizi haziko kwenye umoja huo? UN ina nguvu kuliko OIC, OIC ni bado changa na inahitaji mchango wa nchi kama Tanzania ili iweze kutimiza agenda zake.
Kumbe mchango wa Tanzania unahitajiwa ili kutimiza ajenda za OIC. Hima wananchi OIC inahitaji msaada wetu na wakati wa kutoa misaada ndio huu. Masikini OIC !!
Uganda ina matatizo kwa ajili ya Rebel Force army ijulikanayo kama LRA(Lords Resistance Army) ambayo inaongozwa na wakristo na si waislamu, hapo pia ninaomba ungeihoji UN au hoji Umoja wa Africa Mashariki (EAC)! Afghanistan ilivamiwa na Marekani na Uingereza ambazo ni mmoja kati ya nchi zinazopiga vita Uislam, na Wa-afghani wanahaki ya kutetea ardhi yao na uhuru wao na pia OIC iko 'against' conflict katika nchi zote ulizotaja na inajitahidi kadri iwezayo kutatua matatizo yaliokumba nchi hizi.
Kumbe tunatakiwa kutetea uislamu tukiingia OIC na kwa maana hiyo lengo mojawapo la OIC ni kuwapinga Marekani na Uingereza kwa kupiga vita uislam. Lo, sasa kichwa kinazunguka.
Ninawashauri watanzania wenzangu kujiunga na OIC ili wote tusimame na tutokomeze uonevu, umasikini, ufisadi na matatizo yote yanaetukumba sisi nchi masikini!
OIC kimbilio la wanyonge na masikini. OIC dawa ya uonevu na ufisadi. Kumbe kujiunga kuna manufaa kiasi hiki. Basi na mimi nakubali tujiunge na OIC tukitaka ndege yetu ipae kwa mbwembwe.