Mwankijiji,
Kuhusu hizo Jumiya za Kiislaam, nakuomba unambie Jumuiya ya Kiislaam ambayo wewe unaifahamu tumejiunga nayo ama tunaruhusiwa kujiunga!..Ama kwa kukurahisishia nambie Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislaam ambayo iko Tanzania..
Mwanakijiji, unaposema wengine tungeendelea kupinga tu ni vumbi la macho, mkuu nakufahamu vizuri sana inapofikia maswala haya..menigne tuyaache kama yalivyo. sina haja ya kuingia ndani zaidi
Tanzania ni imo ktk baraza la Wanawake duniani na wanaotuwakilisha ni wanawake..Bado unatumia mifano ya Ukatoliki, mkuu waislaam na katoliki hawafanani hata kidogo!.. Ujenzi wa jumuiya zenu hauwezi kuwa sawa na waislaam hata kidogo na pengine katiba imeandikwa kwa misingi ya Ukristu, hivyo waislaam hawakutazamwa, Kumbuka wewe ni mwanaume huna shoga mkuu, na unapozungumzia mwili jaribu kuziona tofauti zako kwanza.Ndio sababu Makanisa ya Kiprotestanti Tanzania yanaweza kujiuna na Baraza la Makanisa Duniani (WCC) bila kulazimisha nchi nzima ya Tanzania kujiunga. Kuna taasisi mbalimbali duniani za Waislamu ambazo jumuiya za Kiislamu ni wanachama na hakuna mtu anayepinga wala mwenye haki ya kupinga hivyo.
Kuhusu hizo Jumiya za Kiislaam, nakuomba unambie Jumuiya ya Kiislaam ambayo wewe unaifahamu tumejiunga nayo ama tunaruhusiwa kujiunga!..Ama kwa kukurahisishia nambie Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislaam ambayo iko Tanzania..
Mkuu hili ni baraza (conference) ya wanawake na OIC ni baraza (Conference) la nchi za Kiislaam, tofauti hapa ni Wanawake na Waislaam kwa hiyo mipaka yake lazima haitakuwa sawa unapo address wasiohusika...Wanawake vs wanaume, Waislaam vs wasiokuwa Waislaam.Hapa umekosea kidogo. Mama Mongela alikuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Wanawake kule Beijing. Mkutano huu ulikuwa ni wa Umoja wa Mataifa (nchi ambayo Tanzania ni mwanachama). Hivyo Tanzania haikuwa imejiunga na jumuiya mpya bali ni Jumuiya ya Umoja wa Mataifa.
Mkuu sheria inaposema kila mtu ana haki ya kuamini dini aitakayo unafikiria hilo ni jukumu la dini sio serikali? utaweza vipi kusimamisha sheria kama hiyo bila serikali kuweka mkono wake!Hili ndilo kosa nadhani lililopo. Siyo jukumu la serikali kulinda value za ukristu au Uislamu wa mtu. HIlo ni jukumu la taasisi za kidini. Serikali inapoingilia kati na kufanya kazi ya makanisa na misikiti inavuka mpaka wa kuwa serikali isiyo na dini na kuingia kwenye anga zisizo zake.
Haya sasa maneno, Turkey wamekataa kuwa nchi ya kiislaam lakini wao ni Member wa OIC, kwa hiyo hapa umezidi kujenga hoja yangu. hakuna mtu aliyesema kujiunga kwetu na OIC kunaifanya nchi yako kuwa ya kiislaam. Turkey mfano mzuri sana, shukran!Wangefanya hivyo wengine tungeendelea kupinga tu; ni principle. Wewe unaangalia wingi wa watu kuhalalisha hili mimi naangalia principle. Nchi ya Uturuki ni nchi yenye waislamu wengi lakini kwa makusudi kabisa wamekataa kuifanya nchi hiyo kuwa ya Kiislamu na wakati wowote wanasiasa wanapoisogeza nchi kwenye masuala ya dini, wanapata onyo lililowazi kutoka Jeshi. Hiyo ni principle. Na wale wanajeshi wanaopinga hivyo ni Waislamu vile vile wanapenda maisha yao ya kuwa taifa secular.
Mwanakijiji, unaposema wengine tungeendelea kupinga tu ni vumbi la macho, mkuu nakufahamu vizuri sana inapofikia maswala haya..menigne tuyaache kama yalivyo. sina haja ya kuingia ndani zaidi