Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Huu ni ubabaishaji mkubwa .Habri za ndani kabisa zinasema kwamba waarabu wa OIC baada ya kuwa chini ya JK wanaipa misaada mingi chini ya carpet sasa wamesema hawatatoa hadi Tanzania iingia katika shirikisho lao na ndiyo maana sasa unaona serikali inakuja ku test akili za watu hapa .Membe semeni ukweli tusije mwaga data hapa jamani ikawa soooo
 
Nadhani watanzani wengi watakubali nchi yao ijiunge na OIC endapo:

a. Katiba ya OIC itabadilishwa na kutotambua Uislamu kama kiunganishi cha nchi hizo.
b. Itatoa nafasi za ajira kwa mtu yeyote mwanachama na mtu huyo si lazima awe Muislamu
c. Haitaweka kipaumbele cha kulinda, kuhifadhi, na kutetea tunu za Kiislamu tu
d. Haitataka maamuzi yake kuongozwa na mafundisho ya dini ya Kiislamu
e. Haitalazimisha nchi zote wanachama kukubali Yerusalemu (al Quds) kuwa Makao makuu ya Palestina
f. Itaondoa Bismillah kwenye ufunguzi wa Katiba hiyo na hivyo kuzifanya nchi zinazokubali kujiunga nayo kusema Bismillahi.
g. Kuondoa references zozote zile za dini ya Kiislamu kwenye Katiba na kuifanya jumuiya hiyo iwe ni jumuiya misaada tu isiyounganishwa na dini moja.
h. Kama hayo yote hayawezekani, basi Katiba hiyo iutambue Ukristu na kuweka malengo yenye kulinda, kutunza, na kutetea tunu za Kikristu pia.

Wakifanya hivyo Tanzania inawea kujiunga.
Katika hili jambo tafadhali soma post ya Bw. Mkandara hapo juu. Hujafahamu tu.Achana na misingi ya OIC iliyojiwekea. Nauliza, umemuelewa vyema Mkandara?. Sasa kama kweli tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , na inayotumia busara inabidi iingie OIC, kukidhi haja ya Zanzibar. Achana ma malumbano ya udini. Tunazungumzia hapa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau wake.
 
Huu ni ubabaishaji mkubwa .Habri za ndani kabisa zinasema kwamba waarabu wa OIC baada ya kuwa chini ya JK wanaipa misaada mingi chini ya carpet sasa wamesema hawatatoa hadi Tanzania iingia katika shirikisho lao na ndiyo maana sasa unaona serikali inakuja ku test akili za watu hapa .Membe semeni ukweli tusije mwaga data hapa jamani ikawa soooo
Wewe acha kupotosha umma. Kwa hili chonde chonde unaweza ukajikuta huna hata hiyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jee utarudi uwe tanganyika?
 
Nadhani watanzani wengi watakubali nchi yao ijiunge na OIC endapo:

f. Itaondoa Bismillah kwenye ufunguzi wa Katiba hiyo na hivyo kuzifanya nchi zinazokubali kujiunga nayo kusema Bismillahi.
hivyo Tanzania inawea kujiunga.
Khaa unancheksha. Unaifahamu -Bimsmillah- wewe?. sasa huku kwetu hata mtoto wa miaka mitatu (kindergerten) anaanza kila kitu kufanya kwa kutaja -Bismillah- . . Unataka kuwambia nini hawa?. Hawawezi kuikana Bismillah. Hiyo ndiyo Zanzibar. Na Sio lazima tuwe katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunaweza kurudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
 
Go ahead and try it!You have my blessings as an individual!
 
Wewe acha kupotosha umma. Kwa hili chonde chonde unaweza ukajikuta huna hata hiyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jee utarudi uwe tanganyika?

Naomba unieleze ni wapi ambapo nina potosha .Kuna ushahidi mwingi sana wa OIC kuipa Tanzania misaada kimya kimya na sasa wameamua kuiminya na huu ndiyo ukweli .Membe najua unasoma hapa njoo ukanushe tutoe ushahidi hapa hapa .
 
.............. Hivi Muungano ni kukidhi haja na matakwa ya Tanganyika tu. Ikija matakwa na haja ya Zanzibar tubeze?

......could you please elaborate on this...........
1. hayo matakwa ya Tanganyika tu na ya Zanzibar....ni yepi hayo?.......
2. je una maana Tanzania bara wanaitumia Zanzibar kupitia foreign policies kujinufaisha wao tu?.....tena kwa kujiunga na chombo mfano wa OIC?

Fundi Mchundo,

.......Hivi sasa tumehamia kuwa issue ni kukidhi matakwa ya Zanzibar!!!! eehh.......!!?

...unajua hapa ni bora kujenga hoja za msingi ili kuondoa misuguano ndani mwa jamii yetu...kwa sababu jambo lolote litakaloamuliwa KITAIFA ni kwa faida ya wote na si kundi fulani........huu ushabiki wa dini sijui unatokea wapi........

.......Uamuzi wa Kitaifa ni pamoja na ku-amend "to suit" katiba pale tunapoona inafaa kwa manufaa ya wananchi wote.......hivyo basi na tujenge hoja ili ikibidi tu-amend katiba.....then masuala mengine yataeleweka...........

Bob,
Ndoa ni makubaliano........na mkishakubaliana...mnaweka mi/uongozo (katiba) ili kudumisha familia........ndoa nyingi zilizo na matatizo ni zile zilizokosa makubaliano ya miongozo.......sasa basi kama mume/mke anakuja na matakwa nje ya miongozo iliyopo inabidi tuelimishane na kufikia muafaka................

.......we have to be careful here........pengine ushiriki wetu unaweza kutu-cost zaidi ya hivyo tunavyotarajia kwa kujiunga.........this is what we are supposed to be debating as a family.......thats my opinion
 
Huu ni ubabaishaji mkubwa .Habri za ndani kabisa zinasema kwamba waarabu wa OIC baada ya kuwa chini ya JK wanaipa misaada mingi chini ya carpet sasa wamesema hawatatoa hadi Tanzania iingia katika shirikisho lao na ndiyo maana sasa unaona serikali inakuja ku test akili za watu hapa .Membe semeni ukweli tusije mwaga data hapa jamani ikawa soooo

Itakuwa bora sana kama itazimwaga hizo data hapa ili hili soo lichanganye kisawasawa mkuu
 
......could you please elaborate on this...........
1. hayo matakwa ya Tanganyika tu na ya Zanzibar....ni yepi hayo?.......
2. je una maana Tanzania bara wanaitumia Zanzibar kupitia foreign policies kujinufaisha wao tu?.....tena kwa kujiunga na chombo mfano wa OIC?

Fundi Mchundo,

.......Hivi sasa tumehamia kuwa issue ni kukidhi matakwa ya Zanzibar!!!! eehh.......!!?

...unajua hapa ni bora kujenga hoja za msingi ili kuondoa misuguano ndani mwa jamii yetu...kwa sababu jambo lolote litakaloamuliwa KITAIFA ni kwa faida ya wote na si kundi fulani........huu ushabiki wa dini sijui unatokea wapi........

.......Uamuzi wa Kitaifa ni pamoja na ku-amend "to suit" katiba pale tunapoona inafaa kwa manufaa ya wananchi wote.......hivyo basi na tujenge hoja ili ikibidi tu-amend katiba.....then masuala mengine yataeleweka...........

Bob,
Ndoa ni makubaliano........na mkishakubaliana...mnaweka mi/uongozo (katiba) ili kudumisha familia........ndoa nyingi zilizo na matatizo ni zile zilizokosa makubaliano ya miongozo.......sasa basi kama mume/mke anakuja na matakwa nje ya miongozo iliyopo inabidi tuelimishane na kufikia muafaka................

.......we have to be careful here........pengine ushiriki wetu unaweza kutu-cost zaidi ya hivyo tunavyotarajia kwa kujiunga.........this is what we are supposed to be debating as a family.......thats my opinion
Unataka kuniambia huwaamini wale wa upande wa pili- Zanzibar (SMZ)?
Nitakushangaa na hiyo Jamhuri yako ya Muungano wa Tanzania.
 
......could you please elaborate on this...........
1. hayo matakwa ya Tanganyika tu na ya Zanzibar....ni yepi hayo?.......
2. je una maana Tanzania bara wanaitumia Zanzibar kupitia foreign policies kujinufaisha wao tu?.....tena kwa kujiunga na chombo mfano wa OIC?

Naomba unifahamu vizuri. Mawazo yangu mimi ni kuwa Tanzania Bara(Tanganyika) waneatumia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (na uwezo wake) kukidhi haja na matakwa ya Wa-Tanganyika. Lakini linapokuja suala la Wa-Zanzibar kuitumia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukidhi matakwa yao- inakuwa malumbano why?
 
...nshakufahamu....ndo maana nkakuuliza ni matakwa yepi hayo yakhe...?
 
...nshakufahamu....ndo maana nkakuuliza ni matakwa yepi hayo yakhe...?
Serikali ya Jamhuri ya Muungano iwe inaisikiliza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hiyo ndiyo ina sera na mipango yake ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na hiyo ya kuwa katika (OIC) Sasa suala la OIC ni la SMZ ikiwa na mandate ya Zanzibar(Wananchi wa Zanzibar) ndio wanaotaka huko. Msijitie kulitia katika medani ya kidini -kubabaisha- haliko hivyo. Kuwa mkweli Bwana.
 
........... Hivi Muungano ni kukidhi haja na matakwa ya Tanganyika tu........

yakhe....swali langu ni kuhusu hiyo sentensi yako hapo juu.........hebu tuwekee hayo matakwa ya Tanganyika tu...........
 
Hatuwezi kujiunga na jumuiya fulani kwa "manufaa" ya sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na Zanzibar hata ikitaka haiwezi kujiunga kwani Katiba ya OIC inakataza na sijui waliwezaje kujiunga na OIC in the first place.

Hatuwezi kujiunga na jumuiya kwa ajili ya kuridhisha kundi moja tu la watu au sehemu moja tu ya Jamhuri yetu.

Kwa vile mfano umetolewa mara nyingi ya kwanini Tanzania iwe na Ubalozi wa Vatican, kwanini basi tusikubali OIC na Tanzania zianzishe uhusiano wa kibalozi na tuwe na mwakilishi (Envoy) wetu OIC na wao OIC wakitaka wafungue ofisi pale Kikwajuni au Kibanda Maiti na kuwa na envoy wao?

Kwanini lazima tujiunge?
 
Mwanakijiji,
Mkuu wangu hapa umelewa! nakuaminia sana katika fikra huru lakini kusema kwamba Hatuwezi kujiunga na jumuiya fulani kwa "manufaa" ya sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni sawa na kusema hatuwezi kujiunga na jumuiya fulani kwa "manufaa" ya kundi moja la wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... yet tumejiunga na jumiya za wanawake duniani na Mama Mongella alikuwa secretary General.. Na ni katiba hiyo hiyo inaweza kutumiaka kupinga kitu kile lakini kwa sababu mazngira tunayoishi ndiyo yanasukuma baadhi ya ibara za katiba kuwa na nguvu na zenye msisitizo ktk haki za wananchi wake.

Hivyo hivyo katika swala la Muungano, values za Wazanzibar kama Waislaam ni lazima ziwe sababu kubwa kwao kuweza kuhakikisha hawapotezi values hizo ktk Jamhuri yetu..

Mkuu nina hakika kabisa kama Bara tungekuwa na asilimiam 99 ya wakristu na kuna baraza la wakristu duniani linalosajiri nchi za kikristu, tusingekuwa na mjadala huu hata kidogo. Rais, iwe Nyerere, Mwinyi, Mkapa ama Kikwete wote wangepitisha bila hata kumuuliza mtu..

Mkuu hili ni baraza tu la nchi za kiislaam ambalo lina malengo sawa kabisa na mabaraza mengine yanayokusudia kuendelea Umma wake kwa kupitia mijadala..

Sioni kitu kikubwa ambacho wewe unakizungumzia unaposema wakiondoa hiki ama kile.. Mkuu ni sawa kabisa na mkeo anayetaka kwenda ktk maandalizi ya Kitchen party unaanza kutazama orodha ya maandalizi kama Mwanaume na kutoa suggestion ambazo zinapinga women to be women..Ulichoombwa ni ruksa yako tu..Mkuu wewe hauhusiki na Kitchen party hivi kweli utaweza kuvaa khanga hata wakikualika?..

Ogah,
Bob,
Ndoa ni makubaliano........na mkishakubaliana...mnaweka mi/uongozo (katiba) ili kudumisha familia........ndoa nyingi zilizo na matatizo ni zile zilizokosa makubaliano ya miongozo.......sasa basi kama mume/mke anakuja na matakwa nje ya miongozo iliyopo inabidi tuelimishane na kufikia muafaka................
Hapa mkuu nipo nawe kuwa ndoa ni makubaliano lakini mkuu huwezi kufikiria yote ya kike isipokuwa yale yanayowahusu kwa wakati ule kudumisha ndoa hiyo kama Mume na Mke..

Hakuna ndoa ambayo inaanza na kusema hakuna mwanamme kwenda mpirani ama mwanamke kucheza Upatu...Haya ni mambo unakutana nayo ktk ndoa na utayategemea kuwepo, after all OIC imenzishwa baada ya muungano wetu..

Mara nyingi mkuu ndoa huvunjika nje ya makubalinao ambayo hugusia maswala ya msingi kama vile tutakuwa sote kwa mabaya na mazuri. shida na raha, uzima na Ugonjwa lakini pamoja na makubaliano haya sababu nyingi huwa zinatoka nje ya makubaliano. Tunafunga ndoa zetu kama wajibu kwanza kisha mategemeo ya ndoa zetu ni pamoja na kuanzisha familia mpya, security, kuondoa Upweke, na kadhalika hivyo kuna mipaka ya mtazamo krk ndoa. Na mara nyingi ndoa hutegemea (WATU) wahusika kiasi kwamba dini, kabila, elimu, afya vinaweza badilisha makubaliano ya ndoa moja hadi nyingine..

Mahala (MAZINGIRA) mnapoishi pia kunaweza kutofautisha ndoa moja hadi nyingine kwani Ukimuoa Msukuma Usukumani maswala la kulima, ufugaji na kadhalika yanaingia moja kwa moja kisha jioni kuna Chimpumu ama gongo, hakuna bills za umeme wala maji..Kama mwanaume ukirudi nyumbani lazima unaimba sana kwa kusikifia, kuita mali zako ukiwa mita 100, tofauti na wakazi wa mjini ambao mnatumia usanii mwingine..

Tatizo langu kubwa ktk swala hili la OIC halihusiani na yote haya isipokuwa sehemu moja tu.. Pale unapoweka vikwazo kwa mke/mme kushiriki ktk vikao vya imani yake ya kidini kwa sababu tu wao ni dini tofauti na wewe hali mkeo ni dini hiyo..kisha unadai kwamba huna ubaguzi wa dini na ati kama ungekuwa na ubaguzi usingemuoa!..

Sababu kubwa unayotumia kupinga inatokana na malengo ya dini yake kutokana na mwongozo wa kitabu cha dini hiyo kuanza kuchambua yale usiyokubaliana nayo wakati hakuna hata sehemu moja inakushirikisha wewe kama mlengwa wa mikutano hiyo...Zaidi ya yote haya ndio maana wewe hukuwa dini hiyo in the first place kutokana na kutokubali imani ya dini hiyo iweje leo utake kubadilisha sura za dini hiyo wakati huna imani nayo!

Ogah,
Bara tunatumia sana bendera ya taifa (jina la Tanzania) kuchukua misaada kibao nje na uwekeshaji wake unakwenda bara..ziko kibao na wala hatuna aibu.. Chukulia mfano mdogo tu wa Richmond,(sijui kama nimekosea) fedha iliyotumika sio fungu la halmashauri ya mkoa wa Dar na uzembe umefanyika na viongozi wa bara, yet deni la Taifa linapohesabiwa Zanzibar wamo na bado wanakatiwa umeme kutwa kila wanapopiga kelele!..Miradi kibao ya Kitaifa imetazama Bara kuliko Zanzibar na bado wao wamefungwa ktk Muungano kutoweka deal za nje...

Mkuu kama utasoma vizuri yote yaliytotangulia ktk mada hii utaona chuki na udini mkubwa ambao umefikia hata watu kuutazama Muungano kwa jicho la kidini..

Cha ajabu zaidi watu wanatumia neno misaada kuwa ndio sababu kubwa ya Zanzibar kujiunga, let me tell them something, hakuna maendeleo yoyote ya nchi yoyote duniani kama haina mikopo hata Marekani leo hii inadaiwa mabillioni na China..

Neno misaada lisitumike kama Tanzania itapata fedha ama mafuta bure isipokuwa tunakuwa na mipango ya biashara kati ya nchi zinazohusika hata kama zimepatikana kwa njia tofauti..

Msaada (Aid) inaweza kuwa mtaji ambao utarudishwa kama vile sisi tunavyopata ama kutoa mikopo kwa mtu unayemfahamu na kumwamini (jumuiya)..Lakini wakati huo huo akija mtu usiyemfahamu mkopo wako unakuwa na masharti magumu kuhakikisha fedha yako itakuwa salama na ndio hali inayotukuta toka nchi za Magharibi...

Tatizo la wengi hapa tumezoea kibongo Bongo yaani neno Msaada ni fedha ya Bure!..

Ukimpa mtu usimuulize hata kaitumia vipi unatafuta ugonvi..Na ni kwa sababu hatuna Utaratibu kama huo ndio maana Unaona Mafisadi nchini wakiiba fedha kutafuta mtaji, hakuna njia nyingine zaidi ya kuiba kama hujajaliwa.

Hivyo basi Zanzibar wanataka kuingia chama, pengine niseme Upatu ambao sisi wanaume wa bara tunataka kujua hizo Khanga, wanja na heleni zina faida gani kwetu!... wakuu mambo ya kike haya mnataka ku reason vitu ambavyo mwanamke hatakuelewa kabisa!.. Mkeo akiwa na furaha ndani ya nyumba, ndoa huzidi kuboreka.
 
Mheshimiwa Mkandara, nafurahishwa na mahali unapojitahidi kuupeleka huu mjadala. Najua baada ya kuona ukweli kuwa wote wanaotetea nchi ijiunge na OIC wameshindwa kutoa sababu zenye ushawishi za kwa nini nchi ijiunge, naye umeamua kutwist na kutupeleka kwenye muelekeo mwingine. Angalao hapa kidogo naona zinaweza kupatikana sababu zenye logic kidogo, lakini mmh!, ndugu yangu!. Napata taabu juu ya baadhi ya mambo, nitataja mawili:-

1. Kwa nini tusisubiri kwanza tupate muafaka juu ya muungano wenyewe, naamini wabara wengi kama si wote tunajua wazi kuwa Zanzibar hawaridhiki na muungano. Tuna uhakika gani kuwa mwisho wa makubaliano yetu utakuwa wa neema na wala si matengano?, maana kama tutajiunga kwa ajili ya Zanzibar na baada ya muda kila mtu akachukua time yake faida itakuwa wapi?

2. Wote tunajua kuwa ili kuweza kujiunga na OIC inabidi katiba ifanyiwe marekebisho ili iweze kusuport hatua hii, sasa itakuwaje maana wote tunafahamu kuwa Zanzibar hawaitambui katiba ya muungano?. Je, baada ya kujiunga sasa wataanza kuitambua, au watatambua kipengele hicho kitakacho badilishwa tu kwa ajili ya faida yao?

Naona si rahisi kama watu wanavyojaribu kutaka kufanya, pamoja na jitihada za kutaka kutwist ili kuhalalisha. Aidha tutatengeza mazingira ya kushindwa kudhibiti mambo endapo tutakuwa tayari kuiruka katiba ili mradi tu tunaridhisha baadhi ya watu.
 
Shedafa,
Mkuu hakuna mahala nimejaribu ku twist, yote niliyoandika ndio hali halisi na pengine wewe ndiye unayevuta hata yale yasiyokuwemo..
1. Muafaka ni wa vyama hauhusiani kabisa na katiba ya Muungano..
2. hakuna mahala popote panapoonyesha Zanzibar hawaitambui katiba ya Muungano, kama kweli wasingekuwepo wawakilishi wao ktk bunge la Muungano..

Katika kujadili kwangu najaribu kutumia lugha na mifano ambayo ipo ktk maisha yetu ili kutoa sura nzima ya swala hili. Katiba inaweza kukataza ktk kifungu hiki lakini kuna kingine kinachowezesha hoja kisheria hata misahafu na Biblia inatakiwa uzisome vizuri kuelewa kipi kimetangulia kipi..Misahafu inakataza kuua, lakini pia inaruhusu self defence, jino kwa jino na kadhalika.. hizi zote zinapingana na amri moja kubwa sana!

Mkuu swala la kurekebisha katiba ni swala limeandaliwa na Binadamu sio msahafu, na kutokana na mitazamo kama hii ndio maana haiwezi kubadilishwa leo ama kesho, swala la OIC lipo miaka 14.. na viule vile kuna maswala kibao ya haki ambayo hadi kesho CCM wamekataa kubadilisha, hii haina maana wananchi wakubali waukalie kimya Ufisadi kwa sababu ati umepambwa na Azimio la Zanzibar...
Tunaweza kubisa kupiga vita Ufisadi bila kusubiri marekebisho yoyote, zaidi ya hapo Azimio hilo liliandikwa na watu sawa na katiba inayopigiwa kelele leo ina makosa kibao..Hili ni mojawapo tu.
 
Mwanakijiji,
Mkuu wangu hapa umelewa! nakuaminia sana katika fikra huru lakini kusema kwamba Hatuwezi kujiunga na jumuiya fulani kwa "manufaa" ya sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndiyo mzee, tunajiunga aidha kwa manufaa ya taifa zima au hatujiungi. Kama ni kikundi kimoja cha watu kinatakiwa kujiunga hilo linawezekana kama hiyo taasisi inaruhusu kundi hilo kujiunga.

Ndio sababu Makanisa ya Kiprotestanti Tanzania yanaweza kujiuna na Baraza la Makanisa Duniani (WCC) bila kulazimisha nchi nzima ya Tanzania kujiunga. Kuna taasisi mbalimbali duniani za Waislamu ambazo jumuiya za Kiislamu ni wanachama na hakuna mtu anayepinga wala mwenye haki ya kupinga hivyo.

Ni sawa na kusema hatuwezi kujiunga na jumuiya fulani kwa "manufaa" ya kundi moja la wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... yet tumejiunga na jumiya za wanawake duniani na Mama Mongella alikuwa secretary General..

Hapa umekosea kidogo. Mama Mongela alikuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Wanawake kule Beijing. Mkutano huu ulikuwa ni wa Umoja wa Mataifa (nchi ambayo Tanzania ni mwanachama). Hivyo Tanzania haikuwa imejiunga na jumuiya mpya bali ni Jumuiya ya Umoja wa Mataifa.

Na ni katiba hiyo hiyo inaweza kutumiaka kupinga kitu kile lakini kwa sababu mazngira tunayoishi ndiyo yanasukuma baadhi ya ibara za katiba kuwa na nguvu na zenye msisitizo ktk haki za wananchi wake.
Hivyo hivyo katika swala la Muungano, values za Wazanzibar kama Waislaam ni lazima ziwe sababu kubwa kwao kuweza kuhakikisha hawapotezi values hizo ktk Jamhuri yetu..

Hili ndilo kosa nadhani lililopo. Siyo jukumu la serikali kulinda value za ukristu au Uislamu wa mtu. HIlo ni jukumu la taasisi za kidini. Serikali inapoingilia kati na kufanya kazi ya makanisa na misikiti inavuka mpaka wa kuwa serikali isiyo na dini na kuingia kwenye anga zisizo zake.

Mkuu nina hakika kabisa kama Bara tungekuwa na asilimiam 99 ya wakristu na kuna baraza la wakristu duniani linalosajiri nchi za kikristu, tusingekuwa na mjadala huu hata kidogo. Rais, iwe Nyerere, Mwinyi, Mkapa ama Kikwete wote wangepitisha bila hata kumuuliza mtu..

Wangefanya hivyo wengine tungeendelea kupinga tu; ni principle. Wewe unaangalia wingi wa watu kuhalalisha hili mimi naangalia principle. Nchi ya Uturuki ni nchi yenye waislamu wengi lakini kwa makusudi kabisa wamekataa kuifanya nchi hiyo kuwa ya Kiislamu na wakati wowote wanasiasa wanapoisogeza nchi kwenye masuala ya dini, wanapata onyo lililowazi kutoka Jeshi. Hiyo ni principle. Na wale wanajeshi wanaopinga hivyo ni Waislamu vile vile wanapenda maisha yao ya kuwa taifa secular.

Sasa sisi kama Taifa hatuwezi kujiunga na taasisi hiyo kwa ajili ya upande mmoja tu wa nchi.

Mkuu hili ni baraza tu la nchi za kiislaam ambalo lina malengo sawa kabisa na mabaraza mengine yanayokusudia kuendelea Umma wake kwa kupitia mijadala..

Ni kweli kuwa ni baraza tu la "nchi za Kiislamu" na lina malengo yake ingawa si "sawa" na mabaraza mengine. Malengo ya OIC yamelenga dini ya Kiislamu na hiyo ni haki yake kabisa. Sasa kwa Taifa letu kujiunga ni lazima kwanza ikubali malengo hayo kwa kufanya hivyo itakuwa itakuwa mara ya kwanza katika historia ya nchi kwa serikali kuamua kujiunga na taasisi ya kidini ikiwa imekubali malengo yake yote (kwani haiwezi kujiunga na taasisi kwa kukubali malengo ya misaada tu na kuacha yale mengine)

Sioni kitu kikubwa ambacho wewe unakizungumzia unaposema wakiondoa hiki ama kile.. Mkuu ni sawa kabisa na mkeo anayetaka kwenda ktk maandalizi ya Kitchen party unaanza kutazama orodha ya maandalizi kama Mwanaume na kutoa suggestion ambazo zinapinga women to be women..Ulichoombwa ni ruksa yako tu..Mkuu wewe hauhusiki na Kitchen party hivi kweli utaweza kuvaa khanga hata wakikualika?..

Mzee ingekuwa OIC ni kama mke na Tanzania ni kama mume, hata nisingehangaika kwa maana mambo ya kina mama ni ya kina mama. Hili linahusu Taifa. Ukilifikiria katika picha ya mambo ya mke na mme utamiss uzito wa suala hili.
 
Shedafa,
Mkuu hakuna mahala nimejaribu ku twist, yote niliyoandika ndio hali halisi na pengine wewe ndiye unayevuta hata yale yasiyokuwemo..
1. Muafaka ni wa vyama hauhusiani kabisa na katiba ya Muungano..
2. hakuna mahala popote panapoonyesha Zanzibar hawaitambui katiba ya Muungano, kama kweli wasingekuwepo wawakilishi wao ktk bunge la Muungano..

Katika kujadili kwangu najaribu kutumia lugha na mifano ambayo ipo ktk maisha yetu ili kutoa sura nzima ya swala hili. Katiba inaweza kukataza ktk kifungu hiki lakini kuna kinginer kinachowezesha hoja kisheria hata misahafu na Biblia inatakiwa uzisome vizuri kuelewa kipi kimetangulia kipi..
Mkuu swala la kurekebisha katiba ni swala la Binadamu sio msahafu, na kutokana na mitazamo kama hii ndio maana haiwezi kubadilishwa leo ama kesho, swala la OIC lipo miaka 14.. na viule vile kuna maswala kibao ya haki ambayo hadi kesho CCM wamekataa kubadilisha, hii haina maana wananchi wakubali waukalie kimya Ufisadi kwa sababu ati umepambwa na Azimio la Zanzibar...
Tunaweza kubisa kupiga vita Ufisadi bila kusubiri marekebisho yoyote, zaidi ya hapo Azimio hilo liliandikwa na watu sawa na katiba inayopigiwa kelele leo ina makosa kibao..Hili ni mojawapo tu.

Nilijua utakataa kwa kuwa umedhamiria kufanya hivyo.
1. Unaelewa nilitaka kuzungumzia nini niliposema muafaka(kero za muungano), lakini tena kwa makusudi ukaamua kutwist na ndipo ninaposema taabu ipo. Ndugu sisi ni watanzania hepu tutazame mambo kama watanzania.
2. Najua unajua wazi kwa kauli zao viongozi wa Zanzibar wamesema hawaitambui katiba ya muungano na kwamba haiwahusu, au kwa kuwa uko mbali mkuu hujui yanayotokea nyumbani?. Kumbuka suala la Zanzibar ni nchi au si nchi, halafu jaribu kurecall matamshi ya viongozi wa Zanzibar.

Wala sikusema katiba ni msahafu, ila ninachosema katika hali iliyopo katiba haitoi mwanya huo. Kwangu mimi kushungulikia kero za muungano ndio jambo ambalo lingekuwa la maana zaidi kuliko kukimbilia OIC, maana kama mwisho utakuwa mwema hata nani anataka nini na tufanyeje itakuwa rahisi.
 
Back
Top Bottom