Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Kila dini ina utaratibu wake you can't equate.Hapo tatizo linapokuja.suala hapa ni kwamba kama kujiunga na OIC hakubadilishi wakristo kuwa waislam iweje maaskofu wawe na papara ya kuanza kutoa shutuma kama zile.mimi kama muslama nimekuwa nawaheshimu sana maaskofu kwa sababu walikuwa hawaropoki hovyo but this time wamejidhihirisha kwamba wanachukia waislam.that is bad.wame react kutokana na taarifa za vyombo vya habari bila kuchunguza ukweli wa jambo.tabia hii iko kwa baadhi ya ma-sheikh wetu.watu wa dini hawapaswi kuwa hivyo.hapo shetani amecheza karata yake.kuhusu mashirika ya kidini ya kikristo kutoshirikisha serikali inaeleweka kuwa .ukristo una mfumo wa uongozi wa pyramid lakini kaw dini ya kiislama uongozi wa aina hiyo haupo.
 
Mimi kama muislamu katika uchunguzi wangu nimegundua nchi zote zenye idadi ya wakristo na waislamu inayo karibiana suala la IOC linakua na malumbano na mvutano mkubwa e.g Naigeria.Katika nchi ambayo wakristo ni wengi sana hawalioni swala hili kama ni baya sana kwakua wana 'numerical safety'.Katika nchi ambazo waislamu ni wengi sana hili swala linaonekana 'inevitable'.Kwa Tanzania sidhani kujiunga na IOC ni kuzuri.Kuhusu Kadhi mi naona itakua vizuri kama hii itakuwepo kisheria lakini serikali isihusike kuigharamia na jukumu hili liwe la waislamu.


Unachosema ndugu yangu ni kweli kabisa hasa kuhusu unachoita "numerical safety". Inapotokea kuwa kundi moja ni "considerable minority" swali haliwi tatizo sana kwa sababu tishio linakuwa dogo. Lakini kwa Tanzania hali ni tofauti kabisa na asiyeweza kulitambua hilo haitakii mema nchi hii. Haya malumbano peke yake yanaashiria kuhatarishwa kwa amani kama hekima na busara hazitatumika kushughulikia hili jambo.
 
Bado mi natafuta reasons za kwa nini OIC inakuwa issue leo sijaziona. Ukiangalia waislam it is all emmotions. Hatuoni substance katika argument zao. Ikiwa argument hazina substance Kiasi hicho kwa nini waislam wanang'ang'ania OIC? Hapa ni obvious kuna hidden ajenda iliyoko behind all this. Huwezi kuamini, ukisoma makala zoote zinazotetea kuingia OIC, kuna hoja mbili pekee;

1. Misaada
2. Nchi nyingine zimejiunga na hakuna madhara

Sipendi na sitaamini kuwa hizi ndio sababu pekee zinazofanya jazba zote kuwaka kama ninavyoona. Waislam wametoa mfano wa nchi ambazo zimejiunga huko ambazo hazina madhara yoyote. Lakini wameshindwa kushawishi hiyo misaada imeleta manufaa gani yanayowafanya waislam wa nchi hizo kuwa bora kuliko wa Tanzania.

Kenya kuna Mahakama za Kadhi. Je wanataka watuaminishe kuwa waislam wa Kenya are better of kwa kuwa wanapeleka Mashauri yao ya Mirathi kwenye Mahakama ya Kadhi? Uganda wako OIC. Je waislam wa Uganda ni bora kuliko wale wa Tanzania kwa kuwa Tanzania si mwanachama wa OIC? ..... Ni kweli hayo?

Hivi nini kinatutofautisha Tanzania na Kenya na Uganda? Si ni hii hii misingi ya kuwa na zero tolerance kwenye mambo ya dini na ukabila? Kuna watu hapa wanaamua kutikisa nguzo za hicho tunachojidai watanzania kuwa tunacho....AMANI. Amani haikujengwa kwa lele mama. Tanzania, kati ya vitu tulivyokuwa tunaheshimiwa kwavyo, ni hii ya kuwa na msimamo unaoeleweka kuhusu mambo ya dini na ukabila. Sasa tunawatamani wale walioshidwa kwenye hivi vitu. This is a big cause of concern and shameful.

Nimesema tena sioni substance katika argument za kwa nini tujiunge OIC au tuanzishe Mahakama za kidini ndani ya mfumo wa serikali. Tulikuwa tumefanikiwa ku tenganisha utawala na dini. Sasa tunataka kurudi hatua hamsini nyuma! Lazima wanaotetea haya mambo wanazo sababu ambazo hawazisemi waziwazi. Na hii ndiyo shida yangu kubwa. Waislam, tafadhali tokeni nje mseme sababu hasa ni nini? Kwenye maandamano ya mashehe mojawapo ya jitihada za kutetea kuingia OIC shekhe mmoja alisema mbele ya vipaaza sauti kwamba "hii si tasisi ya kidini". Hivi aliamua kudanganya makusudi au alijua anachokifanya?

Waislam wanadharauliwa, wengine wanasema tunatawaliwa kikristo. Hizo zote ni jazba tuu na huwezi ukazitumia hizo kumshawishi mtu ambaye yuko impartial kuwa waislam wanadharauliwa. Hili suala la waislam ooo hawakusoma sijui nini sasa hivi is non issue. Sasa hivi numbers za waislam waliosoma na wakristo waliosoma hazitofautiani sana. Sema tatitizo ni kuwa jamii yetu yoote bado ni hoi bin taaban kiuchumi na kielimu kwa ujumla wote (the big majority live below poverty line and has less than basic education)

Ndio maana tunataka kukata miguu yetu ili tufanane na Uganda, Sudan, Somalia and the likes. Tunataka na sisi tubaki na mguu mmoja kwa sababu sisi tuna miguu miwili wakati majirani zetu wana mmoja. tunawatamani and this is really shameful!
 
Wajameni mkimaliza mjadala wa OIC, nifahamisheni kwanini tuko katika jumuiya ya Commonwealth!!!

kama kuna vigezo muhimu zaidi ya kujitambulisha kuwa tulikuwa watumwa wa mwingereza!!!!!
 
Field Marshall ES,
.............Kuna watu wanauliza kuhusiana na OIC kuwa haiwezi kutusaidia, ajabu ni kwamba kwa miaka 20 iliyopita Wakristu wamekuwa wakitegemea misaada toka vyombo vya Kikristu, wamejenga mashule, hospital, wamefungua NGO kibao na kadhalika, na hakuna mtu aliyezungumzia kwamba misaada hiyo haitusaidii kitu tena basi kama unakumbuka nilipiga vita swala la Elimu na Afya kuwa mikononi mwa taasisi za kidini hapa hapa JF. Wengi walikanusha na kusema Waislaam nanyi fungueni zenu hakuna mtu anayewakataza.. Leo hii waislaam wamepata chanzo imekuwa swala la nchi yetu haina dini..Je, huko nyuma hamkuliona hilo!

..

Kwanza mkuu kumbuka kuwa vyombo vya kiislamu havijawahi kukatazwa kufanya haya uliyotaja hapo juu. Na pili OIC siyo NGO, ni Inter-governmental organization. Hivyo vyombo vya kikristu unavyosema vimesaidia kujenga mashule nk siyo muungano wa nchi za kikristu, na wala serikali ya Tanzania siyo mwanachama huko. Huu ulinganisho unaoutoa hapa haufanani hata kidogo, na kwa hiyo hauwezi kuhalalisha Tanzania kujiunga na OIC.
 
Phillemon Mikael,

........Kwa hiyo kama kweli Wakristu wanakataa kabisa nchi yetu kujiunga na OIC, basi kuna kila haja ya kutazama NGO zote za kikristu zinazofanya kazi Tanzania.. Kwa sababu hoja kubwa hapa ni kuwa nchi yetu haina dini kwa hiyo hairuhusiwi kabisa Taasisi yoyote kuingia nchini ikiwa na malengo ya kuboresha (kundi la watu) dini ama dhehebu moja..
Laa sivyo basi kuna hatari kubwa ya kuvunjika Muungano ambao mwalimu aliujenga kwa miaka 23.. na dalili zake zimefikkia kikomo..hakuna kurudi nyuma tena!

Nakukumbusha mheshimiwa, OIC siyo NGO, ni muungano wa nchi za kiislamu, yaani serikali zake, hii ni IGO (intergovernmental organization). NGO inapoomba usajili na kufanya kazi nchini, haihitaji nchi hiyo kuwa mwanachama wake, bali yenyewe NGO inafanya kazi nchini kwa kuzingatia masharti itakayowekewa na nchi husika. Hii OIC haiji kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya nchi ya Tanzania, bali yenyewe ndiyo inayoiwekea nchi masharti kuwa lazima ijiunge na ifuate masharti yao ndipo tupate hayo inayoleta.

Halafu kuna NGO nyingi tu za kiislamu zinazofanya kazi Tanzania, zote hizi pamoja na zile za kikristu na zisizokuwa za kidini zinafanya kazi chini ya masharti yanayofanana ambayo ndiyo yanayotawala usajili wa NGOs, na yako wazi kwa mrajis wa NGOs katika Wizara ya Mambo ya Ndani.

Sasa wewe hapo unalalamika kama vile OIC ni NGO ya kiislamu iliyokataliwa kuingia Tanzania, kumbe ni kinyume chake kabisa, yenyewe ndiyo inataka Tanzania iingie huko OIC! Ufananisho kama huu ndugu yangu ni upotoshaji kabisa, na ninapenda kuamini kuwa umefanya hivi bila kutafakari vizuri, maana sidhani mtu kama wewe unaweza kukusudia kupotosha. Tanzania kuna NGO za kiislamu nyingi tu na zinafanya kazi zake kwa mujibu wa katiba ya nchi ndio maana zimeendelea kuwapo.

Hili nitarudia hadi watu wazoee: Nchi inajiunga na umoja wa kimataifa pale malengo ya umoja huo yanapoafikiana na malengo ya nchi husika, bila kuathiri masharti, misimamo ama maslahi yoyote ya taifa hilo au katiba yake. Na huko nyuma nimetoa mifano kwa kutumia malengo ya OIC yaliyoainishwa katika katiba yake, nikasema haya malengo hayaendani na misimamo yetu ya kitaifa, na mengine yanapingana. Hatuwezi kujiunga kama taifa katika taasisi ambayo mojawapo ya malengo yake ni "kueneza mafundisho ya kiislamu" wakati hili si mojawapo ya malengo yetu ya kitaifa, wala hatuna sera ya kidini ya kueneza mafundisho ya dini yoyote. Hapo serikali itakuwa imekosa impartiality.

Ni kama leo kwa mfano usikie kuwa Wizara ya Michezo imejiunga na Timu ya Yanga, pale makao makuu pamegeuka tawi la Yanga ! Sasa hapo wadau wa timu nyingine wakilalamika tutashangaa nini? Kwamba wizara ya michezo badala ya kuweka mazingira ya kuwezesha timu zote kuendelea, kumbe yenyewe imekuwa tawi la timu mojawapo? Hiki ndicho kingine ninachopinga.

Waislamu na watu wa dini nyingine wajiunge na taasisi zao wanazopenda, lakini serikali iendelee kuwa neutral, isijiunge na taasisi ya dini yoyote.
 
Kithuku,
Ni wapi nimeandika kuwa OIC ni NGO? soma vizuri nilichoanmdika labda rudia mara mbili tatu utaelewa zaidi..Tunazungumzia kazi za OIC na kufananisha na NGOs ktk misingi ya vyombo vya dini moja kuwa swala la Taifa ambalo halina dini..
Naelewa wazi kuwa boyfriend sio mchumba, na ni tofauti kati ya mwaname na mwanamke unapolitazama lakini kama swala ni ngono kuharamishwa basi iwe pande zote na sioni sababu ya ndugu kukashifu jinsia nyingine ati kwa sababu tu hawafanani..
Hata hivyo OIC sio chombo kama unavyotaka kukizungumzia. OIC ni Islamic Conference kama ile ya Wanawake duniani ambayo mama Mongella alikuwa secretary General, ama Sullivan na kwa uhakika zaidi imesajiliwa na UN...sio kitu kimeundwa tu chini ya mbuyu.
Mkuu toka nimeandika leo yaweza kuwa hoja ya 100, sijaona mtu akijibu maswali yangu hata moja kwa ufasaha zaidi ya kuzungusha na kutafuta makosa madogo madogo wakati mnaelewa fika nazungumzia kitu gani..Soma malengo ya conference ya Wanawake duniani kisha nambie kuna kipi kinachokubaliana na mawazo ama mtazamo wako..
Nimewauliza maswali mengi kuhusiana na Jumuiya ya Wanawake hamkujibu kitu mnababaisha kuwa swala la Wanawake ni tofauti halafu hamwandiki utofauti wake nini ikiwa ni nyie mnaodai kuwa hamna Ubaguzi..tumekwenda wee na taasisi kutokuwa nchi hadi nimewapa Vatican na kuonyesha wazi kuwa ni Taasisi kwanza kabla ya kuwa nchi..bado mkazunguka kutafuta pa kutokea...
Mnaelewa swala la Wanawake na jinsia, Makabila na Ukabila, rangi na maswala ya racejinsi tunavyoyapiga vita lakini inapofikia swala la Dini mnataka kujenga hoja za Kikomunist huku mkidai hamna Udini..

Nitatumia mfano wa Pundit, kuwa pamoja na kwamba tunategemeana ni lazima kila mmoja wetu ajitegemee..Waislaam kwa Wakristu tunategemeana kama ndugu na taifa moja lakini kila dini ni lazima ijitegemee...Kumwezesha mmoja wetu ajitegemee haina maana ni muhari kwako..Hoja yangu ni katika kujitegemea huko ambako maamuzi ya waislaam hayatakiwi kutolewa na wakristu hali wao hakuna mtu anayetoa maamuzi ya uendeshaji wa dini yao wala marafiki wao...
Mtazunguka weee, lakini ukweli mnaupata, hamna hoja zaidi ya kutaka kuwa madikteta tena wa Kikomunist!...
 
Kithuku,
Nimekujibu ktk moja ya mada kama hii tazama...jenga hoja mkuu usitafute vijisababu.. NGO sio NGO haisaidii kitu kwani hili ni baraza la waislaam duniani mnapiga kelele ingekuwa NGO sii ndoo mngeua mtu!
 
Kuna kisa niliwahi kuambiwa na babu yangu ambacho mila nyingi za kiafrika zimeongelea,zamani za kale kuna mtu alienda kukusanya kuni akakusanya nyingi sana,akazifunga na kujaribu kuzibeba akashindwa.Akaziweka chini na kurudi msituni kuongeza zingine,mtu akapita na kumuuliza mbona hizi zimekushinda huko unaenda kufanya nini,akajibu naukomesha mwili wangu kwa kuniangusha.Mimi naona tuna 'OVERLOAD' the system tungeachana na hilo la OIC ambalo ni la 'prestige' zaidi na kulishugulikia la Kadhi ambalo mi naona litagusa maisha yetu zaidi na kuondoa malalamiko mengi.Halafu tusiwashangae wakristo kwa kustuka na kuhoji kwanini suala la OIC huwa linapamba moto Rais akiwa muislamu.Nilidhani wakati wa Mkapa ulikua mzuri zaidi kumbana atoe maamuzi na kila mtu aendelee na mambo yake.Hii ya kurudisha suala baada ya miaka yote hii itatonesha vidonda.Hii dhana ya kuendeleza nchi kwa kutegemea misaada mimi na wengi humu tunaipinga vikali bila kujalisha misaada inatoka wapi.
 
Thanks MAMA nimekulewa UK’s first official sharia courts na wanatakiwa wengine waisome vizuri kabisa

Pia nataka kumwambia OPAQUE kwamba tuelewe uzuri Serikali sio itabeba mzigo wa OIC itapata manufaa
hichi chama pia ni kwaajili ya kusaidi wailsamu ina wadhamini wa kiislamu huko mbele wananapesa za kutosha na sio mzigo kwa serikari ni kama Roman catholik wanavyopata pesa kutoka Roma
pia tusiifanye nchi kuwa na migongano ya kidini kutokana na Maaskofu kuwa wanasikilizwa na Serikali je Waislamu waki simamsha jambo wanalotaka kufanya Maaskofu Serikali itakuba?
 
Unachosema ndugu yangu ni kweli kabisa hasa kuhusu unachoita "numerical safety". Inapotokea kuwa kundi moja ni "considerable minority" swali haliwi tatizo sana kwa sababu tishio linakuwa dogo. Lakini kwa Tanzania hali ni tofauti kabisa na asiyeweza kulitambua hilo haitakii mema nchi hii. Haya malumbano peke yake yanaashiria kuhatarishwa kwa amani kama hekima na busara hazitatumika kushughulikia hili jambo.

Wacha nikueleze hili. Nakubaliana nawe moja kwa moja. Ila nisikilize na mimi. Tanzania ni nchi mbili Tanganyika (Tanzania Bara) na Zanzibar. Kwa mujibu wa hoja zako mwenyewe kama nchi hizi zingekuwa (separate) Ni mizengwe kidogo kwa Tanganyika kuingia OIC (nakuibaliana nawe-isiiingie). Lakini kwa Zanzibar(ambayo ina 99 asilimia waislamu) siyo tatizo. Sasa hii Zanzibar ndiyo inataka kuingia OIC kwa faida yake na wananchi wake (kama Zanzibar). Tatizo haiwezi kufanya hivyo kwa kuwa haina milki ya dola, milkimya dola (soveirnity) iko kwenye Jamhuri. Sasa kuna tatizo gani kwa Jamhuri kuingia OIC ili ikidhi matakwa ya Zanzibar. Na OIC hii ikaishia huko huko Zanzibar (nchi moja ya Jamhuri) tu. Bara msiwe na hofu sio nyinyi mtaokwenda kwenye vikao vya OIC, bali ni SMZ. na mishafu haitakwenda Peramiho, bali itakwenda Chokocho na Ndijani ambako huko wananchi (Watanzania) wataipigia vigelegele. Tuwe na busara jamani. Tunabishiana kitoto kabisa, na tuna haki ya kuchekwa kwa kukosa busara. Tanzania kama Jamhuri ya Muungano ni lazima iingie OIC sasa, Tanzania kama ni Tanganyika basi na ibakie kulumbana.
 
OIC: Kichocheo cha kiuchumi au mwanzo wa mgawanyiko?




Salehe Mohamed

JUMUIYA ya Nchi Kiislamu (OIC) ni jumuiya ya pili kwa ukubwa katika nchi na kanda mbalimbali duniani, baada ya Umoja wa Mtaifa (UN) na ina wanachama zaidi ya 57 kutoka katika mabara manne.

Jumuiya hiyo iliundwa mwaka 1969 katika mji wa Rabat, Morocco, baada ya mkutano wa kihistoria uliofanyika nchini humo ikiwa na lengo la kusaidia Waislamu kiuchumi, kiutamaduni, kuendeleza amani katika nchi mbalimbali.

Mwaka 1970 mkutano wa kwanza wa mawaziri wa mambo ya nje (ICFM) ulifanyika Jeddah na kuamua kuanzisha sekretarieti ya kudumu, ambayo ilisimamiwa na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo.

Wakati OIC inaanzishwa ilikuwa na wanachama 30, lakini hivi sasa jumuiya hiyo ina wanachama zaidi ya 57 na pia imekuwa ikishirikiana na nchi mbalimbali pamoja na Umoja wa Mataifa katika shughuli mbali mbali.

Jumuiya hiyo imekuwa ikitoa mikopo isiyo na riba kwa nchi wanachama, jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na taasisi za fedha hasa za nchi za Magharibi ambazo zimekuwa zikitoa mikopo hiyo kwa riba, tena kubwa.

Kimsingi huo ndiyo muundo, lengo na kazi za OIC ambayo katika siku za hivi karibuni Tanzania ilitangaza nia yake ya kujiunga nayo kwa lengo la kupata faida zaidi kiuchumi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, katika mkutano wa 12 wa Bunge alieleza kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kutaka kuingia OIC na kuweka bayana kuwa tayari kuna vikao vimefanyika visiwani Zanzibar na wakimaliza huko watahamia bara.

Alisisitiza kuwa Tanzania kuingia OIC kuna faida kubwa zaidi kiuchumi na wala si kuiingiza nchi katika Uislamu, kwani kuna nchi nyingi ambazo si za Kiislamu lakini ni wanachama wa jumuiya hiyo.

Uganda, Msumbiji, Cameroon, Nigeria na nyinginezo ni miongoni mwa nchi zisizo za Kiislamu lakini ni wanachama wa OIC na hazijaingia katika itikadi za dini ya Kiislamu kama ambavyo baadhi ya Watanzania wanahofu iwapo Tanzania ikiingia.

Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo maskini dunia na kila kukicha imekuwa ikitafuta namna ya kujikwamua kwa kuota misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali, kukopa au kwa kutumia rasilimali zake.

Lakini nia ya serikali kujiunga na OIC imezusha malumbano makubwa zaidi miongoni mwa wananchi na kuibua itikadi na malumbano ya kidini, kiasi cha kuonyesha ufa na kuhatarisha umoja uliojengeka kwa muda mrefu ndani ya jamii.

Malumbano hayo sasa yamefikia katika hatua mbaya kiasi cha maaskofu kuonya kuwa mpango huo ni hatari kwa nchi na kama serikali itaendelea nao watajua nini cha kufanya.

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) nalo halikuwa nyuma kujibu hoja hiyo na kuweka bayana kuwa maskofu hao wasijipe makukumu yasiyo yao kazi hiyo iachiwe serikali.

Hali hali inavyokwenda kuna kila dalili nchi kuanza kugawanyika kwa misingi ya dini, jambo ambalo waasisi wa taifa hili, akiwamo Mwalimu Julius Nyerere walilikemea kwa nguvu zao zote. Inawezekana kabisa Tanzania ikaendelea kiuchumi bila kuingia OIC, kwani ina rasilimali nyingi zaidi kuliko nchi nyingi zilizojiunga na jumuiya hiyo.

Tatizo kubwa la Tanzania si OIC bali ni uongozi mbovu usioweza kusimamia vizuri rasilimali za taifa, jambo linaloifanya Tanzania kila kukicha kutembeza bakuli la kuomba misaada nje ya nchi na katika taasisi za fedha ambazo zimekuwa zikitoa masharti magumu katika utoaji misaada au mikopo.

Ni aibu leo hii kwa viongozi wa serikali kufikiria zaidi kuhusu OIC kuliko kufikiria namna ya kulinda na kutumia dhahabu, tanzanite, wanyama, almasi na rasilimali nyingine zinzopatikana Tanzania.

Kila kukicha viongozi hao wanaipigia debe OIC na jumuiya nyinginezo, lakini pia wnakuwa mstari wa mbele kuingia mikataba mibovu ya kumaliza rasilimali za nchi kwa masilahi binafsi au kwa masilahi ya watu kutoka nje.

Nisingependa kuamini kuwa kama Tanzania ikiingia katika OIC itamaliza shida zake za kiuchumi kama Membe anavyotaka Watanzania tuamini, kwani Tanzania imejiunga katika jumuiya nyingi, lakini hadi sasa matunda yake si makubwa.

Kuingia katika jumuiya mbalimbali si njia ya kufanikiwa kiuchumi kama uongozi hautakuwa imara. Badala yake itakuwa ni kuburutwa na kukubalina na kila kitu kinachozungumzwa na nchi wanachama wa jumuiya husika.

Haipendezi hata kidogo hadi leo hii kuna Watanzania wanaishi kwa kupata mlo mmoja kwa siku, hawana huduma za maji, umeme, hospitali, barabara na huduma nyingine za jamii.

Watanzania hao wanafaidika vipi na OIC kama si ushawishi wa viongozi kutaka kupata mirija mingine ya kupata misaada na kuitumia katika matumizi yasiyo ya lazima kama vile kununua magari ya kifahari, samani na kulipana posho?

Fedha za ufisadi wa EPA, Richmond, migodi ya madini na mingineo zinatosha kabisa kuwakwamua wananchi katika hali ngumu ya maisha kama viongozi wataamua kuyavalia njuga kuliko hata misaada itakayopatikani katika OIC.

Kwa nini hoja ya kujiunga katika OIC imeibuka kwa kasi hivi sasa miaka michache kabla ya Tanzania kuingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa na ule mkuu mwaka 2010? Hoja ya OIC ilishawahi kuanzishwa na Zanzibar takriban miaka 12 iliyopita na walipeleka maombi ya kujiunga nayo, lakini waliondolewa kwa maelezo kuwa hawapaswi kuomba wao kwani ni suala la Muungano.

Sasa hoja hiyo imerudi kwa nguvu zote huku ikipata baraka za Serikali ya Muungano. Hakuna sababu kwa Watanzania kuanza kugawanyika kwa misingi ya dini kwa kuwa Tanzania inaamua kuingia OIC, bali wanachopaswa kuanza kukifanya ni kutumia nguvu ya umma kuwabana viongozi ambao wanashindwa kufanya kazi zao ipasavyo.

Kwa hakika kama serikali haitakuwa makini na uamuzi wa kuingia katika OIC kuna kila dalili taifa likashuhudia mgawanyiko mkubwa zaidi wa kidini, ambao haujawahi kutokea na inawezekana kabisa katika siku za usoni zikaanza chokochoko ambazo mwisho wake ni vurugu.

source : Tz daima,jumapili,2,2008


tungewapata waislamu 100, wenye mawazo kama huyu,nchi ingepona.

waberoya
 
Waberoya,
tungewapata waislamu 100, wenye mawazo kama huyu,nchi ingepona.
Hivi wewe unafikiri unajua sana kutukana watu au sio?...
ubora wako nini hasa kwa sababu mkristu?
 
Macho_mdiliko,
Mkuu sikusema hakuna ktk vitabu isipokuwa mimi sijui, elimu yangu ndogo ktk maswala hayo toka vitabu vyote viwili. Na huyu mhuni alitumia maswali hayo akijua pengine hakuna na ndio maana nikalileta kwenu...mimi sina clue kabisaaa na kweli ni maswala nyeti sana.
Nakuomba sana nipe sura inayoizungumzia ubakaji wa watoto na rape utakuwa umenisaidia sana..
Kisha sababu hasa ya kuunganisha na mada hii ilikuwa kwamba sio lazima kila kitu kiwepo ktk katiba ili tuweze kuona mabaya ya kitu fulani... Tusipende sana kutumia vitabu ikiwa hata vitabu vikubwa vya dini kama Kuran na Biblia haikutaja mambo yote, kutotajwa kwa mabo hayo haina maana vitu hivyo ni halali...

Kama ulishakubali kuwa ni muhuni alikuambia hivyo...Hukutakiwa kuuleta mfano huo kwasababu ni wazi haiitaji kuwa na dini kutambua rape na ubakaji wa watoto kuwa ni jambo baya.....Utakuwa unakubaliana na ile notion kwamba bila dini sisi waafrika ni kama wanyama tu.

Dini ni institutions lakini uwezo wa kutambua jema na baya upo ndani ya binadamu mwenye akili timamu haswa inapokuja kwenye issue kama hizo za ubakaji wa watoto ambazo ni against humanity.

Mambo hayo ni mabaya na haijalishi uko dini gani kama wewe mbakaji ni mbakaji tu na sheria itachukuwa mkondo wake...Na ndio maana serikali haiitajiki kuwa na dini kwasababu sheria ni msumeno haujali sheick wala mchungaji...Kwenye sheria za nchi they are all equal...Same to muslims and christians etc.

Kutaka upewe sura za kwenye vitabu vitakatifu ili kujustify issue ya kujiunga na OIC ni beyond comprehension.

Na pia kusema kuwa sio lazima kila kitu kiwemo kwenye katiba ili kujulikana madhara yake na huku ukidai kuwa tuivunje katiba na kujiunga na OIC simply kwasababu ya mfano wako kuwa kutotajwa kwa mambo flani flani kwenye bible,quran ama katiba haina maana kwamba mambo hayo ni halali still ni contradiction na sioni basis za argument yako.....Umeshasema kama "Halijatajwa" haina maana kuwa ni baya...Sasa kwani hujui kuwa tayari "lilishatajwa" kwenye katiba yetu? Kwamba seriakali haina dini?

Ni wazi kuwa kuna waislam na wakristo ambao watapenda kuona kuwa kama kweli mataifa hayo yana nia ya kuwasaidia waislam...Then waendelee kuwasaidia bila ya masharti kama yale ya kikoloni ya zamani...Unconditional help wanajuwa cha kufanya....Mambo ya you are either with us or not hayatatusaidia sisi waafrika....

Ni wakati wa sisi waafrika kuwauliza wao wanaojiita wafadhili na huku wakituwekea masharti ya kutugawa...Ni wakati wa kuwauliza...ARE THEY WITH THE PEOPLE OR NOT? ARE THEY WITH US? I mean US AFRICANS?
Ili kuondoa ambiguity....Hao waarabu wanadai wanataka kuwasaidia wananchi...Then huku wakisema ni kuwasaidia waislam....Sasa nani kawakataza? Kama ni kweli ni kuisadia nchi....Kwanini iwe waislam tu kwa kupitia serikali na uvunjaji katiba?

Kuna institutions nyingi tu za kuweza kupitishia misaada na wanaweza wakafanya utaratibu.

Hata Wakristo wangekuwa na utaratibu kama huu pia ningeupinga kwa nguvu zote..Utaratibu wa kutugawa mpaka unashangazwa na watu kubadilika na kuwa watu wa ajabu ajabu kisa dini.
 
Mkuu wangu heshima mbele, mimi ninaheshimu sana dini za wananchi wenzangu, na naomba uniamini kwamba marafiki wangu wengi wa karibu huwa ni Waisilamu, nikiwa NY nimesaidia sana ndugu wabongo wenzangu waliokwama pa kulala na chakula, na hata kuwatafutia kazi mpaka walipoweza kusimama wenyewe kwa miguu yao,

infact mmoja wao nilimkuta kwenye Subway akiwa hana pa kulala bali analala kwenye hilo treni for at least one month, to the time nilipomkuta, na 95% yao hawa ndugu zangu walipofanikiwa tu nikalipwa mateke, the matter of fact nikiwa na mmoja wao siku moja tulivunjiwa tukaibiwa lakini vilibiwa vitu vyangu tu lakini sio vyake na tukow awili tu kwenye apartment, My point sio kujigamba ila kukufahamisha how sensitive we are kama binadamu, na kwamba na sisi at the end of the day ni binadam pia,

Lakini hapa mbele yetu, kwenye hili la kujiunga na OIC huenda tunaongelea moja ya sababu muhimu ya kuwepo kwetu hapa JF, yaani uchungu wa Taifa letu it is about my nation baby which happens to be yours too, I respect that kwamba mimi na wewe ni wananchi wa taifa moja, na tunaweza kujadili kwa upeo na mapana, bila noma.

Siku ya kwanza tu niliposikia tu hizi habari, nilizungumza na viongozi wetu wengi sana, na kati ya viongozi karibu wote nilioongea nao hiyo siku, kuna mmoja ambaye yuko kwenye Jumuiya moja ya kimataifa ambaye aliwahi kuwa foreign na anaijua hii ishu kwa mapana na marefu, yeye ndiye aliyenifungua macho zaidi kwa kuniwekea karata zote za pande mbili mezani ili niamue mwenyewe kusuka au kunyoa,

Ninaomba nirudie tena kwamba sina ubaya na mwananchi yoyote wa upande wa pili wa this ishu, sina tatizo na mwananchi yoyote wa dini tofauti na yangu, lakini hapa kuna taifa letu, na hii ni ishu moja kati ya chache sana ninayokubaliana na Mwalimu, Baba wa Taifa kwamba sisi Tanzania kwa sababu sio taifa la Kiisilamu, hatuwezi kujiunga na shirika la dini ya Kiisilamu.

Na ninaomba nirudie kwamba kwenye hili I make no bones about it, ni kwamba ninafanya kazi around the clock kwa kutumia kila nguvu niliyonayo mwilini mwangu, ku-reach out kwa anybody ambaye ni politically influencial or connected ninayewaza kumfikia in our nation, kuwaomba kwamba waelewe msimamo wa baadhi ya sisi wananchi wa Tanzania. Hii safari ndefu sana imenifikisha mpaka kwa baadhi ya Wakuu wa wilaya na tarafa, madiwani, RCs na the rest, kwa sababu kwangu hakuna tena ishu nzito katika our time kama hiii.

Ninarudia tena siamini kabisa kwamba behind hii ishu kunaweza kua na any national debate kuanzia level za intellectualism, academism, ideologism, religionism au politically! It is just what it is kwamba ninaamini kuwa shirika la Kiisilamu linatakiwa kuwa na members ambao ni pure Islams, Tanzania we are not!

Ahsante Ndugu Zangu Wote na Hapa ninaweka Chini Kalamu, Back To Work.

Sijui kama nina la kuongeza hapa. Lakini ni wazi kuwa kuna ujinga unaendelea hapa Tanzania. Huwezi kuamini kama waziri mzima kama Membe analeta issue kama hiyo ambayo watanzania wenye akili timamu wa dini zote wanaona si issue ya busara. Nature ya Tanzania na mambo ya dini inaeleweka, busara ni kwenda kwenye basics zetu kuhusu masuala ya dini. Na hiyo ni moja kati ya pillars za stability ya nchi yetu. Seems that Tanzania maslahi ya dini, vyama na watu benafsi yako mbele kuliko ya taifa zima.
 
Jmushi1,
Umeandika nini na mimi nimezungumza nini? hata sikuelewi.. Ulichosema wewe ndicho nilichokuwa nikisema.. soma vizuri maandishi ya mtu upate kuelewa..
Kisha swala la OIC limeingia vipi ktk vitabu vitakatifu?... mkuu hivi kweli unasoma vizuri maandishi ya watu ama?
 
Waberoya,

Hivi wewe unafikiri unajua sana kutukana watu au sio?...
ubora wako nini hasa kwa sababu mkristu?

Mkuu siyo kila mtu anayetoa hoja ya kupingana na wewe kuhusu OIC anakutukana.
Ni bora ujiulize kama wewe ni mwafrika kwanza then muislam ama muislam kwanza and then Mwafrika.
Tuangalie identity zetu ambazo zinatuleta pamoja kuliko denominations ambazo zinatugawanya.
 
JMushi1,
Unachotaka kusema ni kitu gani?.. nasema sikuelewi... wewe soma maandishi yangu kisha jaribu kutafuna kabla hujameza. na hakuna mahala nimesema umenitukana isipokuwa huyo mwandishi aliyetangulia aliposema - Tukipata waislaam kama huyu 100 nchi ita....
Haya ni matusi nikitumia usemi huo huo kwake yeye ama wakristu nitakuwa nimetukana.
 
Jmushi1,
Umeandika nini na mimi nimezungumza nini? hata sikuelewi.. Ulichosema wewe ndicho nilichokuwa nikisema.. soma vizuri maandishi ya mtu upate kuelewa..

Ni baada ya wewe kulinganisha issue ya rape kwa watoto nk kutokuwepo kwenye bible ama quraan....Sasa sijakuelewa ulipolinganisha hilo na katiba yetu..Maana kwenye katiba yetu liko wazi....Na hivyo basi ulitakiwa uelewe kuwa tayari tunaelewa kujiunga na OIC ni uvunjaji wa katiba.
Kusema hunielewi siwezi kushangazwa kutokana na kaluli yako hapo chini....

Originally Posted by Mkandara
Macho_mdiliko,
Mkuu sikusema hakuna ktk vitabu isipokuwa mimi sijui, elimu yangu ndogo ktk maswala hayo toka vitabu vyote viwili.

Hata hivyo nimeyasoma maandishi yako na kujitahidi kuyajibu kwa kadri ya uwezo wangu wa jinsi ninavyoelewa kuwa unataka tujiunge na OIC.
 
JMushi1,
Mkuu sina muda wa kubishana na wewe kwa sababu akili zako zinakutuma kwamba OIC ni Mkandara na hapa unataka kumjadili Mkandara.... sina muda huo.
na hakika hutaweza kunielewa hadi kiyama. Signature yako inatosha kueleza yote!
 
Back
Top Bottom