Hapa sio suala la kila dhehebu kuwa na mahakama, hakuna dhehebu wala dini nyingine isiokuwa uislam yenye sheria moja kwa umma wote. Uislam ni mfumo unaohusisha maisha yote kwa ujumla wake, tunayo madhehebi yetu lakini madhehebi yote hayatakuwa na sheria tofauti kwasababu waislam wote duniani tuansheria moja(japo wasiokuwa waislam wanajitahidi kutugawanya na kutufanya tujione sisi si wamoja) sasa woga wa wasio waislam ni kuwa kama tutaunganishwa na kadhi katika Mahkama na sheria basi inaweza kuongeza umoja wa waislam.
Ndugu kuna jambo moja nimeona niligusie...Kwanza si kweli kwamba kuna watu wanaotaka kuwagawanya waislam...Wao tayari wameshagawanyika na bado wanapigana kwa misingi kama hiyo..Tizama Huko Iraki na Iran....Hawa walizichapa kwa miaka nane...Na ni waislam walioshirikiana na Bush kuivamia Iraki...Na kina Abu Musab Al Zarqawi waliweka wazi kabisa kuwa Shia ni wasaliti wa Uislam na akasema na wao ni target.
Binafsi nachotaka kusema hapa ni kuwa waafrika tutagawanywa sana tu...Hilo halikuanza leo..Kama sio udini utaanzishwa ukabila nk.
Mwarabu na Mzungu tukiwaachia Afrika wataishi kwa amani? Hilo sidhani...Je na wao wanataka kutuachia Afrika yetu? Hilo pia sidhani.
Nachofahamu Afrika ni Tajiri sana...Ila migawanyiko ambayo haiko kwa bahati mbaya inatuangusha na kujikuta tunapiga hatua moja mbele na mbili nyuma.
Kwa mfano ni juzi tu waislam na wakristo walikuja pamoja kwenye issue ya ufisadi..Lakini ghafla hili la OIC likaibuliwa na Membe na kwa kusema ukweli mwisho wake unaweza kupelekea matokeo ya tofauti pale inapokuja kwenye muungano thabiti dhidi ya Ufisadi.
Kabla ya Mzungu na Mwarabu kuja Afrika dini zetu zilikuwa ni nini?
Na kama tuliletewa dini hizi...Ni kivipi zitugawe kiasi hiki?
Jana hapa USA nilienda kwenye ulitility store moja hapa kucheki some stuff for my dreadlocks...Store ni ya familia moja kutoka Egypt...Vijana ndugu wenye store hiyo wakaniuliza nimetokea wapi..Nikawaambia Afrika...Wakawa wanasisitizia Afrika nchi gani...Nikawa nawaambia Afrika na hiyo inatosha...Wao binafsi wakawa wanasema sisi tumetokea huko huko lakini Egypt, baada ya maongezi zaidi nikagunduwa kuwa wao hawaoni kama na wao ni waafrika rather ni wa Egypt.
Sasa kuna Afrika ambayo iko considered kuwa ni middle east..Kwamfano Morrocco, Algeria, Egypt nk...Waislam wao waniziita nchi hizi Masharik...Na magharib ni nchi kama Libya nk.
Sasa ni ramani mpya wanatuchorea Afrika ama?
Je sisi waafrika msimamo wetu bila kujali dini zetu ni upi?
Kwanini sisi watu weusi tuendelee kusikitisha kiasi hiki?
Inanishangaza sana kama tutaendelea kupigania maslahi ya waarabu na wazungu na kusahahu maslahi yetu sisi waafrika ambao tunaujali uafrika wetu.
Nani kasema kuwa kuwategemea hawa watu ndio solution ya matatizo yetu?
Juzi tu hapa tuliambiwa tujiunge na OIC kwasababu ya misaada...Je hao viongozi hawapiti hapa JF na kusikiliza maoni ya wananchi kuwa tatizo sio dini wala misaada bali ni ufisadi?
Hivi kweli viongozi wa Tanzania bila aibu mnadiriki kuwapelekea wananchi hoja kama hizi simply ili kupreserve power na kupata kura?
Ni wazi ccm msamba utapasuka kwasababu mnaendesha serikali kisanii na pia nadhani washauri wa Mh Rais si watanzania kabisa kwasababu hakuna Mtanzania atakayethubutu kuja na sera ya kuwagawa wananchi kama kweli ana fikra za kitanzania ambazo tumejijengea na kuwa mfano bora Afrika.
Ndugu zanguni nilishasema huko nyuma na nitaendelea kusema...Nina uhakika kabisa kuwa kuna waislam na wakristo wanaokubaliana kwenye issue hii kuja na solution itakayo epusha vurugu ama kutokuelewana.
Hivi ndugu zangu waislam mnakubaliana na serikali yetu kuwa ufisadi na umasikini umeenea kwasababu wakristo hawawapendi? Ama kwasababu haki za waislam hazizingatiwi?
Ndio maana JK anafanya analotaka kwasababu anajuwa kabisa ni kivipi atapata kura zake..Lakini sasa hivi wananchi walio wengi wamegunduwa usanii huo wa kulishwa chuki....Hilo linapelekea sana huko uswahilini kuridhika na shida kuliko kupatana na kafiri.
Wale wasiokuwa na elimu ambao ni wengi ni wazi tutawapoteza kwa ccm...Kwasababu kama wanaambiwa kuwa adui yako ni Mkristo...Basi usishangae wakasema kama walivyodai huko nyuma kuwa Mafisadi ndio makafiri....Just imagine kama wakristo na wao wangekuwa na elimu ya dini tu na bila elim dunia...Kungekalika?
Kuhusu maslahi ya Taifa langu nitapigania mpaka mwisho wa pumzi.
I wonder whose playbook all of this shit is comming from...Honestly....Inanikumbushia sana siasa za Karl Rove.
Ama kweli JK alikuja kujifunza politics za division hapa USA.