Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Shefada,

Na viongozi wa Dini nao wamelikoroga.

Ningekuwa mimi ndio uongozi wa Maaskofu, badala ya kutoa tamko la "Membe hatumbembelezi...anaingia kwenye mdomo wa chatu kichwa kichwa," ningejaribu kuomba ka conference na Mashehe na Waziri. Tukawa na dialogue.

Na ningekuwa mimi ndio uongozi wa Mashehe nisingesema tutaandamana "kujibu vikali" Maaskofu "wenye kiburi." Badala yake ningetumia lugha ya kiungwana zaidi.

Maaskofu na Mashehe nadhani hawakuwa responsible hapa.
 
Kuhani,
nafikiri maamuzi mengi yametokana na kutoheshimiana kati ya dini hizi mbili..pengine yawezekana imetokana na kushindwa kuvumiliana kiasi kwamba Uadui fulani uliojengwa rohoni mwetu na hadithi ama mafundisho ya vitabu vyetu ndiyo yanaanza kujitokeza.
Kisha nadhani pia muda wa kubembelezana umekwisha, jeuri ya maskini inaanza kujitokeza kwani siku zote mimi naamini matusi ya maskini ni mazito sana.. iwe kapata kidogo ****** yatalia mbwata, na yule asiyekuwa nacho roho inamkoroga kuhakikisha yeye ngangari jamaa hamtishi na vijisenti!.. Ni hulka yetu kutishana na matusi juu lakini inapofikia misiba sote hujiunga na kuwa ndugu tena..
 
Kuna ubaya gani kuanzisha uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na OIC kama ilivyo Tanzania na Vatikani?
 
Ogah,.................. Umesema misaada sio kabisa hoja ya msingi.. nakuomba unambie WHY?................

1. Tumekuwa tukipata misaada kama Taifa zaidi ya miaka 20...na hakuna mabadiliko zaidi ya hali za wananchi kuw ambaya siku hadi siku......na ndio maana....nika-support hoja ya Deny_all kuwa tusafishe nyumba yetu kwanza.

2. Msaada utakaokuja hapa hautamlenga mtu mmoja mmoja kama Ogah and the like au kikundi fulani cha watu.....utakuja msaada wa Kitaifa, na kama ni wa Kitaifa sababu No1 hapo juu inajieleza.......nothing new

3.Tumeshuhudia nchi kadhaa wanachama bado zikiwa ktik lindi la umaskini and yet no effort toka kwa OIC kuinua hali ya maisha........Rais wa Senegal kalizungumza hilo

4.kama ni Misaada/Mikopo ni one of the objective...............ingekuwa ni busara kwa OIC kuruhusu Islamic Development Bank (eg BADEA i.e. nchi za kiarabu) kutoa mikopo kwa nchi kama yetu......lakini si hivyo......pengine hili lingekuwa initiated na serikali yetu........kwa manufaa yetu sote....wakisharuhusu hilo hapo ni kutwanga project proposals tu.......tunasahau hii migongano isiyo na tija
 
...nafikiri maamuzi mengi yametokana na kutoheshimiana kati ya dini hizi mbili..pengine yawezekana imetokana na kushindwa kuvumiliana kiasi kwamba Uadui fulani uliojengwa rohoni mwetu na hadithi ama mafundisho ya vitabu vyetu ndiyo yanaanza kujitokeza.

Mkandara,

Unadhani tatizo liko katika hadithi na mafundisho ya vitabu vyetu, unaongelea Biblia na Kurani ? Mimi sidhani kama hivi vitabu vimeshambuliana. Nadhani kila kimoja kime claim kwamba kinachoongelewa humo ndio sahihi, lakini hakuna kilichoshambulia kingine. Sidhani.

Lakini nimependa ulivyosema kwamba Waislam na Wakristo hawaheshimiani. Ni watu wachache sana wanakubali kwamba kuna tatizo hapa. Wengi hupenda kusema tumeoleana, tumesoma pamoja, tumechumbiana. Lakini kwa kweli sidhani kama tunapendana kiasi hicho. Sidhani. We angalia mijadala hata hapa, mijadala ya kiutendaji ya NSSF na vifo vya watoto inavyogeuzwa na baadhi ya watu kuwa ya kidini, mijadala ya kiutendaji ya TISS inavyogeuka udini wa viongozi wake. Mambo kibao watu wanaibua udini. Kwa hiyo nadhani hii ya kusema tumeoleana inawezeka kuwa ni kuficha kidonda!!
 
Mwanakijiji,

Vatican is considered a country na je hii OIC nayo?

OIC ni jumuiya ya kimataifa na kama zilivyo jumuiya nyingine unaweza kuwa na hadhi ya kibalozi, ndio maana tuna Balozi Umoja wa Mataifa, tuna Balozi anayetuwakilisha kwenye mashirika ya Kimataifa pale Uswisi n.k Ubalozi si lazima kuwa ni nchi lakini una maana ya kutambuana rasmi, hivyo Balozi wa UNICEF nchini ambaye kwa kweli huitwa "Envoy" na si "Ambassador" (japo anaweza kuwa na hadhi hiyo) yupo.

Marekani ina Envoy (balozi) wake OIC na nchi kadhaa nazo zinazo. Hivyo utaona hakuna tatizo lolote lile la Tanzania kuwa na mwakilishi wake OIC au OIC kuleta balozi wake nchini na kuanzisha uhusiano rasmi. Zaidi ya yote, tayari kuna mahusiano na nchi mbalimbali za kiislamu ambazo zinabalozi nchini na hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye atapinga mahusiano hayo ya kibalozi.

Kuna ubalozi wa Iran, kuna ubalozi wa Libya, Palestina (ingawa hakuna nchi hiyo) n.k Mahusiano haya hayana buri kuimarishwa na kama ilivyotokea juzi wakati Membe alipoenda Iran na kutiliana mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na Irani. Binafsi nakubaliana na Membe hakuna ubaya wowote wa mahusiano hayo. Tatizo linakuja pale ambapo mahusiano mengine yote yanawekwa pembeni na aina moja tu inalazimishwa. Bado sijaelewa kama ni suala la dini, kiburi, ushindani, kisasi, wivu, husuda au kuoneshana ubabe. I still don't get it.
 
...................... Hao maaskofu wangeomba hivyo vyombo vyao kama World Vision wazidishe juhudi zao katika sehemu zilizo duni kimaendeleo. ....................................Nilisikitika hapo awali kumsikia Askofu mmoja akikiri kuwa hajaisoma katikba ya OIC lakini akisisitiza bado kupinga sisi kujiunga nao. Ni kama vile wenzangu walivyompandishia mori Salman bila kukisoma kitabu chake cha Satanic Verses!

........Hao ndio tunawaita maaskofu mbumbumbu!...........nafikri Kuhani kawapa jina sawia kabisa irresponsible askofu........

Kuhusu Word Vision kuzidisha misaada sehemu zilizo duni........ni wazo zuri.....nafikri pia inategemea sana na malengo ya organisation husika..........

....je Tanzania as a nation ni mwanachama wa World Vision?...........au World Vision ni kama NGO tu inayojishughulisha na maendeleo ya jamii?.......honestly inabidi ni-google nijue mlengo wake..........na nimeipata kama ifuatavyo


  • Our vision for every child, life in all its fullness;
    • Our prayer for every heart, the will to make it so
World Vision is a Christian relief, development and advocacy organisation dedicated to working with children, families and communities to overcome poverty and injustice. Inspired by our Christian values, we are dedicated to working with the world's most vulnerable people.

We serve all people regardless of religion, race, ethnicity or gender.
Our Mission
World Vision is an international partnership of Christians whose mission is to follow our Lord and Saviour Jesus Christ in working with the poor and oppressed to promote human transformation, seek justice and bear witness to the good news of the Kingdom of God.
source
World Vision International - Who We Are

na habari zao kwa undani waweza zipata hapa
World Vision International - Home
 

Matatizo ya Uganda, kimaendeleo hayakumalizwa na kujiunga kwao na OIC, kwa hiyo ni hoja finyu sana kwa waziri kutudanganya na hiyo hoja uchwara, Tanzania sasa hivi ni mwanachama wa jumuiya nyingi sana za kimataifa na tunashindwa kwenda popote kimaendeleo, sasa labda ifike mahali as a nation tujiangalie upya kama ni worthy sisi kuendelea na some of hizi international membership na hasa zile zinazohitaji yearly fee kuwa member, ikibidi tujitoe nazo, badala ya kulazimisha kujiunga na jumuiya hizi za kidini ambazo zina-guarantee mgawanyiko wa kisiasa na kidini kwa taifa lolote kama letu ambalo officially halina dini moja kama letu.
I do not care what hii ni jumuiya ya Wa-Islam period, Tanzania we have no business kujiunga na this kind of Jumuiya, kwa sababu sisi sio taifa la Kii-slam, na Membe should apologize to us the public for this nonesense ideas kama amezitoa under ministerial capacity. !

Mkuu!
You have driven the point home....... hii ndiyo hoja ya msingi tunayopaswa kuizingatia. Kwamba ni jumuiya ya dini gani ..si ishu...
Kama nchi ni kupoteza muda kuendelea kujiingiza kila mahali wakati for nearly 4 decades tumeendelea kuwa mkia kimaendeleo.
 
Mkuu Ogah,
Sidhani kama kuna shirikisho lolote la kikristu linalokubali uanachama wa nchi. Haya ni pamoja na World Vision, World Council of Churches etc. Tanzania kama nchi haiwezi kujiunga na haya mashirika. Ni madhehebu tu ya dini husika ndiyo wanachama.
 
Mi nadhani watanzania tunapenda sana malumbano. Hata wasomi ambao ungetegemea wawe na uelewa zaidi akina Membe and co..ndo hao wanatuaibisha.

Swala la OIC kama wachache walivyosema humu...ni swala dogo sana lakini ni kubwa vile vile. Wasomi wananshindwa kulewa kwamba hii IOC tofauti na mashirika mengine inagusa DINI na kama wengi tunavyojua DINI inagusa hisia za kila mmoja wetu Msomi kwa asiyekuwa msomi, mkulima kwa mfanyakazi. Wote wana namna wanavyoichukulia DINI. hivyo basi watawala wetu ingebidi from the beggining waelewe kabisa kwamba hili swala ni VERY SENSITIVE kwa hiyo linahitaji kuongelewa kwa namna ya pekee.

Kitu ambacho Membe na wenzake wangefanya ni kuainisha faida za OIC , ni kipi kama serikali na wananchi wake watafaidika. Na si majibu ya mkato kama wanayotoa wanasiasa sasa hivi. Tuchukue charter ya IOC tuichambue, tuanishe faida na hasara!

Harafu tuache unafiki sasa hivi WRONGLY or RIGHTLY uislamu umekuwa ukihusishwa na mambo negative sana kama ugaidi, kutoheshimu haki za msingi za wananchi wao..especially wanawake..na kukosa torelance in general...... na mengineyo...hili linawaogopesha wengi wanaposikia kwamba NCHI kama NCHI tunataka kujiunga na hiyo jumuia. Wengine wanadhani kwamba tutalazimishwa kusilimishwa! Ni fear kama hizi serikali ingebidi izitolee maamuzi na maelezo sahihi! na sio blah blah za kisiasa. Uislamu ni dini! So i expected jamhuri yetu tukufu kuweka msimamo rasmi kwamba sisi tunatafuta maslahi ya kiuchumi. wangeanza na kuwapa wananchi!

Harafu OIC kwa uelewa wangu ni INTERGOVERNEMENTAL ORGANIZATION ambayo ina malengo na madhumumni yake. Kwa hiyo ni lazima kila nchi inayoingia humo ikubaliane na hayo masharti. Je viongozi wetu wameyasoma na kuyaelewa hayo masharti? Tafadhali sana wananchi wenzangu, it is high timne we say enough is enough Huu mtindo wa kufanya mambo kimkumbo haitusaidii kabisa!

Tujiulize..hii OIC ina faida kwetu kama nchi? tumejiunga na mashirika kibao akina COMESA, SADC, AU, UN, EAC nk..leo inabidi tukae chini tujiulize....tumefaidika nini. Infact tumeondoka COMESA na sasa tuna-moot namna ya kuunganisha SADC, EAC, COMESA kiwe kitu kimoja! UNAKUTA MALENGO YALIYO KWENYE BLOCK MOJA KAMA SADC ndiyo hayo hayo yaliyoko kwenye BLOCK nyingine kama EAC AU COMESA! Infact sasa hivi ndo Project kubwa sana ya Africa Union KUUNGANISHA HAYA MASHIRIKA YA AKINA COMESA, SADC, ECOWAS nk. Maana imeonekana dhahiri yote yana malengo sawa! Sasa ni kipi kilichoko kwenye OIC ambacho hatujawahi kupata huko kote tuliko? kama siyo mkumbo na siasa za kuridhisha makundi fulani ?

Kwangu mimi having seen all these blocks za mashirika..sioni faida ya TANZANIA kama nchi kujiunga na OIC. Sana sana kuduplicate yale yale yaliyokwenye SADC, EAC nk!

Tatizo wengi tunaliangalia hili swala kwa minajili ya UDINI na kwa hapo daima hatutapata suluhisho! kwa sababu kila mtu anadhani ni UISLAMU VS ukristo. ILA WA KULAUMIWA NI WANASIASA WETU AMBAO WANA UPEO MFINYU WA KUCHANGANUA MAMBO ESPECIALLY VITU SENSITIVE KAMA HIVI.

Vatican huwezi kuilinganisha na OIC..ina hadhi ya nchi! Ndo maana wherever you go..Vatican at times known as Holly Sea..ina uwakilishi, sasa hiyo ni historical ambayo mimi na wewe hatujui...huyu Papa ilikuwaje akapata hadhi aliyonayo katika mataifa ya leo!. Hata UN Vatican ana kiti kabisa so is katika mashirika mengine. Ukienda UN..OIC...ina kitu kinaitwa Observer status..ina hadhi sawa kama IGAD, EAC nk...Anyhow..hili swala kiuchumi halina mantiki..ila kidini..big time! na wale wanaoona kwamba waislamu wanaonewa..basi its their chance to let the can loose!

So HII DEBATE..TUKIIANGALIA STRICLTY KWA PREMISE YA KIUCHUMI...I DONT SEE ANY SENSE YA KUINGIA HUKO...ILA KAMA NI KUWARIDHISHA WAISLAMU...BASI WAINGIE WAO KAMA BAKWATA (THOUGH I DOUBT KAMA BAKWATA WANAWEZA KURUHUSIWA..MAANA SIYO NCHI).
 
Bahati mbaya zaidi dini zote mnazozifia mliletewa na watu kutoka mataifa ya mbali na mkasahau na kutupa dini zenu za asili na sasa mko tayari hata kuchinjana kwa dini na kusahau tabia, mazingira, mawazo, fikra, tamaduni, mila na rangi zenu zinawaonyesha nyinyi ni wamoja.

Kwa nini hamtaki dini na viongozi wenu wa dini wasiohojiwe, wasipingwe au hata kukosolewa?. Na hao viongozi wa dini wanajijengea mazingira kwamba wanachosema au kuwaza wao ni sahihi nani kawapa uwezo huo, kama wanavyohojiwa na kuchambulia viongozi wa serikali na wao pia wanatakiwa kupingwa na kuhojiwa vilevile.

Kutukuza viongozi wa dini kuishie katika membari za nyumba za ibada wakitoka nje wajue Nchi haina dini na wachunge kauli zao kwa jamii isio wafuasi wa dini zao kwani hawalazimiki kukubali na kuamini wanachoona wao kinamaana.

Kwanini kila mjadala unaohusu dini uongozwe na jazba! Wabongo hawawezi kudhibiti emotion zao wakati wanajadili dini . Manake viongozi wa dini wanaipiga mkwara hata serikali? Hii sio poa na italeta fujo isiyo ya lazima.
 
http://www.oic-oci.org/oicnew/is11/english/Charter-en.pdf

Ukiangalia namna nchi zinavyoweza kuwa wanachama kuna mashaka kidogo hapa...nafikiri sensa ni muhimu. Pitia link hapa juu Kwa mfano the charter inasema ...Any State, member of the United Nation, having Muslim majority and abiding by the Charter, which submit an application for membership may join the Organisation....

Km tunaongelea Zanzibar ambayo AGs wameshasema ni nchi then wanaendana na Charter ikiwa ni Jamhuri ya Muungano au Tanzania bara (Km nchi....! AGs hawakutueleza km hii nayo ni nchi au kipande cha nchi....!) hapa pana shida kidogo
 
Nadhani wakati umefika sasa kwa serikali yetu ikarudisha uhusiano wa kibalozi na Israel ili Tanzania iweze kunufaika na misaada ya kiuchumi na kimaendeleo kutoka kwa Israel kama ilivyokuwa miaka ya mwanzo baada ya uhuru.

Tutafaidika sana na technologia ya kilimo cha umwagiliaji,ujenzi na technologia ya mawasiliano.
Wito kwa waziri Membe katika hili kwani sababu zilizofanya tuvunje uhusiano na taifa hilo teule la Mungu hazina nguvu kwa sasa kwa kuwa Tanzania tunachoangalia ni pesa na misaada tutakayopata.


Quote of the week :
"Hakuna ubaya kuchukua pesa ya shetani"
by Benard Membe ..Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania.
 
Katika hili la OIC sasa naona ni kwanini sisi tuko nyuma sana ktk kila jambo na pengine sifa yetu kuu ni kuiga, Kibaki aliingia madarakani na neno mafisadi Tz nao tumo na wimbo wa ku copy, hivi hatuwezi ku stick ktk ile misingi yetu kwa faida ya amani ya nchi hii.

Hapa ninamkubali Kambarage alipoweka msimamo juu ya Uongozi hasa ktk mambo ya msingi yanayoihusu katiba ya nchi.

2005 CCM ndiyo chama kilichoshinda, baada ya hapo JK akaunda serikali kwa ridhaa ya CCM, nifahamuvyo mimi ni kuwa " CCM ndio anayestahili kuhubiri policy au kubadili Policy zake, Serikali ya JK ipo pale kutekeleza manifesto ya 2005-10 na siyo kuibua policy mpya. Kazi hiyo ni chama, kama CCM ktk manifesto yao 2005-10 waliahidi kujiunga na OIC kama watapewa nchi vema kwa Membe kutekeleza maagano hayo maana ndio agenda iliyokubaliwa na umma uliwaweka CCM madarakani ila kama hili halikuwemo basi nami naungana na wote wanaomtaka waziri Membe ajiuzuru mara moja ili kulinda heshima ya nchi, Katiba na viapo vyote vya uwaziri na ubunge wake.

Namtaka aondoke kwani kwa makusudi ameamua kuivunja katiba ya nchi ambayo aliapa kuilinda, na kuitetea popote pale, ni mlevi wa madaraka wa wazi ambaye kwa masikio yangu nilikuwa namsikiliza akiongea na wanahabari juu ya hilo.

Huyo ni mvunjaji wa katiba wa waziwazi ambaye hana tofauti na mtoa rushwa au mpokea rushwa na mbaya zaidi huyo anatishia hata uhuru, utawala wa sheria na zaidi ulinzi wa amani.
 
Nadhani hii mijadala miwili inabidi iunganishwe. Ina content zinafanana sana, ile ya OIC na hii.

Pia naomba watu wajadili hoja na si waleta hoja, pia itapendeza msomaji akianzia mwanzo na si mwisho kurudi mwanzo!
 
OIC Members:
Afghanistan, Islamic Republic of 1969 Suspended 1980 - March 1989
Algeria, People's Democratic Republic of 1969
Chad, Republic of 1969
Egypt, Arab Republic of 1969 Suspended May 1979 - March 1984
Guinea, Republic of 1969
Indonesia, Republic of 1969
Iran, Islamic Republic of 1969
Jordan, Hashemite Kingdom of 1969
Kuwait, State of 1969
Lebanon, Republic of 1969
Libya, Socialist People's Libyan Arab Jamahiriya 1969
Malaysia 1969
Mali, Republic of 1969
Mauritania, Islamic Republic of 1969
Morocco, Kingdom of 1969
Niger, Republic of 1969
Pakistan, Islamic Republic of 1969
Palestine, represented by the Palestine Liberation Organization 1969
Saudi Arabia, Kingdom of 1969
Senegal, Republic of 1969
Sudan, Republic of the 1969
Somalia 1969
Tunisia, Republic of 1969
Turkey, Republic of 1969
Yemen Arab Republic 1969 From 1990 as Republic of Yemen united with People's Democratic Republic of Yemen
Bahrain, State of 1970 From 2003 as Kingdom of Bahrain
Oman, Sultanate of 1970
Qatar, State of 1970
Syrian Arab Republic 1970
United Arab Emirates, State of 1970
Sierra Leone, Republic of 1972
Bangladesh, People's Republic of 1974
Gabon, Republic of 1974
Gambia, Republic of the 1974
Guinea-Bissau, Republic of 1974
Uganda, Republic of 1974
Burkina Faso 1975
Cameroon, Republic of 1975
Comoros, Federal Islamic Republic of the 1976

Iraq, Republic of 1976
Maldives, Republic of 1976
Djibouti, Republic of 1978
Benin, Republic of 1982

Brunei Darussalam, Sultanate of 1984
Nigeria, Federal Republic of 1986
Azerbaijan, Republic of 1991
Albania, Republic of 1992
Kyrgyzstan, Republic of 1992
Tajikistan, Republic of 1992
Turkmenistan, Republic of 1992
Mozambique, Republic of 1994
Kazakhstan, Republic of 1995
Uzbekistan, Republic of 1995
Suriname, Republic of 1996
Togo, Republic of 1997
Guyana, Republic of 1998
Côte d'Ivoire, Republic of 2001
Suspended or Withdrawn
Zanzibar Jan 1993 Withdrew August 1993

Observer States
Bosnia and Herzegovina 1994
Central African Republic 1997
Northern Cyprus, Turkish Republic of (as Turkish Cypriot State) 1979 Official 2004
Thailand, Kingdom of 1998
Russian Federation

SOURCE
:Organisation of the Islamic Conference - Wikipedia, the free encyclopedia

Hebu tuelezaneni ukweli JF na wote wanaoshadidia Tanzania kujiunga na OIC kwa takwimu; Je, Uganda na Msumbiji wamepokea msaada wa USD kiasi gani tangu ijiunge na OIC? Mbona kuna nchi nyingi ziko hoi mno kama sisi pamoja kuwa wanachama wa OIC bado hali zao ni duni? Je, hao Wafadhili wa OIC ambao tunataraji msaada kutoka kwao wana utajiri gani kuweza kuzisaidia hizi nchi maskini nyingi?

Huyu Membe na Serikali yake wanatupeleka kusiko (ingawa anajidai amefanya utafiti; atueleze hizo nchi zenye blue font zimepata msaada wa kiasi gani na misaada hiyo imewasaidia kivipi kama nchi (si viongozi).

Mwisho ni vizuri Membe na Serikali kwa ujumla wajue kuwa misaada haitatusaidia kuondokzna na umaskini; lazima watupe maono yao ya kutupeleka huko kwenye Neema walipotuahidi wakati wa kampeni 2005 na si wanapotaka kutupeka sasa kwenye Vurugu tele!
 
Wale wote wenye nia njema na taifa letu, mnachotakwia kutusaidia hapa ni mawazo na maswali serious kuhusu this ishu, ya kafiri na the rest of the story hayawezi kutusaidia anything,

Tuambieni ni kwa nini Mwalimu alipokuwepo, Membe hakuwa na haya mawazo? Halafu kwa nini Waziri mzima wa Jamhuri anakwenda kuongea ishu very sensitive namna hii kwenye majukwaa ya media badala ya kuanzia bungeni kwanza? Why now tena baada ya kutoka Iran ambao historia ya siasa yetu iko very clear kua ndio waliowapa hela za uchaguzi the Mtandaos ambao yeye Membe was very much involved?

Hapa hapahitaji mabishano ya kidini kwa sababu historia iko very clear kuhusu vita vya hizi dini mbili kwamba mara ya mwisho huko Europe walioshinda ni wa-Kristo, na ni none ishu at all katika kuamua iwapo Tanzania tujiunge au hapana,

Binafsi ninapinga kwa nguvu zote hii idea ya Membe, ninaamini kwamba watawala wetu wa sasa wa hili taifa wameshindwa kutuaminisha wananchi kua wana nia njema na taifa letu, na hasa uwezo mdogo wa kuongoza waliouonyesha tayari. Katika kipindi kifupi cha utawala wao wametuingiza kwenye matatizo makubwa sana, hasa inapokuja ishu zinazohusu maamuzi ya taifa letu na mataifa mengine, la mwisho lilikuwa Richimonduli.

Matatizo ya Uganda, kimaendeleo hayakumalizwa na kujiunga kwao na OIC, kwa hiyo ni hoja finyu sana kwa waziri kutudanganya na hiyo hoja uchwara, Tanzania sasa hivi ni mwanachama wa jumuiya nyingi sana za kimataifa na tunashindwa kwenda popote kimaendeleo, sasa labda ifike mahali as a nation tujiangalie upya kama ni worthy sisi kuendelea na some of hizi international membership na hasa zile zinazohitaji yearly fee kuwa member, ikibidi tujitoe nazo, badala ya kulazimisha kujiunga na jumuiya hizi za kidini ambazo zina-guarantee mgawanyiko wa kisiasa na kidini kwa taifa lolote kama letu ambalo officially halina dini moja kama letu.

I do not care what hii ni jumuiya ya Wa-Islam period, Tanzania we have no business kujiunga na this kind of Jumuiya, kwa sababu sisi sio taifa la Kii-slam, na Membe should apologize to us the public for this nonesense ideas kama amezitoa under ministerial capacity. Incompetence ya utawala wa sasa it is just out of hand, I mean waziri mzima hajui kwamba this is a very sensitive political ishu ambayo haiwezi kurushwa tu kwenye media, badala ya sehemu maalum za kisiasa na kisheria?

Hiii incompetence na huu utawala where does it stops? Kwa sababu now karibu wananchi wote tunajua inapoanzia!

Its funy kaka unataka kusaidiwa hapa kimawazo na maswali serious kuhusu this ishu, wakati tayari umeshajenga msimamo thabiti kuhusu hili....

Na hili la kujaribu kumvalisha Membe huu msalaba ukijuwa wazi kuwa akiwa kama Waziri wa Mambo ya Nje ndiye anapaswa kushape mkakati wa sera ya mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa ambayo inalenga maslahi ya kiuchumi ambayo ndio dira ya Tanzania katika kujiunga na OIC ni kumuonea. Kama ni siasa za walioshinda na walioshindwa katika mchakato wa CHIMWAGA 2005 tafadhilini subirini 2010 mpambane tena.....

Kuwa na Waziri ama uongozi wenye kuthubutu kuongelea masuala tunayoyavika kilemba cha UNYETI sio incompetence bali ndio uongozi unatufaa watanzania. Biashara ya kujificha nyuma ya pazia kuogopa kuface the so called sensitive issue imepitwa na wakati na ni gharama kwa watanzania. Tunahitaji utawala wenye kudare hata haya machache kama wanasuasua yale ya EPA.



Tanzanianjema
 
Masheikh wajipanga kuwajibu maaskofu

Mimi sioni kama Maaskofu walikosea kusema jinsi walivyosema. Wana haki ya kutoa maoni kwa mambo yanayowagusa kama Masheikh walivyo na haki ya kuwajibu kwa mambo yanayowagusa pia. Kama Maaskofu hawakuwa na haki ya kusema walichosema basi hata Masheikh hawana haki ya kuwajibu.

Kwangu mimi kadiri tutakvyoelemishana kuhusu mambo yanayotuhusu ni kadiri hiyo hiyo tutakavyopanua uelewa wetu kuhusu mambo yanayotuhusu. Lakini jaziba na kudhani kuwa ni watu fulani tu wanaoweza kutoa maoni yao na wengine hapana, siyo ustaraabu hata kidogo.
 
1.
So HII DEBATE..TUKIIANGALIA STRICLTY KWA PREMISE YA KIUCHUMI...I DONT SEE ANY SENSE YA KUINGIA HUKO...ILA KAMA NI KUWARIDHISHA WAISLAMU...BASI WAINGIE WAO KAMA BAKWATA (THOUGH I DOUBT KAMA BAKWATA WANAWEZA KURUHUSIWA..MAANA SIYO NCHI).

2.
Its funy kaka unataka kusaidiwa hapa kimawazo na maswali serious kuhusu this ishu, wakati tayari umeshajenga msimamo thabiti kuhusu hili....

Na hili la kujaribu kumvalisha Membe huu msalaba ukijuwa wazi kuwa akiwa kama Waziri wa Mambo ya Nje ndiye anapaswa kushape mkakati wa sera ya mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa ambayo inalenga maslahi ya kiuchumi ambayo ndio dira ya Tanzania katika kujiunga na OIC ni kumuonea. Kama ni siasa za walioshinda na walioshindwa katika mchakato wa CHIMWAGA 2005 tafadhilini subirini 2010 mpambane tena.....

Kuwa na Waziri ama uongozi wenye kuthubutu kuongelea masuala tunayoyavika kilemba cha UNYETI sio incompetence bali ndio uongozi unatufaa watanzania. Biashara ya kujificha nyuma ya pazia kuogopa kuface the so called sensitive issue imepitwa na wakati na ni gharama kwa watanzania. Tunahitaji utawala wenye kudare hata haya machache kama wanasuasua yale ya EPA.

Ahsante kaka, naona unajaribu kuwa both side of the coin, ndiyo tabia za kina Beno, Lowassa, Karamagi, Msabaha, Rostam, Mkapa na Membe, siku zote hudhani wa-Tanzania ni wajinga, kumbe wajinga ni wao na wale wote wanaowaunga mkono,

Niliwahi kusema huko nyuma itafika siku mafisadi mtakosa cha kuiba maana mtakuwa mmemaliza kila kitu cha taifa, exactly ndipo mlipo sasa mnajua kuwa vimeanza kuisha vya kuiba serikalini, sasa mnataka kutuingiza mikenge mipya kwenye mashirika ya Kii-Isilamu, cha kusikitisha ni kwamba no matter what lazima wanakuwa na washabiki wao mpaka huku JF wanaowatupia makombo kidogo, tena mpaka wenye PHDddddddd! ambao tungetegemea watusaidie lakini vipande vichahe vya dinari na wao wanatusaliti!

Mliiba urais Dodoma 2005, mpaka leo hamjaridhika ukila nyama ya mtu once matokeo yake ndio haya ndugu yangu lazima ule zaidi na zaidi, sasa mnataka kutupeleka OIC, kesho mtatupeleka wapi?

Bwa! ha! ha! ah! ah! ahhhhhhhhhhh!Tumewashitukia mkono kwenye nyama na kwenye kunde ndio tabia yenu masikini ya Mungu!
 
Back
Top Bottom