Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

deny_all,
mkuu kwanza tazama mwandishi ni nani na anatetea vitu gani.. Ukisoma kwa makini huyu mtu anajaribu kujenga hoja kukandya OIC wakati World vision na red Cross zinafanya kazi hizo hizo..
Huyu mkulu anatangaza maslahi ya vyombo vyao kama vile Lions Club wanavyopiga vita hospital ya magonjwa ya moyo nchini kwa kumtumia mwanzilishi wake kuwa sababu ya kutokubali kuwepo hospital hiyo nchini.. Na wanafanikiwa sana tu.

Ndio maana nimesema ingawa mwandishi sio impartial .....lakini alichoongea kina ukweli ndani yake hasa suala la misaada kwenye nchi za kiislam zinapopata majanga kwa kuwa tumeshuhudia hayo majanga na pilika pilika zote za kutoa misaada.....Ndio maana hoja ya kusema tunajiunga OIC ili tupate misaada inazidi kuwa dhaifu as days go by.
 
Aliyeanza kumtukana Mkandara ni Jmushi, mie nimemkemea hapo juu kuwa si sawa. Japo si sawa Mkandara alivyojibu, lakini nadhani inafaa tatizo likafuatiliwa kwenye chanzo. Tuheshimiane tunapojadili hapa, wengi tu watu wazima wenye heshima zetu.

Kama Mujahidina ni tusi, basi Mushi ndiye the aggresor, kwa hiyo ndugu yangu Mushi kama neno Mujahidina ni tusi, basi ni wewe mwenye makosa bro na ni vyema ukaomba radhi.

Mkuu Bob heshima mbele, kwamba kwenye kujibu hukukimbilia majina mengine, straight kwenye jina lako moja tu hapa JF I love that.

Otherwise hatutaki sura mbili hapa! Maana naona zimeshaanza! now lets move to the next level na huu mjadala muhimu kwa taifa.
 
Ndio maana nimesema ingawa mwandishi sio impartial .....lakini alichoongea kina ukweli ndani yake hasa suala la misaada kwenye nchi za kiislam zinapopata majanga kwa kuwa tumeshuhudia hayo majanga na pilika pilika zote za kutoa misaada.....Ndio maana hoja ya kusema tunajiunga OIC ili tupate misaada inazidi kuwa dhaifu as days go by.

Hapa tupo ukurasa mmoja bro, saafi sana.
 
Whenever there has been a natural disaster, it is the West that has rushed to help. After that earthquake in Istanbul years ago, Western aid, including aid from Israel, came promptly and was so important, while the Arabs did nothing. After the tsunami in Indonesia, Western aid, especially American aid, was critical, especially in Aceh, that most militantly Muslim of Indonesian islands.

After the earthquake in Pakistan a few years ago, the only aid that meant anything came from the United States and a few other Western countries, and those American army hospitals remained in Pakistan to treat Pakistani Muslims --a vocation of charity, like all those Catholic schools in Muslim countries, that are taken advantage of by Muslims.

Yes, we'll see what the O.I.C. has in mind soon enough. It has nothing to do with fabulously rich Muslim states, many with populations of less than a million, actually sharing any of their wealth. And don't think for a minute that, even if they decided to share some of it with poorer Muslims, they would ever contemplate large-scale aid to any of the poor non-Muslims in this world -- not a chance, unless there were a firm promise to accept Islam, or to allow mosque-and-madrasa building, and Muslim campaigns of Da'wa, unhindered and on a large scale.

Maneno mazito sana haya, tunahitaji kuyatafakari sana Tanzania.
 
Kithuku,
Huyu dogo kanianza muda namtazama tu anakokwenda...na tatizo lake anashindwa kujibu hoja kwa hoja zaidi ya kutupa mapande yake..hapa kafika, kifupi haniwezi kabisa kwa lolote.. toka kaingia hapa mada imekuwa jazwa pumba tupu, amekuta watu tunajadili hoja kaingia na pumba zake kama kawaida..

Mkamap, Mkuu lnilitegemea hivyo kwani wewe unachangia kwa rangi zako, hukuona alipoanza na habari za personal attack kuwa sisi ni Mujahidina?..rudi nyuma soma haya maandishi yake..
Wewe unaleta propaganda zako na unataka tukubaliane tu kwasababu na wewe ni Msilam? Hapa ni kuhusu Maslahi ya Taifa vs yenu mujahidina.

Watu kama hawa nawatafuta sana waingie mitaa yangu, huwa nawamaliza tu sina noma..

Wewe ndiyo unaleta pumba..Sasa hopefully na wewe umepewa warning na Pain Killer kwa kunitukania mama yangu.
Nitashangazwa sana kama utakuwa hujapewa warning...Hizi double standards bana.
 
Dear members,

Please refrain from name calling.

Thank you !
 
deny_all,
Hivi kweli unaweza kusema Somalia leo na majanga yake wanahaja ya kujiuliza membership yao na AU ati kwa sababu haiwasaidii kitu?.. je, kosa lipo kwa AU kama chama ama ni viongozi wetu wa AU kina Kikwete ndio wabaya..Pengine pia kosa linaweza kuwa wasomali wenyewe!

Congo wanauana kila siku acha hizo nchi nyinginezo lakini haiwezi kuwa sababu ya kutojiunga na jumuiya zinazotaka kutoa misaada iwe kifedha ama mediation.
Binafsi nachofahamu OIC kama IMF inasaidia sana nchi nyingi isipokuwa watawala wenyewe ndio mtindo wa EPA tu unatumika..
Sasa cha kujiuliza ni kutojiunga na OIC ama kuwaondoa viongozi wabaya wanaotumia vibaya misaada hiyo...Kikwete toka amekuwa mwenyekiti wa AU amefanya nini kuisaidia Somalia.. nothing afadhali hata hao OIC pamoja na kwamba wanapeleka chakula na madawa tu... Uganda wameprovide jeshi la Ulinzi nje kabisa ya matakwa ya AU ama UN..
Ni uongo mkubwa tukisema ati Tanzania haihitaji misaada kwa sasa hivi isipokuwa swala kubwa zaidi kwetu ni kuangalia malipo ya misaada hiyo...
Halafu bob, sii kweli OIC inataka kugawa Utajiri wake! huu ni uongo kaongezea mwandihsi kwa sababu hakuna mtu, taasisi wala nchi inayotaka kugawa Utajiri wake..Kutoa Zaka ama sadaka kanisani ama msikitini hugawi utajiri wako hata kidogo..Hayo ni maswala ya usocialist ambayo yamepitwa na wakati.

Field Marshall Es,
Mkuu nakusikia lakini unajua tupo long hapa na vijana wengi hupenda sana kujaribu watu...vidole huwawasha wakafikiria sisi mazuzu.. kweli naweza kuwa mjinga lakini sii mjinga hivyo!
 
Field Marshall Es,
Mkuu nakusikia lakini unajua tupo long hapa na vijana wengi hupenda sana kujaribu watu...vidole huwawasha wakafikiria sisi mazuzu.. kweli naweza kuwa mjinga lakini sii mjinga hivyo!

Hivi wewe Mkandara una akili timamu kweli wewe?
Ama unadhani na mimi nashindwa kumtukana mama yako?
Wewe unaona ubingwa kutukana na sasa eti unatangaza ushindi!
Kwanza una bahati sana kwasababu ya double standards za baadhi ya hawa moderators...Yani kuna members ambao wako above the rules simply kwasababu kuna Moderators wata waback...Huyo moderator anayejiita Pain killer na yeye kanipa warning kwa tusi lipi hilo?
Wewe mtu mzima kwenye forum unayejiita una akili timamu unatumia jina lako halafu unatukana matusi ya nguoni na unaona ni ufahari.
Ama kweli nimeona mengi hapa JF.
 
.............Nasema ni haki kabisa kwa waislamu kujiunga na taasisi yoyote ya kiislamu wanayoitaka. ............... Hiyo taasisi inapaswa kuweka utaratibu wa kuwawezesha waislamu walioko katika nchi zisizo za kiislamu kujiunga nao bila kuleta mtafaruku kama huu tunaoletewa hapa.

Kithuku you are very right Mkuu...........

Huko nyuma nilisema hivi......
Kuna mwanaJF mmoja kashauri kuwa serikali yetu itafute modality ya kuwezesha wa-Islamu kujiunga na OIC.......ni wazo zuri...................najaribu kufikiria sijapata jibu bado.......on the modality

............In addition nafikri ni rahisi zaidi kwa OIC kurekebisha masharti yao ya uanachama na kuruhusu jumuiya za Kiislamu zinazokubalika na waislamu wa nchi husika ziruhusiwe kujiunga na OIC.........otherwise we will continue with this debate as a nation of differents beliefs to infinity............

.......kama masharti ya kujiunga na uanachama wa OIC unaruhusu jumuiya fulani fulani kujiunga........i don't see any fuss of this debate........
na nikajibiwa hivi......................
Sio rahisi sana kwa sababu na wao kuweka masharti ya kujiunga kuwa hivyo wana maana yao.....
..........ninawashauri viongozi wanaosoma hii habari hapa JF.............this issue is serious and they should not take it lightly.....


Bob............hoja ya kuwa tutapata misaada ni very weak
 
............Tujiunge tu na chombo hiki kwa faida ya wenzetu. Hatutabadilika kuwa nchi ya kiislamu kwa kufanya hivyo.

Amandla.......

Mkuu Fundi,

....hivi ukitaka kujiunga na chama fulani....unaingia tu kichwa kichwa bila kujua sera na malengo ya hicho chama!!!!........leave alone chama.......hata ukitaka uhusiano wa aina yeyote na mtu au nchi.....wee unavamia tu kuwa nataka kuhusiana na wewe..........eehh!!.......... .i don't believe this came from you!!!

Bob.......nakusoma sana mkuu, changamoto yako ya Redcross na World vision inabidi nayo tupate maelezo.........je Tanzania as a nation tunahusiana vipi na hizi taasisi.......ila nakumbuka Alhaji Kimbisa alikuwa kiongozi wa RedCross Tanzania..........jambo ambalo ni kinyume ktk OIC......ni lazima uwe muislam.........ili ufanye kazi OIC.......

Je Tanzania as a Nation ni mwanachama wa World Vision.......?
 
Senegal: Aid Tops Agenda As Islamic Conference Opens in Dakar

Posted to the web 13 March 2008

Hamadoutidiane Sy
Dakar

Co-existence in the same organisation of extremely rich nations (mostly Arab countries) and extremely poor ones (mostly sub-Saharan Africa nations) is among the key issues the host country of the 11th summit of the Organisation of the Islamic Conference (OIC) has attempted to place highly in the agenda of the summit that opened on Thursday.

Ever since he was granted the privilege to host he the summit, five years ago, President Abdoulaye Wade, has pledged to make Arab money, mostly invested in Western countries to also benefit the non oil producing countries in sub-Saharan Africa.

On the eve of the 11th summit, Senegalese Foreign Affairs minister Cheikh Tidiane Gadio, was again strongly defending the position, pointing at what some perceive as a paradoxical situation for an organisation primarily set up to express solidarity "between brothers and sisters" of the same faith.

For Mr Gadio, Africa needs the solidarity and money of the rich Arab nations to overcome its development problems, and he insisted that he is "not talking about Zakat" - the percentage of one's personal wealth that each Muslim should compulsorily give away to the poor once a year.

The Minister, talking to the media with the secretary general of the OIC, Mr Ekemeldin Ishanoglu by his side ahead of the meeting of the heads of state, stressed that the money that was needed in Africa was investment money.

"The Putrajaya summit in Malaysia (held in October 2003) marked a turning point for Asian member countries; the Dakar summit should equally mark a turning point for African Muslim nations", the Senegalese minister said.

Actually he has been saying this for weeks at experts meetings, preparatory sessions, and ministerial conferences. And days before the summit Senegal has convened quite a certain number of such meetings to elaborate proposals on this issue.

"Instead of investing all their money exclusively in the Western world, the rich countries of the OIC should also think of channelling this money to Africa", Mr Amadou Tidiani Diallo, a professor at the Arabic Department of Cheikh Anta Diop University said.

In fact for the past few years, ministers of the "African group" within the OIC have been working to get more support and a "new partnership" with the rich nations of the Islamic community, including debt relief, more investment and aids.

Reminded journalists

During the meeting with the press ahead of the summit, Mr Ishanoglu, reminded the journalists that an extraordinary summit held in Mecca, Saudi Arabia in December 2005 included in its 10 year Plan of action, a whole section on poverty alleviation for the least developed countries, most of which are located in Africa.

One of the outcomes of this summit in the holy Islamic city specified the need for the OIC to strengthen its activities in "the field of socio-economic development" focussing on "poverty alleviation and supporting development in the least developed countries in Africa", according to a draft document of the OIC.

The plan of action also "focuses on ways to utilise the abundant resources and capacities of the OIC member countries to be channelled" to these countries.

To implement these decisions, the Islamic Development Bank (IDB), an agency of the OIC, has been assigned with the task to set up a "special fund for Africa" and the institution has pledged to collect some $10 billion.

But so far, only a quarter of this amount ($2.6 billion) has been gathered, by the financial institution, including its own contribution.


Meanwhile, as the summit opened, it was overshadowed by a confrontation between Chad and Sudan, adds Reuters.

The meeting, however, started on a sour note as Chad accused its neighbour and fellow OIC member Sudan of launching a rebel attack across its border.

"The Chadian government informs national and international opinion that Sudan on Wednesday March 12, 2008 launched several heavily armed columns against Chad," an official statement released in the Chadian capital N'Djamena said.

It was a major embarrassment for President Wade who had billed the summit as the opportunity for a definitive peace deal between the two oil-producing states, after five previous agreements had collapsed.
l
A deal seemed unlikely after Sudanese President Omar Hassan el-Bashir failed to turn up to a meeting with Chadian leader Idriss Deby late on Wednesday, leaving UN Secretary-General Ban Ki-moon, called as witness, waiting for nearly three hours.


source: allAfrica.com

Hivi kweli unaweza kusema Somalia leo na majanga yake wanahaja ya kujiuliza membership yao na AU ati kwa sababu haiwasaidii kitu?.. je, kosa lipo kwa AU kama chama ama ni viongozi wetu wa AU kina Kikwete ndio wabaya..Pengine pia kosa linaweza kuwa wasomali wenyewe!

Congo wanauana kila siku acha hizo nchi nyinginezo lakini haiwezi kuwa sababu ya kutojiunga na jumuiya zinazotaka kutoa misaada iwe kifedha ama mediation.
Binafsi nachofahamu OIC kama IMF inasaidia sana nchi nyingi isipokuwa watawala wenyewe ndio mtindo wa EPA tu unatumika..
Sasa cha kujiuliza ni kutojiunga na OIC ama kuwaondoa viongozi wabaya wanaotumia vibaya misaada hiyo...Kikwete toka amekuwa mwenyekiti wa AU amefanya nini kuisaidia Somalia.. nothing afadhali hata hao OIC pamoja na kwamba wanapeleka chakula na madawa tu... Uganda wameprovide jeshi la Ulinzi nje kabisa ya matakwa ya AU ama UN..
Ni uongo mkubwa tukisema ati Tanzania haihitaji misaada kwa sasa hivi isipokuwa swala kubwa zaidi kwetu ni kuangalia malipo ya misaada hiyo...

Hapa umeongea kuwa tatizo ni sisi wenyewe ikimaanisha hata waje malaika kutuongoza kama hatubadilika miaka nenda miaka rudi tutabaki vile vile. Kwa suala la malipo ya mokopo na utoaji wa misaada ndio hapo watu wengi walipo na wasiwasi mkubwa labda wewe utufafanulie.

....Halafu bob, sii kweli OIC inataka kugawa Utajiri wake! huu ni uongo kaongezea mwandihsi kwa sababu hakuna mtu, taasisi wala nchi inayotaka kugawa Utajiri wake..Kutoa Zaka ama sadaka kanisani ama msikitini hugawi utajiri wako hata kidogo..Hayo ni maswala ya usocialist ambayo yamepitwa na wakati.

Ndio mentality ya nchi nyingi za Kiafrika ilivyo wanajiunga ili kupata misaada,
kama article hapo juu invyosema ambayo hata sisi wengi tunayo. Kama ni misaada tumepokea mingi sana mbona haijatusaidia. Kuna wakati nadhani Tanzania ndio ilikuwa nchi inayopata misaada mingi south of sahara ...lakini angalia tulipo leo. Important of all we need to clean our house first na kutumia resources zetu vizuri. Nchi ambayo inazungumziwa kuwa 3rd producer of gold worldwide hatuhitaji kuwa hapa tulipo.
 
Mkuu Fundi,

....hivi ukitaka kujiunga na chama fulani....unaingia tu kichwa kichwa bila kujua sera na malengo ya hicho chama!!!!........leave alone chama.......hata ukitaka uhusiano wa aina yeyote na mtu au nchi.....wee unavamia tu kuwa nataka kuhusiana na wewe..........eehh!!.......... .i don't believe this came from you!!!

Bob.......nakusoma sana mkuu, changamoto yako ya Redcross na World vision inabidi nayo tupate maelezo.........je Tanzania as a nation tunahusiana vipi na hizi taasisi.......ila nakumbuka Alhaji Kimbisa alikuwa kiongozi wa RedCross Tanzania..........jambo ambalo ni kinyume ktk OIC......ni lazima uwe muislam.........ili ufanye kazi OIC.......

Je Tanzania as a Nation ni mwanachama wa World Vision.......?


Sio Kimbisa tu hata Abdulrahman Kinana ashawahi kuwa head wa Red Cross & Red Crescent Society. Nakumbuka vile vile wakati naishi kinondoni jirani yangu mmoja ambaye pia ni muislam mzuri alikuwa boss mkubwa tu hapo Red cross.
 
................... Kama ni misaada tumepokea mingi sana mbona haijatusaidia. Kuna wakati nadhani Tanzania ndio ilikuwa nchi inayopata misaada mingi south of sahara ...lakini angalia tulipo leo. Important of all we need to clean our house first na kutumia resources zetu vizuri. Nchi ambayo inazungumziwa kuwa 3rd producer of gold worldwide hatuhitaji kuwa hapa tulipo.

...exactly.........!!!
 
Mkuu Fundi,

....hivi ukitaka kujiunga na chama fulani....unaingia tu kichwa kichwa bila kujua sera na malengo ya hicho chama!!!!........leave alone chama.......hata ukitaka uhusiano wa aina yeyote na mtu au nchi.....wee unavamia tu kuwa nataka kuhusiana na wewe..........eehh!!.......... .i don't believe this came from you!!!

Bob.......nakusoma sana mkuu, changamoto yako ya Redcross na World vision inabidi nayo tupate maelezo.........je Tanzania as a nation tunahusiana vipi na hizi taasisi.......ila nakumbuka Alhaji Kimbisa alikuwa kiongozi wa RedCross Tanzania..........jambo ambalo ni kinyume ktk OIC......ni lazima uwe muislam.........ili ufanye kazi OIC.......

Je Tanzania as a Nation ni mwanachama wa World Vision.......?

Mkuu Ogah. Lengo, sera na katiba za hii jumuia ziko wazi kabisa. Kiko kwa ajili ya maslahi ya waislamu. Nilimpinga sana Mkandara alipotaka kutufumba macho kwa kudai kuwa si cha kidini. Ni cha kidini through and through. Hauwezi kupata nafasi ya uongozi katika jumuia hiyo kama umeoa au umeolewa na asie muislamu. Kwa asie muislamu, alie tu. Lakini ukweli ni kuwa hawa ni moderates na kweli lengo lao ni kuwaendeleza wenzao. Hoja yangu ni kuwa kwa vile hadi sasa inaelekea hakuna njia mbadala ya wenzetu kufaidika na fadhila zake bila sisi wote kama nchi kujiunga, basi tujiunge, maana hawa ni wenzetu. Wakipeta, which I doubt, basi ni faraja kwetu sote. Tukiona hakuna maslahi tutajitoa kama tulivyojitoa Comesa.

Kitu ambacho wengi mnakipuuzia ni athari ya kutojiunga kwa jamii yetu. Kufanya hivyo na hasa katika mazingira ambayo viongozi wa wakristu wakiwa mstari wa mbele kutazidi kujenga ufa katika jamii yetu.Imani ya waislamu kuwa sisi wakristu hatuwatakii mema itazidi kuota mizizi. Wale waislamu wetu, tunaooleana na kuzikana tutawakimbiza kwa extremists kama hao waIran.

Wakristu, historia imetupendelea sana. Kuna haja ya kuwa magnanimous na kuwaridhia wenzetu. Kama hatuwezi kufanya hivyo, basi ule undugu tuliokuwa tunajivunia utaonekana ulikuwa ni fix tu. Upo tu pale ambapo mmisheni anafaidika.

Kwa ndugu zangu waislamu. Simamieni hoja bila kujaribu kutafuta visingizio visivyo na maana. Mnapokosea mnapodai kuwa hii ni haki yenu kutokana na uvumilivu wenu dhidi ya kuwepo kwa Balozi wa Vatican State nchini mwetu. Au kukomba kwenye sufuria na kujaribu kufananisha na taasisi za kidini ambamo ni madhehebu ndiyo wanachama na si nchi. Najua hampendi kuelezwa hivi lakini muundo wenu hauruhusu vyombo kama hivi. Kupata mwakilishi tu wa waislamu itakuwa kazi wakati wakristu wana utaratibu wao unaofanya vizuri sana kwenye hili. Sidhani kama Sheikh Mkuu ana madaraka yeyote dhidi ya wafuasi wa dini yake kama waliyo nayo mapadri, maaskofu na makadinali!

Kwa kushikilia hayo mnamwagia mafuta kwenye moto na kuzidisha imani kwa wengi wetu kuwa kuna ka-secret agenda kwenye ishu nzima.

Ni hayo tu.
 
Mkuu Fundi nakusoma.....

.......Umoja ni kitu muhimu sana miongoni mwa jamii zetu........kama sisi si wamoja kwa manufaa ya jamii zetu.......tutaishia kubaya......having said that....mimi kama muislamu je haki zangu au uwezo wangu kimaisha zitapatikana kwa Tanzania kujiunga na OIC....tofauti na ilivyo sasa?..........i don't think so..........mbona tunapata mikopo toka BADEA......na Tanzania sio wanachama huko?........ni kitu gani kinachozuia OIC kuruhusu Benki yao kutoa mikopo kwa nchi yenye waislam wengi?......na hali wakijua fika tunahitaji as islamic society kusaidiwa?
 
Lengo, sera na katiba za hii jumuia ziko wazi kabisa. Kiko kwa ajili ya maslahi ya waislamu.

Wakristu, historia imetupendelea sana. Kuna haja ya kuwa magnanimous na kuwaridhia wenzetu.

Kwa ndugu zangu waislamu...Mnapokosea mnapodai kuwa hii ni haki yenu kutokana na uvumilivu wenu dhidi ya kuwepo kwa Balozi wa Vatican State nchini mwetu.

Ni sahihi nikikuelewa kwamba unasema kimsingi Waislam hawana haki ya kujiunga ila wafanyiwe favor na Wakristo ili kukuza undugu ?

Halafu, misaada ya mikopo ya riba ndogo, ambayo Rais wa Senegal ameiongelea kwenye tundiko moja hapo juu, ikija itawanufaisha Waislam peke yao, au Tanzania nzima ?

Na hii hoja ya uhusiano wa kibalozi na Vatican City ndio consensus argument ya Waislamu walio wengi au ni ya kina Mkandara na wengine wachache ?

Isije ikawa hoja za Waislamu haziwi represented vizuri halafu zinaoneka si madhubuti, ila Waislamu "waridhiwe" tu kama favor. Kitu ambacho kinaweza kuwa ndio kinamshusha Muislamu zaidi.

Inawezekana sijaelewa, lakini najaribu kuwa objective tu. Sina hata uhakika kama Mungu mwenyewe yupo, japo ningependa awepo.

Ila binafsi nishaanza kuogopa huko tunakokwenda, maana ukiona Maaskofu wanasema Waziri ajiuzulu na Mashehe wanasema wataandamana kuwapinga vikali Maaskofu hayo yanatisha tisha kinamna.
 
Ogah,
Kwanza kabisa hapa najibishana na watu wa aina mbili... wale wanaozungumzia content za OIC na wale wanaozungumzia kilichohifadhi (chupa) vilivyomo kwa hiyo inaiuwia vigumu kuweza kuweka hoja zangu kwa mpangilio mzuri ukaeleweka..
Mara zote mimi naweza kabisa kubishana kuhusu jambo lolote kuhusiana na dini maadam liwe ni kwa manufaa ya Umma ktk kielimishana lakini hata siku moja sintathubutu kuzungumzia dini ya Kikristu ama nyingine na kuanza kuichambua wakati sio dini yangu kwa sababu tu mambo yake hayana hifadhi kwangu..wakati huo huo niwatazame wakristu na kuwaita ndugu ya jamii moja. Na wala sintathubutu kuwapangia wao jinsi ya kujiendeleza ktk dini yao ama mipango inayohusiana na dini yao iwe binafsi ama kitaifa. Ni swala lao wakitaka kulichukua sina budi kulikubali maadam halina madhara kwa waumini wa dini nyinginezo..
Mkuu tumemchagua Kikwete kuwa rais wetu na kwa uhakika tulijua hawezi kubadilisha kitu lakini tunaye rais.. tena hii ni hiyari ya mtu, hivyo kuanza kutafuta sababu z matokeo ati kwa sababu ni misaada wakati huo huo tunaunga mkono Kikwete kumwita Bush kutaka misaada hiyo hiyo, tumejiunga IMF na kumsifia Mkapa na kadhalika lakini hakuna hata mtu mmoja aliyesimama na kupinga kuomba misaada hiyo.
Kisha basi OIC mara zote ipo ktk majanga ya Umaskini, haihusiani kabisa na bajeti ya serikali wala kuingilia mipango ya nchi isipokuwa pale panapohitajika misaada.
Kama nilivyotoa mfano wa Somalia, leo hii AU imekaa kando na kutetea Utawala uliopo hali wanao athirika ni wananchi zaidi..UN wenyewe na NATO kazi kupeleka majeshi kulinda meli zao wakati hakuna mtu anayetazama wananchi. Watu hawa bila kutazama dini yao ama rangi yao wanahitaji msaada mkubwa nje kabisa ya Utawala..Kuikomboa Somalia sio swala la OIC isipokuwa kuwapatia hifadhi wananchi kama vyombo vingine vinavyoweza kufanya kazi..

Ndivyo navyolitazama swala la OIC, yawezekana kabisa binafsi sikubaliani nao lakini kama waislaam wameona kuna kila sababu za wao kupenda uhusiano wa karibu na chombo hiki binafsi sina utata wowote maadam tu OIC haiwezi kuingilia Usalama wa taifa letu..kumbuka tu kila napoleta hoja yangu husimama nje ya sanduku na kuitazama issue yenyewe kwa fikra huru...

Muda wote nimekuwa nikitumia Vatican kujaribu kuwaonyesha kuwa sio kila kitu kinakubalika na wote lakini ikiwa wahusika wanakubaliana na mfumo wa dini yao sisi wengine inatubidi tukae kando, tukubali na kuwapa support inapowezekana. ndio maana Pope anapokuja Tanzania tunampokea kama kiongozi wa dini ya Kikatoliki wala sio rais ama mfalme wa Vatican na mfuko wa serikali unatumika ktk maswala mengi ya kidini... Na naheshimu nguvu na uwezo aliokuwa nao pamoja na kwamba binafsi sikubaliani na muundo wa chombo hicho. hawanilazimishi kukubali Ukatoliki na wala muundo wa Vatican haukulengwa kwangu isipokuwa waumini wa dini hiyo, hivyo pilipili nisiyokula yaniwashani!.. mchuzi wote haukuungwa na Pilipili isipokuwa pilipili ipo kwa wanaopenda..
Now, nirudi ktk swala la OIC katika mtazamo wa Kitaifa. Umesema misaada sio kabisa hoja ya msingi.. nakuomba unambie WHY?..hayo maswala ya sisi kujitosheleza na kadhalika waislaam wameisha yatazama na bado wameona kuna haja kubwa ya kujiunga na OIC..Ni chombo chao wamejikusanya na kuamua kufanya hivyo!..
Hizi tofauti zetu tukianza kuzitazama mbele kwa roho za chuki na hasa matunda yake kwetu sote basi ipo haja kubwa sana ya kujiuliza hata kuwepo vyama vya siasa mbali na CCM...Ni ktk mitazamo kama hii tunaweza kujenga Uhasama kati ya CCM na Chadema. Upinzani wa vyama Tanzania imekuwa ni kama dini vile kiasi kwamba ukiwa Chadema basi wewe ni adui wa maendeleo ya Tanzania. Imefikia hata baadhi ya watu kuitwa wao sio Watanzania kwa sababu tu wamejiunga na Chadema. Na kila jambo linalofanywa na Chadema huonekana kama linalenga kundi fulani la watu hata kama ni wana Chadema wakati hakuna mtu aliyekukataza kujiunga na Chadema..imefikia hata watu ku question kwa nini Chadema wanapeleka fungu lao (misaada) sehemu zile tu walizoshinda badala ya nchi nzima...Chadema sio malaika wala sio watawala na watawatumikia tu wale waliowachagua. Sio vibaya wakijipanua zaidi lakini sio haramu kwao kujikita ktk majimbo ambayo wameshinda..
Hii ndio argument yangu...kusema kweli binafsi I would careless OIC, IMF, CCM ama Chadema ikiwa vyama vyote hivi havina malengo mazuri kwa wanachama na raia kwa ujumla..
 
Mkuu Fundi nakusoma.....

.......Umoja ni kitu muhimu sana miongoni mwa jamii zetu........kama sisi si wamoja kwa manufaa ya jamii zetu.......tutaishia kubaya......having said that....mimi kama muislamu je haki zangu au uwezo wangu kimaisha zitapatikana kwa Tanzania kujiunga na OIC....tofauti na ilivyo sasa?..........i don't think so..........mbona tunapata mikopo toka BADEA......na Tanzania sio wanachama huko?........ni kitu gani kinachozuia OIC kuruhusu Benki yao kutoa mikopo kwa nchi yenye waislam wengi?......na hali wakijua fika tunahitaji as islamic society kusaidiwa?

Mkuu. Tatizo ni kuwa debate yenyewe yote imekuwa hijacked na fikra za udini. Ukweli ni kuwa kimaendeleo waislamu au tuseme sehemu zenye majority ya waislamu ziko nyuma. Hii imechangiwa zaidi na sababu za kihistoria. Kwa hali inaeleweka kama watatafuta njia mbadala ya kuwaletea maendeleo. Kilichotakiwa ni kuwa badala ya kuwabeza kuwa wasitupeleke kwenye sharia tufanye wote juhudi za kuwaletea hayo maendeleo kupitia mikondo isiyopingana na katiba yetu. Hao maaskofu wangeomba hivyo vyombo vyao kama World Vision wazidishe juhudi zao katika sehemu zilizo duni kimaendeleo. Hii itabidi ifanyike kwa kushirikiana na wenye nia njema kutoka pande zote. Kama vile kulivyo na haja ya kuwaelimisha wamisheni kuwa si kila chombo cha waislamu ni camouflage ya mujaheedina, nao wenzetu waweeleze kuwa si kila kinacholetwa na wakristu kitawapunguzia uislamu wao.

Mimi ingawa sipingi sis kujiunga na hiki chama lakini sina mategemeo makubwa. Wenzetu wenye mafuta hawana hulka ya kusaidia. sana sana wataleta tende wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu! Misaada itaendelea kuletwa na wamisheni wa nchi za magharibi. Tumaini langu ni kuwa labda tukijiunga na kuambulia patupu ndipo tutakapojifunza kuwa hakuna njia ya mkato kwenye kutafuta maendeleo. Pengine tutarudi tena na kuanza kuziba nyufa za udini zilizoanza kujitokeza katika jamii yetu.

Nilisikitika hapo awali kumsikia Askofu mmoja akikiri kuwa hajaisoma katikba ya OIC lakini akisisitiza bado kupinga sisi kujiunga nao. Ni kama vile wenzangu walivyompandishia mori Salman bila kukisoma kitabu chake cha Satanic Verses!
 
Kuhani,
Sio yanatisha tisha kinamna, yanatisha hasa. Hapa wameanza kupingana kupitia serikali, kinachofuata watapingana uso kwa uso na ndio mwanzo wa mtafaruku. Kumbuka wana watu nyuma yao na si watu wa siasa, maana tumezoea kusema viongozi wa siasa wana njaa ndio maana wananchi tunawapuuza. Lakini hao viongozi wa dini chochote watakachosema kitakuwa hivyo maana waumini hatatuwapuuza, serikali hapa imelikoroga.
 
Fundi Mchundo,
Mkuu umefunga mjadala na mawazo kama haya ndio yanatakiwa kujengwa JF kama chombo cha kuelimishana sio kuja hapa na kushambuliana...trust me muda wote nimekuwa nikisoma nikaanza kuvuta uradi...Kumbe wazungu wanapotuita sisi majina ya N word huwa wanatumia zaidi fikra kama hizi... majibu mengi yamekuwa kama kaburu anavyoweza kumjibu mtu mweusi, wao bora na weusi wafanye hivi ama vile kutokana na tafsiri zao wakijiona wao bora na tofauti na weusi, wao ndio binadamu na umaskini wetu utapimwa na wao ama pengine ni laana ya mwenyezi Mungu..
Hivi kweli tumefikia kiasi hicho!... inauma sana.
 
Back
Top Bottom