Mkuu Ogah. Lengo, sera na katiba za hii jumuia ziko wazi kabisa. Kiko kwa ajili ya maslahi ya waislamu. Nilimpinga sana Mkandara alipotaka kutufumba macho kwa kudai kuwa si cha kidini. Ni cha kidini through and through. Hauwezi kupata nafasi ya uongozi katika jumuia hiyo kama umeoa au umeolewa na asie muislamu. Kwa asie muislamu, alie tu. Lakini ukweli ni kuwa hawa ni moderates na kweli lengo lao ni kuwaendeleza wenzao. Hoja yangu ni kuwa kwa vile hadi sasa inaelekea hakuna njia mbadala ya wenzetu kufaidika na fadhila zake bila sisi wote kama nchi kujiunga, basi tujiunge, maana hawa ni wenzetu. Wakipeta, which I doubt, basi ni faraja kwetu sote. Tukiona hakuna maslahi tutajitoa kama tulivyojitoa Comesa.
Kitu ambacho wengi mnakipuuzia ni athari ya kutojiunga kwa jamii yetu. Kufanya hivyo na hasa katika mazingira ambayo viongozi wa wakristu wakiwa mstari wa mbele kutazidi kujenga ufa katika jamii yetu.Imani ya waislamu kuwa sisi wakristu hatuwatakii mema itazidi kuota mizizi. Wale waislamu wetu, tunaooleana na kuzikana tutawakimbiza kwa extremists kama hao waIran.
Wakristu, historia imetupendelea sana. Kuna haja ya kuwa magnanimous na kuwaridhia wenzetu. Kama hatuwezi kufanya hivyo, basi ule undugu tuliokuwa tunajivunia utaonekana ulikuwa ni fix tu. Upo tu pale ambapo mmisheni anafaidika.
Kwa ndugu zangu waislamu. Simamieni hoja bila kujaribu kutafuta visingizio visivyo na maana. Mnapokosea mnapodai kuwa hii ni haki yenu kutokana na uvumilivu wenu dhidi ya kuwepo kwa Balozi wa Vatican State nchini mwetu. Au kukomba kwenye sufuria na kujaribu kufananisha na taasisi za kidini ambamo ni madhehebu ndiyo wanachama na si nchi. Najua hampendi kuelezwa hivi lakini muundo wenu hauruhusu vyombo kama hivi. Kupata mwakilishi tu wa waislamu itakuwa kazi wakati wakristu wana utaratibu wao unaofanya vizuri sana kwenye hili. Sidhani kama Sheikh Mkuu ana madaraka yeyote dhidi ya wafuasi wa dini yake kama waliyo nayo mapadri, maaskofu na makadinali!
Kwa kushikilia hayo mnamwagia mafuta kwenye moto na kuzidisha imani kwa wengi wetu kuwa kuna ka-secret agenda kwenye ishu nzima.
Ni hayo tu.
Fundi mbona unasisitiza tu kujiunga na OIC bila kunijibu maswali yangu haya:
1. Je Tanzania kama taifa inayaamini na kuyakubali malengo ya OIC kama yalivyobainishwa kwenye charter yao?
2. Watanzania, pamoja na wewe, tuko tayari kushiriki kutekeleza malengo yote yaliyobainishwa humo?
3. Ni sahihi kwa Tanzania kama nchi yenye watu wenye dini mbalimbali kujiunga na kufungwa na maazimio na makubaliano yanayopendelea dini moja tu?
Na hebu tuambie, hiyo OIC charter umeisoma au unashabikia tu kwa sababu kama zile za Bernad Membe?
http://www.oic-oci.org/oicnew/is11/english/Charter-en.pdf
Ukiangalia namna nchi zinavyoweza kuwa wanachama kuna mashaka kidogo hapa...nafikiri sensa ni muhimu. Pitia link hapa juu Kwa mfano the charter inasema ...Any State, member of the United Nation, having Muslim majority and abiding by the Charter, which submit an application for membership may join the Organisation....
Km tunaongelea Zanzibar ambayo AGs wameshasema ni nchi then wanaendana na Charter ikiwa ni Jamhuri ya Muungano au Tanzania bara (Km nchi....! AGs hawakutueleza km hii nayo ni nchi au kipande cha nchi....!) hapa pana shida kidogo
Je watanzania tunaitii/kuikubali "charter" hiyo? Mimi siikubali, na ninajua wapo wengi sana wasioikubali. Kwa nini tulazimishwe kushiriki kitu tusichokubaliana nacho?
hii statement inaturepresent watanzania wote? hapo umeandika kwa ajili ya wangapi msiokubali?
Kwa ajili ya sisi tusiokubali, maana kwa ushahidi wa wanaochangia mjadala tu hapa siko peke yangu.
well and good, nice statistical analysis, very representative kwa Watanzania..... sikujua ati.
Ni hivi mama, haiwezi kuwakilisha watanzania wote maana wapo hao wanaotaka kujiunga na OIC. Ninachosema ni kwamba haki za wasiotaka hiyo OIC pia ziheshimiwe, wasilazimishwe kuwa sehemu ya utekelezaji wa malengo wasiyoyaamini wala kuyakubali. Na kikubwa ni kwamba itakuwa ni kinyume cha haki na katiba kwa nchi kuwa mwanachama wa taasisi yenye malengo yaliyokusudiwa kwa ajili ya dini moja tu katika nyingi zilizoko nchini, huku yakikinzana na imani za hao wasio wa dini hiyo. Jambo lenye manufaa lingekuwa kuwawezesha waislamu kujiunga na hiyo OIC bila kuwaathiri watu wa dini nyingine.
Mkuu. Tatizo ni kuwa debate yenyewe yote imekuwa hijacked na fikra za udini. Ukweli ni kuwa kimaendeleo waislamu au tuseme sehemu zenye majority ya waislamu ziko nyuma. Hii imechangiwa zaidi na sababu za kihistoria. Kwa hali inaeleweka kama watatafuta njia mbadala ya kuwaletea maendeleo. Kilichotakiwa ni kuwa badala ya kuwabeza kuwa wasitupeleke kwenye sharia tufanye wote juhudi za kuwaletea hayo maendeleo kupitia mikondo isiyopingana na katiba yetu. Hao maaskofu wangeomba hivyo vyombo vyao kama World Vision wazidishe juhudi zao katika sehemu zilizo duni kimaendeleo. Hii itabidi ifanyike kwa kushirikiana na wenye nia njema kutoka pande zote. Kama vile kulivyo na haja ya kuwaelimisha wamisheni kuwa si kila chombo cha waislamu ni camouflage ya mujaheedina, nao wenzetu waweeleze kuwa si kila kinacholetwa na wakristu kitawapunguzia uislamu wao.
Mimi ingawa sipingi sis kujiunga na hiki chama lakini sina mategemeo makubwa. Wenzetu wenye mafuta hawana hulka ya kusaidia. sana sana wataleta tende wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu! Misaada itaendelea kuletwa na wamisheni wa nchi za magharibi. Tumaini langu ni kuwa labda tukijiunga na kuambulia patupu ndipo tutakapojifunza kuwa hakuna njia ya mkato kwenye kutafuta maendeleo. Pengine tutarudi tena na kuanza kuziba nyufa za udini zilizoanza kujitokeza katika jamii yetu.
Nilisikitika hapo awali kumsikia Askofu mmoja akikiri kuwa hajaisoma katikba ya OIC lakini akisisitiza bado kupinga sisi kujiunga nao. Ni kama vile wenzangu walivyompandishia mori Salman bila kukisoma kitabu chake cha Satanic Verses!
Nashukuru ndugu Kithuku kwa maelezo yako mazuri.
Naomba kuuliza maswali ya nyongeza kama ifuatavyo:
Je kuna jambo lolote kwenye katiba ya nchi ambalo linakinzana na imani ya kiislamu?
Kama lipo, je na hao waislamu wakianza kudai hili jambo lenye manufaa ambalo limeathiriwa na dini nyingine watatimiziwa haja yao.
Je kujiunga na IOC kunaathiri vipi dini zingine?
Na je dini zipi hizo ambazo zinaathiriwa?
Bila kupoteza mwelekeo wa mjadala, ni kwamba msingi wangu wa kupinga nchi yetu kujiunga na OIC ni kwamba sikubaliani na malengo ya OIC, basi. Hao wanaokubaliana na malengo hayo wana haki ya kujiunga, lakini wafanye hivyo kwa namna ambayo haitawalazimisha wengine kushiriki utekelezaji wa mambo wasiyoyaamini.
Nashukuru ndugu Kithuku kwa maelezo yako mazuri.
Naomba kuuliza maswali ya nyongeza kama ifuatavyo:
Je kuna jambo lolote kwenye katiba ya nchi ambalo linakinzana na imani ya kiislamu?
Kama lipo, je na hao waislamu wakianza kudai hili jambo lenye manufaa ambalo limeathiriwa na dini nyingine watatimiziwa haja yao.
Je kujiunga na IOC kunaathiri vipi dini zingine?
Na je dini zipi hizo ambazo zinaathiriwa?
.........hakuna ubaya uka-highlight hicho ki/vipengele.........ili tuvivalie njuga.......kwani katiba yatakiwa iwe neutral.............we should not forego onething in order to fight ahead of something else!!!..............
..........hatuwezi kuendeleza makosa eti kwa sababu kuna makosa mengine somewhere............
sikijui, ndio nauliza kujua kama katiba iko fair. Kama haikofair basi iwe overhauled kama inawezekana ili kuondoa kutokuridhishwa kwa pande husika, hasa kwa wote dini zao, zisiathiriwe na dini nyingine.