YNIM,
Nawe umekosa objectivity. Nimeuliza kwa kuwa tumeambiwa kuwa maslahi ya Waislamu ni duni na hivyo kulinda na kujenga maslahi yao ni kujiunga OIC. Ama tumeambiwa kuwa Waislamu wana unyonge na njia ya kufungamana na kujenga umoja ni kujiunga OIC.
Nimeuliza, je Waislamu wa Saudi na kwingineko ambao ni predominantly Islamic state (or declared to be Islamic state and they are rich) wamefanya nini kuhudumia adha za Umasikini na Unyonge wa jamii zilizoko katika nchi zao ambao ni Waislamu?
Kwangu mimi, vita dhidi ya Umasikini na Unyonge haina rangi, dini, kabila, umri au jinsia. Ni vita Universal ambayo ni shurti kila mtu aifanye na atumie bidii zake kuvunja nguvu zinazolea Umasikini na Unyonge.
Kwa mantiki hiyo, historia inatuonyesha kuwa kukua kwa jamii kulitokana na ubaguzi, nako kukazaa Umasikini na Unyonge. Ubaguzi huu haukujifunga kwa Mzungu dhidi ya mweusi tuu au Mwarabu dhidi ya Mwasia, ni hata Mwafrika kwa Mwafrika, Mwarabu kwa Mwarabu, Mkristo kwa Mkristo, Muislamu kwa Muislamu, Wanaume kwa Wanaume, Wanawake kwa Wanawake na kadhalika.
Sasa tukisema Tanzania ijiunge OIC ili kudhibiti Unyonge na Umasikini wa Waislamu, swali linakuja, jee ni jukumu la nani kuangalia na kudhibiti kwa nchi yetu Unyonge na Umasikini wa Wakristo, Wapagani, Wahindu na Mabudha? Je tutasema ni Jukumu la Vatican ambayo ni Nchi? what about Lutherans, Anglicans, Baptists, Pentecostal who are not Catholics or believe in Vatican and Papacy?
Kama Serikali yetu inajiunga kama nchi katika umoja kama huu ambao ni shirikisho la nchi za Kiislamu lenye kukaribisha nchi na jumuiya za Kiislamu kujiunga, basi iwe ni haki kwa Tanzania kama nchi (si taasisi binafsi na za Kidini) kujiunga na World Council of Churches, World Council of Pagans, Atheists na Agnostics!
Nafahamu, kuwa CCT (Church Council of Tanzania) ni mwanachama wa World Council of Churches, TEC ya Wakatoliki iko chini ya Universal Roman Catholic Church, ELCT (Evangelical Lutheran Church of Tanzania) ni mwanachama wa Lutheran World Federation na Uanachama wa Taasisi hizi katika jumuiya hizi ambako maslahi ya kawaida ya kiroho na kimwili ya Wakristo wa madhehebu haya huzungumzwa na si kutumia mwavuli wa Nchi.
Labda niulize, kwa nini Bakwata haijajiunga OIC independently bila kutaka Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania iwe mwanachama wa OIC?
Mnaposema kuwa Vatican ni nchi ya Kidini, je mnasahau kuwa Saudi Arabia ni Nchi ya Kidini?
OIC na Vatican are two different things. One is an organisation of Islamic Countries, similar to AU for African Countries and the other one is a Country, yes the head of Country is Pope who is the leader of Catholic church, Similar to the King of Saudi Arabia a Muslim country who is the defender and protector of Islam and its holy places in Saudi Arabia!