Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

SINA TATIZO NA KUJIUNGA OIC, ILA WASIWASI WANGU NI JE WAKRISTO WAKIAMUA KITU SAWA NA HIKI WAISLAMU WATAKUBALI.

NI MUDA SASA UMEPITA WAISLAMU KILA MAHLI DUNIANI WANAJIONA INFERIOR, WAGOMVI WAO, WALALAMISHI WAO, MASKINI WAO, WANAOJILPUA WAO.WAISLAMU THEY DONT HAVE SOUND MIND, WAO NI WABISHI FOE EVERYTHING, NI WATU WA KUDAI HAKI KILA SIKU KILA MAHALI, UTHIBITISHO WA JAMII YA KIISLAMU IMEDHARAULIKA DUNIANI HATA NA BAADHI YA WAISLAMU WENYEWE UAELEZE AMISINGI YA DINI HII, KUWA ILIENEZWA KWA CHUKI NA UPANGA.

message sent

I wonder what have the rich Islamic states done to eradicate poverty and inferiority feelings amongts it citizen and follower of Islam! Like Saudi Arabia, Kuwait, Brunei, Oman, Bahrain, Syria, Indonesia, UAE, Jordan, Iran, Turkey and others!
 
Ndugu yangu Mkamap,

Jana kwenye post yangu nilidiriki kunukuu kwa urefu kabisa Katiba yetu inasemaje kuhusu swala hili la dini. Kulingana na Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali haina dini, wala haijihusishi na masuala yoyote kuhusu dini, kwani Katiba inasema, mambo yote yanayohusu dini ni masuala ya mtu binafsi na hivyo serikali haitaingilia masuala hayo, hivyo basi suala la Serikali kujaribu kujiunga OIC au kujiingiza kwenye mchakato wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi ni kinyume na ukiukwaji wa Katiba. Kwa kifupi nanukuu tena Ibara (kifungu) ya 19 cha Katiba ya Jamhuri wa Mungano wa Tanzania:

19(1)- Kila mtu anastahili kuwa uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.

19(2)- Kazi ya kutangaza dini, kufanya Ibada na kueneza dini itakua ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuia za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya Nchi.

19(3)- Hifadhi ya haki zilizotajwa katika ibara hii itakua chini ya taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama wa jamii, amani katika jamii maadili ya jamii na umoja wa kitaifa.

19(4)- Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana ua kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.


Hivyo basi, naomba kusisitiza kauli yangu kwamba, Katiba yetu ipo wazi kabisa kwamba serikali haina dini wala haijihusihi kwa namna yoyote na masuala ya dini, Kama ni kujiunga na OIC basi BAKWATA inaweza ikajiunga kama institution na sio Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kujiunga kama Nchi.

Mkuu
Hapo ndipo inabidi tuanze kujadili na watetezi watuthibitishie kua-
1.Uislamu sio dini maana OIC ni jumuia ya waislamu.
2.KADHI si ibaada na wala haiusiani na suala la DINI.

Maana mustaafu wetu yani KATIBA imeyaweka mambo kinaganaga .Sasa kufanya mambo bila kufuata misingi ya katiba yetu ni uhuni mkubwa sana.

Huu uhuni wa kutofuata SHERIA ama KATIBA ya nchi zinasema je ndio umetufikisha hata ktk masuala ya ufisadi yasioisha.MWIZI tangu lini akapewa nafasi ya kuripa deni bila kumfikisha ktk chombo husika yani mahakama na mahakama ndio iamue kutia hatiani aripe ama aachiwe huru.
 
Naomba nitoe mchango wangu kuhusu hili swala la Mahakama ya kadhi.

Kwa muda mrefu sasa, Serikali imekua ikikwepa kutolea tamko la wazi kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa Mahakama ya Kadhi nchini Tanzania. Kuna research nyingi sana zimeshafanywa na pia, hivi karibuni, Tume ya Kurekebisha Sheria ilifanya utafiti kuhusu uanzishwaji wa Mahakama hiyo lakini cha kushangaza haikuweka hadharani matokeo ya utafiti wake.

Pamoja na hayo, kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi, kunaonekana au kunatafsiriwa na watu wengi kwamba, Serikali ya Tanzania inaonekana kuegemea upande mmoja kitu ambacho ni kinyume kwa Serikali isiyo na dini (circular State).

Kutokana na taarifa za awali za Law Reform Commision, imeonekana uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kunaweza kuleta mgongano ndani ya jamii kwani kuna jamii mbalimbali ambazo nazo zinaweza kutaka nazo kuanzisha mahakama zao, madhalani, kwa wale wanaofuata dini za kimila, nao wanaweza wakadai mahakama zao za kimila kama zizokwepo wakati wa Ukoloni chini ya Machifu na Watemi.

Pili, kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ambayo itahudumiwa na Serikali ni kinyume cha sheria na katiba kwani kulingana na Ibara ya 19 ya Katiba ya Jamhuri wa Muugano wa Tanzania, Serikali haina dini wala haijihusishi na dini.

Tatu, Mahakama ya Kadhi itakapoanzishwa je, itahudumiwa na fedha kutoka wapi? Bajeti ya Serikali au? Na kama ni bajeti ya serikali, je ni halali kutumia kodi za wananchi (wenye dini na wasio na dini, wakristo na madhehebu mengine) kwenda kuendeshea mahakama ya Kadhi ambayo wao hawajihusishi nayo?

Hivyo basi, kitendo cha serikali kushindwa kutoa hoja za moja kwa moja, kumechangia watu kulifanya hili swala la Mahakama ya kadhi kuwa ni la kisiasa, na baadhi kujaribu kutafuta nalo umaarufu, kumbe suala hili la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ni suala la kisheria na la Kikatiba zaidi na ambalo jibu lake liko waaazi kabisa...!
 
Mkuu
Hapo ndipo inabidi tuanze kujadili na watetezi watuthibitishie kua-
1.Uislamu sio dini maana OIC ni jumuia ya waislamu.
2.KADHI si ibaada na wala haiusiani na suala la DINI.

Maana mustaafu wetu yani KATIBA imeyaweka mambo kinaganaga .Sasa kufanya mambo bila kufuata misingi ya katiba yetu ni uhuni mkubwa sana.

Huu uhuni wa kutofuata SHERIA ama KATIBA ya nchi zinasema je ndio umetufikisha hata ktk masuala ya ufisadi yasioisha.MWIZI tangu lini akapewa nafasi ya kuripa deni bila kumfikisha ktk chombo husika yani mahakama na mahakama ndio iamue kutia hatiani aripe ama aachiwe huru.

Kwa wale watakaopenda kuyasoma mojakwamoja maandishi ya katika kuhusiana na hili swala, yako ukurasa wa 22 ukifungua hapa chini:
[media]http://www.habarinamatangazo.com/constitution.pdf[/media]
 
halafu sio huruka ni hulka....una matatizo mengi tu ya msingi ambayo inabidi ujikwamue mwenyewe kwanza kabla ya kujifanya mjuaji wa mambo complex kushinda uwezo wako wa kufikiri.....unasikitisha!!

Mkuu YNIM, hivi ni kwanini majadiliano yako mengi huwa ni ya tone ya kukandya kandia sana ndugu?! .... kweli tunashindwa kujadiliana bila kuonesha hali ya dharau kwa maoni ya wenzetu? Tuendeleze kijiwe hiki kwa kupingana kwa hoja jamani.

Ni maoni yangu tu ndugu. Akhsante.
 
YNIM,

Nawe umekosa objectivity. Nimeuliza kwa kuwa tumeambiwa kuwa maslahi ya Waislamu ni duni na hivyo kulinda na kujenga maslahi yao ni kujiunga OIC. Ama tumeambiwa kuwa Waislamu wana unyonge na njia ya kufungamana na kujenga umoja ni kujiunga OIC.

Nimeuliza, je Waislamu wa Saudi na kwingineko ambao ni predominantly Islamic state (or declared to be Islamic state and they are rich) wamefanya nini kuhudumia adha za Umasikini na Unyonge wa jamii zilizoko katika nchi zao ambao ni Waislamu?

Kwangu mimi, vita dhidi ya Umasikini na Unyonge haina rangi, dini, kabila, umri au jinsia. Ni vita Universal ambayo ni shurti kila mtu aifanye na atumie bidii zake kuvunja nguvu zinazolea Umasikini na Unyonge.

Kwa mantiki hiyo, historia inatuonyesha kuwa kukua kwa jamii kulitokana na ubaguzi, nako kukazaa Umasikini na Unyonge. Ubaguzi huu haukujifunga kwa Mzungu dhidi ya mweusi tuu au Mwarabu dhidi ya Mwasia, ni hata Mwafrika kwa Mwafrika, Mwarabu kwa Mwarabu, Mkristo kwa Mkristo, Muislamu kwa Muislamu, Wanaume kwa Wanaume, Wanawake kwa Wanawake na kadhalika.

Sasa tukisema Tanzania ijiunge OIC ili kudhibiti Unyonge na Umasikini wa Waislamu, swali linakuja, jee ni jukumu la nani kuangalia na kudhibiti kwa nchi yetu Unyonge na Umasikini wa Wakristo, Wapagani, Wahindu na Mabudha? Je tutasema ni Jukumu la Vatican ambayo ni Nchi? what about Lutherans, Anglicans, Baptists, Pentecostal who are not Catholics or believe in Vatican and Papacy?

Kama Serikali yetu inajiunga kama nchi katika umoja kama huu ambao ni shirikisho la nchi za Kiislamu lenye kukaribisha nchi na jumuiya za Kiislamu kujiunga, basi iwe ni haki kwa Tanzania kama nchi (si taasisi binafsi na za Kidini) kujiunga na World Council of Churches, World Council of Pagans, Atheists na Agnostics!

Nafahamu, kuwa CCT (Church Council of Tanzania) ni mwanachama wa World Council of Churches, TEC ya Wakatoliki iko chini ya Universal Roman Catholic Church, ELCT (Evangelical Lutheran Church of Tanzania) ni mwanachama wa Lutheran World Federation na Uanachama wa Taasisi hizi katika jumuiya hizi ambako maslahi ya kawaida ya kiroho na kimwili ya Wakristo wa madhehebu haya huzungumzwa na si kutumia mwavuli wa Nchi.

Labda niulize, kwa nini Bakwata haijajiunga OIC independently bila kutaka Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania iwe mwanachama wa OIC?

Mnaposema kuwa Vatican ni nchi ya Kidini, je mnasahau kuwa Saudi Arabia ni Nchi ya Kidini?

OIC na Vatican are two different things. One is an organisation of Islamic Countries, similar to AU for African Countries and the other one is a Country, yes the head of Country is Pope who is the leader of Catholic church, Similar to the King of Saudi Arabia a Muslim country who is the defender and protector of Islam and its holy places in Saudi Arabia!
 
hahahahaha kwahiyo umeniona mie tu!?? au kwasababu nipo upande mwingine wa ule ambao wewe unauunga mkono? nina agenda......na ndio maana nipo kama nilivyo ktk jina langu la bandia, YNIM!! unaweza kuni-ingore (huo ni ushauri wa bure)

Sijali kuhusu mtu yeyote hapa JF anavyofikiria kuhusu mimi na sipo hapa kutafuta rafiki au masifa...kama navunja rule(s) za JF basi adhabu yangu nifungiwe zaidi yapo na namnukuu FMES, spade nitaita spade!! sorry steve......kwahiyo ni huruka au ni hulka?? kosa lipo wapi??

watu bwana....

Yalikuwa maoni yangu tu YNIM. Samahani kama nimekukwaza. Tuendelee na mjadala. Shukrani.
 
mie sijali kama umenikwaza au vinginevyo....mie nafanya nionavyo mie sahihi, iwe popular or unpopular, sijali kabisa!!

hapa ktk thread hii mie nipo against hii tone ya udini iliyowekwa na Mkamap na wengi wenu kushindwa kuikemea.......udini dini na mie ni kama paka na maji, sitaki kusikia!!!

kama nakandia watu basi ni haki yao kwasababu ni wadini....je tupo pamoja anko?

Tupo pamoja. Akhsante.
 
Hi to you all discussants!

Nimefuatilia mjadala unavyoendelea na mawazo ambayo yameshatolewa mpaka sasa, nashawishika kabisa kuwa hili suala lina uhusiano kwa kiasi kikubwa na muungano. Huu muungano tulionao kwa kweli ni wa mashaka. Na mara zote, matatizo yote yanayohusu muungano yaanzia kwa wenzetu wa visiwani. Kama ninawaelewa, ni kama vile kwa kuwa kwenye muungano kuna faida wanazipoteza (mnaofahamu zaidi mtanisahihisha). Hili suala kwa kweli limekuwa linanikera haswa kwa kuwa binafsi sijui faida hata moja ya muungano (kwa upande wa bara). Labda tunaposafiri ng'ambo na kuitaja Zanzbar kama kivutio cha utalii kinachopatikana Tanzania, labda! Hata wakijitenga, we can still send tourist to enjoy beautiful beaches they have. Utalii si biashara? Now, hoja yangu ya msingi ni kuwa wakati umefika wa kuwapa uhuru wa-zanzbari; wa kuchagua ama muungano au la. Wakati wa kuwabembeleza umekwisha. Dunia ya kubembelezana ilikwisha kitambo. To the best of my knowledge, hv visiwa vinategemea bara kwa mambo mengi sana. Na mara nyingi wanapewa huduma kutoka bara at a subsidised rates (eg. umeme). Anyway, mimi nafikiri tuwaache wajitegemee kama nchi huru. Nimefikiri sana sioni hasara tutakayoipata. Maybe I am jumping into conclusion but really I don't see any negative impact. It's sad that while every state in the world wants to win the synergy by joining their forces, our fellow zanzbar's are keen to secede from the union. Well, let them go. Otherwise, they will bring us more bad than good.

Regards,
 
Yurnameis Mine,
Mkuu umezungumza exactly kile kilichokuwa akilini mwangu..Yaani watu wameshindwa kujiuliza maswwali madogo madogo ya msingi kama ulivyosema.
Kila siku, kila kukicha waislaam hivi waislaam vile kwa sababu tu wanaoomba kitu hicho ni wanasiasa waislaam na kitu hicho kinahusiana na waarabu kwa hiyo ni lazima kiwe cha waislaam...
Kuna siku nimewahi kusoma mtu akiuliza ati kwa nini tunaita umoja wa nchi za kiafrika wakati nchi kama Egypt, Algeria, Morocco, Tunisia na Muaritania ni za waarabu..
I mean jamani tuwe tunafikiri zaidi ya kuweka imani pofu kama hizi...

Mkuu Rev. Kishoka,
Samahani sana lakini iweje sisi tukubali mikopo ama kusaidiwa na nchi kama Marekani wakati ina maskini wengi sana ndani ya nchi hiyo? kama wao wanashindwa kuwasaidia maskini wao wataweza vipi kutusaidia sisi?...
Hili ni swali linalofanana sana na swali lako na kusema kweli sijui hata utalijibu vipi?...unajua unaikumbusha maskini mmoja zamani sana nilimwita kumpa msaada akanitaza kisha akaniendelea kuomba wenye magari waliokuwa waki park karibu na msikiti.. hiyo sadaka yangu nikampa mwenziwe tena nadhani mwanaye..alipokuja kuambiwa kiasi nilichompa huyo mtoto basi kila siku yulemaskini alipokuwa akiniona alikuwa akinikimbilia...sikumpa kitu ila kila siku nilimpa yule mtoto..
 
Yurnameis Mine,
Mkuu umezungumza exactly kile kilichokuwa akilini mwangu..Yaani watu wameshindwa kujiuliza maswwali madogo madogo ya msingi kama ulivyosema.
Kila siku, kila kukicha waislaam hivi waislaam vile kwa sababu tu wanaoomba kitu hicho ni wanasiasa waislaam na kitu hicho kinahusiana na waarabu kwa hiyo ni lazima kiwe cha waislaam...
Kuna siku nimewahi kusoma mtu akiuliza ati kwa nini tunaita umoja wa nchi za kiafrika wakati nchi kama Egypt, Algeria, Morocco, Tunisia na Muaritania ni za waarabu..
I mean jamani tuwe tunafikiri zaidi ya kuweka imani pofu kama hizi...

Mkuu Rev. Kishoka,
Samahani sana lakini iweje sisi tukubali mikopo ama kusaidiwa na nchi kama Marekani wakati ina maskini wengi sana ndani ya nchi hiyo? kama wao wanashindwa kuwasaidia maskini wao wataweza vipi kutusaidia sisi?...
Hili ni swali linalofanana sana na swali lako na kusema kweli sijui hata utalijibu vipi?...unajua unaikumbusha maskini mmoja zamani sana nilimwita kumpa msaada akanitaza kisha akaniendelea kuomba wenye magari waliokuwa waki park karibu na msikiti.. hiyo sadaka yangu nikampa mwenziwe tena nadhani mwanaye..alipokuja kuambiwa kiasi nilichompa huyo mtoto basi kila siku yulemaskini alipokuwa akiniona alikuwa akinikimbilia...sikumpa kitu ila kila siku nilimpa yule mtoto..

duuh!! Bob una mambo wewe.... 🙂
 
This is getting tedious. Kwa mara ya mwisho......

Kwa hiyo nilipokuuliza umepata wapi habari hii najua kabisa hukusoma between line kuelewa uongo uliopo ktk taarifa nzima ya mwandishi...
Si kweli kwamba Islamilia hawatambuliwi kama waislaam na kama haya maneno ni ya kweli basi msingesema huko Iraq wanapigana waislaam kwa waislaam. Tofauti za madhehebu ndani ya dini moja hakuwezi kuondoa uhalali wa dhehebu jingine ni sawa kabisa na ukimuuliza Anglican kuhusiana na Mkatoliki.. Wewe unatakiwa kujua tofauti hizi kabla hujaandika kitu kuhusiana na dini unayojaribu kuipaka tope. Ismailia ni dhehebu ndani ya Shia Muslims na wamejitenga kutokana na sababu sawa na zile za makanisa mengine yalivyoitenga toka Ukatoliki..lakini pamoja na tofauti zao zote wote wanasoma Biblia.. Hakuna tofauti yoyote na madhehebu ndani ya Uislaam ni tofauti za kawaida na hazina maana dhehebu moja linatambulika zaidi ya jingine hali sisi sote hatufahamu kilichoko huko juu... Hilo moja.

Waismailia ni wafuasi wa Imam Ismail bin Jaffar, mtoto wa kwanza wa kiume wa Imam Jaffar al-Sadiq. Sisi tunaowaita wa Ismaili haswa ni waNizari ambao ni wafuasi wa Aga Khan. Waismailia wengine ni wadruze (lebanon, syria na Israel), Mabohora (India) n.k. Hawa wanatofautiana na washia wenzao, waithnasheri, ambao wanamfuata mdogo wake Ismail aliyeitwa Musa al-Kazim. Waismailia wengine wanajihesabu kuwa wao ni tofauti na washia,ambao kwa mtazamo wao, ni hao waithnasheri. Wote hawa, tofauti na wasunni, wanamtambua Imam wao wa wakati huo kama mwakilishi halisi wa Mwenyezi Mungu hapa duniani. Kwa wa Ismailia (waNizari) Imam wao wa 49 ni Karim Aga Khan. Imam wao wa 46 alikimbilia Mumbai kutoka Iran. Waismailia wanaamini kuwa Imam wao ndiye atakayeamua idadi ya swala wanazotakiwa kufanya kwa siku. Wafuasi wa Aga Khan kwa wakati huu wanaswali mara tatu kwa siku. Kitabu chao kikuu baada ya Quran ni Ginans. Imani yao imechangiwa kwa kiasi fulani na imani za wahindu k.m. imani katika Yuga 4 kupitia Sat, Treta, Dwapar na Kali. Wanaamini tena kuwa kila muumini anatakiwa atoe 1/8 ya baki la pato yake kama khumms. Hii imechangia sana kwenye utajiri wa imam wao. Aga khan ametumia utajiri wake kuanzisha vyombo vya maendeleo kama the Aga Khan Development Network inayowekeza katika nchi zinazoendelea. Waismailia wengine ni waDruze. Hawa hawatambui hata Hijja ya kwenda kwenye Kaaba! Wao wanaamini katika reincarnation. Hawaamini Taharah kama wengine, badala yake wanaamini kwenye Shahada. Pamoja na tofauti zote hizi na nyingine, wote hawa wanajihesabu waislamu.

Ninaposema kuwa baadhi ya waislamu wengine hawawatambui kama waislamu haswa ni kutokana na imani hizo. Sisi tulionje tunawaona kuwa wote ni waislamu lakini ni hao wenye dini yao ndiyo wanatoa utambuzi au lah. Kwetu sisi wakristu, baadhi yetu hatuwatambui Mashahidi wa jehovah kama wakristu kutokana na kupinga kwa utatu mtakatifu na imani juu ya jehanam. Hii haina maana kuwa wao hawajioni kuwa ni wakristu. Vile vile kwa Mormons ( Church of Jesus Christ of latter day saints). wao wanaamini kwenye kitabu chao cha Mormon ambacho wakristu wengine hawakitambui. Ndiyo maana Romney alikuwa na kazi kuthibitisha kuwa yeye pamoja na umormon wake ni mkristu!

Ni dini gani nimeipaka matope? Kwani tukisema washia na wasunni wanauana huko Iraq kutokana na kutokukubaliana katika uislamu wao tutakuwa tunakosea? Itakuwaje muislam mmoja aone ni halali kumlipua mwenzie kama haoni huyo amepotea kwa hiyo hata uislamu wake una dosari? Hao unaowaona sasa hivi ni maswahiba, wakatoliki na waanglikana waliuana kwa muda mrefu, kila upande ukiamini kuwa mwingine amepoteza ukristu wake kwa hiyo ni halali kuuawa. Soma historia na uielewe.


Pili ni wewe uliyezungumzia kwamba EAMWS founder wake ni AghaKhan kutokana na habari uliyoisoma na kuiamini ndio maana umeitoa hapa. Sasa ikiwa founder ni AghaKhan imekuwaje tena chombo hiki hiki alichokianzisha kiwe ni chombo cha Shia Muslims lakini kabla hakijaanza kazi huyo huyo founder wake ajipinge na kusema ni chombo cha Waislaam wote hali yeye mwenyewe ndiye founder!....
Hapa ulichokosa kuangalia ni between the lines kuwa EAMWS kilikuwa chombo cha waislaam kilichoanzishwa (registered) na waislaam wahindi kwa kupata support ya mfuko toka kwa sponsor ya mfuko wa AghaKhan na chombo chake (Network) AKDN..huu ni utaratibu wa kawaida kabisa lakini kwa sababu gazeti haliwezi kuandika kila hatua ya vitu hivi kwa sababu zao wenyewe huwa kuna mapungufu ambayo untakiwa kusoma kwa makini kuweza kuyachambua... siku zote hapa lugha yetu ni kutoa pumba ktk mchele, haina maana waandishi wengine nje ni exceptional.

Nilichosema ni kuwa Aga Khan alikuwa mmoja wa waanzilishi wa EAMWS na mmoja wa wafadhili wake wakuu. Aga khan, pamoja na kuwa baadhi ya waislamu hawamkubali, kila siku anajihesabu kuwa ni muislamu kwa hiyo si ajabu kuwakaribisha waislamu wengine kwenye hicho chombo. Hivi hao wahindi waislamu unaowazungumzia ni nani kama sio waismailia (Nizari) na mabohora ambao ndiyo waliojikita sana Afrika ya Mashariki? na unaamini kweli kuna muismaili au bohora atakayejiunga na chombo kisichopewa baraka na imam wake? Naona hauwajui. With all due respect, kusoma kwako between the lines kuna hitilafu kama ilivyo argument yako. Isome tena uone kama imekaa sawa!

Mathlan, nitakupa mfano mmoja kisha uweke ktk kuanzishwa kwa EAMWS. Tuseme World Vison ni chombo kilichoanzishwa na wazungu kuwasaidia wakristu Africa kwa kupitia kanisa la katoliki (vatican) haina maana chombo hicho ni cha wazungu na mwanzilishi wake ni papa Paul..Na yawezekana kabisa mwandishi mkatoliki, mzungu mkazi wa vatican akasema founder wa World Vision ni Papa Paul akiwa na maana ya support yake na pengine hata kuhudhulia kukata utepe wa ufunguzi rasmi wa chombo hicho lakini ukweli sii yeye mwanzilishi..
Kwa hiyo kaa mimi Muislaam nitasoma bila kuangalia between the lines naweza kusema kanisa katoliki limetuingilia nchini na pengine kutoa tafsiri kama zako kuhusiana na tofauti zilizopo kati ya Wakatoliki weusi na wazungu na kuzitumia kisiasa kuuhabarisha umma.

Unakosea tena. World Vision ni shirika la kikristu na hauwezi kukana hiyo. Hauwezi kujiunga na shirika hilo kama si mkristu ingawa misaada yake haiangalii dini. na moja ya lengo lao ni kueneza neno la Mungu na kumenzi Yesu Kristu. Kwa sababu wazungu wengi ni wakristu na ndio wenye uwezo, bila shaka sehemu za uongozi zitashikwa sana na wazungu. Si kuwapaka matope. Ndiyo ukweli. sasa kukataa kuwa OIC ni chombo cha kiislamu kinachoongozwa kwa sehemu kubwa na waarabu ni kuwa disingenuous.

Hakuna, mkatoliki, raia wa Vatican anayeweza kuanzisha chombo kama hicho bila kupata baraka ya Pope. Akikitambulisha kama chombo cha wakatoliki ndiyo kabisa.

Lakini nilichokisema mimi, kwa kunukuu web site ya muislamu mwenzio, ni kuwa Aga Khan alikuwa mmoja wa waanzilishi. Kama unapinga, pinga kwa kunieleza ni wakina nani walikuwa waanzilishi!


World Vision is an international partnership of Christians whose mission is to follow our Lord and Saviour Jesus Christ in working with the poor and oppressed to promote human transformation, seek justice and bear witness to the good news of the Kingdom of God.

Akija Pope kukata utepe, na kutangaza kuanzishwa kwa shirika hili nchini, wewe kama muislamu utakuwa na haki kabisa kulitilia mashaka kiimani na kuamua kukataa lupokea misaada yake. Kudai kupokea misaada kutoka kwa na kuwakataza kuhubiri utakuwa hauwatendei haki maana toka awali linajulikana kama shirika la kidini.

Nne, Sii kweli kwamba EAMWS kilikuwa hakipendwi na waislaam wa TANU wakati ukweli ni kwamba waislaam wote waliokuwa TANU wakati huo walikuwa wanachama wa EAMWS nadio walioanzisha chama cha TA iweje tena hao waislaam waliokuwa TANU wajipinge wenyewe...
Kisha kwa taarifa kamili na yenye ukweli nakuomba kamtafuta mzee Ally Skyes ambaye ni mmoja wa waasisi wa TANU pamoja na kwamba kajitoa ktk siasa muulize vizuri nafasi ya EAMWS ndani ya TANU kabla ya mwaka 1968...
Maelezo yaliyotangulia na mwandishi haya make sense at all!... isipokuwa kama msomi mzuri inabidi uzame ndani zaidi kuelewa kilichotokea.

Unakosea tena. Nilichosema, kwa kunukuu tovuti ya muislamu, ni kuwa BAADHI ya waislamu waliokuwa wanachama wa TANU walikitilia mashaka EAMWS. Si wote, baadhi. Na hao baadhi walichangia katika kupigwa kwake marufuku. TANU ilianzishwa mwaka 1954 na EAMWS mwaka 1958, sasa itakuwaje wanachama wa EAMWS waanzishe TANU? Bila shaka kuna wanachama wa TANU waliojiunga na EAMWS. Hata huyo Ally Sykes inawezekana kuwa alikuwa mwanachama wa pande zote mbili. Sina haja ya kumtafuta. Ninachoshauri, mwambie aandike article itakayoelezea yote haya anavyoelewa yeye, aitoe hadharani ili na wengine waliokuwepo wachangie. Ingawa mimi ni mtu mzima, sikuwepo wakati huo, lakini nawajua waliokuwepo, mbali ya Sykes. Hakuwa peke yake muasisi wa TANU.

Maelezo yaliyotangulia na mwandishi haya make sense at all!... isipokuwa kama msomi mzuri inabidi uzame ndani zaidi kuelewa kilichotokea.
Huko nyuma nimekueleza vizuri nini ilitokea na kitu gani kichosababisha mwalimu kukiua chombo hiki ambacho kusema kweli Waislaam kutokana na mchango wao ktk kutafuta Uhuru walianza kutamani fadhila fulani za madaraka au fehda kama binadamu.. kama haya yanayompata Kikwete leo hii toka kwa wafadhila wake wa uchaguzi uliopita.
Kisha kwa sababu hawa jamaa hawakupata kile walichokitaka walijaribu kufanya mapinduzi ambayo hayakufanikiwa. mwalimu alikuwa Arusha ktk mkutano akabonyezwa na Sheikh Kassim Bin Jumaa kuhusiana na jaribio la kumwondoa madarakani na wahusika kwa bahati mbaya wengi wake walikuwa waislaam na kama nilviyosema viongozi wote wa kiislaam ndani ya TANU wakati huo walikuwa members of EAMWS..

Sasa hapa unasema nini? Kuwa wanachama wa EAMWS walitaka kufanya mapinduzi, kumwondoa mwalimu madarakani lakini wakastukiwa. Na aliyewachongea ni muislamu mwenzio! Sasa haya si mambo ya kisiasa na sio dini? Sasa huu si mfano wa mgawanyiko uliokuwepo katika jamii ya waislamu, uliochangia kwa kiasi kikubwa kupigwa kwake marufuku. Kuwa mwanachama na kuwa na imani nacho ni vitu viwili tofauti. Si wanachama wote wa CCM wana imani nacho! Argument yako haina mantik.

Hapa mwandishi alijaribu kuweka tabaka kuingiza siasa ktk maswala ya dini kwamba ikiwa mwenyekiti wa EAWMS ni toka chama cha Upinzani basi waislaam wa chama kingine watakikataa chombo chao cha dini kwa sababu za kisiasa hali wapinzani wakubwa wa mwalimu miaka ya 1968 walikuwa ndani ya chama chake mwenyewe yaani TANU pamoja na kwamba wengi wao walikuwa waislaam na ndio maana nikawataja kina Kambona..
hapa nikiwa na maana hata wewe mwenyewe umetaka kuchanganya dini na siasa ukitumia vigezo vya rangi za watu kufikia maamuzi. hakuna kabisa uhusiana wa karibu kati ya maswala haya ya siasa na mahakama ya kadhi ikiwa huna imani kuwa swala la mahakama ya kadhi linahusiana na siasa.. na sijui kama unataka kusema hata hiyo mahakama ya kadhi aliyeianzisha ni Agha Khan..

Umekiri kuwa waanzilishi wa EAMWS walikuwa wahindi. Umekiri kuwa kuna watu katika EAMWS walitaka kumpindua (maneno yako) Nyerere. Halafu unanishutumu mimi kuwa ni mdini na mbaguzi wa rangi? Kusema kuwa wazungu waingereza na wajerumani walitutawala nako utaita ni ubaguzi wa rangi? Wakina Kambona walikuwa maswahiba wakuu wa Nyerere hadi walipotafautiana miaka ya kati ya 60. Wakina Zuberi Mtemvu na Fundikira walikuwa wapinzani wa wazi mara baada ya kupata uhuru. Au tuseme kwa sababu wakina Kambona, Kamaliza, Chipaka walikuwa wakristu basi wakristu walikuwa ndio wapinzani wakubwa wa Nyerere? Ukiulizwa Bibi Titi Mohamed nae alikuwa mkristu? Hapana, usitake kupoteza mada. hapa tunazungumzia EAMWS, chombo cha waislamu, hatuwezi kuepuka masuala ya dini. Kusema kuwa baadhi ya waanzilishi walikuwa waismailia na mabohora si kuwa mbaguzi wa rangi. Ni facts. Kusema kuwa mahusiano kati ya waswahili wenye ngozi nyeusi na wenzetu wenye ngozi za kahawia una matatizo ni fact. Waswahili hawakutoa neno ghabacholi kwa kuonyesha mapenzi. Kukana matatizo ni kuwa kama ostrich.

sasa hilo la mahakama ya kadhi na Aga Khan limetoka wapi? Au unataka kusema Mahakama ya Kadhi ni mbadala ya EAMWS. Ni payback time kwa kuwafutia chombo chenu?


Ni wewe uliyesema ama kuamini mwanzilishi wa EAMWS ni Aghan Khan na kuwa kilikuwa cha wahindi Ismailia, kikapigwa marufuku wakati wa Nyerere ukauliza kwa nini wasiifungue tena wakati wa Mwinyi bila kujiuliza why Muslims weusi ambao hawana asili ya kihindi ndio wanaopiga kelele leo kuhusiana na chombo hicho?..Yote ni katika kukuonyesha kwamba EAMWS kilikuwa ni chombo cha waislaam kwa waislaam sawa na BAKWATA ambacho ni chombo cha waislaam kwa ajili ya maslahi ya watawala na hujiulizi kuhusiana na mwanzilishi wake ambaye alikuwa Nyerere, asili yake ama dini yake, sasa sijui hapa utakuwa na story gani mpya kuhusiana na chombo hiki Bakwata kuwa nacho ni chombo cha watu gani!...wakatoliki na Wazanaki au?... hii ndio shida ya kuangalia rangi na ukashindwa kutazama upande wa pili kwa kipimo kile kile. Muda wote nimekuwa nikijaribu kukufahamisha ukweli huu..

Haya sasa Nyerere ndiye aliyeanzisha Bakwata! Hauoni kuwa unawatukana waislamu wenzio wengi tu kuwa hawawezi kufanya kitu bila kufanyiwa na mkristu. Hakuna chama kinachokubalika na wote katika jamii. EAMWS hakikubalika na waislamu WOTE ( majority pengine lakini si wote) na hivyo hivyo kwa BAKWATA. EAMWS ilifutwa na haijafufuliwa. Wenzetu, kutokana na experience yao, ni wachache wanaopenda kujiingiza katika mambo yenye mvutano. Kwenye siasa tumeanza kuwaona kwa wingi hivi karibuni ukiondoa wachache kama Jamal, kassam na Bryceson. Wahenga walisema, once bitten.........

Kwa bahati mbaya, kama hivi ndivyo unavyotetea hoja zako, hamna siku utakayo ni convince!

Kuna wakati nilikwambia sina busara. Ukaniambia hauwezi kubadilishana mawazo na mtu asiye na busara. Nikakuridhia lakini ukashindwa kuvumilia ukaniingiza katika haya malumbano! Narudi tena katika kukosa busara. I am out of here. Endelea na wengine wenye busara. Ila kumbuka kuwa hii ni enzi ya utandawazi. Karibu kila kitu kinapatikana!
 
Mkuu Rev. Kishoka,
Samahani sana lakini iweje sisi tukubali mikopo ama kusaidiwa na nchi kama Marekani wakati ina maskini wengi sana ndani ya nchi hiyo? kama wao wanashindwa kuwasaidia maskini wao wataweza vipi kutusaidia sisi?...
Hili ni swali linalofanana sana na swali lako na kusema kweli sijui hata utalijibu vipi?...unajua unaikumbusha maskini mmoja zamani sana nilimwita kumpa msaada akanitaza kisha akaniendelea kuomba wenye magari waliokuwa waki park karibu na msikiti.. hiyo sadaka yangu nikampa mwenziwe tena nadhani mwanaye..alipokuja kuambiwa kiasi nilichompa huyo mtoto basi kila siku yulemaskini alipokuwa akiniona alikuwa akinikimbilia...sikumpa kitu ila kila siku nilimpa yule mtoto..

Bro Mkandara,

Marekani, Canada, India, China, Pakistani zimetupa misaada bila kuweka masharti ya Udini. Zimetupa misaada huku inajulikana wazi kuwa kuna umasikini katika nchi zao.

Nilichokiletea hoja ni kile cha kusema kuwa OIC inajali maslahi ya Waislamu wa Nchi za Kiislamu na kutaka kuyafanya yawe bora. Ndiyo maana nikauliza, hizo nchi tajiri za Kiislamu, zimefanya nini kuondoa Umasikini na Unyonge kwa jamii zao katika nchi zao kabla ya kukimbilia kusajili nchi za kiafrika na kusema kuwa ni kwa kutumia Udini pekee ndipo maslahi ya Waislamu kushinda Unyonge na Umasikini kutakuwa na mafanikio kwa kujiunga kwenye umoja huu?

Mada hii inahusu OIC na Uislamu, si Marekani, China, Canada, India au UK.

Kama mada ingekuwa inazungumzia kwa nini Tanzania iwe mwanachama wa UN, AU, Commonwealth, WB,IMF, Non-Allign, Comesa na kuhoji mshikamano wa kiuchumi na vita dhidi ya Umasikini na Unyonge, nako ningehoji kama ninavyohoji peremende ya Ubepari na Demokrasia tunayolishwa na Marekani huku kwao kwenyewe kuna Umasikini, Unyonge na Ubaguzi!
 
Mhafidhina,
Mkuu mimi nakuelewa vizuri isipokuwa tunatofautiana sana ktk mtazamo wa swala zima...
Mahakama ya kadhi iliondolewa kisheria na haiwezi kurudi kama haikupitishwa kisheria Kikatiba kwa sababu kama hukumu ikitolewa na mahakama hii bila kutambuliwa kisheria, mkosefu anaweza kukataa hukumu hiyo na wasimfanye kitu. Hadi hapa tupo pamoja na inaleta maana kabisa kwani vitu hivi vinafanyika hadi hivi sasa hivi tunavyozungumza.
Mfano kuna wajomba huchukua mali za urithi wa mke na kumfukuza mke wa marehemu ndani ya nyumba kwa sababu mali ilikuwa ya bwana... wengine mke wa pili huwa hana sheria ikiwa hakupata baraka za mke wa kwanza naye hufukuzwa tena huitwa malaya tu. Mke aliyeachika (kutokana na matamanio ya bwana nje ya ndoa) lakini kazaa watoto huwa ana tatizo kubwa la uhusiano kati yake na mmewe, mke mwenza, watoto wao na kadhalika hii haina dini.... ni masiha ya kila Mtanzania..
Mahakama ya kadhi inaweza kuamua mali walochukua Wajomba irudishiwe kwa mke na watoto lakini kwa sababu mahakama hii haina sheria kikatiba, Wajomba wanaweza kukataa kurudisha mali kwa mke na msiwafanye kitu...Hii ndio sababu hasa ya viongozi wanaotaka ama kudai mahakama hii wanaomba serikali kutambua mahakama ili hukumu yake iwe inatambuliwa na hatua za kisheria zinaweza kuhukuliwa na vyombo vya serikali kama hakuna utiifu... sio maswala ya fedha ama gharama zake nani atazipokea kama wanavyodai jamaa zetu humu..nakubaliana na wewe kuwa wazushi hawaishi kutafuta sababu ambazo hazina msingi wakati waathirika bado wanapata taabu kupewa haki zao.

Binafsi naamini kabisa sheria siku zote inatungwa kutokana na kuwepo waathirika, sheria ina waprotect victims wanaokuwa abused na system mbovu isiyowatazama iwe ktk dini, rangi ama jinsia..
sasa basi kwutokana na misingi hiyo ndipo swala la mahakama ya kadhi limeingia ili kuondoa matatizo ya ndoa za kiislaam na mirathi ya watoto wao na mimi naongezea kusema tusikomee kwa waislaam kwani hata wakristu wana tatizo hilo hilo, shukran kwa viongozi wa kiislaam kuileta hoja hii ambayo kumbe haiwaathiri waislaam tu ila kila mtu kwa imani tofauti. na ndio maana hata swala la wao kuomba mahakama zao zinakuja kwa sababu waislaam wanashindwa kuelea kwamba tatizo la ndoa na mirathi sio lao pekee ila ni la jamii nzima.... (yale yale matatizo ya madai ya Tarime kujitenga kiuchumi).

Mimi nachosema ni kwamba hadi pale nyie waislaam mtakapo weza kufuata ibada hii kwa ufasaha labda ndipo mnaweza kudai mahakama ya kadhi lakini sasa hivi kila Muislaam anaoa anavyopenda yeye. Watoto wa nje ya ndoa kibao na mahakama ya kadhi haiwezi kuwatambua hivyo tatizo la waathirika litabakia pale pale..
Huwezi kuweka mahakama ikiwa hakuna tatizo na hakuna waathirika kutokana na results za ndoa mbovu ambazo hazikufuata misngi ya dini.
Hivyo hivyo Ukitazama kwa wakristu, ngoma ipo pale pale kuna victims wa ndoa zao ktk mfumo huo huo wa nguvu za mwanamme ktk ndoa na mirathi. Wanaume wengi wakristu wanaoa wake zaidi ya mmoja (kimila) wana watoto nje ya ndoa na inapofikia mirathi wale waotot nje ya ndoa ndio wanaathirika kwa matendo machafu ya baba yao.
Sisi wote waislaam na Wakristu baba zetu na mama zetu ni vibaka...Fedha imekuwa ivutio cha ndoa na uzalishanaji wa watoto nje ya taratibu za kidini hivyo ili kuwakinga wanawake na watoto ambao wamekuwa wakitumiwa ovyo na wanaume ni muhimu sheria itungwe kuhusiana na hilo maadam sisi sote waislaam na Wakristu tumeshindwa kufuata maadili ya dini zetu then serikali ina kila haki ya kuamua ndoa zetu ama mirathi...
Hadi sasa hivi ktk ndoa za kihalali iwe ktk dini ya kikristu ama kiislaam sheria zinazotumika hazina tofauti kabisa na matakwa ya sheria za dini zote mbili ikiwa mke ni mmoja...
bahati mbaya ni kwamba waislaam wameruhusiwa wake wanne lakini taratibu zake hazifuatwi na wakristu pamoja na kuzuiwa kuoa zaidi ya mmoja wanaoa wake zaidi ya huyo mmoja (taratibu hazifuatwi)...kwa hiyo ule uhuru wa ibada hii ya ndoa na mirathi tumeupoteza sisi wenyewe...hakuna jibu isipokuwa kutungwa sheria itakayo watazama na kuwalinda victims wanaoolewa na watoto wanaozaliwa ktk mfumo huu wa kienyeji..hukumu zake haziwezi kuwa za kienyeji isipokuwa kuwapa fungu la haki hawa waathirika ili kesho sisi sote tunapotaka kuoa ni lazima tuzingatie kuwa sheria inawalinda hata wale tuliowadanganya na kuzaa watoto ambao leo hii watu wanadiriki hata kuwaita watoto wa haramu.
 
Mahakama ya Kadhi ni ya kidini. Jumuia ya OIC ni ya kidini. Sasa utavizungumziaje hivi vitu bila kuingiza dini? Swala kama hao waliolileta ni wawakilishi wa waislamu sio sehemu yake hapa. Hatuwezi kusema kuwa hizi ni njama za wanasiasa tu kwa kutumia udini basi tukatae kujadili! Kama wametumia kigezo cha dini basi wakina Mkamap na wengine wana haki kuhoji nafasi yake katika mjadala wote huu. Kama waislamu wanaona hawa hawazungumzii, wajitokeze kuwapinga. Kwa kukaa kwao kimya ndiyo kunawafanya hao walioleta hizi ishu kujiona kuwa wako nyuma yao. Kuziba masikio na macho hakutafanya hili suala lipotee. Tutawezaje kusema kuwa dini haina nafasi katika serikali yetu bila kuzungumzia dini?????? Si wote wanaopinga hoja hizi wanapinga kwa sababu zimetoka kwa waislamu. la hasha, wengine wanapinga kwa sababu zina harufu ya udini. Hata ingekuwa ni Mahakama ya wakristu au serikali kutangaza kuwa ni lazima biblia liwepo kwenye ofisi zote za serikali tungelipinga! Na ndio, inapobidi, tutatumia wino mwekundu!
 
Womenofsubstanc,
Heee! hivi umeelewa alichoandika Sanda matuta!.. ebu soma tena upya kisha tuonyeshe BAKWATA imeingia vipi...

Mkombisi,
Mkuu huwezi kuandika hoja yako bila kuwataja waislaam, mbona uloandika ndio Pumba na sidhani kama unawakilisha Wakristu!..

Ngekewa,
Hayo uliyoyaandika ni kweli tupu lakini binafsi nasema kwa nini hizo sheria za kiislaam ambazo zinahusiana na ndoa na Mirathi zisiwe sheria kwa watu wote nikiwa na maana kwamba hata mkristu au Pagani ambaye ameoa wake zaidi ya mmoja huyu pia anatakiwa sheria..Sheria za urithi za kiislaam ndizo zinatumika sehemu nyingi sana isipokuwa tofauti kubwa ni fungu la mgao wenyewe baina ya mke na watoto. lakini hata ktk sheria za kawaida hawa Wajomba na mashangazi hawana ruksa kudai mirathi kama inavyotokea sana nchini.

Kinachotokea Tanzania Wajomba na Shangazi kingilia mirathi (baada ya kifo cha mzazi hasa BABA) ni jambo la jadi zaidi ya dini ama sheria. Binafsi nachokitazama hapa ni sheria ambayo itatumika ktk korti zetu hizi hizi bila kuanzisha korti za kadhi kwa sababu hata huyo hakimu wa kadhi hana CV ama elimu fulani ambayo inatambulika na kukubalika ktk sheria za dini..Na hakuna mahala popote ktk hadithi inayosema hakimu Mkristu hawezi kutoa maamuzi ya mirathi kwa ajili ya waislaam hata kama atatumia sheria za kiislaam. Kwa hiyo sioni sababu ya kuwa namahakama nyingine kwa waislaam ambo ndoa zao na hata upatikanai wa watoto wao haukufuata misngi ya dini toka mwanzo..Itakuwa tunahumu wa tu kwa kufuata majina yao badala ya kufuata imani zao. Unajua vizuri kuwa kuoa mke wa pili na hata wa wtatu ni vigumu sana kama sheria itafuatwa...Matatizo mengi yanayotukuta yanatokana na ndoa hizi kufungwa kiholela (kiasili) kwa hiyo kwanza simanisheni ibada ya ndoa kabla hamjahukumu mtu.

Mimi nilichokiona hapa na hasa mada nyingi zinazokuja sasa hivi zzinatokana na watu kukosa tumaini na serikali iliyopo ama Kikwete amekuwa kama ndio beki aliyepwaya hivyo kila mipira inapitia upande wake...
Tanzania ya leo maisha yetu sisi ktk miji yetu hasa baada ya kifo cha baba yetu mlezi (UJAMAA) basi kila mahala unapopatazama watu wanadai mirathi ya mali iliyoachwa.. Kwa bahati mbaya aliyeshika mali hizo ni mjomba na Shangazi yetu (CCM) ambaye anazitumia mali hizo kwa kuedesha falimia yake akiwatupia watoto chenji zilizobakia. Hivyo ktk mahesabu yetu kuna wale walioridhika na chenji hizi na wengine kati yetu ndio hao wanaotaka kujikata wapewe chao ieleweke kwamba hawapo tena ktk urithi... Wanachasahau tu ni kwamba tutagawana umaskini hivyo kuzidi kudidimia zaidi ktk umaskini.
Kinachotakiwa ni sisi watoto yaani Watanzania wa kila rangi iwe dini kabila ama jinsia tuwe pamoja na kuweka matakwa yetu pamoja...UMOJA wetu sisi sote ndio pekee unaoweza kuondoa hawa Wajomba ktk mirathi laa sivyo haya yote ni marudio ya mifarakano ambayo ipo ktk familia za Kiafrika hasa sisi Wadanganyika. Siku mzazi anapokufa ndio utaona kila mtoto akijitokeza kudai haki fulani wakati haikuwa haki yake siku zote za nyuma..
Tanzania imekosa dira hatuna tena mwelekeo..

Mkamap,
Duh! mkuu mimi nilidhani umesha zipitia hizo sheria na ndio maana hukubaliani na mahakama ya kadhi kumbe unachotumia hapa ni ushabiki mtupu! Doooooh mkuu wangu noma.. Yaani hadi hapa ume judge kitabu kutokaa na cover lake badala ya kusoma yaliyomo..
Na hii ni hulka ya wengi hasa inapofikia swala la Waislaam.. watu wengi wakisha sikia tu Waislaam basi kitu kinachokuja akilini ni mambo ya Iran na Afghanstan..Wanapinga na watapinga hata kutembelewa na Ahmadinajad ambaye ni rais tu kama marais wengine hatungi wala hana nafasi ktk Uongozi wa dini huko Iran, yet kwa sababu ni muislaam na Marekani wamesha sema ni shetani basi hukumu hiyo inachukuliwa kama ilivyo..Binafsi na imani yangu dhaifu sina hakika nani shetani kati ya huyo na Bush...

Bob Mkandara,

Swadakata kwa maelezo yako ya busara.

Hivi kwanini tusikuundie chama ukagombea Urais kwa niaba yetu?
 
Fundi mchundo,
hata siku moja huwezi kuelewa naandika kitu gani kwa sababu huelewi ulichosema wewe mwenyewe.
Mimi nimemtaja Nyerere kwa sababu ambazo wewe umemtaja AghaKhan na nimekuonyesha mifano mingi ambayo hutaki kuitazama kama mifano ya jinsi unavyokosea kutazama kitu..
Nguvu ya Nyerere kuisimamisha Bakwata ni sawa kabisa na ile ya AghaKhan kama ulivyoandika ama kuamini na ndio nikakupa mfano kuwa unakosea.. Kuwepo kwa Bakwata sio wazo la waislaam ni wazo la serikali yetu hata kama walengwa ni waislaam na imeandikwa ktk maandishi yako mwenyewe ulonukuu na kuyaweka hapa... nakuomba soma tena maandishi yako mwenyewe kuhusiana na Bakwata itaipata picha kamili.
 
Rev. Kishoka,
Mimi mzee wa baraza tu kazi yangu ni kuhakikisha vijana wanaelewa kile wanachozungumzia nje ya darasa maanake wengi hapa wamesoma sana lakini hawakupitia maisha nje ya elimu zao..
Mimi namshukuru Mungu kuwa nimekula chunvi, nimetembea sana na nimekutana na watu wa kila rangi, imani na jinsi.. wenye kila namna ya kufikiria kiasi kwamba wamenijenga sana ktk kuyatazama maswala ya dunia hii.. Kifupi Elimu dunia ipo mkuu, lakini haina maana naweza kuongoza kundi la watu au kijiji acha nchi nzima... ushauri ndio kazi yangu na hakika namshukuru Mungu kwamba nimekwisha yaona matunda mengi sana kwa wale wote waliowahi kunisikiliza na wkafuata...Sina malalamiko.
 
Rev. Kishoka,
Mkuu asikudanganye mtu kuwa nchi kama marekani zinatupa misaada bila masharti... Ni lazima tujiunge na kundi fulani kulipa fadhila zao...Ni sawa na mwamake akwambie ati mzee fulani huwa anamopa hela bila kumwomba mchezo!.. comeon mkuu kuna kitu huyo mzee anataka.
OIC ni politics tupu ktk dini hakuna la maana zaidi ya kuwa sawa na SADC ambao wanadai wao waafrika wa kusini while kumejaa vibaraka na pengine nchi ambazo hazipo kusini..Kwa hiyo wanapotumia OIC kama kweli ingekuwa ni swala la dini basi bila shaka wasingekuwa Kenya ama Uganda ila hawa jamaa wanamtafuta binti yetu kama wanavyomtafuta Wamarekani..
Tatizo la mada hii ni kwamba sisi tunamtazama OIC kama muislaam kaleta posa, mama (waislaam) anamkubali kwa sababu ni muislaam mwenzake lakini baba hataki mume huyu kwa sabau ni muislaam. sasa mama anapouliza dini ya Bush baba anasema Bush hakuja kuomba mke kwa misingi ya dini...Kwa hiyo he is out of question..Mke bado haelewi kwa sababu bado haiondowi ukweli kuwa Bush ni mkristu pamoja na kwamba hakutaja dini yake..
To join OIC haikulazimishi uwe muislaam isipokuwa misaada yake inawafuata wale waliojiunga..hawasimamishi sala tano wala kufanyia mikutano yao misikitini...
Mkuu nenda pale Lions club huwezi kuingia ndani kama wewe sio member lakini kua kwako member wa Lions Club haikufanyi wewe kuwa mhindi ama uzungu fulani kiasi kwamba tofauti hizo ukaziweka kulinganisha na viwanja viwanja vinginevyo ambavyo havihitaji membership... kote wanaitaka fedha zako..Swala la Marekani, pakistan na kwingineko mkuu umekuanzisha wewe mwenyewe kwa sababu umechukulia tu kuwa member OIC ni Uislaam...OIC haiko ktk hata kitabu kimoja cha Uislaam...iweje OIC ni Uislaam. Mkuu hapa canada tuna Jumuiya ya watanzania na kuna Wakenya, Waganda, Wazambia nao wamejiunga nasi sasa sijui wao nitasema vipi hali kuna jina la Umoja wa WaTanzania.
 
Fundi mchundo,
hata siku moja huwezi kuelewa naandika kitu gani kwa sababu huelewi ulichosema wewe mwenyewe.
Mimi nimemtaja Nyerere kwa sababu ambazo wewe umemtaja AghaKhan na nimekuonyesha mifano mingi ambayo hutaki kuitazama kama mifano ya jinsi unavyokosea kutazama kitu..
Nguvu ya Nyerere kuisimamisha Bakwata ni sawa kabisa na ile ya AghaKhan kama ulivyoandika ama kuamini na ndio nikakupa mfano kuwa unakosea.. Kuwepo kwa Bakwata sio wazo la waislaam ni wazo la serikali yetu hata kama walengwa ni waislaam na imeandikwa ktk maandishi yako mwenyewe ulonukuu na kuyaweka hapa... nakuomba soma tena maandishi yako mwenyewe kuhusiana na Bakwata itaipata picha kamili.

Instead the pro-TANU Moslems, with several leading Qadiriyya sheikhs playing important roles, formed with the support of TANU the new national organization Baraza Kuu la Waislam wa Tanzania (Tanzania Muslim Council), BAKWATA, whose constitution was in large parts a copy of the TANU constitution. Because of the close connection to the ruling party and many leading Moslem politicians' interference in BAKWATA's activities, the role of the organization has been controversial.

BAKWATA ilianzishwa na waislamu wapenzi wa TANU, pamoja na baadhi ya waislamu maarufu wa Qadiriyya wakipigwa taf na chama cha TANU. TANU si serikali ingawa ilikuwa wakati wa chama kimoja! Naam, na katiba yake ilifanana fanana na ile ya TANU.
 
Back
Top Bottom