Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

........... Kama kukipata ni lazima serikali yetu ijiunge, so be it. Tukiona kubaya si tutajitoa na kuwaeleza wenzetu kwa nini tumefanya hivi. Viongozi wa kikristu kwa kulishikia bango suala hili ndiyo kunazidisha imani kuwa wakristu hawawatakii mema wenzao. Kichuguu tunakigeuza mlima sisi wenyewe.

Kuna ishu za kusimamia kidete ( Mahakama ya Kadhi ikiwa ni mojawapo) lakini si hili. Tujiunge tu na chombo hiki kwa faida ya wenzetu. Hatutabadilika kuwa nchi ya kiislamu kwa kufanya hivyo.

Amandla.......

Sikiliza Fundi. Kitu ambacho huna uhakika ni sumu au la, hakijaribiwi kwa kukionja! Kinapelekwa maabara kuchunguzwa. Maabara zetu za masuala ya kijamii ni majukwaa kama haya ya JF.

Maswali muhimu ya kujiuliza kabla ya kupendekeza kujiunga kwenye hiyo OIC ni haya: Je sisi watanzania kama taifa tunayaamini na kuyakubali malengo ya OIC kama yalivyoainishwa kwenye OIC charter? Na je tuko tayari kama taifa kushiriki kutekeleza malengo hayo? Hebu isome kwanza hiyo charter, inapatikana kirahisi tu kwenye google.

Mimi binafsi siiamini wala siikubali hiyo OIC charter kwa ujumla wake, na hivyo siko tayari kuwa sehemu ya utekelezaji wake. Na ninaamini kuwa kama hiyo kitu ikiwekwa wazi watanzania wote wakaijua, wako wengi tu watakaokuwa na msimamo kama wangu. Na zaidi ni kwamba malengo ya charter ile kwa nchi kama yetu yenye mchanganyiko wa kiimani, hayawezi kutekelezwa na nchi maana yatakuwa yanapingana na katiba ya nchi ya kutofungamana na dini yoyote.

Lakini ninakubali na ninaheshimu haki ya waislamu kushiriki mambo ambayo wanayaamini, ikiwamo ya kujiunga na jumuiya kama hizo. Ndio maana nasema hiyo OIC itoe nafasi kwa waislamu wa nchi ambazo si za kiislamu kujiunga nao katika nafasi yao ya uislamu na si kupitia kwa serikali. Lakini hii ya kutaka misimamo ya kidini ipewe nguvu za kiserikali (ndilo linalotafutwa kwa kudai serikali ijiunge na OIC) kamwe haliwezi kukubalika katika nchi ya utawala usio wa kidini.
 
Basically OIC ilianzishwa kwasababu ya wapalestina huko Jerusalem kutokana na vurugu zilizoathiri Al Aqsa Mosque...Pamoja na maisha ya wapalestina kwa ujumla...Hivyo basi OIC ni ya kulinda maslahi ya waislam dhidi ya wale wanaosadikika kuwa maadui wa uslam.

Ni muhimu sana tukatofautisha maslahi ya Taifa na ya Dini flani flani.
Narudia tena...Kigezo kilichotumika eti ni kwasababu ya misaada ndio tujiunge si kigezo madhubuti.

Hapo chini ni quote inayoelezea wazi kuwa maslahi ya waislam yalikuwa hatarini na OIC ikaanzishwa ili kuyalinda na hivyo basi ni sawa na kuchaguwa upande kati ya Israel na Palestine.

Hizi issue ni very wide na extremelly sensitive viongozi wetu wajuwe.
Hata kama wapo upande wa wapalestina siyo lazima wajiunge na OIC ili kuwaonyesha waarabu kuwa na sisi tunajali haki za binadamu ambao ni waislam...Hata waafrika na wao wana suffer...Kwanini na sisi tusiungane na tuseme wenye kutaka rasilimali zetu wajiunge na Afrika?

We ought to be carefull here ladies and gentlemen.

The Organization was established upon a decision of the historical summit which took place in Rabat, Kingdom of Morocco on 12th Rajab 1389 Hijra (25 September 1969) as a result of criminal arson of Al-Aqsa Mosque in occupied Jerusalem.
 
Fundi mchundo,

Mkuu swali langu halina maana zaidi ya ukweli wa nchi. Huyo Papa awe ni mfalme au chochote kile unachotaka kukiita nambie nchi hata moja yenye kiongozi wake na baraza la mawaziri ama Utawala ambo sio raia wa nchi hiyo..
Kifupi nachojaribu kusema hapa ni kuwa Vatican ni Taasisi kwanza kabla hujafikiria kupasisha kuwa ni nchi. Nimekupa mfano wa Pengo ambaye ni raia wa Tanzania na pengine yawezekana kabisa kuwshika nafasi juu ya utawala wa Vatican..
Kwa hiyo bado hujanijibu kama Benedict ni raia wa vatican au Germany! msiendelee kuzungusha wakati hoja iko wazi kabisa!

Kithuku,
Sawa mkuu hivi kama mimi leo hii na waislaam wengine tunapinga muundo wa Vatican au sababu zozote ambazo sisi waislaam tunaziona kuwa ni za msingi tunaweza kudai kutohusiana na Vatican kwa sababu nchi yetu sio ya Wakatoliki!...
 
Mkandara
Mchundo kakueleza vizuri.
Kifupi huyu mkuu ni raia wa VATICAN na akifa hapo anazikwa hapohapo ktk nchi yake.Kuzaliwa ujeruma si tija.mimi hapa naweza kuwa Rais wa IRAN je utaandamana eti kwa vile nimezaliwa TZ?

Mbona huyu ROSTAM AZIZI ni raia wa IRAN mbona ni mbunge wa IGUNGA na tena angepiga tikitaka nzuri angekuwa Rais wetu.

Mkuu Mkandara hilo kweli lilikuwa swali la kuuliza eti pope ni Raia wawapi? unafahamu mwanzo nilliignore hilo swali kwa kuasume jibu lake ni obvious.
 
OIC ilianzishwa kwa madhumuni ambayo yako wazi...Na sisi tuna watu ambao ni watumwa wa akili wenye kupenda ushabiki tu bila msingi.
Wengine wanapiga kelele tu kuhusu mabwana zao eti waarabu na wazungu.

Kazi ipo....Kwahiyo viongozi wetu wanataka kutumia vigezo vya umasikini wetu ili kujiunga na OIC...Sasa kwanini hizo nchi ambazo tayari ni wanachama wasiisaidie Tanzania as individual countries kama ni waislam wanawapenda? Masharti ya kujiunga yana ulazima gani?

Ama kama ni maslahi ya waislam si wanajuwa misikiti ilipo? Watowe hiyo misaada cha muhimu iwafikie walengwa...Kusema nchi ijiunge si lazima sana...Nashangazwa sana kuona issue hii inakuwa kubwa...Ni siasa hizi.
 
Jmushi1,
Hizi issue ni very wide na extremelly sensitive viongozi wetu wajuwe.
Hata kama wapo upande wa wapalestina siyo lazima wajiunge na OIC ili kuwaonyesha waarabu kuwa na sisi tunajali haki za binadamu ambao ni waislam...Hata waafrika na wao wana suffer...Kwanini na sisi tusiungane na tuseme wenye kutaka rasilimali zetu wajiunge na Afrika?
Ndio taabui ya ku copy na ku paste bila kuelewa.. sasa nambie wewe OAU ilianzishwa kwa sababu gani na kuna ubaya gani kuwepo kwa OAU kwa nchi ambazo sio za Kiafrika!..
Mkuu, mkutano huo uliitishwa kuzungumzia swala la arson la msikiti lakini haikuwa agenda ya mkutano huo kuunda chombo kinachohusika na arson hiyo..
Yaani hamna hata pa kuegamia mnadandia kila kitu kuonyesha mapungufu wakati roho zenu zimejaa Udini.

OIC imeanzishwa
 
Mkamap,
Uraia wa Vatican kaupata lini?...nionyeshe mahala au katiba ya Vatican inayosema Benedict ni raia wa Vatican, Je Pengo akiukwaa UPope atautema uraia wa Tanzania?..
Rostam Aziz ni raia wa Iran... heee! ama kweli nazungumza na watu wasiojua maana!
 
Acha vijembe vya kizembe mkuu usiende huko na sitaki kwenda huko.
Unataka Tanzania ipiganie maslahi ya Waislam kwasababu ya misaada?
 
Jmushi1,
Kama unaweza kwenda huko nenda... lakini nachojua hukuelewa kile ulichoandika. Ndio ukweli.
 
Mkamap,
Uraia wa Vatican kaupata lini?...nionyeshe mahala au katiba ya Vatican inayosema Benedict ni raia wa Vatican, Je Pengo akiukwaa UPope atautema uraia wa Tanzania?..
Rostam Aziz ni raia wa Iran... heee! ama kweli nazungumza na watu wasiojua maana!

Mkuu
Tatizo sijui ni nini?
Ile ni nchi lazima iwe hivyo Pengo akiwa pope hatorudi tena TZ labda kutembelea ndugu jamaa ama kikazi.Yeye maisha yake ni huko huko hadi kaburi lake.

Ili mtu mgumu kuukubali ukweli ni lazima umpe picha ya mazingira.

wewe chukuwa passport yako nenda VATICAN bila VIZA.Si taasisi kama OIC nayo nikitaka kuitembelea inatoa VIZA sio? ama hapo iko je?
 
Jmushi1,
Kama unaweza kwenda huko nenda... lakini nachojua hukuelewa kile ulichoandika. Ndio ukweli.

Wewe unaleta propaganda zako na unataka tukubaliane tu kwasababu na wewe ni Msilam?
Hapa ni kuhusu Maslahi ya Taifa vs yenu mujahidina.
Umeshindwa kujibu swali langu la msingi kuwa kama ni right kutetea maslahi ya uislam simply kwasababu ya misaada ya waarabu...Nyie mnalipeleka wapi Taifa letu nyie?
Hiyo wewe uliyodai kuwa ni Arson kwenye Al Aqsa...Hukuona kuwa kwa wakati huo ilikuwa ni occupied land tayari?
Mambo ya OAU yanahusiana nini na issue hii?
 
Mkamap,

Mkuu hata hujanipata kabisa... nadhani huelewi jinsi navyojenga hoja zangu..
Sijapinga kuwa Vatican ni nchi isipokuwa ina matatizo ambayo mimi binafsi hayanihusu kama Muislaam na hainipunguzii kitu kuhusiana nayo kama nchi ama Taasisi.. Lakini naweza kuyajengea hoja ikaonekana haifai kuhusiana nayo..
Kitu muhimu hapa nachojaribu kuwaambia ni kwamba kuna mambo mengi ambayo yanahitaji kuvumiliana na kukubali kuwa nchi hii si ya mtu mmoja ni yetu sote...
Kubali kuwa Papa ni rais, raia wa Gemany na baraza lake lote ni raia wa nchi tofauti wakati inapewa hadhi ya kuwa nchi kutokana na Taasisi iliyojengwa na wao wenyewe. hakuna mkono wa mtu kukataza kwani ni haki yao kimsingi.
 
Sikiliza Fundi. Kitu ambacho huna uhakika ni sumu au la, hakijaribiwi kwa kukionja! Kinapelekwa maabara kuchunguzwa. Maabara zetu za masuala ya kijamii ni majukwaa kama haya ya JF.

Maswali muhimu ya kujiuliza kabla ya kupendekeza kujiunga kwenye hiyo OIC ni haya: Je sisi watanzania kama taifa tunayaamini na kuyakubali malengo ya OIC kama yalivyoainishwa kwenye OIC charter? Na je tuko tayari kama taifa kushiriki kutekeleza malengo hayo? Hebu isome kwanza hiyo charter, inapatikana kirahisi tu kwenye google.

Mimi binafsi siiamini wala siikubali hiyo OIC charter kwa ujumla wake, na hivyo siko tayari kuwa sehemu ya utekelezaji wake. Na ninaamini kuwa kama hiyo kitu ikiwekwa wazi watanzania wote wakaijua, wako wengi tu watakaokuwa na msimamo kama wangu. Na zaidi ni kwamba malengo ya charter ile kwa nchi kama yetu yenye mchanganyiko wa kiimani, hayawezi kutekelezwa na nchi maana yatakuwa yanapingana na katiba ya nchi ya kutofungamana na dini yoyote.

Lakini ninakubali na ninaheshimu haki ya waislamu kushiriki mambo ambayo wanayaamini, ikiwamo ya kujiunga na jumuiya kama hizo. Ndio maana nasema hiyo OIC itoe nafasi kwa waislamu wa nchi ambazo si za kiislamu kujiunga nao katika nafasi yao ya uislamu na si kupitia kwa serikali. Lakini hii ya kutaka misimamo ya kidini ipewe nguvu za kiserikali (ndilo linalotafutwa kwa kudai serikali ijiunge na OIC) kamwe haliwezi kukubalika katika nchi ya utawala usio wa kidini.

Umeongea ukweli Kithuku,

Watu wengi inawezekana tunajadili hapa lakini hata hiyo charter ya OIC hatujaipitia kujua kilichomo ndani yake. Ili mjadala uwe na tija ni vizuri kila mtu akaipitia isije ikaonekana watu wengine wanapinga kwa nongwa while they have actual facts in hand na wele wanaosema tujiunge tu hawana any facts.

Kuna mchangiaji mmoja nadhani alizungumzia kuhusu suala la Uganda kutaka kujitoa OIC na waislam wa Uganda kupinga......lakini cha kujiuliza ni kwa nini watake kujitoa kama kuna manufaa? It is better to know.
 
Jmushi1. Maslahi ya Taifa unayajua wewe ama unazungumza ili mradi kufurahisha baraza..
 
Deny_all,
haya ndio maneno mkuu wangu na kwa kuongezea tu mimi binafsi sikubaliani na matakwa ya hopja za mahakama ya kadhi wakati ni Muislaam...
Wakati huo huo hoja hiyo kwenda bungeni sio kosa kabisa kwani Waislaam ni kati yetu sote na litazamwe swala kwa manufaa ya waislaam (WATU) ktk mazingira wanayoishi na sio kuweka vizingiti dhidi yao. Mahakama ya kadhi sio solution ya matatizo ya Waislaam na naweza kutoa sababu za wazi ambazo zinawahusu walengwa.
Kwa hapo nakubaliana sana na Kithuku kuwa swala hapa ni OIC yenyewe kuitazama kama ina manufaa kwa Waislaam wa Tanzania ktk mazingira wanayoishi..
 
Jmushi1. Maslahi ya Taifa unayajua wewe ama unazungumza ili mradi kufurahisha baraza..

Mkandara una tatizo moja sugu..Ni lazima uelewe kuwa si kila wakati hoja yako itakubaliwa.
Sometimes hata kama huelewi msingi wa hoja bado utaendelea kubishana tu.
Usichaguwe cha kujibu simply kwasababu unataka hoja yako ishinde..Rather ni bora ujibu hoja kwa hoja kwani thats the only way we learn.
Nimeshakuuliza bado hutaki kujibu...Wewe unataka Taifa lipiganie maslahi ya uislam kwasababu ya misaada ya waarabu?
 
Gambia News : Gambian President urges OIC members to do more in fighting poverty
Mar 17,2008 by

Dakar, Senegal - Gambian President Yahya Jammeh Friday challenged rich member states of the Organisation of Islamic Conference (OIC) to do more in fighting poverty in the least developed Islamic countries, national broadcaster, Gambia Radio and Television Services (GRTS) reported.

Jammeh was speaking at Banjul International Airport, on his return from Dakar, t he capital of Senegal, where he attended the just-concluded OIC Summit.

The Gambian leader urged the rich Islamic nations to help their economically-wea k and poor sister countries, based on the spirit and teachings of the Islamic faith which, according to him, encouraged the culture of sharing and caring for each other.

He said the richer nations should channel financial assistance through Islamic Development Bank from which poorer states could turn to for soft-term loans.

"We are not asking for charity, but financial help by way of loans based on provisions of 'Sharia' (or Islamic law)," he reiterated.

President Jammeh also hailed the 'Kuwaiti Fund' for carrying out numerous development projects in poor countries, and urged other rich member states to emulate K uwait.

The Gambian leader was welcomed home by his Vice-President, Isatou Njie-Saidy, cabinet ministers, security chiefs and senior government officials.

source: Gambia News : Gambian President urges OIC members to do more in fighting poverty

*************************************************************
Kumbe wengine waliomo tayari siku nyingi wanalalamika na kuomba kuangaliwa kuhusu misaada au mikopo sasa sisi tutakaojiunga karibuni itakuwaje?

Hoja ya kwamba tunajiunga OIC ili tupate misaada inazidi kuwa dhaifu.
 
Kithuku,
Sawa mkuu hivi kama mimi leo hii na waislaam wengine tunapinga muundo wa Vatican au sababu zozote ambazo sisi waislaam tunaziona kuwa ni za msingi tunaweza kudai kutohusiana na Vatican kwa sababu nchi yetu sio ya Wakatoliki!...

Kuweka suala hili vizuri, kumbuka tu kwamba Tanzania si mwanachama wa Vatican bali tu ni kwamba Vatican ina balozi wake nchini. Na kama OIC ikiwa na status ya nchi na ikataka kuweka balozi wake Tanzania, sitapinga hata kidogo na ninaamini hata wenzangu wanaopinga Tanzania kujiunga na OIC hawatapinga OIC kuwa na mwakilishi mkazi Tanzania.

Na haya maneno nitayarudia mara nyingi sana pengine nitaeleweka. Nasema ni haki kabisa kwa waislamu kujiunga na taasisi yoyote ya kiislamu wanayoitaka. Lakini si haki hata kidogo kwa sisi tusio waislamu kulazimishwa kuwa wanachama wa taasisi ya kiislamu kama OIC. Hiyo taasisi inapaswa kuweka utaratibu wa kuwawezesha waislamu walioko katika nchi zisizo za kiislamu kujiunga nao bila kuleta mtafaruku kama huu tunaoletewa hapa.
 
Quote: OIC

The Organization has consultative and cooperative relations with the UN and other inter-governmental organizations to protect the vital interests of the Muslims and to work for the settlement of conflicts and disputes involving Member States.
 
Gambia News : Gambian President urges OIC members to do more in fighting poverty
Mar 17,2008 by

Dakar, Senegal - Gambian President Yahya Jammeh Friday challenged rich member states of the Organisation of Islamic Conference (OIC) to do more in fighting poverty in the least developed Islamic countries, national broadcaster, Gambia Radio and Television Services (GRTS) reported.

Jammeh was speaking at Banjul International Airport, on his return from Dakar, t he capital of Senegal, where he attended the just-concluded OIC Summit.

The Gambian leader urged the rich Islamic nations to help their economically-wea k and poor sister countries, based on the spirit and teachings of the Islamic faith which, according to him, encouraged the culture of sharing and caring for each other.

He said the richer nations should channel financial assistance through Islamic Development Bank from which poorer states could turn to for soft-term loans.

"We are not asking for charity, but financial help by way of loans based on provisions of 'Sharia' (or Islamic law)," he reiterated.

President Jammeh also hailed the 'Kuwaiti Fund' for carrying out numerous development projects in poor countries, and urged other rich member states to emulate K uwait.

The Gambian leader was welcomed home by his Vice-President, Isatou Njie-Saidy, cabinet ministers, security chiefs and senior government officials.

source: Gambia News : Gambian President urges OIC members to do more in fighting poverty

Yaaani kumbe na huko OIC kwenyewe sio paradise kama tunavyoambiwa na Membe?
 
Back
Top Bottom