Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Sitashangaa kusikia jamaa anajisifia kuwa juhudi zake zimemfanya Papa aahidi kuja Tanzania, 'kutoa misaada'.
Mwanakiji, Nchimbi alisema kuwa raisi hawezi kukaa ikulu 'kulinda njiwa', kwa hiyo lazima atasafiri kama mara mbili tatu kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Ningependa sana kama angezuru Mkoani Mbeya pia, atoe ufafanuzi wa mbolea ya ruzuku, maana wakulima hawaelewi kabisa somo la mawaziri na wakuu wa wilaya.

Ee bwana katika 'mistari iliyotulia' mwaka huu nadhani na huu ni mmoja wapo, mininge nadhani ni kama vile:

"Hakuna haja ya wananchi kujua gharama itakayotumika kwa ajili ya mawaziri…ziara hii ya siku saba ni sehemu ya kazi…mbona wananchi hawahoji wapinzani wanapozunguka nchi nzima wakiwa na helikopita?" -Dk Batilda Buriani, quoted in Tanzania Daima (21.10.2007)

"Hawa wapinzani walioungana ni sawa na paka waliofungwa mikia yao pamoja na nawaambia hawa hawajaungana, ukiwapelekea panya mbele yao kila mmoja atataka amkamate, wangojeni mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu utaona watakavyoachana"(Ibid.)

Kweli siasa imekwua si hasa mwaka huu..huenda tukasikia mengine zaidi...

Na yale ya Ditto Tabora kuna anayekumbuka?
 
Hivi kuna Rais mwingine hapa duniani anayeweza kuwa nje ya nchi yake for 3 weeks or so? Najiuliza pia huko anapoenda atakuwa anawapa shida sana, kwa mfano alipokuwa US, waliwezaje kum-keep busy for 3 weeks? Ku-host ugeni wa Rais for 3 weeks sio mchezo jamani, yaani in 3 weeks katika nchi moja alikuwa anafanya nini hasa? Kuna mwenye Ratiba kwa mfano alipokuwa US?

Nauliza tena hivi kuna Rais mwingine duniani hii anayeweza kuwa nje ya nchi yake for 3 weeks kwa ziara ya kikazi? Nisaidieni wanadiplomasia!
 
Duh! Hivi kumbe alikuwa nje ya nchi kwa muda wote huu? Ebwana eeh huyu kweli joker!!
 
Hivi kuna Rais mwingine hapa duniani anayeweza kuwa nje ya nchi yake for 3 weeks or so? Najiuliza pia huko anapoenda atakuwa anawapa shida sana, kwa mfano alipokuwa US, waliwezaje kum-keep busy for 3 weeks? Ku-host ugeni wa Rais for 3 weeks sio mchezo jamani, yaani in 3 weeks katika nchi moja alikuwa anafanya nini hasa? Kuna mwenye Ratiba kwa mfano alipokuwa US?

Nauliza tena hivi kuna Rais mwingine duniani hii anayeweza kuwa nje ya nchi yake for 3 weeks kwa ziara ya kikazi? Nisaidieni wanadiplomasia!

Ndo maana huwa anapata muda wa kuangalia na mpira live, si nasikia wakati akiwa UK alipata 'muda' wa kuhuduria mechi mojawapo?
 
Hivi ktk hili la kumtembelea Papa hatuoni kuna jambo jema la kukubaliwa kwa mwaliko wa kutembelea Tanzania, basi hatuwezi hata kumpongeza kwa hilo?

Nakubaliana na Kada kwa mwendo huu hata haoi waliokuwa wanaichukulia JF kama serious forum wanaona kumbe ni genge la walalamishi fulani...

Njia iliyo nzuri zaidi ni pamoja na wewe na wengine wote walio na hoja zinazotetea upande unaolalamikiwa na wao watuwekee uchanganuzi huo, kuliko kuendelea kuilaumu JF kana kwamba ndiyo inayowatuma waikosoe CCM na serikali yake.

Kama kutembelewa na papa ni jambo la tija, lijengee hoja na tutakusoma na kukupongeza.
 
Njia iliyo nzuri zaidi ni pamoja na wewe na wengine wote walio na hoja zinazotetea upande unaolalamikiwa na wao watuwekee uchanganuzi huo, kuliko kuendelea kuilaumu JF kana kwamba ndiyo inayowatuma waikosoe CCM na serikali yake.

Kama kutembelewa na papa ni jambo la tija, lijengee hoja na tutakusoma na kukupongeza.

Hili nalo nahitaji kujengewa hoja ili kuonyesha kuwa lina tija? Talk abt IQ, now understand why Watson said that...
 
Kwa kweli kwa swala la Jk kumwona Papa hilo halina matatizo kwa sababu alikuwa Italy tayari lakini alipita huko huko alipokwenda kuwatembelea Real Madrid.

Rais katika hotuba zake alisema safari za nje zingekwisha tangu mwezi wa sita, sasa tupo mwezi wa kumi na safari inaonekana ndiyo zimeanza, je anaweza kufuta ile kauli aliyokuwa ameitoa mwanzo?

Mimi naomba Robert Mugabe ashindwe au azuiwe kwenda kwenye mkutano wa EU na Africa ili JK afanye kazi zilizolimbikizana nyumbani, kwa mwendo huu atakuwa kwenye Guiness Book of records kwa kuwa rais wa kwanza kufanya kazi za urais, uwaziri wa mambo ya nje na Ubalozi kwa wakati moja na kufuja pesa za walipa kodi bila huruma.
 
Hivi ni lini mmesikia kuwa Papa kakataa mwaliko wa kwenda nchi yoyote? Vyombo vya habari vimepotosha kusema "Papa kuzuru Tanzania"... !!
 
Mahakama ya Kadhi Constructional Amendment in Sukumaland

Let us have freedom of worship. Let people be allowed to set up structures which enable them to manage their worship effectively and within the law of the country.

Let us not set up micro governments to govern peoples of a certain worship group according to laws based on their religious beliefs. If we do we will have a very complex federal government whose ideal structure would be that every definable society should have their own geographic area which can be governed according to laws and rules based on their faith.

Let's take a sample, Sukumas. This consists of two principal groups. Un adulterated Sukumas, that is those who are pure Sukumas, no education, no new religion such as Islam, Christianity, Buddhism, etc. Of course they believe in god that is why they called him "Mulungu". They believe in witchcraftry, which the Christians also do, but they differ in how to deal with it. The un adulterated Sukumas believe in instant justice; killing the red eyed old women witches. The adulterated Sukumas who are Sukumas converted to Christianity have a way of dealing with witch-craftry, they call it spiritual warfare, they have spiritual weapons which can deal with any power of witchcraftry. They use the name of Jesus and they send the evil spirit running ultra Olympic style. In Christian terminology they have authority over all evil powers and nothing is supposed to harm them.

For each of these two principal groups to live peacefully each administering their laws, rules and regulations according to their faiths, Sukumaland would have to be divided into two areas one for Sukumapure, and Sukumachrist.

But hardly each group would have moved into their area would they realise a problem; in these two areas there would be, alas, though not so many, some Moslems and some Buddhists. So some areas would have to be created for these and any other similar groups to be settled into.

But there would be further complications. Firstly the Sukumapure would realise that they themselves have different denominations also; the bagika, bagalu, bazwilili, bachweji, etc. Each would have to live in their own sub district to be able to administer their laws effectively.

Suckumachrist would face a similar problem. Groupings would differ in doctrine and they would like not only to worship differently but also govern themselves accordingly.

So there would be the SDA area where meat of animals whose hooves are not split and fish without scales would not touch the markets. Also cars, cookers, fridges, air conditioners, trains, aircrafts, heart pacemakers etc would be programmed not work on Sabbath (known as Saturday in Tanzania). All hospitals would be closed because healing is not supposed to be done on Sabbath.

Then in Sukumachrist you would have the Protestants. Many of them are not supposed to drink, smoke, use snuff, etc. Priests have to be married as a rule.

The job of creating the districts and tarafas and katas and vijijis is really complicated in this new constitution. In Protestantsshire you would have the mainliners, i.e. the Moravians, Anglicans, Methodists, Lutherans. Actually although these could co exist in an area called CCT it would be better that each would be in their own sub district .

Then you would have the Charismatics, groupings in this areas have very subtle differences, amazingly these may not need only distinct areas; each area may have to be fenced.

Time up to describe Protestansshire. Then there would also be the Catholicshire. This is an area where priests are not allowed to marry but can mingle with women at will. Liquor can be absorbed in any quantities provide it does not show. Please confirm the following with the nearest Paroko otherwise treat it as hear say: if you are rich and are not living right to the mark and die and get consigned to pulgatory, some district in hell, your relatives can incur the cost of a mass in which you can be prayed out of hell. In Charismaticshire you would qualify persona non grataship if you were caught praying for salvation of the dead.

Tired of Sukumapure and Sukumachrist? Sample the Sukumaslamic. Here you would find quite some diversity of laws. Start with the really marketable ones. You can marry a reasonable number of wives. Difficult part about this is you would be required to treat them impartially. Consolation though is that partiality is not punishable here on earth. Something also pleasant in the marriage set of laws is that you can divorce any time provided you have pen and paper at your disposal.

Now the more serious laws of the Sukumaslamic. An eye for an eye, a tooth for a tooth. Difficult to imagine the sub section of the law which prescribes appropriate punishment for the lady who tempers with a man's generator; Kadhi wouldn't be the job for me.

If you consulted chronicles or Hon retired president Mwinyi on Moslems in Bukoba, I suspect he would strongly advise that even Sukumaslamic should be divided into at least two sub areas.

A very interesting subject under the sun is marketing. I have evidence it is like electricity, it can be switched on and off. You cannot understand until you visit the tiny districts of Buddhashire and Hindushire in restructured Sukumaland. The people here are serious business men. They can market anything and they can enter into any business and succeed. If the restructured Sukumaland will allow intershire trade Buddhashire and Hindushire will be manufacturing and supplying most of these areas. But I doubt if the laws will permit. Even high marketing skills may not succeed under this regime. This will not be the first time though when marketing skills could not be exploited in existing Sukumaland by these groups. They have been so poor at marketing their religion to anybody to the extent that people have come to believe that in this sector marketing has been banned or switched off like electricity.

Because other people are not evangelised into these sects and therefore cannot report openly proceedings of these societies, people have come up with all sorts of unbelievable stories which one can only print to demonstrate how unbelievable they are. You cannot believe this can you? That a girl from these communities gets deported from under the sun should she conceive foreignly. I am not a lawyer by the way, but the approximate absolute absence of mixed marriages with these sects in current Sukumaland is not legal evidence of anything, I should caution!

By the way, if you are close to President Karume, I advise you chat with him. One of his regrets may be that his Oldman was made to leave too early, otherwise President Karume may perhaps by now have in his family a mixed marriage.

Under these circumstances if Sukumaland will remain a unit it will have to have an overall federal government so that all these districts are governed together as a unit.

Of course there may be a grouping which will be happy to adopt federal laws only. Such a group will have also to be allocated a district too.

This is far from the whole treatise on the issue, but considering it is the small hours of the morning and I need to turn in I should stop by observing as follows:

In the olden times there was the Sukumaland Federation which consisted of nine chiefdoms. Its seat was initially at Usagara some 18 km from Mwanza on the way to Shinyanga. Later this was shifted to Malya. I believe the current District Council there is housed in the old federation premises. It was headed by a Paramount Chief, the last Paramount Chief being Majebele. This Federation was not without problems. Will federating the above areas under the restructured Sukumaland pursuant to Mahakama ya Kadhi Constructional Amendment which will give equal rights to every society to govern themselves according to laws based on their religious beliefs be easy?
 
serikali itachagua kadhi wake wa BAKWATA na wale waislam pori watawafuata hao BAKWATA

Hapo ndipo utakapowapenda wakristo maana huoni ujinga huu wa kuingiliwa na serikali
 
MKJJ, Good question!

Kama nimekuelewa, ikiwa rais wa Zanzibar ni, kwa mfano, "Adam Mwakanjuki" au "Isaac Sepetu", je anaweza "kumteua" Kadhi Mkuu wa Zanzibar?


Je, Katiba ya Zanzibar inasema chochote kuhusu uwepo wa Kadhi Mkuu? Ofisi yake (Kadhi Mkuu) inaendeshwa kwa pesa za SMZ?

hili mbona suali jepesi unajua kuwa kadhi naidara ya wakfu na mahakama yakadhi kule zanzibar iko kwenye wizara ya sheria na utawala bora, ambayo aliiongoza mwakanjuki kabla ya kupelekwa mawasiliano na uchukuzi.

na yeye akawa bosi wa chombo hicho na kuhusika na teuzi zake.

kwani rais akiteuwa si huteuwa kwa mujibu wa sheria ziliopo auvp?

hilo sio tatizo mwamba
 
Kwa sasa hili suala limewakalia kooni watawala wao waliona kitu rahisi kuahidi jambo ambalo walijua ni kinyume na katiba ya nchi ili kuwarubuni waislam.Sasa wanafikiria wachomoe vipi na si kutekeleza hilo kutokana na unyeti wake.Vinginevyo labda wabadili katiba iliyopo jambo ambalo sijui kama litapokelewa vema na watu wa dini zingine.
 
Hoja za Makakama ya Kadhi ni Dhaifu
(Makala ya Gazeti la Kulikoni)

Mchungaji/Mwanasiasa Christopher Mtikila amefungua kesi mahakamani kupinga rasmi uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini kwa madai kuwa ni kinyume na Katiba. Mjadala huu siyo mgeni na umekuwepo katika jamii yetu kwa muda mrefu na bila ya shaka ni lazima ufikie wakati ambapo unamalizwa kwa kuanzisha mahakama hiyo kama ndugu zetu Waislamu wanavyotaka au kutoanzishwa mahakama hiyo kama baadhi ya watu wengine wanavyotaka (wawe Wakristu au vinginevyo). Kama Taifa, lazima tujifunze kuanzisha mijadala na kuihitimisha ili tuendelee na mambo mengine. Ni kutotumia muda vizuri kama tutakuwa tunaendelea kuzungumzia jambo lile lile miaka nenda, miaka rudi badala ya kuamua kuzungumza jambo na kulimaliza, hasa linaloweza kumalizika kiungwana, kitaalam, na kidugu kama suala la Kadhi.

Binafsi naamini kuwa hoja ambazo zinatolewa hadi hivi sasa kuhusu haja, ulazima, na haraka ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo Tanzania bara ni hoja dhaifu ambazo bado hazina nguvu. Ni mpaka pale watetezi wa uanzishwaji upya wa mahakama ya Kadhi watakapojenga hoja zenye nguvu, ambazo zinaweza kusimama siyo katika kuvutia hisia za watu, bali katika kushawishi akili zao na kuona kuwa ni hoja za msingi na zisizopingika kirahisi, basi kuanzishwa kwa mahakama hiyo nchini kutaendelea kuchelewa na kwa hakika kunapaswa kuchelewa.

Kabla ya kuziangalia hoja hizi na kuonesha udhaifu wake, naomba kwanza niseme mambo machache ambayo ni muhimu kuyazingatia katika mjadala huu. Kwanza kabisa, kesi iliyofunguliwa na Mch. Mtikila kuhusu kupinga uanzishwaji wa mahakama hiyo ni suala la kwake kama raia wa nchi hii. Isichukuliwe hata kidogo kuwa Mtikila anawakilishwa Wakristu wa Tanzania katika kesi hii. Hivyo basi kauli zake zenye kuumiza hisia za Waislamu zichukuliwe kama ni kauli zake na zisichukuliwe kama ni maneno ya Wakristu dhidi ya ndugu zao waislamu. Na kama ilivyokawaida ya viongozi wetu wa Kikristu hakuna aliyetokea hadharani na kupinga kauli za Mtikila kuwa haziwakilishi mawazo au misimamo ya makanisa nchini. Ingekuwa jambo la kupendeza kusikia TEC, CCT, na Muungano wa Makanisa mengine kutoa kauli zao kupinga madai ya Mtikila kuwa kuanzishwa mahakama ya kadhi kutachochea Ugaidi na kuleta vurugu.

Jambo la pili ni kuwa, binafsi sina tatizo na uanzishwaji wa mahakama ya Kadhi Tanzania bara, na sina sababu ya kuwa na hofu ya kuwepo kwake.

Jambo la tatu hapa ni kuwa, utakapofika mwisho wa mjadala huu ni lazima tubakie na heshima na hisia yetu ya Utanzania. Itakuwa jambo baya na la hatari kama tutafikia mwisho wa mjadala huu na kujikuta ni “watanzania wapenda Kadhi” na “Watanzania wapinga Kadhi”. Tofauti ya maoni na mitazamo ni kiini cha utawala wa demokrasia kwani kwa kutofautiana ndipo tunapata nafasi ya kupata mawazo mazuri na yenye nguvu zaidi. Kwa sababu hiyo basi, kusiwe na Mtanzania yeyote yule mwenye hofu ya mjadala huu. Wale Mashehe waliozungumza kwenye kipindi cha “Jenerali on Monday” wasitupe sababu ya kuwa na hisia ya vurugu au uvunjifu wa amani. Katika maneno yao ya mwisho siku ile, ndugu zetu hawa “waliwasihi” Waislamu nchini kuwa “wawe watulivu na kutoleta vurugu”. Ni nani kawaambia kuwa Waislamu ni watu wa shari au wanataka kuleta vurugu kwa sababu tu Mtikila kafungua kesi Mahakamani? Ni lazima wao viongozi wa dini waoneshe imani kwa Waislamu wenzao kuwa wanafahamu umuhimu wa utulivu na amani, na wao si chanzo cha uvunjifu wa amani kisa tu ya mjadala wa Kadhi. Na katika hili, ningependa kuona viongozi wengine wa Kiislamu wakiwaweka sawa hawa wenzao ambao waliashiria kuwa Waislamu si watu wa amani na utulivu. Kama vile maaskofu walivyokaa kimya kuhusu Mtikila, vivyo hivyo Maimamu na Mashehe wengine nao wamekaa kimya katika hili.


Baada ya kusema hayo turudi kwenye kichwa cha habari cha hoja ya leo kuwa hoja zinatolewa ili Mahakama ya Kadhi irudishwe Tanzania Bara ni hoja dhaifu. Naomba nieleweke sisemi kuwa hoja hizi ni za kupuuzia (kama watu wengine wafanyavyo wasipoweza kujibu hoja), bali ni hoja zenye kujibiwa. Udhaifu wake unatokana na ukweli kuwa zikiangaliwa moja baada ya nyingine tena kwa karibu zaidi bila hata ya kutumia darubini utaona kuwa zimepotoka ndani kwa ndani (inherently flawed). Kwa muda mrefu sasa nimesubiri kuona kama kuna mtu ambaye atathubutu kuzijibu hoja hizi na kuzionesha kuwa hazifai. Mtu huyo hajatokea na badala yake yupo mtu aliyekimbilia mahakamani. Hetu tuziangalie hizi hoja ambazo hutajwa sana kuwa kwanini Mahakama ya Kadhi ianzishwe tena kwa sheria ya Bunge na uwepo wake uunganishwe katika utaratibu wa mahakama za Tanzania. Kwa maneno mengine, kwanini Waislamu wanataka serikali ianzishe mahakama ya Kadhi Tanzania Bara.

Hoja ya 1: Mahakama ya Kadhi imeahidiwa na serikali ya CCM, hivyo Chama cha Mapinduzi kitimize ahadi yake ama sivyo watakiona 2010.

Nimepata nafasi ya kuangalia Ilani ya Uchaguzi ya CCM, na kuhusu suala la kadhi ahadi waliyoitoa inasema hivi “CCM itazitaka Serikali ziendelee na hatua zilizoanza kuchukuliwa ili kuiboresha Sekta ya Sheria kusudi nayo itoe huduma bora zaidi kwa jamii. Yatakayosisitizwa katika kipindi hiki ni pamoja na yafuatayo…. Kulipatia ufumbuzi suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara”

Hivyo utaona kuwa CCM haijatoa ahadi ya kuanzisha mahakama ya Kadhi Tanzania bara, bali “kulipatia ufumbuzi suala la kuanzishwa” kwa mahakama hiyo. Hii ina maana ya kuwa CCM inaweza kabisa kushiriki kwa namna fulani (kwa sera au utunzi wa sheria) kuhakikisha kuwa mahakama ya kadhi inapokuwepo Tanzania bara. Hilo bila ya shaka limechukuliwa kumaanisha kuwa CCM itarudisha Mahakama ya Kadhi kwa kuitungia sheria ya kuianzisha, kuitengea bajeti, na kuiendesha mahakama hiyo. Hii si tafsiri sawa sawa au ya pekee (inawezekana kuwa ni tafsiri mojawapo ya ahadi hiyo) kama nitakavyoonesha baadaye.

Hata hivyo mtu anaweza kusema ahadi hiyo ina maana ya kurudisha mahakama ya kadhi na mimi nimeielewa vibaya. Katika hotuba yake ya bajeti ya mwaka 2005/2006 aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. H. Bakari Mwapachu alisema hivi kuhusu sehemu hiyo ya Ilani, “aidha, (kuhusu) suala kadhi, litafanyikwa kazi”. Na hata katika bajeti ya wizara hiyo chini ya Waziri Mpya Bi. Mary Nagu na yeye hakutoa ahadi mpya ila iliyokuwemo kwenye ilani ya CCM kuwa katika mwaka huu Wizara yake kwa kutumia Tume ya Kurekebisha Sheria itapitia mambo mengi miongoni mwake ni “kulipatia ufumbuzi suala la Uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, Tanzania Bara”.

Kwa kifupi, serikali ya CCM haikuwaahidi waislamu kuanzisha Mahakama ya Kadhi. Ilichoahidi ni kutafuta ufumbuzi jinsi gani inaweza kuanzishwa pasipo kupingana na sheria au kutengeneza sheria itakayowezesha kuanzishwa kwake. Kilichofanyika ni sawa na mtu kuahidi kuwa kwa vile una matatizo ya mahali pa kuishi basi “atafanya kila jitihada kukutafuta ufumbuzi wa tatizo lako la makazi ili na wewe uweze kujisitiri na famili yako”. Itakuwa ni jambo la kuchekesha kama mtu atatoka na kuanza kudai nyumba kutoka kwa aliyetoa ahadi!!

Sasa haina maana kuwa serikali haitarudisha mahakama ya kadhi bali ina maana katika kutafuta ufumbuzi wa suala la kadhi, kurudisha kwa kutunga sheria inayounda Mahakama ya Kadhi kama zilivyo sheria za Mahakama ya Biashara kwa mfano, ni mojawapo tu ya vitu vinavyowezekana, na kwa hakika siyo jambo pekee.

Hivyo ili hoja hii iwe na nguvu kidogo, ndugu zetu Waislamu wawabane CCM na kuwauliza walichowaahidi hasa ni nini? Je wameahidiwa Kurudishwa kwa Mahakama ya Kadhi au kutafutiwa ufumbuzi wa kurudishwa kwa mahakama hiyo? Baadhi ya Wabunge wa CCM wameoneshwa kukerwa na utata huu wa makusudi na wamehoji iweje ahadi ya kushughulikia suala la kadhi inachukua zaidi ya miaka kumi sasa?

Hoja ya 2. Mahakama ya Kadhi ilikuwepo wakati wa Ukoloni, hivyo kama ilikuwepo wakati wa Ukoloni kwanini isiwepo sasa?

Hoja hii ina nguvu kidogo lakini msingi wake unamashaka. Jambo kufanywa na wakoloni au kuruhusiwa na wakoloni hakulifanyi jambo hilo kuwa jambo sahihi au ambalo tuliendeleze jinsi ile ile. Wakoloni katika nchi mbalimbali walifanya mambo mbalimbali kwa malengo tofauti tofauti. Kuna mambo ambayo wakoloni waliyafanya au taasisi walizozianzisha ambazo sisi kama nchi huru tuliamua kuachana nazo.

Zaidi ya yote, tangu lini tumeanza kutukuza wakoloni? Hivi kweli hoja haiwezi kujenga ikasimama wenyewe hadi tupige magoti na kuonesha kile “walichofanya wakoloni”. Huku ni kujidhalilisha kusiko kwa lazima. Na kama jambo lilifanywa na wakoloni haina maana jambo hilo lilikuwa sawa. Si hawa hawa wakoloni wanaolalamikiwa na Waislamu kuwa ndio walioweka misingi ya kuwapendelea Wakristu? (soma kitabu cha Hamza Njozi na kile cha Mohammed Said). Si ndiyo hawa wakoloni waliowatenda vibaya waislamu kwa mambo yao kama yanavyosimuliwa katika nyaraka mbalimbali za kihistoria? Ni lazima tukubaliane kuwa kutumia Wakoloni kama msingi wa kujenga hoja ya kadhi ni mkakati mbovu.

Hoja ya 3. Nchi nyingine majirani na za kiafrika zina mahakama ya kadhi kwanini sisi tuogope?

Hoja hii ukiingalia kwa haraka ina nguvu ya “kufanana” na ushawishi wa “ukaribu”. Mara nyingi katika hoja hii kauli inayofuatia ni “mbona hata Zanzibar Mahakama ya Kadhi ipo kwanini isiwepo hapa Bara?” Hoja hii nayo ina msingi lakini haina nguvu ukiingalia kwa karibu. Kwa kuzihusu nchi nyingine hoja hii ina udhaifu mkubwa ufuatao, Tanzania ni nchi huru inayojiamulia mambo yake yenyewe na haishinikizwi kwa namna yoyote ile kufuata kile ambacho nchi nyingine inafanya.

Kuna mambo ambayo nchi nyingine zinafanya na sisi hatufuati. Kuna nchi ambazo zinatambua uwepo wa mahakama ya Kadhi lakini zina mambo mengine ambayo hatuambiwi tuyafuate pia. Afrika ya Kusini inayo Kadhi lakini hao hao wanaruhusu mashoga kuoana. Sasa kama vinavyofanya na sheria za nje ni mambo ya kufuata kwanini tufuate la kadhi tu na tusifuate la kuruhusu mashoga kuoana?

India ambako tuna ukaribu zaidi wa kisheria labda kuliko sehemu nyingine yoyote katika jumuiya ya Madola, wao wanazo mahakama za kadhi lakini hazitambuliki na sheria ya India lakini hazipingwi na maamuzi yake yanakuwa ni ushauri tu usio na nguvu ya kisheria na uamuzi huo hamzuii Muislamu kwenda katika mahakama za serikali. Kwanini tuchague kufuata ya Kenya na siyo ya India? Nchi kama Uturuku ambazo zina Waislamu wengi kuliko Tanzania hazina Mahakama ya Kadhi jinsi zinavyotakwa hapa Tanzania. Wao (Waturuki) ingawa mahakimu wao wanaitwa “Makadhi” kutokana na sababu za kihistoria lakini hawahukumu kwa sheria za Kiislamu.

Kwa kifupi ni kuwa, suala la kadhi linawahusu Watanzania na ni Watanzania ambao wagonganishe vichwa vyao wakikusanya mang’amuzi ya utaalamu wao mbalimbali na kutafuta suluhisho ambalo ni la Watanzania na la Kitanzania.
Nimebahatika siyo tu kuishi na Waislamu bali pia kukulia na kusoma kati yao na kuwa na marafiki wa karibu na wengine imefikia familia zetu kuoleana n.k Siwezi kuamini hata kidogo kuwa Watanzania wenzetu hawa ambao ni Waislamu watageuka na kuwa Afghanistani au Iraq na kuanza kututendea vibaya kisa tu ati mahakama ya kadhi imeanzishwa. Waislamu wa Tanzania ni mfano bora kabisa katika ulimwengu wa mahusiano mazuri kati ya watu wa imani tofauti katika nchi. Ni lazima tujivunie tofauti yetu na hasa pale ambapo tofauti hiyo inatufanya tuzungumze kwa uhuru, kwa heshima, na kwa upendo kati yetu.

Itaendelea wiki ijayo kwa kuangalia hoja nyingine zilizosalia na zile hoja zenye nguvu.
 
Mimi najiuliza Hivi Tanzania Ilikuwa na dini gani kabla ya maharamia kuweka nanga? Subira yetu ipo wapi? Mwanakijiji nisaidie!
 
Mimi najiuliza Hivi Tanzania Ilikuwa na dini gani kabla ya maharamia kuweka nanga? Subira yetu ipo wapi? Mwanakijiji nisaidie!

unaposema maharamia una maana gani maana maharamia ni Pirates.. sasa unazungumzia maharamia gani? na hilo linahusiana vipi na hoja ya Mahakama ya Kadhi?
 
Lakini mkumbuke kuwa mtu aliingia madarakani kwa promise ya kusaidia kufasnikisha kuwepo kwa mahakama ya kadhi. You can always take a word of gentlemen. No doubt kuwa Tanzania/Tanganyika or whatever identified it before coming of the Arabs kulikuwa na dini za kuabudu mizimu. Lakini sijui kama dini hizo zilikuwa na itikadi za kigeni zinazoleta mivutano kwenye jamii.
Lakini kwa upande mwingine naona kuwa hii inaweza pia kusaidia wakristo nao watafute some form of mahakama zao. Kwa sababu all of we Tanzanians are supposed to be subjected to same set of laws without regard of religion, tribes and race. Kuwa na mahama kama hizi ni one step back kwenye umoja wetu.
 
why say no? unaweza kuwakataza watu wasiabudu? Mahakama ya Kadhi ni sehemu ya ibada ya Waislamu...
 
Mie sijasoma maelezo yote juu kuhusu maana ya mahakama ya kadhi nini..kama wanakusudia kuhukumu Kiisilam yani kwa dini ya kiisilam hadi sasa hata hao ambao ni nchi za kiisilam bado hawajaweza..ikiwa miongoni mwake ni saudia..ukiacha nchi za kiarabu tu ambazo sio za kiisilam..sasa sisi tanzania bado kabisaaa
 
Nadani ni vema kabla ya kutoa mchango wowote tuangalie mahakama ya kadhi ni nini,inawalenga akina nani itakuwa inafanya kazi vipi na hivyo ndio tuweze kuchangia.Kwa upande wangu sioni ubaya wakuwa na mahakama ya kadhi provided itakuwa inafuata misingi ya katiba na itasaidia kutatua mrundikano wa kesi hata ndogondogo mahakamani ambazo zilikuwa zikiendelea kupangiwa tarehe na mahakimu kulingana na uwingi wa kazi walizonazo.
 
Binafsi napinga sana kwa serikali yetu kusimamia mahakama ya kadhi sasa hivi. Najua ni serikali hiyo hiyo ilifuta mahakama hiyo miaka ya 60s na bila shaka ilikuwa na sababu ya kufuta. Swali je ni kwanini ilifuta? Je sababu iliyosababisha kufutwa imerekebishwa? Kama ilifuta kwasababu tu inaingilia mwenendo wa mahakama za kikioloni basi swala hilo lirudishwe mara moja kwani kwa sasa mahakama hiyo ni sawa na taasisi za kiislamu. LAKINI kamwe lisiingizwe katika KATIBA YA TANZANIA. Kwasababu kwa jinsi ninavyojua mahakama ya kadhi kazi yake hicho kimbembe kitakachofuata itabidi sisi wengine tulindwe na katiba hiyo ambayo inataka kuingiliwa.
 
Back
Top Bottom