Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Binafsi napinga sana kwa serikali yetu kusimamia mahakama ya kadhi sasa hivi. Najua ni serikali hiyo hiyo ilifuta mahakama hiyo miaka ya 60s na bila shaka ilikuwa na sababu ya kufuta. Swali je ni kwanini ilifuta? Je sababu iliyosababisha kufutwa imerekebishwa? Kama ilifuta kwasababu tu inaingilia mwenendo wa mahakama za kikioloni basi swala hilo lirudishwe mara moja kwani kwa sasa mahakama hiyo ni sawa na taasisi za kiislamu. LAKINI kamwe lisiingizwe katika KATIBA YA TANZANIA. Kwasababu kwa jinsi ninavyojua mahakama ya kadhi kazi yake hicho kimbembe kitakachofuata itabidi sisi wengine tulindwe na katiba hiyo ambayo inataka kuingiliwa.

Bubu yaani kwanini tujipalie mkaa eti tusubili yakisha tukuta ndo tukimbilie katiba?

We simply say No to Kadhi period. Hasa hasa kwamba kodi zetu wote zilipie taasisi ya wachache?? No No a big Nooooo!!
 
Lakini mkumbuke kuwa mtu aliingia madarakani kwa promise ya kusaidia kufasnikisha kuwepo kwa mahakama ya kadhi. You can always take a word of gentlemen. No doubt kuwa Tanzania/Tanganyika or whatever identified it before coming of the Arabs kulikuwa na dini za kuabudu mizimu. Lakini sijui kama dini hizo zilikuwa na itikadi za kigeni zinazoleta mivutano kwenye jamii.
Lakini kwa upande mwingine naona kuwa hii inaweza pia kusaidia wakristo nao watafute some form of mahakama zao. Kwa sababu all of we Tanzanians are supposed to be subjected to same set of laws without regard of religion, tribes and race. Kuwa na mahama kama hizi ni one step back kwenye umoja wetu.

Bongo,Siku zote CCM imekuwa ikitawala kiujanja-ujanja kwa kutumia shida na ujinga wertu Watanzania ili wapate ridhaa ya kutawala na hii ni hatari kubwa. Ishara ya hatari hii ni hii Waislamu kudai mahakama ya Kadhi (pamoja na hoja nzuri za Mwkjj kuhusu hoja hii). Ukiangalia kwa undani CCM wametumia shauku (shida) ya kundi mojawapo lenye ushawishi kwenye jamii ili kupata kura za kuendelea kutawala.

Nathubutu kusema iwapo Mahakama hii itakuwepo tutashuhidia kuparanganyika kwa Taifa letu kutakosababishwa na ujanja-ujanja huu wa CCM maana Mahakama ikianzishwa tu lazima makundi mengine yenye ushawishi mkubwa katika nchi hii (Wakristo) nao watadaisheria za Kanisa zitambuliwe Kikatiba na kutumika na kwa hila hizo hizo za CCM kutaka kuendelea kutawala basi watakubali (hawatakuwa na sababu ya kukataa wakati wamekubali kutambua Mahakama na mamlaka ya Kadhi)na hivyo tutashuhudia Taifa letu likiongozwa na sheria tatu tofauti zinazopingana. Mfano, Kanisa haliruhusu talaka wakati Sheria za Kiislamu zinatambua na Serikali hutambua; je, itakuwaje pale ambapo mtu na mke wake au mumewe kila mmoja anataka ifuatwe sheria tofauti kuhusu talaka katika shauri lake? Sijui Makarasinga na Wahindu nao wakitaka sheria za dini zao zitumike itakuwaje.

Hili litapelekea mwishowe kila dini iwe na eneo lake la kujitawala ambapo sheria zake ndiyo zinatambuliwa na kutumika kama vile Islamic territory, Christian territory na Government/Secular territory.

Nathubutu kusema kuwa kama Serikali ya CCM iko makini na haitaki kuliingiza taifa kwenye madhara Mahakama ya kadhi haitakuwapo na ikiwepo basi Sheria za kanisa nazo itapaswa zitumike, what a contardiction! Sulal la Mtikila (ingawa watu wanamwona kuwa ni kama Chizi katika suala la Mahakama ya Kadhi) ni ishara tu ya mambo yatakavyokuwa pindi Mahakama ya kadhi itaanzishwa.

Serikali ya CCM itabidi ituambie kwa nini iwakubalie Waislamu kutumia sheria za kidini katika masuala yao na kutukatalia sisi Wakristo kutumia sheria zetu!
 
Ndugu zangu Mahakama ya kadhi si sehemu ya Ibada.Ingawaje Mahakama ya kadhi itatumia sheria za Kiislamu itakuwa si ibada.

Serikali hapa ingeliwakusanya wanasheria wa madhehebu mbali mabali ili waweze kutunga sheria ambazo zitawahusu Watanzania wa madhehebu yote. Dini ya Kiislamu, Kikisto na Kiyahuud dini hizi zimetungwa kwa misingi ambayo inafanana. Waislaamu wameambiwa (Surratt Albakrah) kwamba "SISI WAISLAMU TUNAAMINI VIATBU VYOTE VILILETWA..... na MITUME YOTE TOKA NABII MUHAMMAD, MUSSA(Moses), Issa bin Maryam(Jesus)... Ibrahim.........nk."

Hii inamaanisha kwamba katika vitabu vitatu hivi tunaweza kupata skeria ambazo zitatufaa sote. Kwa mfano hakuna mahali popote katika vitabu hivi ambapo pamesema rushwa ni hali. Wahayuud waliambiwa wale wanaofanya rushwa wafukuzeni nchini(iko katika msahafu aya hii).

Mtu una abudu Mungu.Ibada yako ni kati yako wewe na Mwenyenzi Mungu.Swala zako ni kati yako wewe na Mwenyenzi Mungu.

Dini iliondolewa katika katiba ya (Tanganyika)/Tanzania ili kuepuka mvurugano. Kila mtu aabudu MUNGU WAKE.

Ndugu Waislaam fuateni masomo ya Kur'an hasa sura iaanzayo na msemo "KUL-YAA AYYUHAL KAAFIRUNA................." mkisoma hiyo mpaka mwisho na mkitafsiri mtapata jawabu. Mtume Muhammad(S.A.W) aliaambiwa asome sura hiyo wakati alipubughudiwa wa Wakristo na Wayahuu. Sura hiyo inamalizia na kusema "KILA MTU AABUDU ANAVYOTAKA"(LAKUM DIINU KUM WALIYADIIN).

Nadhani ni kwa sababu hii Dini iliondolewa katika katiba ya Tanzania.
 
Mimi najiuliza Hivi Tanzania Ilikuwa na dini gani kabla ya maharamia kuweka nanga? Subira yetu ipo wapi? Mwanakijiji nisaidie!

Fafanua kidogo swali lako.
1. Maharamia gani waliweka nanga?
2. Tanzania imeanzishwa mwka 1964, je unamaanisha kulikuwa na dini gani kabla ya hapo?
 
Ndugu zangu Mahakama ya kadhi si sehemu ya Ibada.Ingawaje Mahakama ya kadhi itatumia sheria za Kiislamu itakuwa si ibada.

Serikali hapa ingeliwakusanya wanasheria wa madhehebu mbali mabali ili waweze kutunga sheria ambazo zitawahusu Watanzania wa madhehebu yote. Dini ya Kiislamu, Kikisto na Kiyahuud dini hizi zimetungwa kwa misingi ambayo inafanana. Waislaamu wameambiwa (Surratt Albakrah) kwamba "SISI WAISLAMU TUNAAMINI VIATBU VYOTE VILILETWA..... na MITUME YOTE TOKA NABII MUHAMMAD, MUSSA(Moses), Issa bin Maryam(Jesus)... Ibrahim.........nk."

Hii inamaanisha kwamba katika vitabu vitatu hivi tunaweza kupata skeria ambazo zitatufaa sote. Kwa mfano hakuna mahali popote katika vitabu hivi ambapo pamesema rushwa ni hali. Wahayuud waliambiwa wale wanaofanya rushwa wafukuzeni nchini(iko katika msahafu aya hii).

Mtu una abudu Mungu.Ibada yako ni kati yako wewe na Mwenyenzi Mungu.Swala zako ni kati yako wewe na Mwenyenzi Mungu.

Dini iliondolewa katika katiba ya (Tanganyika)/Tanzania ili kuepuka mvurugano. Kila mtu aabudu MUNGU WAKE.

Ndugu Waislaam fuateni masomo ya Kur'an hasa sura iaanzayo na msemo "KUL-YAA AYYUHAL KAAFIRUNA................." mkisoma hiyo mpaka mwisho na mkitafsiri mtapata jawabu. Mtume Muhammad(S.A.W) aliaambiwa asome sura hiyo wakati alipubughudiwa wa Wakristo na Wayahuu. Sura hiyo inamalizia na kusema "KILA MTU AABUDU ANAVYOTAKA"(LAKUM DIINU KUM WALIYADIIN).

Nadhani ni kwa sababu hii Dini iliondolewa katika katiba ya Tanzania.

Dr. Khamis, Mashehe wa Tanzania ambao ni watetezi wa Mahakama ya Kadhi wanasema kuwa kufuata hukumu za Kiislamu kama zinavyotakiwa katika Qurani na Sunna ya Mtume (SAW) ni kama sehemu ya ibada. Msimamo huo ulitolewa pia na Mufti Mkuu wa Israeli kuhusu mahakama za kadhi kule Yerusalemu Magharibi na ni kwa sababu hiyo Israeli wameruhusu Mahakama ya Kadhi.
 
Mzee mwanakijiji, naona kama umeruka hatua moja!!!!

Ingependeza ungeanza na jinsi ya mahakama ya kadhi itakavyofanya kazi TZ. Si vibaya ungetupa na mifano michache kwa jirani zetu kama Kenya, Mozambique, Uganda n.K. Yawezekana Wanaotetea Mahakama ya Kadhi, wanatoa hoja ya kuwepo mahakama ya kadhi ktk nnji hizo kama jibu kwa wanaopinga kwa hoja kuwa Mahakama ya kadhi itagawa wanannji na kuleta vurugu!! Pengine wao wanauliza mbona huko hamna vurugu???

Mzee mwanakijiji pengine pia ktk makala yako inayoendelea yafaa utafiti kipi kilichofanya mahakama ya kadhi ifutwe TZ baada ya ukoloni. Pengine ktk hili wanaotetea kuwepo mahakama ya kadhi pia wanahoji vipi ukoloni uliruhusu waTZ wenyewe wafute?? Mbona Ubote, Kenyata, Samora hawakufanya kama alivyofanya Nyerere kufutilia mbali mahakama hiyo?? pengine kwa kuonyesha hasara/matatizo waliyopata hao jirani zetu kwa kuendeleza mahakama za kadhi inaweza kuonyesha sasa tunapata hoja zenye nguvu! Vinginevyo itakuwa tunapoteza muda, kwani hatutakuwa na tofauti na waliotoa hoja za kutetea mahakama hiyo.

Kuhusu ahadi ktk ilani ya uchaguzi ya CCM, mzee umeliweka sawa!!
Kama waislamu wanafikiri wamepigwa changa la macho basi kazi kwao 2010.

Mzee mwanakijiji, nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa hoja zako. Nyingi kama si zote ziko ktk msitari. Naamini hii pia iko katika usawa. Umeianza vizuri! Naomba uiweke vizuri zaidi kwa kuimalizia kwa Kuelezea hoja za wanaopinga kama zina nguvu au la!! Kwa hili ni vizuri hata kama utahitimisha kwa kuonesha madhara yatakayotupata kwa kurejeshwa mahakama ya kadhi. Wanaotoa hoja kuwa zitaleta uhasama kati ya waislamu na wakristo, kuwa ni kosa kutumia pesa za walipa kodi kunufaisha kundi la jamii fulani nk hawajanishawishi kuona kuwa hoja zao zina nguvu. Bado naona kama ni ushabiki wa kidini tu!!!

Mwisho, nami nihitimishe kama mzee ulivyoanza kuwa ni vizuri tulijadili suala hili tukijua kuwa ni kwa faida yetu kama matokeo ya mjadala yatakuwa mazuri kama itakavyokuwa hasara kwetu tukiboronga!! Tukizingatia hilo ndio tutaishia kuwa wamoja mwisho wa mjadala badala ya kugawanyika kati ya wanaotaka na wasiotaka Mahakama ya kadhi.


uhuru wa kweli, amani ya kweli na haki ya kweli tutajiletea waTZ wenyewe.
 
Fafanua kidogo swali lako.
1. Maharamia gani waliweka nanga?
2. Tanzania imeanzishwa mwka 1964, je unamaanisha kulikuwa na dini gani kabla ya hapo?

1. If I am not mistaken Vasco de gama and his cronies!
2. It is known that Africa was influenced by Islam as early as the 8th cuntury -I would have thought islam would play a big role in our culture, especially Tanzania. Therefore Hii mahakama ya kadhi must have existed somehow during that period! Q. Au?
My intentions were to go back in history and then answer some questions before asserting the status quo!
 
Usiwe na shaka nitaonesha pia ni hoja gani zina nguvu na ambazo ni vigumu kuzivunja. Na pia ninaonesha Mahakama ya Kadhi tanzania inaweza kuwa vipi kwani hazifanani nchi mbalimbali.. na anayedhania kuna template ya mahakama ya kadhi ambayo itachukuliwa toka nje na kuwekwa Tanzania bila modification atakuwa amekosea.
 
Nafikiri ulimaanisha Serikali ya Tanzania na dini wapi na wapi? Au?
 
that b.s and you know it! uislam ni nguzo tano, vilivyobaki ni sunna....sasa define sunna, and we will take it from there!!! Hint: why go thru all this trouble ambayo inaweza ku-jeopardize national unit kwa sunna tu??. Nameona umetoa mfano wa west jerusalem, hiyo ni complete different story toka kwa hii.....unless unataka kufanya hii issue political na ni hapo ndipo wakina sisi tunapoona walakini......JUST SAY NO!!!.

national unit? Kuna kadhi Zanzibar kwa miaka 100 sasa... umesikia kuna mkiristu kafikishwa mahakama ya Kadhi? Lini ulisikia kuna Muislamu kakatwa mikono Zanzibar? Huu ni woga usio na msingi.
 
Several weeks after this fatwa was publicized in the official newspaper of the Islamic Movement, another fatwa was issued – this time by the highest religious authority in Palestine, the mufti of Jerusalem, sheikh ‘Akrama Sabri. Sheikh Sabri is an appointee of the Palestinian National Authority, and his rulings have no legal standing in Israel.

Nevertheless, he is considered a highly respectable ‘alim, and the opponents of the legislation amendment sought to recruit his voice in support of their struggle. Zahi al-Majidat – secretary of the Mizan Association22 affiliated with the Islamic Movement – addressed a query (istifta') to mufti Sabri, asking for his opinion with regard to the
proposed legislation amendment. Sheikh Sabri responded with an unequivocal fatwa:23 Matters of personal status – which include in addition to the issue of waqf such issues as marriage and divorce, maintenance, guardianship, bequests and so forth – belong to the domain of acts of worship (‘ibadat).

Therefore Muslims are forbidden to act in discordance [with shari‘a rules] in these matters. A Muslim must perform God's directives with regard to maintenance or bequests, just as he must perform God's directives with regard to the duties of prayer, alms giving and the Hajj, even if he lives ina non-Muslim state.

- The implementation of non-Islamic laws in matters of personal status is hence considered a direct assault on the realm of worship and therefore it is forbidden for Muslims to resort to courts which adjudicate in these matters in a non-Islamic manner. What we need is to safeguard the shari‘a courts, and to invest effort in broadening their jurisdiction so that it will include all aspects of life, and not in reducing it.
you can read the rest of the story HERE
 
Mzee mwanakjj, andaa makala baba tuimalize hii issue kwa hoja. Wanaotaka kuliongelea suala hili kwa jazba waache waendelee, ni haki yao ya msingi humu JF.

Ladies and gentlemen JUST SAY NO!!!!!.

Hivi wengine nao wakisema just say YES itakuwaje?!! Tunataka YES or NO that has strong or at least reasonable supporting evidence.

Muslims are about 50% of TZ populace, their voice can not be ignored just by saying NO!!!! NO can not stand alone, it is not enough if it is not supported by facts.

Leo nimesikia kuwa eti kuna kundi la waislamu wanataka serikali isitishe uhusiano na VATICAN. Mwafikiri itatosha mtu aseme JUST HALT diplomatic relationship with vatican?? Alaa, ujinga gani huo??

Kesho pengine tutasikia wengine wakisema nao wanataka Ijumaa iwe siku ya mapumziko, hivyo serikali iamue kuwa na siku 3 za mapumziko au wafute moja kati ya J2 na Jumamosi, tutasemaje??? Nao wakitaka ofisi za serikali na mashirika ya umma zipambwe siku za EID kama zinavyokuwa kipindi cha X-MAS itakuwa udini??? Na mwingine akitaka mwaka mpya uwe kwa kalenda ya kiislamu itakuwaje???

Japo katika makala yake mwanakjj aliwalaumu wale mashekhe waliohojiwa katika Jenerali on Monday, kwa kuwaomba waislamu wawe watulivu, ukweli ni kuwa wale mashekhe kwa kauli yao ile wameitendea jambo jema sana nchi yao. Waislamu hawana subira pale wanapoona haki yao inachezewa (zaidi mtu anapotoa maneno ya kashfa kwa mtume na mwenyezi mungu). Nina hakika Mwanakjj alitumia busara kuelezea vile akijua fika kuwa kwa kuficha ukweli huo ingeimarisha subira ya waislamu katika jambo hili.

Yawezekana kabisa, kuwa si waislamu wote wanaotaka mahakama ya kadhi lakini ikumbukwe kuwa Unapozungumzia watu takribani 20 milion, moja ya kumi tu ya asilimia yao moja itatosha kuleta vurugu kubwa watakapoamua kuingia mitaani.

Hapa ndipo napoungana na mwanakjj, kuwa haya mambo yanahitaji hoja zilizo wazi, busara na hekima kuliko jazba. Ni vizuri tukalizungumzia suala hili tukiwa kitu kimoja badala ya kuwa SISI na WAO. SISI na WAO inapendeza tu tukiwa tunaizungumzia kwenye blogu, magazeti, TV, maofisini na sehemu kama hizo, ikifikia SISI na WAO mitaani ni Janga kuu la kitaifa!!!

Bado nina amini kuwa waTZ wanajali na kuthamini uhuru na amani tuliyonayo. Itachukuwa muda na nguvu nyingi kuvunja hazina hizo za nchi, hata hivyo tunawajibika kwa pamoja kuzilinda kwa gharama yoyote kwani hakuna kitu chenye thamani yake!!!
 
Kwa kweli mimi sikuwa najua kama Serikali yetu inauhusiano rasmi wa kibalozi na Vatikano! kwani tangu enzi za Mwalimu nchi yetu ilikuwa haina dini na katiba yetu iko wazi kabisa kuwa Serikali haina dini!

sasa haya yamekujaje tena kwani leo nimesoma gazeti moja linaripoti kauli za viongozi wa Kiislamu kuitaka Sirikali kusitisha uhusiano huo mara moja soma hapa ..http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/11/7/habari3.php na mimi nawaunga miguu na mikono viongozi hao kwa uwamuzi wao na kuwashauri waishitaki Serikali Mahakamani kwa kuvunja katiba ya nchi!
 
CRAP........Tuanze kwanza kusitisha uhusiano na Saudia Arabia na Iran. Kuwa na rafiki mwislamu haina maana ya kulazimishwa kuwa mwislamu, na kuwa na rafiki mkristo haina maana ya kulazimishwa kuwa mkristo, na kuwa na uhusiano na nchi pagani kama Tanzania hakuna maana kuwa unalazimishwa kuwa mpagani. Nyerere mwenyewe alizungumzia haya vizuri sana.
 
Huyu mkuu Kaodogoo,

Ndio zake hizo toka BCS, yeye udini tu ndio utamkuta Mkuu Kadogoo mbona umepotea sana mkuu siku hizi?
 
Kuu Es the news has been spilled out na si swala la Kadogoo ila wamekaa Maelezo jana na kutoa msimamo .Sasa hapa Kadogoo udini wake ni kuleta mada hapa ?

Mimi nilisema ahadi zingine zitaleta balaa kisa madaraka . Now these guys they wany kadhi na hapa ndipo kazi inakuja maana Nchi haina dini ila watu wana Dini zao .What is next ?
 
Udini udini huo umeanza. Vatican ni state si mahakama ya kadhi ambayo ninaweza kusema taasisi kama zilivyo taasisi zingine. Kinachokatazwa hapa ni ukadhi huu kuingizwa katika katiba ya nchi. Kama kadhi ingekuwa ni state kama Vatican na hawa Wakristo wakawa wanaipinga basi na upande wa pili ulikuwa na haki ya kuipinga Vatican.
 
Kitu walichochanganya hao masheikh ni kuwa hawajui kuwa siyo balozi wa Roman Catholic bali ni balozi wa Vatican.

Sure Bongolander, nani anahusisha uhusiano wetu na Iran, Sudan nk na masuala ya dini? No one!
 
I have never and never will I understand Moslems and Christians in my life.These people think that ONLY them have all rights in this world over people of other religions.Yaani wakristo na waislamu ni wajinga sana na ni wabinafsi since time immemorial.Ni hiziz dini 2 pekee ambazo zimeua na kuibia watu wa dini nyingine kwa kisingizo cha "kueneza neno la Mungu",ni dini hizi hizi 2 ambazo zimewagawa watu wa bara la Afrika na ni dini hizi ambazo zimechochea na zinazidi kuchochea chuki miongoni wa binadamu leo hii duniani.Hebu tutazame,hawa Waislamu wanadai Mahakama ya Kadhi ambayo itakuwa fully supported financially na Serikali ya Nchi katika kutekeleza kazi za dini hiyo tu.Does that make sense to any sensibly thinking individual?Yaani Budha au Mwanamalundi au whoever it may be achangie kusubsidize imani ya mwingine!!!

Hata hawa Wakristo na vivyo hivyo,huwa wanaibuka na madai yao ya ajabu tu,yaani nchi hii utafikiri ni ya Waislamu na Wakristo pekee...what about Hindus,Afrikan Traditionalists,Budhists,etc?Don't they have the same rights accorded to Christians and Moslems?Or is it because Islam and Christianity are the only "true" religions?

What sheer religious hipocrisy!!!
 
Back
Top Bottom