JKT kurejeshwa, wazo zuri au limepitwa na wakati?

Ngugu mwana JF
JKT ilitukutanisha watu wa kutoka kila kona ya nchi yetu na fani mbali mbali, hii leo kwa aliyepitia JKT karibu kila ofisi atakayoingia atakutana na mtu walipitia pamoja jeshini. lilitujengea umoja ambao thamani yake ukiwa na mtizamo finyu utaona kama ilikuwa ni kupoteza mda, mfano wa Kenya si unaona yanayotokea sasa ni mapungufu kwa kiasi fulani yaliyotokana na kutowaweka vijana pamoja kujifunza nidhamu na uvumilivu

Wrong! Kenya kuna National Youth Service NYS tena iko more organized kuliko JKT ilivyokuwa na ipo mpaka leo, usitoe maneno bila uhakika, nimeweka link huko juu hebu isome ujionee.
 
Hii akina dada kujirahisisha na kupenda mteremko wala haihusiani na jeshi! Hata vyuoni -mimi nilisoma UD -na nakumbuka akina dada waliopewa marks za chupi- as they were not hardworking!

Huko serikalini wako wengi tu wanaopenda mteremko- wanapewa safari mikoani, promotion n.k! Tena wengi tu ni wake za watu- sema wanapenda kujirahisisha!

Hili swala la akina dada kupenda mteremko is not unique to JKT- na tabia, makuzi na msimamo wa mtu!
 
Wakuu Kasana na FMES,
msi-generalize sio wasichana wote wapenda shushu waliokuwa wanajirahisi vilevile haimaani kuwa kama msichana anapenda shushu basi atajirahisi kwa afande; nawajua wengi waliokuwa wanapenda shushu ambao walibobea katika kujongo, C za matron ama uselule na walikula shushi vilevile...

Mkuu Mwakilishi,

I stand for what I said, kuwa 99% ya wasichana waliokuwa wakijirusha na maafande, walikuwa wanataka wenyewe, kutokana na nafasi yangu in the real life nilikuwa nina-hang out sana na maofisa, na hasa ukumbi wa maofisa na weekend mjini baada ya shuruba, I could not believe jinsi wasichana walivyokuwa wakigombania kupangwa kule ukumbi wa officer's, wengi walikuwa wakinililia niwaunganishe na maofisa, I was in a total shock! kwamba wasichana wenye elimu na safi pia wanavyoweza kujishusha hivyo kwa ajili ya shushu wakati wala haikuwa lazima,

Siku nilipoenda kuripoti kambini, nilienda na mtoto mmoja wa kike wa Mtei, kwa jina Lilian, huyu ndiye aliyekuwa mfano wa kuigwa, kwanza alikuwa mtoto wa kiongozi halafu wamo pia, pamoja na shuruba zote maafande walizojaribu kumpa na waliishia kumuacha kama alivyo maana alikuwa akiwacheka tu, tulikuwa na msichana anaitwa Tumpe Mwaijande maafande mpaka walishia kumuacha kama alivyo aligoma kata kata, na ninakumbuka wasichana waliokuwa ngangari mpaka kwenda kushitaki kwa CO na wale waliokuwa wakiwasumbua kupewa adhabu za guard na hawakuguswa,

Ukweli ni kwamba kuna element ya wasichana kupenda favors hata pasipobidi hii scientific fact, nilijifunza kule JKT. Ni kweli watoto wengi wa wakubwa walikuwa wakipelekwa some kambis, lakini haikuwa-guaranteee shushu, the matter of fact wao ndio waliokuwa wakiteswa sana kuliko raia wa kawaida, mambo mengine ni fact of life kwamba kiongozi ataenda ku-lobby mtoto wake kwenda Ruvu karibu na Dar ili aweze kumuona kwa urahisi, lakini haikuwaokoa shuruba za kule, mimi ninamuheshimu Mwalimu, kwa JKT kwa sababu kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilijifunza kuwa niko sawa na binadamu wengine, sisahau siku moja ilipofanyika operation ondoa vinyesi katika maeneo ya kambi kuruta wote tulishiriki kuokota vinyesi vyetu wenyewe kwa mikono yetu, na hii ilikuwa adhabu kwetu kutokana na kutopenda kutumia vyoo vya JKT, it was nice kwa sababu ni kitu ambacho nisingetegemea kukiona licha ya kusimuliwa,

lakini guess what? kuna wasichana waliojaribu kukwepa hilo na kujirahisisha kwa maafande, lakini kuna wasichana tulioshiriki nao ambao hawakuguswa, scientifically ni tabia ya wasichana kama sio wanawake kupenda favors hata zisipotakiwa.

Ahsante Mkuu.
 
Kasana hebu nambie ni mazingira gani yaliyokuwa yanapelekea hadi mtu 'anafungwa' mara kupelekwa 'mahakamani'...mi sijapita huko na nahisi nimekosa mengi kweli

Mkuu JKT, kulikuwa na sheria za kijeshi, ukivunja unapelekwa Court Marshall, ambako judge ni CO mkuu wa kikosi, kisheria anaweza kukuhukumu kwenda kufungwa uraiani, siku moja utlipewa likizo ya wiki mbili na CO, wale wote waliochelewa kurudi siku tukyoambiwa utrudi, wote waliswekwa jela uraiani mwezi mmoja. Amri ya jeshi huwa haichezewi mkuu, na jeshi walinifundisha one important thing nacho ni fanya amri kwanza halafu utalalamika baadaye!
 
Kama kuna kosa ambalo lilifanyika ni kuondoa JKT. Lakini, kisheria JKT bado ipo kwani sheria iliyoiunda haijafutwa, kilichofanyika nadhani ni kusimamisha kutekeleza sheria iliyowataka wanafunzi wanaomaliza form six na wanavyuo kwenda JKT kwa mujibu wa sheria. Naona siku hizi wanachukuwa vijana wanaenda JKT.

Pamoja na yote JKT bado ni muhimu sana, kuna mengi mazuri ya kujifunza kama vile ukakamavu, uvumilivu, kujifunza kazi nk. Pia ni sehemu ya kujifunza. Wale waliokuwa Ruvu "operation Miaka thelathini ya Uhuru" wana mngi ya kueleza na wale wote mlikuwa katika kambi zingine. Kwa hakika pia ni sehemu ya burudani, mnawakumbuka afande "Mungu', afande "Kibuyu", afande "Kisiti". Nilitumika JKT makambi matatu Ruvu, Mgulani, Malamba. ilikuwa ni adventure ya aina yake. Naweza kusema kwamba Mpaka leo hii, ninaweza kuvumilia na kuishi maisha yoyote magumu hapa Tanzania na sehemu yoyote ya nchi hii.

Nikikumbuka enzi hizo pia huwa nacheka sana, maana nilikuwa mhandisi wa kutengemewa sana pamoja na kwamba sikusomea uhandisi na wala sikuwahi. Hiyo ndio JKT. Bila kusahau mbinu za medani ambazo niliweza kusave "Mabogi" (Transfer)ya kwenda Chita. Nadhani ni wakati muafaka sasa Form six waende JKT, maana siku hizi vijana wamekuwa walegevu sana! slake slake" wakajifunze ukakama na utaifa kwa kukutana kutoka ila kona ya nchi.

Tuendelee.............................
 
Mtanzania,

Naona umevitaja kwa majina kabisa vitu ambavyo hukufundishwa jeshini yaani umalaya, uongo na wizi, sasa nitakosea kama nitahitimisha kuwa ulifundishwa vile ambavyo hukuvitaja hapo juu, yaani nidhamu ya woga na unafiki?


Kweli kabisa, vilevile walikuwepo wengi walioshindwa "kuweka msimamo", hapo sasa ndipo linapokuja suala la je ilikuwa haki wasichana kuwekwa katika hali kama ile ya kudhalilishwa vile?


Ukweli ni kwamba unaweza kujifunza uvumilivu na kujituma popote pale sio JKT peke yake, nadhani bila shaka hata wewe unawafahamu watu wanaojituma na wenye uvumilivu ambao hawajapitia jeshini.

Jeshini sanasana unachochea survival instinct zako tu, maana lengo linakuwa ni kupitisha siku bila kuhenyeshwa au kufanyishwa kazi ngumu, hence kujongomea kwa sana, kutafuta posti zenye ubwete, maana the next morning, aliyejongo na asiyejongo ngoma droo, mnaanza upya, uwajibikaji sifuri.

Leo hii tunashangaa tumepata wapi viongozi wasiowajibika wakati tabia hiyo tumeipalilia kwa bidii tokea jeshini, kama ambavyo Wadanganyika tunavyojivunia kutokufanya kazi, bila shaka umeshasikia maneno kama "nimeingia ofisini saa nne nikazugazuga pale saa saba huyo nikatimua" halafu tunajiona wajanja kumbe wajinga tu. JKT ni hivyo hivyo, mtu anayejongo ndiye anayeonekana mjanja mpaka maafande ndio wanamuona poa sana ila ukiwa kila siku upo tu kombania eti "unajituma" ndio unaonekana bonge la zezeta...

Mwakilishi,

I hope na wewe ulipitia JKT maana kama hukupita basi ni ngumu kutuelewa.

Mimi sasa nakutana na vijana wengi sana wa Kitanzania ambao hawajapita jeshini wakiwemo wadogo zangu, yaani kuna mambo mengi sana ambayo naona wangepita jeshini wangefaidika.

Hata hapa UK kuna vijana wengi ambao walikuwa wanajeshi na sasa ni wataalamu kwenye professions mbalimbali, nidhamu na utendaji wao ni bora kuliko vijana wengine ambao hawakupita jeshini.

Jeshi linaweza kuwa na matatizo yake lakini pia lina faida kubwa hasa nidhamu kwa vijana. Vijana waliotoka JKT ukiwaajiri baadaye hata kuwa walinzi huenda kukawa na ufanisi mzuri kuliko hao vijana wanaochukuliwa mitaani.

Unaweza kusema kuna nidhamu ya woga, mimi nitakuambia hiyo ni culture ya jeshi, inakufundisha kuheshimu aliyejuu yako na yeye anamheshimu mwingine na inaenda hivyo hivyo mpaka juu. Matokeo yake jeshi zima linakuwa na nidhamu.
 
Mkjj JKT ilikuwa bomba kwelikweli japo mwanzoni hali ngumu ajabu.Mtu unasema ukikutana na afande uraiani ama zake ama zangu.Lkn baada ya miezi sita poa tu.Siku ya kwanza ukiona mbaazi,unaapa hutakuja kuzila.Siku tu chache zikipita na ule mwendo wa mbio wa kuruta,mbaazi bonge la msosi na hutaki hata shoga aje kukudoea.Nilikuwa nafurahia tu zile mbinu za mtu kuishi
kwa kujongo na kukimbia kazi,watu wa ruvu tulikuwa tunakimbilia usawa wa nyani.Kwa kweli si ufisadi,ile tu kusota pamoja na mtoto wa kimario na vibosile wengine mtu unaona kweli hapa wote sawa tu.juhudi yako tu kutafuta c.

Ikarusi mama kumbakumba
Ikarusi mama kumbakisa
Elule lule elule,elule
Tutamaliza.

Bingwa Coy hiyo(Operation Okoa)
 
Askari ee, vitani ee
Anabeba, anabeba Bunduki, Mustini
Kibuyu cha Maji, vitani eeh!!!

Nyie mshawahi kuona mtu ananyosha magwanda hadi yanasimama!?

Yote tisa, kuna ulazima kufanya JKT kuwa compulsory tena? Vipi kuhusu yale mafunzo ya Mgambo ambao wale ambao hawakupitia JKT hata wakiwa viongozi walitakiwa kuyapitia? Namkumbuka Simba wa Vita na magwanda yake ya mgambo..!

Binafsi naamini Mgambo iwe volunteer lakini JKT irudishwe na kuwa ya lazima.

Back to ufisadi, kweli JKT haikuwa kiini cha ufisadi maana baadhi (kama siyo wengi) ya waliokatika utumishi leo hii ni hawa hawa tuliokuwa nao Mafinga, Maramba, Oljoro n.k Ni hawa hawa tuliosota nao kwenye mitaro na kwenye operesheni nyingi tu. Inawezekana vipi ule uzalendo upandwe ndani ya mioyo ya sisi na wao wapandikizwe ufisadi?
 
Ndugu yangu, mtu asipuuze JKT sitamsikiliza kamwe. Elimu ya msingi ya kujua mambo ya kitabuni, nilisomea huko katika shule ya msingi na sekondari, na ile ya kazi inayonilisha nilisomea huko university, lakini ile ya maisha yenyewe, mahusiano na jamii, ukakamavu, ustahimilivu, kukabiliana na hali mbalimbali, kutokata tamaa, na mengine mengi, haya niliyasomea JKT, na yananifaa hadi leo. Zile survival skills tulizokuwa tunatumia kule nimegundua zina-apply kila pahala. Ingawa mambo mengine yalikuwa vichekesho vitupu, siku za weekend, tunafanya outing kwa kutokomea porini na mahindi ambayo tukiwa humo tunayakaanga kwenye bati na kuyala, tukishushia na maji (yasiyochemshwa) na hatukuugua chochote hata siku moja. Siku zote nilizoripoti naumwa ilikuwa ni mbinu tu ya kupata C, na kwenye dispensary yetu aliyekuwepo clinical officer alikuwa kuruta mwenzetu (hakukuwa na afande mwenye sifa hiyo, inawezekana sasa baada ya JKT kufutwa ile dispensary imefungwa, sijui).

Nazikumbuka sana safari za kwenda shimo la mungu, bogi la Makuyuni na Maramba (ambayo yote nilisevu kinamna), jinsi nilivyofanikiwa kudanganya kuwa mimi ni mwanamichezo nikaenda "kula nchi" det ya Sakina, iliwachukua wiki 2 maafande kugundua sijui mchezo wowote! Nilipelekwa farming Coy baada ya kudanganya kuwa ni mtaalamu wa mifugo, baadae katika sakata la kugawa pororo za maziwa kwa maafande nikaonekana mbaya nikatimuliwa (maziwa yalikuwa hayatoshi, baadhi wakakosa wakasingizia nimewanyima kuwakomoa), lakini mwenzangu aliyepewa hicho kitengo maziwa yakawa hayapungui, wote wanapata na yanabaki. Kumbe mwenzangu alikuwa mjanja, yale maziwa ya kuwagawia wale ambao hawako kwenye list na yale ya kupikia chai officers mess alikuwa anaongeza maji! Na jamaa aliniambia hiyo kitu baada ya kumaliza JKT! Nikapewa (sijui adhabu) kazi ya kufuatilia order kila siku kule CTS, naenda na maziwa ya wakuu wa kule narudi na "amri za kila siku zitolewazo na A. Karubi, Kanali". Kasheshe ilikuwa kukatiza pale smart area kwenda kuchukua hiyo karatasi, kulikuwa na RSM mmoja simkumbuki jina alikuwa na mustachi hadi unafunika mdomo, duh ukikutana naye smart area utakoma!

Na ile njia ya kwenda Arusha mjini kwa miguu kupitia Nadosoito sitaisahau kamwe, tumekatiza sana hilo pori. Vile vijiwe vya "gongo" na "dadii" huko Muriet, Moita Ngiloriti, Duka Mbovu, na kwingineko.

Lakini yote ujumla wake ni kuwa jeshi lilinifaa sana, hasa kwa kuzingatia umri niliokuwa nao wakati ule, bado naona ile ilikuwa namna muafaka kabisa ya kuutumia muda wangu ule.
 
Mwanakijiji umenikumbusha anzi za mchaka mchaka...apo kulikuwa na ubeti unaanza tena na 'anavaa'...sijui unaendeleaje?
Mgambo hadi sasa hivi kuna maeneo yanaendeleza hadi miaka ya karibuni mfano kijijini kwangu watu walikuwa bado wanakamata kamata kwenda jeshi la mgambo.

Nakumbuka kama jeshi la mgambo linapita tulikuwa tunasimama kiukakamavu kama wakati wa kupandisha bendera ya taifa maana ukionyesha kuwacheka kidogo tu wanakumalizia hasira zao
 
Mwanakijiji umenikumbusha anzi za mchaka mchaka...apo kulikuwa na ubeti unaanza tena na 'anavaa'...sijui unaendeleaje?
Mgambo hadi sasa hivi kuna maeneo yanaendeleza hadi miaka ya karibuni mfano kijijini kwangu watu walikuwa bado wanakamata kamata kwenda jeshi la mgambo.

Nakumbuka kama jeshi la mgambo linapita tulikuwa tunasimama kiukakamavu kama wakati wa kupandisha bendera ya taifa maana ukionyesha kuwacheka kidogo tu wanakumalizia hasira zao


Nakulilia hicho kipande kipo hivi,


"Ana vaa , anavaa kombati, butii, kofia ya chuma vitanii eeeeh.
 
Kama kuna kitu ambacho mpaka leo Taifa letu lilikipoteza ni kile cha kila kijana anayetazamia na kujiunga na vyuo vya juu kupitia Jeshi La Kujenga Taifa. Nakumbuka kulikuwa na sisi Volunteers and watu ambao ilikuwa compulsory kwao (form six leavers).

Hiki ni kitu ambacho mpaka leo kinafanya tofauti kati ya raia na jeshi kuwa ndogo kwani wengi tumepita huko huko! Pamoja na kwamba wanajeshi hufanya Mafunzo zaidi lakini wote tuliopita huko tunajivunia kulijua jeshi. Mwanajeshi hawezi kukutishia kuhusu jeshi kwani wote tumelionja!

IMF na WB ndio walioshinikiza jeshi lifutwe kama kitu kilichokuwa kinapoteza hela LAKINI thamani ya mshikamano unaopatikana kwa kupita jeshini na kukutana na watu kutoka sehemu mbali mbali na tabaka mbalimbali ni kitu ambacho huwezi kukiquantify. Fikiri mtu kasoma Kibaha, mwingine huko Kibohehe mwingine Mkwawa na wengine kwenye maseminary...mwisho wa siku wote mnakutana jeshini na kuunga urafiki mkiwa jeshini! Baadaye maishani you bump into each other and though you come from different parts/classes you still know each other! JKT ni sehemu moja iliyosaidia ku"humble" watu. You really got to appreciate that maharage na ugali!

Sielewi hawa IMF na WB kwanini waliamua kutuwekea conditions hizo lakini nchi mbali mbali duniani zina hii compulsory National Service/ Military Service. Baadhi ya nchi hizo ni: Albania, Armenia, Austria, Belarus, Bermuda, Brazil,Chile,China (PRC),Colombia,Cyprus,Denmark, Egypt, Finland, Germany, Greece,Iran, Israel, Korea, South, Malaysia, Mexico, Norway, Poland, Russia,Serbia, Singapore, Sweden, Switzerland,Taiwan (ROC),Turkey,Ukraine.

I don't know with the current terrorism trend in the world kama Western Powers watakubali watu wengi wafundishwe katika jeshi then waachiwe kama ilivyokuwa kwa sisi. Mimi mpaka leo naikumbuka drill ya kupiga LMG vizuri sana na naamini I will perform better in combat than the current university leavers ambao hawakupita jeshini. Uzalendo pia ulijengwa kwa nguvu, wengi mtakumbuka DISCO. Wengi tumejifunza kuimba mbele ya watu na kuongea mbele ya watu bila ya woga tukiwa jeshini.

Nafikiri article hii chini inatoa mwanga kuliko wangu. JKT inaweza kujisustain yenyewe kama tutapata maafande viongozi wenye vision. Such labour force if properly managed can produce wonderful results!!

_________________________ beyond my box ___________________________________

Jean Jacques Rousseau argued vehemently against professional armies, feeling it was the right and privilege of every citizen to participate to the defense of the whole society and a mark of moral decline to leave this business to professionals. He based this view on the development of the Roman republic, which came to an end at the same time as the Roman army changed from a conscript to professional force.[13] Similarly, Aristotle linked the division of armed service among the populace intimately with the political order of the state.[14]
Some ideologies and cultures, and those based on collectivism or statism, value the society and common good above the life of an individual.[citation needed] Those ideologies and world-views justify the state to force its members to protect itself and risk their lives for the common good. In states based on society-centered ideologies, world-views and religions, conscription is the natural way of raising the army.[original research?]
In the era of total war, the conscription is the only alternative for a small nation to build an army of credible strength without depending on alliances. This is particularly the case when the opposing state is significantly larger. In such a case, a voluntary force could not, regardless of its quality, stand against the sheer numbers of the opposing force.[15]
The right of the state to conscript its citizens can be founded on utilitarianist principles.[citation needed] If a greater good would achieved, every thing considered, by sacrificing some soldiers a state should be willing to make this sacrifice.[original research?] This assumes that state have right to use its citizens for achieving greater good for the humankind.
Conscription can give the conscripts a lasting patriotic view and readiness to die for the good of the whole.[citation needed] Such readiness should, according to many world-views, be present in a virtuous citizen at all times, but through training, the readiness becomes a grim reality, not rhetoric.[citation needed] This may decrease the admiration of the military, but may also promote militarism and lead into readiness to use violence in everyday life to solve marital problems.[citation needed] On the other hand, the fact that every person understands that a war — any war — means that they themselves, friends, and relatives will be dying or at the least, facing mortal danger, decreases the willingness to enter an armed conflict.[citation needed] In practice, engaging a conscript force in an aggressive war for a prolonged period results in morale degradation both at home and on the front, testified by Afghanistan and Vietnam Wars.[original research?]

source: http://en.wikipedia.org/wiki/Conscription


Haa haa haa

Maelezo yako ynaonyesha wazi wewe hukuwa Volvo hata kidogo.
Ulipiga shule ndo ikakuponza kwenda jeshini.
 
Sasa, swali la msingi ni je JKT ilikuwa na mafanikio na manufaa kwa Taifa? Je ni chombo ambacho wakati wake umefika kurudishwa na kuboreshwa zaidi badili ya ilivyo sasa ambapo ni chombo cha uzalishaji "mali". Hivi wale walioenda jeshini miaka hii ya karibuni wanapata experience (mang'amuzi) kama ile ya wazee wa "kwata"?

Maana kuna wale waliosoma Boarding schools (hasa zile za wazazi) ambazo mang'amuzi yake yanalingana kwa namna moja au nyingine na maisha ya kambini.

Kama ukitakiwa kulifanyia marekebisho ambayo yataboresha JKT utatoa mapendekezo gani?
 
Frantz Fanon katika kitabu chake Wretched of the Earth alisema"the major weapon of the colonizers was the imposition of their image of the colonized on the subjugated people. These latter, in order to be free, must first of all purge themselves of these depreciating self-images". Ukibadilisha mwanamke kwa colonised na mwanaume kwa colonizer utakuta unazungumzia jamii yetu.

Mwanamke amekuwa kila wakati akilaumiwa kwenye vitendo kama hivi. Aidha anaambiwa alijiweka katika namna (kwa mavazi, miondoko n.k) mwanaume hakuwa na jinsi ila atembee naye au kwa nini hakuwa jasiri wa kuhimili jitihada za wanaume kutaka kutembenea nae, kwani hajui wanaume ndivyo walivyo.

Jamii tunaipima kwa jinsi inavyowalinda wale waliokuwa dhaifu na sio waliokuwa na uwezo. Huyo binti wa profesa na wengine wana haki ya kusifiwa lakini mimi nina zungumzia mtoto kutoka kijijini aliyemaliza darasa la saba ambaye lengo lake kuu maishani ni kuajiriwa katika jeshi. Hawa ndio haswa wanaohitaji msaada wa jamii. Kwa bahati mbaya hawa wamekuwa expendable, toka wale wanaotuhudumia katika sehemu zetu za starehe hadi wale walioingia jeshini kwa kujitolea. Nawashangaa mnaowabeza kuwa walijirahisisha ambapo wengi wa wanaume wasingeweze theluthi ya suluba walizokuwa wakipata hadi hapo watakapojiachia. Wajanja waliotambua wazi kuwa mwisho wa safari ni nini waliamua kutafuta mtetezi mapema kwa ujira ule ule.Wanaume wangapi tutafahamu adha ya kutangaziwa hadharani kuwa una e.d. ya matron? Kweli tunaamini wale wangekuwa na njia mbadala wangetembea na hao wapishi na maafande waliokuwa wanastahili kuwa babu zao? Naam, hivi vitendo vipo katika jamii lakini hii si sababu ya kuvitetea. JKT ilikuwa ndio kioo cha jamii yetu in a concentrated form. Na picha iliyotuonesha haikuwa nzuri kama mnavyotaka kutuambia.

Nimesoma posti nyingi humu ndani na sijaona mahali ambapo pameonyesha jinsi tulivyojengwa uzalendo tukiwa huko? Kwa kuwa na disko kila ijumaa na kufundishwa siasa na mtu ambaye hajui lolote isipokuwa kunukuu fikra sahihi za kiongozi wetu? Kufundishwa kinachoitwa mbinu za medani na watu wanaoshindwa ku'spell' miscellaneous? Kwenda porini ambako zaidi ya kutooga siku tatu, kuchimba mahandaki( vita gani ya hivi leo inapiganwa kwenye trenches?) na kuimba 'hap hap' hakuna cha maana kilichofanyika? Kujifunza kujongo? Hayo yote yanakusaidia vipi kuwa raia mwenye uchungu na nchi yake? Hizo nchi mnazozitolea mfano, vijana kweli hufundishwa mbinu za kijeshi na wanarudi kila mara kunolewa na mbinu mpya mpaka wafikie umri fulani. Uzalendo hautafundishwa katika kipindi cha mwaka mmoja na petty tyrants ambao ndoto yao ni kuwakomesha wanaowaona kuwa ni wasomi.

Kama tunataka kulirudisha, ni lazima tuangalie strength zake pamoja na mapungufu yake bila kificho. Pale palipokuwa na maonezi ziwekwe sheria ambazo zitamlinda yule aliye mnyonge katika sisi na si kuwatumia wenye uwezo kama ndio the lowest common denominator. Tuangalie upya malengo ya JKT na tuhakikishe kuwa yanatimizwa kwa ufanisi. Nje ya hapo ni kupotezana wakati. Nawasilisha.
 
Kasana hebu nambie ni mazingira gani yaliyokuwa yanapelekea hadi mtu 'anafungwa' mara kupelekwa 'mahakamani'...mi sijapita huko na nahisi nimekosa mengi kweli
Mkuu
vifungo nilivyovipata vilitokana na kujongo, mara ya kwanza tulijongo wengi kikosini, maafande walisambazwa pale mlandizi ili kila waliyekuwa wanamsuspect walimpeleka kambini, nakumbuka tulikamatwa kama 20 hivi.
Tukapelekwa mahakamani kama FMES alivyosema na kuhukumiwa kifungo siku 14 na kazingumu (pale pale kambini), kule selo of ulikuwa unalala chini,kama ulivyo na nguo zako, hakuna godoro wala chandarua etc.

Asubuhi wakati wa mchakamchaka utawasikia wenzako (mimi nilikuwa A coy) (wanakuimba). Kingine ilikuwa ni drill asubuhi kabla hamjapangiwa kazi n.k. Baada ya siku saba tukawa tumezoeana na maafande pale na tukawauliza kwa nini walikuwa wanatufanya vile (katika drill) wakasema tulipokamatwa hatukuwapa mikate na chapati tulizokuja nazo.

N.B
Tulipokamatwa tulikuwa na vikorokoro tulivyotoka navyo nyumbani, wakati tunaingizwa mahabusu tulinvuliwa mikanda, kamba za viatu, na vyote vyenye ncha kali ambavyo vingeweza kuhatarisha maisha. Tukaambiwa tule na kunywa vile tulivyobeba kabla ya kuswekwa selo. Tulikula bila ya kuwakaribisha au kuwapa. (kutokana na uoga na hatukujua kama walikuwa wanataka). Hiyo ilitucost sama kwenye drill asubuhi.
 
Katika hotuba zake Mwalimu alisema kuwa wakati wenzetu wanatembea sisi ni lazima tukimbie.

Nilipata bahati kusoma nchi za Africa, Mashariki na Magharibi. Ukweli wa mambo JKT was Mental mental retardation.

Na wanaotaka JKT irudi are pure retards.

Kwa mfano wanafunzi wanasoma boarding ambazo zimechanganya watu kutoka makabila na mikoa mbalimbali kwa miaka minne na baada ya hapo wanakwenda vyuo au high school miaka miwili au mitatu, je mwaka mmoja wa JKT unasaidia nini?
 
Mara ya tatu sikufungwa kwa sababu nilikuwa nimeshakuwa mjanja, kwenye 'statement' nilikataa kuandika kosa nililokutwa nalo, hivyo wakati nasomewa mashitaka hakukuwa na kosa nililodeclare na nilijitetea kuwa pass niliyopewa niliifulia,kama ningekuwa nimetoroka na bila kuwa na extension nisingepitia main gate. nikaachiwa huru.(infact niliiharibu ile pass makusudi kwani makao makuu walikataa kunipa extension)
 
Katika hotuba zake Mwalimu alisema kuwa wakati wenzetu wanatembea sisi ni lazima tukimbie.

Nilipata bahati kusoma nchi za Africa, Mashariki na Magharibi. Ukweli wa mambo JKT was Mental mental retardation.

Na wanaotaka JKT irudi are pure retards.

Kwa mfano wanafunzi wanasoma boarding ambazo zimechanganya watu kutoka makabila na mikoa mbalimbali kwa miaka minne na baada ya hapo wanakwenda vyuo au high school miaka miwili au mitatu, je mwaka mmoja wa JKT unasaidia nini?

Bin Maryam.. unaendeleza vizuri hoja lakini kitendo cha kuwaita unaopingana nao kwa hoja si cha kiungwana na ni jaribio dhaifu la kulazimisha hoja. Hoja hujibiwa kwa hoja si matusi au kejeli.
 
Back
Top Bottom