JKT kurejeshwa, wazo zuri au limepitwa na wakati?

Na dhani huyo Mwanakijiji ni mmoja wa wale ambao kwa sababu zao au familia zao walizuiwa kwenda JKT.
katika mambo ambayo mimi binafsi nasikitika ni kusitshwa kwa mafunzo ya JKT.
JKT iliweka uwanja sawa kwa wale "those who have and have not".
JKT iliongeza mshikamano na kuunganisha utanzania wetu, jambo ambalo ndugu zetu wa kenya wanalikosa na kuzidisha ukabila.
Kwa hali ya kawaida mtu ambaye umepata naye shida na mwisho mka-survive ni nduguyo na haiwezekani ukamtendea jambo lolote la kukatisha maisha yake.
JKT ilikuwa ni kama formation camps ukiachilia mbali uzalishaji.

Ufisadi uliosababisha mpaka JKT kuonekana kama wanatumia zaidi ya kila wanachozalisha ni kitu henzi hizo kilikuwa kinaitwa POLOLO.
POLOLO kwa maana rahisi ilikuwa ni kuchukua bidhaa za jeshi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani hasa wale askari. Lakini ilikuja fikia kiasi kwamba WAKUU WA JESHI WANACHUKUA MALORI YA MAHINDI, MPUNGA N.K KWA MFUMO HUO WA POLOLO. LAST hasara hiyo ikawa inatokea katika makambi mengi ya JKT na kusababisha Serikali kushindwa kuhimili hasara hizo. WAKUU HAO KWA SASA NDIO WAKUU WA MAWILAYA, WAKUU WA MIKOA N.K
Kwa maoni yangu NYERER ALIKUWA NA MAONO MAZURI SANA KTK UANZISHWAJI WA KAMBI HIZO ISIPOKUWA WALE WALIOPEWA DHAMANA YA KUSIMAMIA NDIO WALIKUWA MAFISADI.
 
Bin Maryam.. unaendeleza vizuri hoja lakini kitendo cha kuwaita unaopingana nao kwa hoja si cha kiungwana na ni jaribio dhaifu la kulazimisha hoja. Hoja hujibiwa kwa hoja si matusi au kejeli.

Mwanakijiji,

Hizo si ndio Nyerere alisema HOJA ZA NGUVU? Ili kuwatisha watu wasiendelee na hoja mtu anatumia matusi, mapanga, bunduki ili mradi kuwamaliza wote wenye mawazo tofauti na yake. Huyo mheshimiwa uliyemtaja mimi nimeamua sitajibu jumbe zake maana ni kupoteza muda na hakuna unaloweza kujifunza zaidi ya kuishia kutukanwa.

Israel wana kitu kama JKT na limesaidia sana kuwaunganisha. Hapa UK sasa
Brown anapendekeza kitu kama JKT kwa vijana kati ya miaka 16 na 18 japo bado haijapitishwa lakini vijana watatakiwa kukaa kambini kwa muda wakijifunza mambo karibu sawa na tuliyokuwa tunajifunza JKT. Hata sasa kwa
UK bado vijana wanategemewa kutumia mwaka mmoja baada ya kumaliza A-level kwenda kusaidia jamii sehemu mbalimbali hapa nchini na hasa third world. Idea ni ile ile kwenda kujifunza kujitegemea, kupambana na taabu, kusaidia walio na dhiki kuliko wewe nk. Japo sasa wanaoenda ni wachache, hii ni kwasababu ya gharama na wala sio kutokuwa na maana. Wenye vipato bado wanaenda, hata prince William alienda huko South America na kwa mara ya kwanza kujifunza kusafisha nyumba, kukata kuni mpaka kujipikia.

Ukisoma hapa wanaopinga wengi ni wale ambao hawajapita JKT. Ni kweli kabla ya kwenda JKT mtu ulikuwa unaogopa sana lakini baada ya kufika hiko na kumaliza unagundua kuna mengi ya faida umejifunza kuliko taabu ulizopata.
 
Mtanzania, si kuhenya tu na Kaboya nilienda kumtoa nduli Idi Amin! Wangapi humu wanaweza kusema hilo? Haya ninayoyasema sikusimuliwa.
 
Mkuu kama wewe ulienda kumtoa nduli hakika nakuheshimia kwa hilo na kwa umri, hapo ulipo nahisi hukosi mjukuu! Mie niliingia JKT wakati sera za IMF zimeshaanza kutusigina, karibu miaka 10 baada ya ile vita, na huyo nduli tulikuwa tunamuimba kwenye mchakamchaka na ruti machi:

"Idi Amini wa Uganda
Kaivamia Kagera
Alipoivamia Kagera
Alipigwa ndani ya Uganda.

Kwela mazulu kwela x 4
"

Nyingine:

Kiitikio: "Kimbunga ni cha nini, majeshi kuvamia mpakani?"
-Wazazi nao wauliza wale watoto wetu wamekwenda wapi? (rudia kiitikio)
-Wazee nao washangaa, na wajukuu zetu wanakwenda wapi? (rudia kiitikio),
nk.

Kuna wimbo mmoja wa ruti machi tulikuwa tunaimba:
"Amini akifa siwezi kulia, nitaenda baharini na nigeuke mamba!"

Na pia baadhi ya nyimbo zinazoimbwa na TOT siku hizi kwenye kampeni za CCM melodi zake ni za nyimbo tulizokuwa tukiimba JKT. Kwa mfano kuna ule wimbo unaosema "Wapinzani tuwalete tuwachanechane tuwatupe", sisi kule JKT tulikuwa tunaimba "Idi Amini tumlete tumchanechane tumtupe", hapo TOT wanaposema "CCM tuilete tuikumbatie tuibusu" sie kule JKT tuliimba "Nyerere tumbebe tumkumbatie tumbusu" nk.
 
Ukweli ni kwamba pamoja na kujivunia huo uzalendo tunaodai tulijengewa huko JKT parapanda lilipolia la kwenda kumkabili adui aliyeingia nyumbani kwetu wasomi ( wale wa mujibu wa sheria) waliingia mitini! Walioenda na kupoteza maisha yao wengi wao walikuwa ni volunteers. Hao waliokuwa wanajifanya mabingwa wa kuhenyesha watu, kukimbiza mchamchaka wote walirudi nyuma!

Yote mnayosimulia ni kama vituko walivyovifanya watu wakiwa boarding school. Si vya kujenga uzalendo. Uzalendo si huu mnaousilimuliana humu ndani. Na hautajengwa kwa mtindo uliokuwa wa JKT. Kama kweli tunataka kuujenga itatubidi tuangalia huko wanakotoka hao vijana,namna tunavyowatendea wanapokuwa mikononi mwetu na namna gani taifa litafaidika na wao kufaidika kwa kuwemo kwao katika JKT.
 
Fundi Mchundo,

Mimi nina kaka zangu ambao walikuwa JKT hiyo 78&79 na walienda kupigana vita Uganda. Pia kuna walimu wengi ambao walikuja mashuleni baada ya vita ambao pia walienda kupigana Uganda.

Nafikiri hata Kichuguu kama sikosei ameshawahi kuandika hapa kwamba alienda Uganda kumtoa Amin.

Japo kuna watu walikimbia lakini walioenda kupigana ni wengi zaidi.

Katika kila vita kuna askari ambao wanakimbia, hata JWTZ wenyewe kuna askari ambao walitumia njia mbalimbali kukwepa kwenda Uganda.

Hawa ndugu zetu ambao mlienda JKT mwaka mmoja lakini bila ya kutegemea mkajikuta mnaenda Uganda ni Wazalendo wetu na mlilisaidia taifa letu kumtoa Nduli Amin.

Mkuu tgupe michapo vipi ilikuwaje huko? je hukufikiria kutoroka?
 
Fundi Mchundo,

Mimi nina kaka zangu ambao walikuwa JKT hiyo 78&79 na walienda kupigana vita Uganda. Pia kuna walimu wengi ambao walikuja mashuleni baada ya vita ambao pia walienda kupigana Uganda.

Nafikiri hata Kichuguu kama sikosei ameshawahi kuandika hapa kwamba alienda Uganda kumtoa Amin.

Japo kuna watu walikimbia lakini walioenda kupigana ni wengi zaidi.

Katika kila vita kuna askari ambao wanakimbia, hata JWTZ wenyewe kuna askari ambao walitumia njia mbalimbali kukwepa kwenda Uganda.

Hawa ndugu zetu ambao walienda JKT mwaka mmoja lakini bila ya kutegemea wakajikuta wanaenda Uganda ni Wazalendo wetu na walilisaidia taifa letu kumtoa Nduli Amin.

Unasimuliwa, nilikuwepo. Wasomi walioenda walikuwa wachache sana. Wengi wao walikuwa kwenye kikosi cha mizinga. Wengine ni wale waliotokea kwenye kambi kama ya Nachingwea na hivyo kuchelewa kuwasili Dar es Salaam. Walipofika wakakuta wakati wa kulazimishana umepita. Wengine walikuwa wauguzi, naam, kuna wakina dada walikuwa mstari wa mbele. Wengine madaktari. Hawa wengi wao walikuwa katika sehemu zilizokuwa relatively salama kama kambi ya Kaboya. Serikali ilifikia hatua ya kutaka kuzuia watu kuingia Chuo Kikuu bila uhakikisho kutoka jeshini kuwa aidha uliachiwa kutokana na sababu za kiafya au ulitumikia kikamilifu. Wako walioenda Minziro lakini idadi kubwa walitoroka. Waulize vizuri hao ndugu zako. Watakufahamisha.
 
Bin Maryam.. unaendeleza vizuri hoja lakini kitendo cha kuwaita unaopingana nao kwa hoja si cha kiungwana na ni jaribio dhaifu la kulazimisha hoja. Hoja hujibiwa kwa hoja si matusi au kejeli.

Mwanakijiji:

Mambo mengine tunayofanya yanaonyesha kabisa we are a laughing stock. Kuna watu waliomaliza jeshini na kwenda vyuo au vyuo vikuu kusoma mambo art hawaoni mapungufu makubwa ya JKT.

Lakini kuna watu waliomaliza JKT na kupata bahati ya kusomea Math, science na engineering ndani na nje ya nchi wanaona ni jinsi hizo tulivyo nyuma na tunavyopoteza muda kwa mipango yenye sababu nzuri za kisiasa kuliko za mabadiliko ya kweli.

Moja ya sababu ya kuwalazimisha wasomi na wasomi watalajiwa kwenda jeshini ilikuwa ni kuwafanya wakubali kwenda kufanya kazi katika mazingira magumu vijijini.

Sababu ya pili ilikuwa ni kupunguza migomo ya wanafunzi na wasomi kudai maslahi mazuri yanayolingana na usomi wao. Walichoona wanasiasa ni kutoa mafunzo ya kijeshi ambayo yatawafanya wasomi kuweza kuishi kwenye mazingira magumu kwa kutumia ushupavu na ukakamavu.

Na sababu nyingine ilikuwa ni kuiga tu bila kuangalia wenzetu wanaofanya hivyo walikuwa na nia gani.

Nikianza na sababu ya kwanza, soko la kazi ndilo linalomfanya mtu aende kufanya kazi sehemu fulani na sio ushupavu na ukakamavu wa mwili wake. Kwa mfano wakati wa ukoloni kulikuwa na shule chache vijijini lakini hakuna mwalimu aliyekataa kwenda kufanya kazi vijijini. Kwa sababu mishahara na mazingira ya kazi yalikuwa mazuri watu walikwenda kufanya kazi vijijini bila kuhitaji mazingira ya huko.

Pamoja na Urusi kuwa ni nchi ya Ujamaa, walielewa umuhimu wa soko la kazi kwa undani kabisa. Na kuwavutia watu wafanye kazi katika magumu kama vile frontier za Siberia, Urusi ilitoa maslahi makubwa kwa waliokwenda kufanya kazi huko.

Kwa maoni yangu serikali iache kulipa mishahara kwa kima sawa. Kwa mfano walimu wanaofanya kazi vijijini walipwe mara tatu ya wale wa mjini na tuone nani atakayetaka kukaa mjini.

Kuhusu sababu ya pili, Nyerere ali-model mfumo mzima wa elimu wa Tanzania kufuatana na maisha yake mwenyewe. Alikuwa mtulivu shuleni. Na kabla ya kwenda University alifanya kazi kwanza. Hivyo aliona umuhimu wa wanafunzi kuwa wavumilivu wakiwa shule na kutumia muda wao wa shule kujifunza. Mafanikio aliyaona baada ya wanafunzi kumaliza shule na sio wakati wakiwa shuleni. Kilichowezekana kwake sio lazima kiwezekane kwa mtu mwingine.

Kwa maoni yangu, wanafunzi wa Tanzania wanatakiwa wa-enjoy maisha yao wakiwa shuleni na vilevile kuwa na nafasi ya kuchagua vile wanavyotaka kufanya baada ya shule. Mpaka sasa wanafunzi wa Tanzania wana mitaala mibovu isiyoangalia matarajio ya wasomi wenyewe na vilevile kuinua kiwango cha ubunifu. Kwanini mwanafunzi aliye Stanford University au MIT, anaweza kufanya kazi ya ziada na mwanafunzi wa UDSM hawezi kupata muda huo.

Kuhusu sababu ya tatu. JKT ilichukua model ya makambi ya Kibbutz zilizopo Israel. Israel ni nchi iliyoundwa na wayahudi kutoka mataifa mbalimbali. Na makambi ya Kibbutz yatoa nafasi kwa watu hawa kujifunza kuishi pamoja.

Kuna ukweli kuwa watanzania ni watu wa makabila tofauti. Lakini pamoja na tofauti zetu tulishaishi pamoja kwa karne nyingi. Tulikuwa na lugha moja na kipato kilikuwa hakipishani sana. Vilevile tuliiga bila kuangalia kwa undani mkubwa falsafa ya Kibbutz. Wayahudi wengi walihamia Israel walitoka nchi za Ulaya mashariki na walikuwa na siasa kali za kijamaa zinazokataza matabaka. Hata matabaka ndani ya familia yalikatazwa. Kwa mfano mtoto kutumia maneno ya baba na mama yalikatazwa kwa sababu yalionekana kama ni tabaka. Hivyo mtoto alimwita baba au mama yake kwa kutumia majina yao.

Mwisho kabisa ni kuwa Israel na nchi nyingine zilikuwa na bajeti za kuendesha makambi yao. Pamoja na makambi yetu kuwa na shughuli mbalimbali za uzalishaji, hazikuweza kujiendesha bila kutegemea bajeti za serikali.
 
Ukweli ni kwamba pamoja na kujivunia huo uzalendo tunaodai tulijengewa huko JKT parapanda lilipolia la kwenda kumkabili adui aliyeingia nyumbani kwetu wasomi ( wale wa mujibu wa sheria) waliingia mitini! Walioenda na kupoteza maisha yao wengi wao walikuwa ni volunteers. Hao waliokuwa wanajifanya mabingwa wa kuhenyesha watu, kukimbiza mchamchaka wote walirudi nyuma!

Yote mnayosimulia ni kama vituko walivyovifanya watu wakiwa boarding school. Si vya kujenga uzalendo. Uzalendo si huu mnaousilimuliana humu ndani. Na hautajengwa kwa mtindo uliokuwa wa JKT. Kama kweli tunataka kuujenga itatubidi tuangalia huko wanakotoka hao vijana,namna tunavyowatendea wanapokuwa mikononi mwetu na namna gani taifa litafaidika na wao kufaidika kwa kuwemo kwao katika JKT.

Mkuu hii ya wasomi kuingia mitini wakati wa kwenda kufa mbona mie naiona ni natural response kabisa! Hata mie ningekuwapo huko wakati huo ningelala mbele! Kama kwenda shambani Embakasi au "Dunia" tulikuwa tunalala mbele kama hatuna akili nzuri, sembuse suala la uwezekano wa kulambishwa mchanga, hapo mkuu usingeniona, ndio maana nimekupongeza sana kwa kushiriki kwako katika vita, naamini ulishiriki kwa hiari, na kama ulilazimishwa nakupa pole mkuu. Unajua kijana anayejiunga JKT kwa mujibu wa sheria, amemaliza form six na matarajio ya kwenda university akajitafutie taaluma ya kumsaidia maishani ni tofauti sana na wale waliokuwa wakiitwa volunteers. Mie kwa mfano nilipoingia JKT nilikuwa na umri wa miaka 22, nilikuwa na matumaini makubwa katika maisha yangu ambayo sidhani kama ningekubali kwenda vitani kufa wakati nafasi ya chuo kikuu ilikuwa mbele yangu na niliamini ingenipa maisha mazuri. Kuchagua maisha is a very natural choice. Wale volunteers wengi walikuwa hawana matumaini makubwa na future yao, kwa hiyo ilikuwa muhimu "wajipendekeze" kwa jeshi ili angalao wakimaliza muda wao liwafikirie katika ajira, kwa hiyo kwao kwenda vitani kungewaongezea cv na sifa za kuajirika. Wale "wasomi" nadhani hawakuhitaji sifa ya kupigana ndipo waende chuo kikuu, kilihitajika tu cheti kuwa wamepitia JKT. Kwa hiyo kitendo cha "volunteers" kuchangamkia kwenda mstari wa mbele sidhani kama kinawapa sifa ya kuwa ati ndio bora zaidi kuliko wenzao hao "wasomi", bali hiyo ilikuwa ni opportunity waliyoichangamkia zaidi kwa kuamini ingewafaa baadae, kwa hiyo kwangu wote (volunteers na mujibu wa sheria) walikuwa opportunistic kwa namna walivyo-respond kwa wito wa kwenda kupigana. Kwa hiyo mkuu nakuomba usiwasute sana hao wenzio "waliolala mbele"!
 
Haujanielewa. Mimi siwasuti waliokimbia kwenda kupigana. Kwani unauhakika gani kuwa mimi sikuwa mmoja wao? Point yangu ni kuwa huo uzalendo unaodaiwa kujengwa katika JKT unatiwa chumvi. Waliojikuta wanakuwa mashujaa ni wale ambao wengi wao walikuwa hawana jinsi na si kwa sababu ya mapenzi na nchi yao! Wako wachache ambao mapenzi ya dhati yatawapeleka kuhatarisha maisha yao kwa ajili yake.
 
Hapa nakubaliana na wewe mkuu. Naona katika dhana nzima ya JKT, ends na means zilipishana. Lakini bado katika kupishana huko kuna faida za wazi sana tuliozipata tuliokwenda huko, ingawa baadhi ya matokeo hayakuwa yale yalokusudiwa. Kuna mambo yanayokusudiwa na bado yasiwafae wakusudiwa, na yapo yasiyokusudiwa lakini yakawafaa wanayokutana nayo. Yote haya tuliyakuta huko JKT. Tunaihitaji JKT leo? Jibu langu ni NDIYO, lakini si kwa sababu za mwaka 1963 lilipoanzishwa na si kwa njia zilizotumika wakati huo, bali kwa sababu za karne ya 21 na means za karne ya 21.
 
Mpaka leo nashukuru kupitia JKT. Experience hiyo imenifanya kuwa na edurance katika maisha.
 
Haujanielewa. Mimi siwasuti waliokimbia kwenda kupigana. Kwani unauhakika gani kuwa mimi sikuwa mmoja wao? Point yangu ni kuwa huo uzalendo unaodaiwa kujengwa katika JKT unatiwa chumvi. Waliojikuta wanakuwa mashujaa ni wale ambao wengi wao walikuwa hawana jinsi na si kwa sababu ya mapenzi na nchi yao! Wako wachache ambao mapenzi ya dhati yatawapeleka kuhatarisha maisha yao kwa ajili yake.

Fundi:

Chukua tano. JKT haijengi uzalendo wowote ule. Kama ingekuwa inajenga, viongozi wengi waliopo madarakani sasa walipitia JKT na sioni uzalendo wao.

Kuna vitu vinafanyika kwa muda mrefu katika jamii na baadaye kuwa jadi au mila. Lakini ukiuliza jamii husika nini faida ya jadi na mila zenyewe wanakuwa hawana maelezo yoyote ya maana.

JKT ni jadi ya watanzania lakini haikuwa na maana yoyote 1963 au leo. Serikalini nyingi duniani zinakuwa ni mradi iitwayo WHITE ELEPHANT. Miradi inafanyika lakini haina maana yoyote.
 
Mpaka leo nashukuru kupitia JKT. Experience hiyo imenifanya kuwa na edurance katika maisha.

Kwanini serikali ichukue majukumu ya wazazi wako ambao walitakiwa wakufanye wewe kuwa na endurance katika maisha? serikali sio baby sitter, kama wazazi wa mtoto hawataki kuchukua majukumu ya kulea watoto wao, basi itakuwa ni wajibu wa mtoto to reach stars on his/her own steam.
 
JKT ilisaidia kwa kiasi kikubwa kuleta,japo kwa muda mfupi, hali ya vijana kushirikiana bila kujali hali za kwao. Nakumbuka kulikuwa na watu ambao walikacha miaka ya 70, darasa la saba (volvo), form 4 waliomaliza kozi za zaidi ya mwaka mmoja na pia form 6. Wote hawa waliunganika katika moja mbinu za kukacha. Ni wazi, kama ilivyo sehemu yeyote ile, kuna ambao ilikuwa suluba kwa kukosa mbinu au kuwa na bahati mbaya ya kushikwa kila fiat 682 la makao makuu likija na mizigo kwenda kupakua!! Faida ya JKT haiwezi kupimwa in monetary terms. Binafsi sijutii kupitia JKT na sikuathirika kielimu kwani it was a needed break and a good lesson.
 
Fundi:

Chukua tano. JKT haijengi uzalendo wowote ule. Kama ingekuwa inajenga, viongozi wengi waliopo madarakani sasa walipitia JKT na sioni uzalendo wao.

Kuna vitu vinafanyika kwa muda mrefu katika jamii na baadaye kuwa jadi au mila. Lakini ukiuliza jamii husika nini faida ya jadi na mila zenyewe wanakuwa hawana maelezo yoyote ya maana.

JKT ni jadi ya watanzania lakini haikuwa na maana yoyote 1963 au leo. Serikalini nyingi duniani zinakuwa ni mradi iitwayo WHITE ELEPHANT. Miradi inafanyika lakini haina maana yoyote.

Bin Maryam,

Nakubaliana nawe kuhusu suala la kuwa na viongozi "waliopinda" japo walipitia huko JKT, kwamba labda JKT haikuweza kuwasaidia katika suala la uzalendo, kwani badala ya kuwa wazalendo wamekuwa mafisadi. Lakini mafisadi hao hao wana elimu nzuri tu, na dini! Na vyote hivyo havikuwasaidia kuwajengea maadili na kuwaepusha na ufisadi. Sasa hatuwezi kusema ati kwa kuwa kuna jamaa wamesoma na bado wakawa mafisadi basi elimu haisaidii, tuache kusomesha! Au hao jamaa licha ya kuwa na dini bado ni mafisadi, kwa hiyo dini hazisaidii, wanetu tusiwabatize wala kuwapeleka katika madrasa za dini nk! Kwa maelezo haya sidhani kuwa JKT ilikuwa "White Elephant", kuna kasoro zilizofanya mfumo ule ukashindwa kuleta matokeo yaliyokusudiwa katika baadhi ya maeneo kama hayo uliyotaja, lakini bado mchango wake ulikuwa mzuri. Ni mfumo tunaouhitaji wa kutayarisha watu wa kulijenga taifa (na si kujenga matumbo yao kifisadi). Kwa maoni yangu, JKT ni mradi mzuri uliofeli (kutokana na matatizo ambayo wengi wameyasema hapa) kama yaliyofeli mashirika ya umma na Azimio la Arusha. Bado tunalihitaji, haifai sasa kwa kuwa imeshatuponyoka kujiridhisha tu kwa kudai "after all lilikuwa baya!" hiyo itakuwa dhana ileile ya "sizitaki mbichi hizi". Tunahitaji JKT, ya kisasa, ya karne hii, kwa malengo ya taifa linaloendelea karne hii likitumia resources za karne hii. Tunahitaji kuurekebisha mfumo tutakaochagua wa kuendesha JKT (ama mbadala wake), uwe efficient na ukidhi malengo na mahitaji.
 
Pamoja na juhudi za serikali za kutoa elimu ya bure, namba za wasomi wa kiwango cha juu wanaoweza kubadilisha mchanga kuwa sambusa ni ndogo sana kulinganisha na nchi nyingine za kiafrika. Tuko chini kielimu na hatuwezi kupoteza pesa kwa miradi isiyo na maana.

Kwa mfano nilipokuwa jeshini boot niliyovaa ilitoka uingereza na thamani yake ilikuwa 15 Pounds. 15 Pounds ikiwekwa kwenye lab ya shule ya msingi, sekondary au chuo zitafanya mabadiliko ya juu sana.

Put Your Money Were Your Mouth Is. Kwa kipindi cha sasa Tanzania inatakiwa kutumia kiasi kidogo tulichonacho kwenye mambo ya elimu na energy kwa hizo ndizo challenges za 21 Century.

Kuhusu mifano yako ya elimu na dini haina uhusiano wowote na JKT. Elimu haikufundishi ethics, imekazania michepuko. Hivyo unachokiona ni mapungufu ya elimu nzima. Kuhusu dini, dini ina manufaa kwa mtu binafsi na sio ya taifa. Hivyo mfuasi wa dini ana choice ya kipi akifuate.

Katika masuala ya kitaifa. Ni lazima tuangalie ni equation gani itatupa short cut katika masuala ya maendeleo na sio kuwa na miradi ya kuzungukazunguka.
 
JKT ilisaidia kwa kiasi kikubwa kuleta,japo kwa muda mfupi, hali ya vijana kushirikiana bila kujali hali za kwao. Nakumbuka kulikuwa na watu ambao walikacha miaka ya 70, darasa la saba (volvo), form 4 waliomaliza kozi za zaidi ya mwaka mmoja na pia form 6. Wote hawa waliunganika katika moja mbinu za kukacha. Ni wazi, kama ilivyo sehemu yeyote ile, kuna ambao ilikuwa suluba kwa kukosa mbinu au kuwa na bahati mbaya ya kushikwa kila fiat 682 la makao makuu likija na mizigo kwenda kupakua!! Faida ya JKT haiwezi kupimwa in monetary terms. Binafsi sijutii kupitia JKT na sikuathirika kielimu kwani it was a needed break and a good lesson.

Kama ulikuwa unahitaji break na mafunzo. Kwanini usirudi nyumbani kwa wazazi wako na kupumzika? Kwanini likizo yako iingizie gharama serikali?
 
pamoja na mazuri ambayo yalitokana na jkt, lakini si vyema kukataa au kujifanya vipofu kwa yale mabaya yaliyotokea jkt.

tunakataa kujifunza utoro lakini tunajisifu kujongo, tunakataa kujifunza uongo lakini tunajisifu kudanganya uanamichezo wetu na tunaita mbinu za medani, tunakataa kujifunza kuita watu malaya, wezi nk lakini tunajikumbusha kwa mapenzi nyimbo za mchakamchaka,
tunaita wadada zetu wapenda shushu lakini tunasahau sulba ambazo baadhi ya wadada walizipata ili kuwalazimisha kutoa "vitu" na kwa wale waliogangamala tunasahau vidonda vya kisaikolojia ambavyo walivipata.

nasema tena jkt ilikuwa na mazuri yake lakini kama nikiambiwa irudi leo ningependa isije kama ile niliyopitia mimi bali iwe na mabadiliko muhimu.
 
Back
Top Bottom