JKT kurejeshwa, wazo zuri au limepitwa na wakati?

mhhhhh ha ahaha haha haha...hapa najua tutasikia mengi na kudanganywa tutadanganywa najua...haya ongezeni chumvi mtutie wivu!

Koba...Ijumaa leo kaka....
We hujamstukia tu Mwanakijiji....? Jiulize tu mwenyewe ufisadi na JKT vinahusiana nini?
 
Honestly, ijapokuwa sikupita JKT, hata ikitokea sasa hivi wakaita vijana kwenda JKT nahsisi nitakuwa wa kwanza kuripoti...sijui hasa ni kwa sababu gani lakini kuna kitu kwa ndani kinaniambia JKT was a good thing, hivi nilisikia serikali ilikuwa na mpangoi wa kureintroduce JKT kama kitu cha lazima imeishia wapi?
 
JKT ilinipotezea muda wa mwaka mzima kabisa. Vile vile ilinifanya nikosane na kimwana wangu tuliyekuwa tumekutana high School na kuahidiana kuoana (kama kweli ahadi hiyo ilikuwa serious). Jambo nililochukia JKT zaidi ilikuwa ni ile tabia ya watu kuwa na discipline ya woga na unafiki ambao ulikuwa unatokana na yale mafunzo ya msuli yaliyokuwa yakitolewa.

Hata hivyo JKT ilinikutanisha na watu wengi sana na kunifanya nijifunze mengi sana kuhusu jamii yetu. Ingawa sasa hivi sikumbuki hata mtu mmja kati ya marafiki hao niliokutana nao JKT, kwa miaka mitano ya kwanza tangu kumaliza JKT nilikuwa nakutana nao sana na walinisaidia sana kujenga network yangu hapo Dar.

Jambo ninalokumbuka sana ni pale nilipomaliza mafunzo ya ukamanda pale Ruvu na kupewa tepe moja ya kijani na kupandishwa cheo kutoka Serviceman na kuwa "Volunteer Lance Corpolar" au "Green Kwanja." Kwa miezi sita niliyotumia cheo hicho cha V-L/Cl niliwafanya kuruta walioinngia Januari waione JKT kama sehemu ya mafunzo zaidi ya mateso; sikuhimiza discipline ya woga na nilikuwa mkali sana ninapopewa nidhamu ya ya kinafiki. Kwa bahati mbaya juhudi zangu zilikuwa ni kama punje ya mchele kwenye gunia zima; laiti wale makamanda wengine nao wangejifunza kwangu namna ya kuwafundisha kuruta wale kiakili na kijamii zaii ya mafunzo ya msuli tu.
 
Kwa mtazamo wangu JKT kweli ni kupoteza muda na wakati kama si kujifunza wizi, uongo, umalaya na kugombana na maafande.

Umoja na mshikamano katika Tanzania tumefundishwa toka tukiwa mashuleni kwa kupitia somo la siasa kwa wale wazee wenzangu na kwa sasa wanaita jina lingine.

Tanzania ilikuwa inahimiza sana umoja na mshikamano (Pitia katiba ya TANU) na kidogo pia katika katiba ya CCM.
Nyimbo nyingi tulizoimbishwa JKT pia tulikuwa tunaimba mashuleni katika Mchakamchaka nk. Pia katika baadhi ya mikoa tulikuwa na chipukizi, game scouts, Tanu youth league nk.

JKT ni kupoteza muda na wala si lolote zaidi.

Hey, you see waste, I see opportunity, lets move on tusubiri kutoa mazao ya talanta!
 
MKJJ,

mbona unaleta uchokozi tenaaa.........Kwa kweli Jeshi ilikuwa saafi sana, wengine humu tulifahamiana JKT, na hata huku mtaani tumekuwa tukishirikiana kwa baadhi yetu........i can't find words kuelezea uzuri wa JKT.........watu tulifanya kazi kwa bidii, na kama asemavyo Rev...........ule Moyo wengi wetu tukiuendeleza......hii nchi itapiga hatua sana tu........... very unfortunate kuna VIRUS anaitwa CORRUPTION + UFISADI......

Tukidhamiria tutashinda
 
Lakini Mwanakijiji kauliza swali kama JKT lilikuwa ufisadi? Mpaka sasa hamna mtu aliyejibu zaidi ya kutoa stori....
 
Lakini Mwanakijiji kauliza swali kama JKT lilikuwa ufisadi? Mpaka sasa hamna mtu aliyejibu zaidi ya kutoa stori....

KUna mchangiaji mmoja , nadhani anaitwa Kisura, kauliza relevance ya neno fisadi hapa ni nini? hakuna haja ya kurudia

Muhimu kakumbusha mambo ya JKT ndo naona watu wakijikumbusha maana its just too emotional,,,xperience ambayo mtu usingependa kuikosa....uzalendo wangu ungekuwa 105% nadhani ningepeta bahati hiyo
 
MKJJ bwana....., kwani hatukujui kama wewe ni mojawapo waliolia walipofuta hii kitu, unawa-enjoy wenzako bure tu ili wajione mpo wengi mnaopinga. Tupo wachache sana tusiokubaliana na hii kitu. hivi Kenya hawakuwahi kuwa na hiki kitu kumbe, ndio maana jamaa wanajua sana kupauka, self-discipline sifuri kabisa.
 
JKT ilinipotezea muda wa mwaka mzima kabisa. Vile vile ilinifanya nikosane na kimwana wangu tuliyekuwa tumekutana high School na kuahidiana kuoana (kama kweli ahadi hiyo ilikuwa serious). Jambo nililochukia JKT zaidi ilkikuwa ni ile discipline ya woga na unafiki ambao ulikuwa unatokana na yale mafunoz ya msuli yaliyokuwa yakitolewa.

Hata hivyo JKT ilinikutanisha na watu wengi sana na kunifanya nijifunze mengi sana kuhusu jamii yetu. Ingawa sasa hivi sikumbuki hata mtu mmja kati ya marafiki hao niliokutana nao JKT, kwa miaka mitano ya kwanza tangu kumaliza JKT nilikuwa nakutana nao na walinisaidia sana kujenga network yangu hapo Dar.

Jambo ninalokumbuka sana ni pale nilipomaliza mafunzo ya ukamnada pale Ruvu na kupewa tepe moja ya kijani na kupandishwa cheo kutoka Serviceman na kuwa "Volunteer Lance Corpolar" au "Green Kwanja." Kwa miezi sita niliyotumia cheo hicho cha V-L/Cl niliwafanya kuruta walioningia Januari waione JKT kama sehemu ya mafunzo zaidi ya mateso; sikuhimiza discipline ya woga na nilikuwa mkali sana ninapopewa nidhamu ya ya kinafiki. Kwa bahati mbaya juhudi zangu zilikuwa ni kama punje ya mchele kwenye gunia zima; laiti wale makamanda wengine nao wangejifunza kwangu namna ya kuwatraini kuruta wale kiakili na kijamii.

Pole mzee kwa kupoteza waridi la milele!:(
 
Lakini Mwanakijiji kauliza swali kama JKT lilikuwa ufisadi? Mpaka sasa hamna mtu aliyejibu zaidi ya kutoa stori....

Ulikuwepo sana hasa kwenye ngono, watu kibao walivunja uchumba na inasemekana kama ingeendelea hali ya VVU ingekuwa mbaya zaidi.
 
mwanakijiji you are not serious today. Kama kuna kitu kinachonipa raha ninapokumbuka historia ya maisha yangu basi si kingine ila ni JKT. Nani anawakumbuka kina Afande Mtono wa Mlale na Mlay wa Mafinga? Sikumbuki kama niliwahi kuwa na uvumilivu katika maisha kama wakati ule. Halafu ilikuwa ni burudani ya pekee kwa makoplo kuongea kiingereza cha kuvunja ili waonekane na wao ni wasomi.

Nakumbuka koplo mmoja alinotolea mpya aliponiamrisha kuchanganya chakula changu na cha kuruta mwingine kwenye mustini (sic) moja ile nimpatie mustini yangu: Akaja na hii kali: "wewe rikututa, confuse chakura chako na cha mwenzio kwenye mustini moja nataka hiyo mustini yako niitumie. Umesiki?"

Nurujamii,

Sisi tulikuwa Mafinga kwa Afande (CO) Mlay. Basi tulikuwa tunazalisha sana mahindi, mboga na kujenga nyumba za jenshi na licha ya baridi ya Mafinga- sikumbuki mda I enjoyed my life ktk nikiwepo JKT!

Basi siku moja tulitoka shamba Idetero kule Saw Hill tumechoka- wakawa wamemwandika CO kwenye magazeti- sasa tulipigwa 'Dril' kali wote- basi tukakubaliana watu watatu wajifanye 'wafaint' watatu- ndo yule CO akaotuonea huruma- ndo tukapona!

Sikuwahi kuona mtu strict kama CO Mlay- na hii imenifundisha uvumivilvu sana wa kupambana ktk maisha!

Actually ile miezi 3 ya mwisho tulinenepa sana na hata nilipofika home- watu hawakuamini kama jeshi kuna mateso!

Well JKT was a good opportunity- a must to Tanzanian youth- those who were not given such opportunity=- they must be missing something!

Je mnakumbuka 'green vest ya kijani?' na ukisema huna 'appetite' basi afande anakuambia azima kwa mwezio?? JKT ilikuwa burudani tupu!

Mimi nyimbo za kizalendo kama 15 au zaidi nazozijua leo hii tulijifunza JKT!
 
Lakini Mwanakijiji kauliza swali kama JKT lilikuwa ufisadi? Mpaka sasa hamna mtu aliyejibu zaidi ya kutoa stori....

You need to know the character of Mwanakijijito figure out the relationship of JKT and Ufisadi.

Ndio maana wengine tumeng'amua mtego wake na kuanza kuhubiri "mema" na wengine kulalamika!
 
Kenya hawakuwa na JKT na wamekuwa nchi nzuri tu, tena iliyoendelea kiuchumi. Muda mrefu ambao wengi wetu tungekuwa tumeshamaliza elimu ya juu tulitakiwa kwenda kuchimba mitaro, mahandaki, kujenga nyumba, kuchoma matofali na wale waliokuwa ruvu watakumbuka mpunga!

Kama ningetaka kujenga nyumba au kulima mashamba ningefanya ya kwangu mwenyewe. Mbona sasa hivi watu hawalazimishwi kwenda JKT lakini bado wana uzalendo? Nadhani ile ilikuwa ni hofu ya vita baridi zaidi kuliko kitu kingine chochote.

Mwanakijiji,

Inaelekea huijui JKT na hivyo hujui hata faida zake. Kila nikiangalia vijana wa siku hizi, nagundua kweli katika vitu muhimu nilivyopitia ni pamoja na JKT.

Imetufanya wengine tuweze kuishi popote duniani bila matatizo makubwa.

Nitachangia zaidi nikipata muda.
 
JKT tulikuwa tunafundishwa uwongo, umalaya, wizi, nidhamu ya woga na unafiki na wala si kingine.

Matokeo ya mafunzo hayo ya JKT leo hii tunayaona dhahiri kwamba Taifa limejaa viumbe waoga ambao wanashindwa ama wanaogopa kudai haki zao kisheria.

Tazama nchi inavyoendeshwa leo hii, wananchi ile kuandamana tu kuonesha kwamba hawafurahishwi na hali iliyopo inakuwa ngumu. Huo ni woga na wala si uzalendo kama mnavyodai hapa.

JKT ilikuwa ni nyimbo za kumsifu Nyerere, Chama na viongozi wa chama tawala na kukutisha wewe kijana kwamba bila Nyerere, Chama tawala na viongozi wa chama hicho basi hakuna la maana litakalotokea Tanzania.

Pia JKT ilitumika sana katika kutunywesha maji ya bendera ya CCM kinguvu, kutuvunja matumaini ya kuweza kujitawala, kutunyima uhuru wetu kifkra (kimawazo).

JKT serikali ilikuwa inatumia pesa nyingi kuliko mapato yaliyokuwa yanapatikana kutokana na shughuli za uzalishaji makambini humo.

tulichotakiwa kukifanya katika kipindi kile cha mwaka mzima ni kuwatuma vijana wetu waende kufanya kazi kwa kujitolea tokana na fani zao walizosomea. Kama umesomea ubwana mifugo basi ukafanye kazi ya ubwana mifugo chini ya mtaalam wa mifugo bila mshahara, ila upatiwe maradhi, chakula nk. Lakini JKT ilivyokuwa ni kwamba unapelekwa kambini ambako unakutana na afande (standard seven), kwanza anawivu na wewe umesoma, maelewano madogo zaidi ya kuongopeana na kuogopana, kupeana mateso yasiyo kichwa wala miguu wakidai huo ndiyo ukakamavu.

Kama lengo la JKT (Jeshi La Kujenga Taifa) ni kujenga taifa, sasa kwanini kuna kupigana mikwara na maafande?. Kwa nini makambi yalishindwa kujiendesha yenyewe ama kujitegemea?.

Kwa upande wangu there is no way I will send my kids to JKT kama itarudishwa leo hii hata kwa mtutu wa bunduki.
 
Mtambo,

Mimi sikufundishwa uongo, umalaya, wivu, wizi, unafiki au woga. Wewe ni muongo na mzushi kwa kusema hili! Na kama haya ndiyo uliyotoka nayo ulipokwenda jeshini, basi wewe ni utashi wako binafsi kuwa ulihitimu kwa wizi, umalaya, woga na unafiki. Hongera sana!

Hivi ni Watanzania wangapi walipitia JKT mpaka uoanishe na maandamano? Je ni mafanikio na mazao gani ambayo JKT iliyapata kwa Taifa ambayo unayapinga?

Kuhenyeka ni kawaida katika chombo kama jeshi, Hata Marekani, Urusi na Israeli ambako ndio walituundia JKT na mfumo mzima wa JKT, ukiwa kuruta hata kama una Phd, utakurupishwa.

Jeshi halifundishi nidhamu ya woga au utiifu tuu kwa ajili ya vyeo. Linafundisha mambo mengi sana ndio maana utaona wale waliopitia Jeshini wengi wao wana nidhamu ya hali ya juu na si suala la woga pekee.

Haya ya uzinzi, utoro, ubangaizaji ni ya kawaida ya jamii na si JKT ya kulaumiwa.

Ikiwa Binti yako akiamua kuwa mwachiaji basi tukupe wewe lawama kwa kuwa ni Baba? Je yeye hastahili lawama kwa kushindwa kufuata mafundisho yako? ni vipi kama yeye akimtumia hausi gelo anachumpa kwenda viwanja kujirusharusha huku wewe umeangusha gari zito kutokana na uchovu wa kujibishana na Rev. Kishoka? Je anapozembea kuosha vyombo au kufua nguo zake ni wewe ubebeshwe lawama zote?

Kila kitu dunia hii kina mafanikio na mapungufu. Tukianza angalia mapungufu, tujiulize ni yapi tulikuwa na uwezo wa kuyatatua kabla ya kuwa mapungufu! Jee tumejifunza nini kutokana na mapungufu? je tuna mbinu mpya za kurekebisha hayo mapungufu ama tutainua mikono juu na kusema "mapungufu" haya ni makubwa sana, tuache tusijisumbue kutatua?
 
Yeah, kids used to be so apprehensive - those first days - oooh, the first day you enter that camp, pale pale hata kabla hujakaa sawa afande wanakudaka/wadaka na kuwahenyesha. Vifurushi/vikoba hamjaweka sawa, mnaambiwa mguu sawa na kelele nyiiiingi, na kuhenyeshwa na kiafande cha darasa la saba/nane. Kiburi kinakatika in a day or two.
By the time mnaambiwa nendeni nyumbani, wengine hawataki kuondoka kwa mazoea ya maisha na urafiki uliotokana na njia hii!

Huo ulikuwa ni wakati mrwa kweli kweli katika uhai wa kijana wa kiTanzania. Silaumu na sisikitikii muda huo nilioutumia huko JKT.
 
Kuna vitu ambavyo namuunga mkono Nyerere lakini hili lilitupotezea muda wa mwaka mzima kusota kwenye mitaro na yare "maafande".

Mkuu Mwenzangu kweli ulikwenda huko au? Mkuu mimi nilikwenda Oljoro, chini ya Mnauye, na baadaye Major Kahamsini, under Surgent Mwaligunga, chini ya Luteni Kitila, mkuu bila ya zile shuruba za kunywa uji wa chumvi, nisingeweza kupanda meli. Ninasikia uchungu kuwaona vijana wa kisasa ambao hawakwenda huko maana kuna something wana-misss kikubwa sana kwenye ku-excute ideas na malengo ya maisha yao, nikiwaangalia ninawonea huruma sana maana wale tulioenda tulipata direction, pamoja na discpline ya maisha, ukakamavu, uvumilivu, kuheshimu wenzako maana kule wote tulikuwa panya tu, hakuna cha mtoto wa nani wote tulikuwa sawa,

Kama kuna ninachokubaliana na Mwalimu, ambayo huwa ni machache sana, hili ni moja. Again, JKT was fun, maana some very expensive chiks kwenye real life kule walikuwa ni kawaida tu, and I surerly had fun, muziki wa bila gharama, oh no that was fun, mkuu hata tulipoambiwa kuwa inakaribia kwisha bado nilikuwa na hamu ya kuendelea angalau kidogo,

Mkuu MMJ, baada ya kusoma bure kuanzia Vidudu, Primary School, Secondary School, na High School, ilikuwa ni lazima somehow kulilipa taifa, kwa njia moja au nyingine, and I am proud kwamba I was able to do that, yaaani kulilipa taifa langu, ingawa most of the time nilikuwa kwenye timu ya soccer ya kikosi, lakini pia nililima sana mashamba kule karibu na tajiri Mollel, kwa hiyo mkuu kama hukwenda, ulikosa sana mkuuu!
 
JKT tulikuwa tunafundishwa uwongo, umalaya, wizi, nidhamu ya woga na unafiki na wala si kingine.

Matokeo ya mafunzo hayo ya JKT leo hii tunayaona dhahiri kwamba Taifa limejaa viumbe waoga ambao wanashindwa ama wanaogopa kudai haki zao kisheria.

Kama lengo la JKT (Jeshi La Kujenga Taifa) ni kujenga taifa, sasa kwanini kuna kupigana mikwara na maafande?. Kwa nini makambi yalishindwa kujiendesha yenyewe ama kujitegemea?.

Kwa upande wangu there is no way I will send my kids to JKT kama itarudishwa leo hii hata kwa mtutu wa bunduki.

Ninajiridhisha kuwa hukwenda JKT wewe! Yaelekea hizi stori wewe umesimuliwa.
Umalaya, wizi , uongo ni hulka ya mtu binafsi, tazama vyuo vikuu, mashuleni, n.k umalaya umejaa wa kutupwa.
Kuimba nyinbo za ccm and the likes wakati wa mchaka mchaka, disco au wakati wowote (kuruta zaidi ya mmoja) ulikuwa hulazimishwi kuimba.
Kuhusu uongo, uongo uliokuwa kule ulikuwa wa kujidefend wewe mwenyewe, mfano umebambwa ulikuwa unatoroka, utasemaje?

JKT ilikuwa bomba!
 
Back
Top Bottom