JKT kurejeshwa, wazo zuri au limepitwa na wakati?

green29

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
311
41
JKT ilianzisha na Israel na hata sasa wanafufua JKT kwa kuwashirikisha.

Mzee Madela wa madilu point yako katika thread ya Ubalozi wa israel imenikumbusha kitu muhimu sana kuhusu jeshi la kujenga Taifa JKT na ule utaratibu wa vijana wote kupitia huko. Sisi wengine hatukubahatika kupitia huko japo wakati mwingine tunadandiaga stori za huko kwa style ya Brazameni.

Sina hakika kama mada kama hii imeshawahi kujadiliwa lakini ningeomba tutoe maoni na mchango wetu labda wahusika wanaweza kupata points flani hapa ili iwapo kutakuwa na sababu ya Kurudisha JKT basi iwe na manufaa kwa Taifa.

Nyakati zinabadilika na mahitaji pia huwa yanabadilika. Inawezekana kabisa sababu za kuwa na JKT miaka hiyo hazitoshi tena kuhalalisha kurudisha hili jeshi.

Je makusudi ya kuanzisha JKT miaka hiyo yalikuwa ni yapi? Nilisikia kuwa JKT ilifutwa sababu ya gharama kuwa kubwa. Hii ilinifanya nijue kuwa JKT haikulenga kuzalisha mali bali kuwafundisha vijana kuzalisha mali; au inawezekana ililenga kuzalisha mali lakini ikashindwa kufikia malengo. Swali kubwa ni kuwa JKT inataka irudishwe kwa makusudi mapya au hayohayo ya mwanzo? JKT ikirudishwa itawezaje kuisadia nchi yetu na vijana kwa ujumla?

Nilikuwa naongea na kijana mmoja toka Ghsna akaniambia huko kwao wana utaratibu wa Kufanya kazi kwa mwaka mmoja kuchangia maendeleo ya jamii mara baada ya kumaliza masomo ya sekondari, vyuo vya ufundi, afya, au chuo kikuu. Ni kama kazi za kujitolea lakini wanakuwa wanalipwa posho flani kuwawezesha kujikimu. Na hii wamelenga kufikisha huduma za elimu, na afya maeneo amabayo bado hayajafikiwa.

Kwa Tanzania hivi karibuni wameanzisha mtindo wa kuwapa mafunzo ya mwezi mmoja vijana waliomaliza kidato cha sita kisha wanawapeleka kufundisha sekondari kwenye maeneo ya vijijini ambayo hayana walimu wa kutosha. Mpango huu kwa kiasi flani "umesaidia" kupunguza tatizo la walimu japo kwa mtazamo mwingine umeonekana ni mpango unaoshusha kiwango cha elimu.

NI kweli kuna maeneo ya nchi yetu yana hali mbaya sana ukizingatia hakuna incentives kwa wataalam mbalimbali kuishi na kufanya kazi huko. Nakumbuka mwaka juzi wakati wanaajiri wataalam wa afya kwenye BENJAMIN MKAPA HIV/AIDS FOUNDATION, walisema mpango wao umelenga kupeleka wataalamu wa afya kwenye wilaya zenye mazingira magumu na ukosefu wa wataalamu.

Cases nilizozitoa hapo juu zinanifanya nione kuwa JKT inaweza kutumika sio kwa kujifunza gwaride tu lakini pia kutoa mchango wa maendeleo kwenye sehemu za nchi yetu na kwa watanzania wenzetu waishio maeneo ambayo wataalamu wetu wanashindwa kufanya kazi. Serikali inaweza kufanya trade off kwa kugharamia elimu ya juu na kisha badala ya kulipa madeni watu wakafanya kazi ya kujitolea kwa vipindi maalum kupitia JKT. Kuna watu wengi wanapomaliza masomo wanakaa zaidi yamwaka mmoja wakitafuts kazi. Humu wamo madaktari, walimu, manesi, engineers, wanasheria, watu wa ustawi wa jamii, architects, n.k. Na wanapotafuta kazi wanaambiwa wawe na ujuzi.

Kwa maoni yangu zoezi hili litasaidia kupunguza tatizo la wataalamu kwenye maeneo yenye mazingira magumu na pia litawajengea uwezo (uzoefu) wataalam wapya maana itakuwa ni kama internship ilivyo kwa madaktari na wanasheria. Kwa upande mwingine serikali inaweza kuendelea kuwasomesha watanzania bure katika Elimu ya juu kwa makubaliano na kujua kuwa baada ya kuhitimu mtu atawajibika kujitolea kwa mwaka mmoja.

Serikali inaweza kuwalipa wataalam hawa posho za kujikimu kwa kipindi chote cha kujitolea kwa mtindo ambao wizara ya Elimu inafanya kwa walimu wa leseni.

It sounds like siasa ya ujamaa na kujitegemea lakini Ni mtazamo wangu, nakaribisha mitazamo tofauti kwa lengo la kujenga nchi yetu.
 
JKT.

ilikuwa muhimu jana ni muhimu leo na itakuwa muhimu kesho na hata milele.
Mwalimu nyerere aliona mbali sana kuanzisha jeshi hilo.

Jambo moja kubwa lilio ua JKT ni kuingiza siasa jeshini.

Sisi tukiweko Jeshini tulithubutu kuliita Jeshi lakula Tu.

JKT ilianzishwa kwa Kukopi kitu kiitwacho Kibudzi huko Israel.

Vijana wanafundishwa ukakamavu na uzarishaji mali.

JKT Tanzania iligeuka kuwa mtafunaji wa fedha ya serikali.

Fikiria kwamba Jeshi lilikuwa linashindwa kujitoshereza kwa chakula.

Jeshi lilishindwa kujenga nyumba za kudumu za maafande. Kuanzisa Burombora Makutopora, Msange, Behemba mapka Mafinga JKT Maafande wengi walikuwa wakiishi kwenye mbavu za mbwa. Vipi waiishi kwenye mbavu za mbwa wakati kuna vijana zaidi ya 1000 wenye uwezo wa kufyatua tofari kuzichoma kuchora ramani kujenga na kupaua?

Kuna mambo mengi yalikuwa yakiudhi sana.
Mtu alo soma kilimo anapelekwa kupika.
Alosoma ujenzi anapelekwa bustanini.
Alosoma kupika na kushona anapelekwa kujenga banda la mbavu za mbwa.

Kulikuwa na watu wanaitwa walimu wa siasa hilo ndo lilikuwa kundi la watu wajinga kuliko wote jeshini.

Ma OC wengi walikuwa hawana vision hata kidogo. Lile kundi la wasomi wa high schoo na vyuo kwao ma CO lilikuwa ni sawa na nyati au pundamilia kwao hawakufikia hata status ya wanyama wa kufugwa.

JKT kama yalivyo mashirika mengi ya serikali ilibidi ife kwani uligeuka mzigo mkubwa wa kumlemea kila mtu.

Sasa hivi tuna rais Afande lakini kwa kumsikiliza tu unajua kichwani hakuna vision yeyote ila ubabaishaji.
Sisiti kusema Mvuto mkubwa alo nao MH Kikwete ni wa U handsome Boy na si uwezo wa kuongoza na kulikwamua taifa kwenye janga la umasikini.

JKT ina manufaa mengi.
JKT ni kma wet land ambazo kazi yake ni kumeza maji wakati wa masika na kuyaachia taratibu wakati wa kiangazi ili kuwianisha ujazo wa mito na kuzuia mafuriko.
Tumekata miti na kufugia mifugo kwenye wetland sasa tuna mafuriko na ukame.
JKT iliweza chukua vijana wengi wa kujitolea ambao walikaa pale miaka 2 na kugeuka kuwa ngangari kiasi cha kuhitimu na kurudi makwao kufanya mambo ya maana kuliko kuwa mzigo kwa taifa.
madereva wengi wenye nidhamu kwenye mashirika na ofisi za serikali wamepita JKT.
Siku hizi vijana wengi walo hitimu kidato cha 6 hawana nidhamu na moyo wa kujituma na uvumilivu, siyo kwa sababu wanapenda kufanya hivyo la hasha kuna kitu wanakosa. JKT.

Maofisa wa jeshi wa kizazi kipya wanatakiwa kwenda kujifunza operesheni za JKT huko Israel ili wakirudi walifanye Jeshi liwe ni sehemu ya suruhisho la matatizo ya nchi kuliko kuwa mzigo wa taifa.
 
JKT.

ilikuwa muhimu jana ni muhimu leo na itakuwa muhimu kesho na hata milele.

JKT ina manufaa mengi.
JKT ni kma wet land ambazo kazi yake ni kumeza maji wakati wa masika na kuyaachia taratibu wakati wa kiangazi ili kuwianisha ujazo wa mito na kuzuia mafuriko.
Tumekata miti na kufugia mifugo kwenye wetland sasa tuna mafuriko na ukame.
JKT iliweza chukua vijana wengi wa kujitolea ambao walikaa pale miaka 2 na kugeuka kuwa ngangari kiasi cha kuhitimu na kurudi makwao kufanya mambo ya maana kuliko kuwa mzigo kwa taifa.
madereva wengi wenye nidhamu kwenye mashirika na ofisi za serikali wamepita JKT.
Siku hizi vijana wengi walo hitimu kidato cha 6 hawana nidhamu na moyo wa kujituma na uvumilivu, siyo kwa sababu wanapenda kufanya hivyo la hasha kuna kitu wanakosa. JKT.

Maofisa wa jeshi wa kizazi kipya wanatakiwa kwenda kujifunza operesheni za JKT huko Israel ili wakirudi walifanye Jeshi liwe ni sehemu ya suruhisho la matatizo ya nchi kuliko kuwa mzigo wa taifa.

Nashukuru kwa mchango wako Mad-Mad!
NIngependa kufahamu ni mkakati gani uliokuwepo sasa hivi katika serikali kulifufua jeshi la JKT kuna chochote kinachoendelea au ni unfounded wishes tu?
 
Green, Madela wa Madilu,

Hizo point wa Madilu ni nzito!

Jambo moja muhimu zaidi- JKT ilitumuka sana ktk kuleta umoja wa kitaifa, kuondoa ukabila na kujenga uzalendo! Hizi ni faida za kisaasa - na muhimu sana kwa kila taifa duniani.

Tulijifunza nyimbo za Kitanzania, na ukakamavu na uzalishaji pia!

Sii kweli MAdilu, kuwa JKT ilikuwa hasara -mimi nikukuwa Mafinga na tulikuwa na zaida kubwa ajabu ya mahindi, mboga n.k. Tulilisha JKT makao makuu na kuuza- hii ilikuwa wakati wa CO Mlay- sijui yuko wapi sasa hivi- ila nilijifunza uzalendo na uvumilivu kwa hali ya juu nikiwa JKT!

Sababu ingine unajua threat ya Apartheid na aggression ilikuwa sana kubwa ni 60s, 70s, na 80s! Baada ya SA kuondoa aparthied na nchi zote kusini kuwa huru- umuhimu wa JKT 'kujilinda na adui' ulipungua!

Nadhani msumari wa mwisho ni wakati in early 90s IMF na WB walitoa masharti kupunguza matumizi ya serikali- ikiwa pamoja na JKT!

JKT limenimbusha sana mbali! Ni vema Tz ikabuni mbinu mpya ya Mtz anapomaliza chuo kujitolea kwa nchi yake (bila malipo) say kwa miezi 6 na iwe ktk sheria- hii inajenga sana utaifa na uzalendo!

Tonaposema Tz hakuna ukabila- JTK ilichangia sana ktk kutuweka pamoja!
 
Green,

Dawa ya kukopa ni kulipa! Hawa wanafunzi wanaochukua mikopo ni lazima walipe ili kuwa na revolving fund iwe kubwa na wengine waweze kukopa zaidi! Hii isihusiane na JKT!

Hili wazo la JKT au kujitolea kwa nchi ni hiari- na serikali haitakiwi kulipa- may be chakula tu na posho kidogo kujikimu! Halafu sheria inakuwa kwamba huwezi ili kupata ajira onyesha kuwa umejitolea, say kwa JKT au kuwahamashisha wananchi vijini usafi na kutunza mazingira,n.k for 6 months or more! Nchi nyingi duniani bado wana utaratibu huu!
 
Kuna watu walioenda jeshini na wengine hawakwenda. Kuna stori nyingi za kutoka jeshini. Hivi kulikuwa na sababu gani ya kuwapeleka vijana na kuwalazimisha kujiunga na jeshi na kuwapotezea muda ambao wangeweza kuendelea na masomo ya juu. Naamini kama kuna vitu ambavyo vimepoteza muda sana kwa wananchi ni suala la JKT.

Kulikuwa na mazuri lakini siamini kama Nyerere angefanya hivyo kwani wale vijana wote wangekuwa wanafundishwa mambo ya biashara na sayansi badala ya kusota Mpwapwa, Mafinga, Oljoro, Maramba, Ruvu n.k

Kuna vitu ambavyo namuunga mkono Nyerere lakini hili lilitupotezea muda wa mwaka mzima kusota kwenye mitaro na yare "maafande".
 
Last edited by a moderator:
Mimi nina mtazamo tofauti kidogo. Lengo la JKT lilikuwa zuri na kiasi fulani ilisaidia kujenga ukakamavu, uzalendo, usawa (wote tulivaa sare za aina moja, kulala sehemu ziazofanana na kula kwenye Mess tins) na mtandao(Nikipita ofisi mbali mbali TZ hukutana na watu tuliokuwa jeshini pamoja).
JKT ilikuja kuharibiwa kutokana na ubadhirifu na hujuma za waliopewa dhamana ya kuisimamia. Aidha, viongozi na wachache wenye uwezo, nao walichangia kuiua JKT kwa kuwa hawakupenda kuwaona watoto wao wanapata "shida".
I enjoyed my time at the National Service and I am not regreting it-Mpiganaji
 
Kati ya Vitu ambavyo vinanifanya kujisikia nilijitolea na kujifunza uvumilivu wa nchi yangu ni kuwepo JKT!

JKT was one of building blokcs of umoja na utaifa na uzalendo wetu through vijana

Hii kujitolea kwa taifa for 6 months au 1 year iko ncji nyingi tu na ni compulsory!
 
Kenya hawakuwa na JKT na wamekuwa nchi nzuri tu, tena iliyoendelea kiuchumi. Muda mrefu ambao wengi wetu tungekuwa tumeshamaliza elimu ya juu tulitakiwa kwenda kuchimba mitaro, mahandaki, kujenga nyumba, kuchoma matofali na wale waliokuwa ruvu watakumbuka mpunga!

Kama ningetaka kujenga nyumba au kulima mashamba ningefanya ya kwangu mwenyewe. Mbona sasa hivi watu hawalazimishwi kwenda JKT lakini bado wana uzalendo? Nadhani ile ilikuwa ni hofu ya vita baridi zaidi kuliko kitu kingine chochote.
 
Mwanakijiji, I will differ with you from this.

JKT was modern day JANDO and UNYAGO!


JKT was a transitional moment that defined majority of us. The passion that we had for our country and ability to be free from helms of our parents for a whole year. What we learned was how to be indastrious and patriotic. JKT gave us sense of Nationalism and it was at this time when the civic teachings of kuishi pamoja, juhudi na maarifa became almost reality.

We were able to produce quality products using primitive tools and limited resources. Proof of this could be witnessed ay SabaSaba. Tembelea Banda la JKT au Magereza.

Even though after the pass out parade, majority of us left the indastrious attitudes at the gate and we became big headed individuals holding our degrees from UDASA and elsewhere and eventually demanding to run our country. Since we left the skills at the gate, we lost our focus and ability to build cohesive and dynamic institutions that could have resulted in robust economy.

JKT failed due to the fact it was becoming an economic machine despite the internal sabotage and squandering or mismanagement of assets and revenues.

Private enterprise could not compete with JKT, so by powers vested on Mlungula, they were able to convince Wakuu and JKT was declared a failure!
 
Kama kuna kitu ambacho mpaka leo Taifa letu lilikipoteza ni kile cha kila kijana anayetazamia na kujiunga na vyuo vya juu kupitia Jeshi La Kujenga Taifa. Nakumbuka kulikuwa na sisi Volunteers and watu ambao ilikuwa compulsory kwao (form six leavers).

Hiki ni kitu ambacho mpaka leo kinafanya tofauti kati ya raia na jeshi kuwa ndogo kwani wengi tumepita huko huko! Pamoja na kwamba wanajeshi hufanya Mafunzo zaidi lakini wote tuliopita huko tunajivunia kulijua jeshi. Mwanajeshi hawezi kukutishia kuhusu jeshi kwani wote tumelionja!

IMF na WB ndio walioshinikiza jeshi lifutwe kama kitu kilichokuwa kinapoteza hela LAKINI thamani ya mshikamano unaopatikana kwa kupita jeshini na kukutana na watu kutoka sehemu mbali mbali na tabaka mbalimbali ni kitu ambacho huwezi kukiquantify. Fikiri mtu kasoma Kibaha, mwingine huko Kibohehe mwingine Mkwawa na wengine kwenye maseminary...mwisho wa siku wote mnakutana jeshini na kuunga urafiki mkiwa jeshini! Baadaye maishani you bump into each other and though you come from different parts/classes you still know each other! JKT ni sehemu moja iliyosaidia ku"humble" watu. You really got to appreciate that maharage na ugali!

Sielewi hawa IMF na WB kwanini waliamua kutuwekea conditions hizo lakini nchi mbali mbali duniani zina hii compulsory National Service/ Military Service. Baadhi ya nchi hizo ni: Albania, Armenia, Austria, Belarus, Bermuda, Brazil,Chile,China (PRC),Colombia,Cyprus,Denmark, Egypt, Finland, Germany, Greece,Iran, Israel, Korea, South, Malaysia, Mexico, Norway, Poland, Russia,Serbia, Singapore, Sweden, Switzerland,Taiwan (ROC),Turkey,Ukraine.

I don't know with the current terrorism trend in the world kama Western Powers watakubali watu wengi wafundishwe katika jeshi then waachiwe kama ilivyokuwa kwa sisi. Mimi mpaka leo naikumbuka drill ya kupiga LMG vizuri sana na naamini I will perform better in combat than the current university leavers ambao hawakupita jeshini. Uzalendo pia ulijengwa kwa nguvu, wengi mtakumbuka DISCO. Wengi tumejifunza kuimba mbele ya watu na kuongea mbele ya watu bila ya woga tukiwa jeshini.

Nafikiri article hii chini inatoa mwanga kuliko wangu. JKT inaweza kujisustain yenyewe kama tutapata maafande viongozi wenye vision. Such labour force if properly managed can produce wonderful results!!

_________________________ beyond my box ___________________________________

Jean Jacques Rousseau argued vehemently against professional armies, feeling it was the right and privilege of every citizen to participate to the defense of the whole society and a mark of moral decline to leave this business to professionals. He based this view on the development of the Roman republic, which came to an end at the same time as the Roman army changed from a conscript to professional force.[13] Similarly, Aristotle linked the division of armed service among the populace intimately with the political order of the state.[14]
Some ideologies and cultures, and those based on collectivism or statism, value the society and common good above the life of an individual.[citation needed] Those ideologies and world-views justify the state to force its members to protect itself and risk their lives for the common good. In states based on society-centered ideologies, world-views and religions, conscription is the natural way of raising the army.[original research?]
In the era of total war, the conscription is the only alternative for a small nation to build an army of credible strength without depending on alliances. This is particularly the case when the opposing state is significantly larger. In such a case, a voluntary force could not, regardless of its quality, stand against the sheer numbers of the opposing force.[15]
The right of the state to conscript its citizens can be founded on utilitarianist principles.[citation needed] If a greater good would achieved, every thing considered, by sacrificing some soldiers a state should be willing to make this sacrifice.[original research?] This assumes that state have right to use its citizens for achieving greater good for the humankind.
Conscription can give the conscripts a lasting patriotic view and readiness to die for the good of the whole.[citation needed] Such readiness should, according to many world-views, be present in a virtuous citizen at all times, but through training, the readiness becomes a grim reality, not rhetoric.[citation needed] This may decrease the admiration of the military, but may also promote militarism and lead into readiness to use violence in everyday life to solve marital problems.[citation needed] On the other hand, the fact that every person understands that a war - any war - means that they themselves, friends, and relatives will be dying or at the least, facing mortal danger, decreases the willingness to enter an armed conflict.[citation needed] In practice, engaging a conscript force in an aggressive war for a prolonged period results in morale degradation both at home and on the front, testified by Afghanistan and Vietnam Wars.[original research?]

source: http://en.wikipedia.org/wiki/Conscription
 
Kenya hawakuwa na JKT na wamekuwa nchi nzuri tu, tena iliyoendelea kiuchumi. Muda mrefu ambao wengi wetu tungekuwa tumeshamaliza elimu ya juu tulitakiwa kwenda kuchimba mitaro, mahandaki, kujenga nyumba, kuchoma matofali na wale waliokuwa ruvu watakumbuka mpunga!

Kama ningetaka kujenga nyumba au kulima mashamba ningefanya ya kwangu mwenyewe. Mbona sasa hivi watu hawalazimishwi kwenda JKT lakini bado wana uzalendo? Nadhani ile ilikuwa ni hofu ya vita baridi zaidi kuliko kitu kingine chochote.

Na mimi kama baadhi ya waliokutangulia, napingana na hoja yako. Lengo la kuwepo JKT ni zuri na linatakiwe liendelee kuwepo hadi leo na kesho na siku zijazo.

Juu ya jirani zetu wa Kenya, nadhani wao walihitaji chombo cha mfano kama huo ili kuwakomboa kifikra vijana wa vizazi vijavyo. Sasa hivi matatizo yanayoikumba Kenya ni matokeo ya ukabila ambao sote tunaufahamu ulivyo kule Kenya. Wakati wote ninapokuwa nimejumuika na wakenya hutamani na wao wangelikuwa kama watanzania yaani watu wamoja wasiuliza makabila yao. Lakini ukweli kabisa wakenya hutambuana kwa makabila yao kwa mfano utasikia wakisema yule jamaa mkamba jirani yangu amekuja kwangu na yule mtoto wa kiluhya. Na hata wakitaka kusaidiana kwanza wanaulizana wewe ni wa wapi.
Kwetu sisi watanzania kizazi kilichopo hapa tayari kilishapikwa huko nyuma ndiyo maana tunaendelea kuwa wamoja, isispokuwa gap inayojengwa sasa kwa vijana wetu itakuja kutoa matokeo yake hapo baadae.
JKT ni bora.
 
mwanakijiji you are not serious today. Kama kuna kitu kinachonipa raha ninapokumbuka historia ya maisha yangu basi si kingine ila ni JKT. Nani anawakumbuka kina Afande Mtono wa Mlale na Mlay wa Mafinga? Sikumbuki kama niliwahi kuwa na uvumilivu katika maisha kama wakati ule. Halafu ilikuwa ni burudani ya pekee kwa makoplo kuongea kiingereza cha kuvunja ili waonekane na wao ni wasomi.

Nakumbuka koplo mmoja alinotolea mpya aliponiamrisha kuchanganya chakula changu na cha kuruta mwingine kwenye mustini (sic) moja ile nimpatie mustini yangu: Akaja na hii kali: "wewe rikututa, confuse chakura chako na cha mwenzio kwenye mustini moja nataka hiyo mustini yako niitumie. Umesiki?"
 
JKT was something else.

Fierce competition from Uzalishaji Mali, Gwaride, Kulenga Shabaha, Route March, to Choir, Michezo na Sanaa.

Damn enjoyed my time and how proud we were for our companies. We lived as a team, worked as team and we were proud of our team and all players. We picked up where some of our team members were failing because our focus was winning as a team not as individuals! That was true spirit of solidarity!

Bugudha za maafande was very minimal once you had built your immune system from their barking orders.

I wish the competitiveness spirit from JKT could have had chance to stream in our blood veins today!

"ee Chali we Chiwawa , ChaleKoy Chiwawa ni mfano!, kuruta wake chiwawa, afande wake chiwawa ni mfano"
 
mhhhhh ha ahaha haha haha...hapa najua tutasikia mengi na kudanganywa tutadanganywa najua...haya ongezeni chumvi mtutie wivu!
 
Kwa mtazamo wangu JKT kweli ni kupoteza muda na wakati kama si kujifunza wizi, uongo, umalaya na kugombana na maafande.

Umoja na mshikamano katika Tanzania tumefundishwa toka tukiwa mashuleni kwa kupitia somo la siasa kwa wale wazee wenzangu na kwa sasa wanaita jina lingine.

Tanzania ilikuwa inahimiza sana umoja na mshikamano (Pitia katiba ya TANU) na kidogo pia katika katiba ya CCM.
Nyimbo nyingi tulizoimbishwa JKT pia tulikuwa tunaimba mashuleni katika Mchakamchaka nk. Pia katika baadhi ya mikoa tulikuwa na chipukizi, game scouts, Tanu youth league nk.

JKT ni kupoteza muda na wala si lolote zaidi.
 
mhhhhh ha ahaha haha haha...hapa najua tutasikia mengi na kudanganywa tutadanganywa najua...haya ongezeni chumvi mtutie wivu!

Koba,

When were you born? I guess you must have missed opportunity to live and see the actual events and you are just a recipient of "fairy tales" read by Babu or Kijiweni about stuff that took place before you were born.

Pole kukosa Uhondo na Mhenyeko wa JKT!
 
Back
Top Bottom