JKT kurejeshwa, wazo zuri au limepitwa na wakati?

Pundamilia07

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2007
Messages
1,434
Points
1,195

Pundamilia07

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2007
1,434 1,195
JKT ilinipotezea muda wa mwaka mzima kabisa. Vile vile ilinifanya nikosane na kimwana wangu tuliyekuwa tumekutana high School na kuahidiana kuoana (kama kweli ahadi hiyo ilikuwa serious). Jambo nililochukia JKT zaidi ilkikuwa ni ile discipline ya woga na unafiki ambao ulikuwa unatokana na yale mafunoz ya msuli yaliyokuwa yakitolewa.

Hata hivyo JKT ilinikutanisha na watu wengi sana na kunifanya nijifunze mengi sana kuhusu jamii yetu. Ingawa sasa hivi sikumbuki hata mtu mmja kati ya marafiki hao niliokutana nao JKT, kwa miaka mitano ya kwanza tangu kumaliza JKT nilikuwa nakutana nao na walinisaidia sana kujenga network yangu hapo Dar.

Jambo ninalokumbuka sana ni pale nilipomaliza mafunzo ya ukamnada pale Ruvu na kupewa tepe moja ya kijani na kupandishwa cheo kutoka Serviceman na kuwa "Volunteer Lance Corpolar" au "Green Kwanja." Kwa miezi sita niliyotumia cheo hicho cha V-L/Cl niliwafanya kuruta walioningia Januari waione JKT kama sehemu ya mafunzo zaidi ya mateso; sikuhimiza discipline ya woga na nilikuwa mkali sana ninapopewa nidhamu ya ya kinafiki. Kwa bahati mbaya juhudi zangu zilikuwa ni kama punje ya mchele kwenye gunia zima; laiti wale makamanda wengine nao wangejifunza kwangu namna ya kuwatraini kuruta wale kiakili na kijamii.
Inawezekana ulikuwa na muono (vision) lakini hukujua jinsi ya kuigeuza iwe kweli na endelevu. In short you failed.
 
Bin Maryam

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2007
Messages
685
Points
0

Bin Maryam

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2007
685 0
Kuna watu walioenda jeshini na wengine hawakwenda. Kuna stori nyingi za kutoka jeshini. Hivi kulikuwa na sababu gani ya kuwapeleka vijana na kuwalazimisha kujiunga na jeshi na kuwapotezea muda ambao wangeweza kuendelea na masomo ya juu. Naamini kama kuna vitu ambavyo vimepoteza muda sana kwa wananchi ni suala la JKT.

Kulikuwa na mazuri lakini siamini kama Nyerere angefanya hivyo kwani wale vijana wote wangekuwa wanafundishwa mambo ya biashara na sayansi badala ya kusota Mpwapwa, Mafinga, Oljoro, Maramba, Ruvu n.k

Kuna vitu ambavyo namuunga mkono Nyerere lakini hili lilitupotezea muda wa mwaka mzima kusota kwenye mitaro na yare "maafande".

Hapa tutakuwa Kambi moja. JKT what a waste.
 
Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,233
Points
1,225

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,233 1,225
Rev unawakumbuka SELULE!!.......na wale watu waliokuja JKTna vijisababu kibao kuwa eti wao ni wagonjwa.......na walikuwa wanapewa C kwa saanaa........hawa ndio siku zote waliliona Jeshi ni mateso na mambo mengine ya ajabu, na wameondoka JKT wakiwa na hiyo picha ya ajabu ajabu.......na ndio hao hao Maafande they were taking advantage of them

Kwa wale tuliojichanganya kisawasawa........JKT tulijifunza mengi
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2007
Messages
4,793
Points
1,250

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2007
4,793 1,250
Nadhani wengi tunao 'wax nostalgic' kuhusu JKT ni wanaume. Ni kujidanganya tu kama mtu unakataa kuwe vile vitendo vya kuwalazimisha wasichana kutembea na maafande havikuwa ni vya kibakaji. Jamii yetu imezoea kumuona mwanamke kuwa ni chombo cha kutumiwa na mwanaume na mahali kama JKT mawazo haya ndiyo yaliyotawala. Mara ngapi tulishuhudia tukiadhibiwa kwa kuimba bez kwenye mchamchaka ikiwa wazi afande anamtafuta msichana aliyekuwa miongoni mwetu? Mara ngapi tulimsihi yule msichana atuokea kwa kile ambacho mmoja wetu amesema kujiachia? Ni wachache sana waliokuwa na fortitude ya kuhimili adhabu zisizoisha na vilio vya wenziwe ati azingatie maadili ya wazazi wake! Tuwe realistic. Watoto wangapi waliomaliza darasa la saba walikuwa wakilazimishwa (kwa vitisho au ahadi za kupewa diko diko) kutembea na watu waliokuwa wakilingana na babu zao? Ni wasichana wangapi walikuwa wakifanywa hasusa ya viongozi ili hao wakubwa wakitembelea kambi wasipigwe na baridi? Tukumbuke hawa wasichana walikuwa na umri kati ya miaka 15 ( waliojitolea wengine walikuwa chini ya hapa)hadi 20. Wachache sana walikuwa na umri zaidi ya hapa na hawa ni mara chache maafande wenye ulafi wa fisi kuwataka. Wapo waliofanya uamuzi mapema kutumia asset zao kwa namna hiyo lakini wengi wao hawakuwa na jinsi. Nakubali kuwa kuna mengi mazuri nilijifunza JKT lakini vile vile nilishuhudia maovu mengi tu. hili la mwisho mpaka leo linaisuta nafsi yangu.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Wasichana waliopenda shushu, ndio waliojiiingiza kwenye noma, lakini kuna waliodinda mpaka mwisho, kuna mmoja alikwenda mpaka jela uraiani lakini aligoma kata kata, na ndicho haswa tulichokwenda kujifunza kule kuwa ngangari.

Lakini kuna walioshindwa, sio kule tu JKT, hata uraiani wako vile vile tu, yaaani magoi goi!
 
Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,625
Points
2,000

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,625 2,000
Wasichana waliopenda shushu, ndio waliojiiingiza kwenye noma, lakini kuna waliodinda mpaka mwisho, kuna mmoja alikwenda mpaka jela uraiani lakini aligoma kata kata, na ndicho haswa tulichokwenda kujifunza kule kuwa ngangari.

Lakini kuwa walioshindwa, sio kule tu JKT, hata uraiani wako vile vile tu, yaaani magoi goi!
Ni kweli,

Mimi ninamfahamu msichana mmoja anbaye sioni ubaya wa kutaja jina lake kuwa alikuwa ni binti wa Profesa Omari; huyu aliweka ngumu kabisa na hakuna hata afande mmoja aliyediriki kumzengea. Ingawa sijamwona dada yule kwa takriban miaka 20 sasa, nina imani kuwa popote alipo ni mtu mwenye msimamo anayesimamia analoamini na kwa vyovyote ni mama ambaye atakuwa amefanikiwa sana.

Hata hivyo,

Siwalaumu wale dada zangu walioshindwa kuwa na msimamao wa aina hiyo (including mrembo wangu wa high school) kwa vile mazingira yale yalikuwa ya kuwafanya washindwe kujiamani na wawe na discipline ya woga.

Kwa jumla,

JKT ilikuwa na mazuri yake mengi lakini uongozi ulishindwa kuweka mazingira mazuri ya kuendesha programa nzima ikawa kama vile kundi la predators wa kubaka watoto wa kike fresh kutoka mashuleni.
 
Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,233
Points
1,225

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,233 1,225
Wasichana waliopenda shushu, ndio waliojiiingiza kwenye noma, lakini kuna waliodinda mpaka mwisho, kuna mmoja alikwenda mpaka jela uraiani lakini aligoma kata kata, na ndicho haswa tulichokwenda kujifunza kule kuwa ngangari.

Lakini kuna walioshindwa, sio kule tu JKT, hata uraiani wako vile vile tu, yaaani magoi goi!

Fundi Mchundo,

hapo juu ndio ukweli wenyewe.............hata mtaani wapo ambao wakishupaliwa.....wanajiachia...too bad...

unajua ile nidhamu ya Jeshi ndi watu walikuwa hawaipendi na kuanza kuijengea kila aina ya stories zikiwemo hizo za wanawake kunyanyaswa....................kama alivyosema Mkuu FMES................waliokuwa wavumilivu (moja ya mafunzo..."UVUMILIVU") haya mambo wala hayakuwepo
 
Kasana

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2007
Messages
417
Points
195

Kasana

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2007
417 195
Fundi Mchundo,
umeandika kwa machungu kuhusu dada zetu. napishana na wewe kwa hilo, mimi nilikuwa Ruvu JKT, na jinsia yangu ni she.
Hayo yote tuliyaona na sidhani kama maafande waliwalazimisha wasichana, mabinti walio wengi kama FM alivyosema walikuwa wanapenda shushu zaidi au zile kazi mlegezo (kusave sergent mess, kwa CO n.k,). Mara nyingi tulishuhudia kama afande anamtaka binti kweli alikuwa anatoa kazi ngumu, lakini baadae mnakuwa marafiki na mnamtania (serviceman.
Mimi nilipita vitengo vyote hivyo kusave kwa Co, sergent mess, kufagia mess (tuliyokuwa tunalia),kumwagilia bustanini, kwata nimepiga, mbinu za kijeshi nimefanya, root match, na hadi kuchimba misingi ya nyumba za maafande (na zile shule za wanavijiji), ikiwemo kulinda rear gate, phase II n.k, nilifungwa mara mbili na kupelekwa mahakamani mara tatu.
It was good experience in fact.
 
Mwakilishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2007
Messages
484
Points
195

Mwakilishi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2007
484 195
Nyie mnaowasakama hao wasichana mnaowaita "waliojiachia" yaani kwa maneno mengine mnamaanisha kuwa wale maafande walikuwa justified kuwataka kwa nguvu mpaka kufikia hatua ya kutesa kombania nzima kwa kisingizio cha kuwafundisha uvumilivu au? Siwaelewi...

Halafu tusifungane kamba, kulikuwa na kambi na kambi, watoto wa vigogo aka mafisadi walikuwa mostly Ruvu na Makutupora; watoto wa walalahoi, Bulombora, Masange na kwingineko. Hata vyakula tofauti wakati kuruta huko Masange au Bulombora wanalalamika uji hauna hata na chumvi, wenzake wa Ruvu, Makutu wanalalamika chai haina maziwa ya kutosha, mayai leo hakuna, mikate haina siagi...

Viongozi wa juu wa chama na serikali ukisikia wametembelea JKT basi itakuwa Ruvu au Makutu wakijitahidi sana Oljoro au Mafinga, kiongozi gani aende eti sijui Bulombora...

Hamna cha kujifunza uvumilivu wala nini, mliokwenda mtakubaliana nami kuwa kule hujifunzi wala hufundishwi responsibility ya aina yoyote, yaani ukijongo leo ndio imetoka hiyo kesho yake mnaanza upya, (tena ma-odali koplo watasema eti ulitumia Mbinu za Medani).

No wonder tuna viongozi leo wasiowajibika kwa lolote na bado tunaendelea kuwapa madaraka maana "wamejongo" wakafanikiwa ndio imetoka hiyoo...

Halafu Kenya wao walikuwa na National Youth Service tokea 1964 hivyo si kweli kwamba hawakuwa na "JKT" yao. Someni hapa:
http://www.youthaffairs.go.ke/downloads/nys.pdf
 
Mwakilishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2007
Messages
484
Points
195

Mwakilishi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2007
484 195
Wakuu Kasana na FMES,
msi-generalize sio wasichana wote wapenda shushu waliokuwa wanajirahisi vilevile haimaani kuwa kama msichana anapenda shushu basi atajirahisi kwa afande; nawajua wengi waliokuwa wanapenda shushu ambao walibobea katika kujongo, C za matron ama uselule na walikula shushi vilevile...
 
Masatu

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2007
Messages
3,284
Points
1,195

Masatu

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2007
3,284 1,195
Pamoja na mapungufu machache JKT ilitupa nafasi kujijenga kiakili na kimwili ktk kukabiliana na maisha. Akina sie tuliotaka moja kwa moja kwenye malezi ya wazazi wetu ilikuwa ni nafasi ya mwanzo kuanza kuona namna ya kushi kivyako na kupambana na changamoto za maisha zinazotukabili mbele yetu.

Kazi za kilimo, ufugaji, gwaride bila kuasahau michezo vimetusaidia sana kujiona sisi ni watanzania na the fact kuwa tulikuwa tuatoka mikoa tofauti ilikuwa ni nafasi ya kipekee kujenga urafiki.

Kulifuta jeshi lilikuwa ni kosa nadhani wangefanyia kazi hayo mapungufu na kuliboresha kwa kutilia mkazo matumizi ya akili zaidi badala ya maguvu pia suala la akina dada kwa kweli walikuwa wanawekwa ktk kona ambayo namna ya kujikwamua ni "kukubali" yaishe tu

All said and done nili enjoy time yangu pale JKT
 
Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Points
1,225

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 1,225
JKT tulikuwa tunafundishwa uwongo, umalaya, wizi, nidhamu ya woga na unafiki na wala si kingine.

.
Mtambo,

Huo Umalaya, Uwongo na Wizi ulikuwa unafundishwa kwenye kambi ipi? Mimi nilikuwa Oljoro na Itende na wala sikufundishwa hivyo vitu.

Kuna wasichana wengi tu ambao pamoja na maafande kutumia kila njia kuwawania lakini waliweke misimamo mpaka dakika ya mwisho.

Kama kuna mtu alikuwa malaya au mwizi JKT basi yalikuwa ni matatizo yake.

Mazingira ya JKT yalikuwa magumu na kuna watu waliona njia ya kupunguza huo ugumu ni kuwa wake au mabwana wa maafande. Watu kama hao sitashangaa hata kwenye ugumu wa maisha mitaani wakiishia kuwa wezi.

JKT ilikuwa inatufunza uvumilivu na kujituma na hivyo vitu viwili ni muhimu hata kwenye maisha ya uraiani.
 
Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Points
1,225

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 1,225
Nadhani wengi tunao 'wax nostalgic' kuhusu JKT ni wanaume. Ni kujidanganya tu kama mtu unakataa kuwe vile vitendo vya kuwalazimisha wasichana kutembea na maafande havikuwa ni vya kibakaji. Jamii yetu imezoea kumuona mwanamke kuwa ni chombo cha kutumiwa na mwanaume na mahali kama JKT mawazo haya ndiyo yaliyotawala. Mara ngapi tulishuhudia tukiadhibiwa kwa kuimba bez kwenye mchamchaka ikiwa wazi afande anamtafuta msichana aliyekuwa miongoni mwetu? Mara ngapi tulimsihi yule msichana atuokea kwa kile ambacho mmoja wetu amesema kujiachia? Ni wachache sana waliokuwa na fortitude ya kuhimili adhabu zisizoisha na vilio vya wenziwe ati azingatie maadili ya wazazi wake! Tuwe realistic. Watoto wangapi waliomaliza darasa la saba walikuwa wakilazimishwa (kwa vitisho au ahadi za kupewa diko diko) kutembea na watu waliokuwa wakilingana na babu zao? Ni wasichana wangapi walikuwa wakifanywa hasusa ya viongozi ili hao wakubwa wakitembelea kambi wasipigwe na baridi? Tukumbuke hawa wasichana walikuwa na umri kati ya miaka 15 ( waliojitolea wengine walikuwa chini ya hapa)hadi 20. Wachache sana walikuwa na umri zaidi ya hapa na hawa ni mara chache maafande wenye ulafi wa fisi kuwataka. Wapo waliofanya uamuzi mapema kutumia asset zao kwa namna hiyo lakini wengi wao hawakuwa na jinsi. Nakubali kuwa kuna mengi mazuri nilijifunza JKT lakini vile vile nilishuhudia maovu mengi tu. hili la mwisho mpaka leo linaisuta nafsi yangu.
Fundi Mchundo,
Kisheria hakuna kambi wala kiongozi ambaye alikuwa na uwezo wa kumlazimisha msichana kulala na afande. Ni kweli maafande walikuwa wanatumia weaknesses za baadhi ya wasichana kutembea nao, lakini hilo tatizi lipo kila sehemu kwa maisha ya TZ. Hata kwenye idara za serikali hayo mambo yapo, hata ukienda vyuoni, mambo kama hayo yapo.

Wasichana ambao walikuwa tayari kulitumikia jeshi sawa na mtu mwingine yeyote waliweza kuvuka bila matatizo hayo. Ni wale waliokuwa wanataka favours ndio waligeuzwa kuwa nyumba za maafande.

Naamini wasichana waliosema NO kwa maafande jeshini, hata huko vyuoni au makazini walikuwa na uwezo wa kusema hapana. Lakini wale walioona njia rahisi ni kuuza miili yao ili wafikie malengo yao, wanaweza kufanya hivyo hivyo hata maofisini kwa maboss wao au hata vyuoni.
 
Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Points
1,225

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 1,225
Fundi Mchundo,
umeandika kwa machungu kuhusu dada zetu. napishana na wewe kwa hilo, mimi nilikuwa Ruvu JKT, na jinsia yangu ni she.
Hayo yote tuliyaona na sidhani kama maafande waliwalazimisha wasichana, mabinti walio wengi kama FM alivyosema walikuwa wanapenda shushu zaidi au zile kazi mlegezo (kusave sergent mess, kwa CO n.k,). Mara nyingi tulishuhudia kama afande anamtaka binti kweli alikuwa anatoa kazi ngumu, lakini baadae mnakuwa marafiki na mnamtania (serviceman.
Mimi nilipita vitengo vyote hivyo kusave kwa Co, sergent mess, kufagia mess (tuliyokuwa tunalia),kumwagilia bustanini, kwata nimepiga, mbinu za kijeshi nimefanya, root match, na hadi kuchimba misingi ya nyumba za maafande (na zile shule za wanavijiji), ikiwemo kulinda rear gate, phase II n.k, nilifungwa mara mbili na kupelekwa mahakamani mara tatu.
It was good experience in fact.
Kasana,

Mmmhhh!!!! wewe ulishindikana, kufungwa mara mbili? Naona ulifunga kufuri kweli kweli kwi kwi kwi!!!!

Hongera sana kwa kuwa na msimamo!
 
Joined
Sep 13, 2007
Messages
10
Points
0
Joined Sep 13, 2007
10 0
Kenya hawakuwa na JKT na wamekuwa nchi nzuri tu, tena iliyoendelea kiuchumi. Muda mrefu ambao wengi wetu tungekuwa tumeshamaliza elimu ya juu tulitakiwa kwenda kuchimba mitaro, mahandaki, kujenga nyumba, kuchoma matofali na wale waliokuwa ruvu watakumbuka mpunga!

Kama ningetaka kujenga nyumba au kulima mashamba ningefanya ya kwangu mwenyewe. Mbona sasa hivi watu hawalazimishwi kwenda JKT lakini bado wana uzalendo? Nadhani ile ilikuwa ni hofu ya vita baridi zaidi kuliko kitu kingine chochote.
Ngugu mwana JF
JKT ilitukutanisha watu wa kutoka kila kona ya nchi yetu na fani mbali mbali, hii leo kwa aliyepitia JKT karibu kila ofisi atakayoingia atakutana na mtu walipitia pamoja jeshini. lilitujengea umoja ambao thamani yake ukiwa na mtizamo finyu utaona kama ilikuwa ni kupoteza mda, mfano wa Kenya si unaona yanayotokea sasa ni mapungufu kwa kiasi fulani yaliyotokana na kutowaweka vijana pamoja kujifunza nidhamu na uvumilivu
 
Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Points
1,225

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 1,225
Nyie mnaowasakama hao wasichana mnaowaita "waliojiachia" yaani kwa maneno mengine mnamaanisha kuwa wale maafande walikuwa justified kuwataka kwa nguvu mpaka kufikia hatua ya kutesa kombania nzima kwa kisingizio cha kuwafundisha uvumilivu au? Siwaelewi...

]
Mwakilishi,

Hakuna anayesema hivyo vitendo vilikuwa vizuri. Tunachosema ni kwamba kwa jamii ya Tanzania hivyo vitendo vipo kila sehemu. Predators wanatumia mazingira magumu na tamaa ili kuwanyanyasa dada zetu. Chukulia mfano kwenye vyuo vikuu, makazini na sehemu zingine.

Njia ya kuondokana na hayo mambo ni kwa sheria kufanya kazi lakini pia kwa wahusika na hasa wasichana kutokubali kuuza utu wao kwa sababu ya favours au kufaulu mitihani au kupanda vyeo.

Jeshini afande alikuwa anaweza kutesa Krutas lakini ilikuwa inafika mahali anashindwa tu. Hivyo hivyo vyuoni kama umefaulu hawawezi kukufelisha, ni wale wanaotaka marks xza haraka haraka ndio wanakuwa affected zaidi.

Hivyo hivyo kazini, kama ni mchapa kazi mzuri utapanda tu hata kama utacheleweshwa.
 
Steve Dii

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2007
Messages
6,417
Points
1,225

Steve Dii

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2007
6,417 1,225
Is it really necessary to use the term "fisadi"?!?
Koba...Ijumaa leo kaka....
We hujamstukia tu Mwanakijiji....? Jiulize tu mwenyewe ufisadi na JKT vinahusiana nini?
Lakini Mwanakijiji kauliza swali kama JKT lilikuwa ufisadi? Mpaka sasa hamna mtu aliyejibu zaidi ya kutoa stori....
Mimi nadhani sasa tunali-abuse hili neno Ufisadi....
I agree maana context ya mada jinsi alivyoleta Mwanakijiji haviendani na kichwa cha habari!
You need to know the character of Mwanakijijito figure out the relationship of JKT and Ufisadi.

Ndio maana wengine tumeng'amua mtego wake na kuanza kuhubiri "mema" na wengine kulalamika!
Wote naona tumeanza kuwa mafisadi wa lugha sasa!!
Mkjj kauliza kitu kingine kabisa, lakini kwa ufisadi wake wa lugha, katumia neno ufisadi ili sote tuliofisadika na neno fisadi, tutoe maelezo tofauti na yale aliyolenga hivyo nasi kuwa mafisadi wa maongezi katika hoja hii ya ufisadi wa JKT!!

Je mnakumbuka thread hii: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=4321&highlight=ngono

JKT irudishwe, mimi sikubahatika kwenda kule, ila itakuwa nafasi nzuri kwa watoto wangu, nitapeleka ('vijana wangu wawili' wenye umri tosha)... labda tujiulize, kwanini Israel, Poland bado wanapeleka vijana wao jeshini..
 
NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2007
Messages
560
Points
0

NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2007
560 0
Fundi Mchundo,
umeandika kwa machungu kuhusu dada zetu. napishana na wewe kwa hilo, mimi nilikuwa Ruvu JKT, na jinsia yangu ni she.
Hayo yote tuliyaona na sidhani kama maafande waliwalazimisha wasichana, mabinti walio wengi kama FM alivyosema walikuwa wanapenda shushu zaidi au zile kazi mlegezo (kusave sergent mess, kwa CO n.k,). Mara nyingi tulishuhudia kama afande anamtaka binti kweli alikuwa anatoa kazi ngumu, lakini baadae mnakuwa marafiki na mnamtania (serviceman.
Mimi nilipita vitengo vyote hivyo kusave kwa Co, sergent mess, kufagia mess (tuliyokuwa tunalia),kumwagilia bustanini, kwata nimepiga, mbinu za kijeshi nimefanya, root match, na hadi kuchimba misingi ya nyumba za maafande (na zile shule za wanavijiji), ikiwemo kulinda rear gate, phase II n.k, nilifungwa mara mbili na kupelekwa mahakamani mara tatu.
It was good experience in fact.
Kasana hebu nambie ni mazingira gani yaliyokuwa yanapelekea hadi mtu 'anafungwa' mara kupelekwa 'mahakamani'...mi sijapita huko na nahisi nimekosa mengi kweli
 
Mwakilishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2007
Messages
484
Points
195

Mwakilishi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2007
484 195
Mtambo,

Huo Umalaya, Uwongo na Wizi ulikuwa unafundishwa kwenye kambi ipi? Mimi nilikuwa Oljoro na Itende na wala sikufundishwa hivyo vitu.
Mtanzania,

Naona umevitaja kwa majina kabisa vitu ambavyo hukufundishwa jeshini yaani umalaya, uongo na wizi, sasa nitakosea kama nitahitimisha kuwa ulifundishwa vile ambavyo hukuvitaja hapo juu, yaani nidhamu ya woga na unafiki?

Kuna wasichana wengi tu ambao pamoja na maafande kutumia kila njia kuwawania lakini waliweke misimamo mpaka dakika ya mwisho.
Kweli kabisa, vilevile walikuwepo wengi walioshindwa "kuweka msimamo", hapo sasa ndipo linapokuja suala la je ilikuwa haki wasichana kuwekwa katika hali kama ile ya kudhalilishwa vile?

JKT ilikuwa inatufunza uvumilivu na kujituma na hivyo vitu viwili ni muhimu hata kwenye maisha ya uraiani.
Ukweli ni kwamba unaweza kujifunza uvumilivu na kujituma popote pale sio JKT peke yake, nadhani bila shaka hata wewe unawafahamu watu wanaojituma na wenye uvumilivu ambao hawajapitia jeshini.

Jeshini sanasana unachochea survival instinct zako tu, maana lengo linakuwa ni kupitisha siku bila kuhenyeshwa au kufanyishwa kazi ngumu, hence kujongomea kwa sana, kutafuta posti zenye ubwete, maana the next morning, aliyejongo na asiyejongo ngoma droo, mnaanza upya, uwajibikaji sifuri.

Leo hii tunashangaa tumepata wapi viongozi wasiowajibika wakati tabia hiyo tumeipalilia kwa bidii tokea jeshini, kama ambavyo Wadanganyika tunavyojivunia kutokufanya kazi, bila shaka umeshasikia maneno kama "nimeingia ofisini saa nne nikazugazuga pale saa saba huyo nikatimua" halafu tunajiona wajanja kumbe wajinga tu. JKT ni hivyo hivyo, mtu anayejongo ndiye anayeonekana mjanja mpaka maafande ndio wanamuona poa sana ila ukiwa kila siku upo tu kombania eti "unajituma" ndio unaonekana bonge la zezeta...
 
Forum statistics

Threads 1,381,711
Members 526,174
Posts 33,809,221
Top