Kama ni kweli RO katoswa, hili ni kubwa sababu zifuatazo:
-RO amekuwa analalamika sana kwenye korido kuwa ushauri anaompa JK hauheshimiwi, ni mbishi na anawaamini sangoma zaidi kuliko idara ya RO.
Mkuu ebu tuambie anamlalamikia na nani ni ushauri gani aliompatia Rais akauweka pembeni.
-RO ameonekana amechoka sana siku za karibuni na hata kutishia kujiengua yeye mwenyewe. Kama hii ni kweli, atakuwa amefurahi sana.
Mkuu hapa tena napatwa kigugumizi RO hawezi kujiengua hata siku moja labda serekali nyingine lakini siyo hii ya Mkwere hakuna mtu wa kujiuzulu wa kujiengua.
-Kuna watu ndani ya idara wamekuwa wanamkalia kooni kwa kudai hakustahili kuteuliwa yeye kwa nafasi hiyo. Yupo Prof mmoja wa Chuo cha Diplomasia, ndiye kinara wa movement hii na inasikika kuwa ndiye possible mteule.
Taarifa nilizonazo RO atamalizaa salama kipindi chake cha ushushu labda nguvu ya umma itumike kumwondosha Mkwere magogoni.
-JK anamtuhumu RO kuwa amejiunga na kambi ya mzito fulani kwa mbio za 2015, na kambi hiyo si chaguo la JK.
Mkuu RO ni kambi ya Lowasa ndiye aliyemsaidia kushika wadhifa huo wakti akiwa waziri mkuu.RO kama mwanadamu lazima arejeshe fadhila hata ingekuwa usingefanya tofauti na anavyofanya sasa.Sidhani kama Lowasa si chaguo la Mkwere hii haitaji utabiri wa Shehe Yahaya au umesahau Lowassa aliwahi kusema hawajakutana barabarani.Tafakari chukua hatua okoa Tanzania kabla ya mwaka 2015 CCM ionekane kama chama cha kitchen party kuendela kukilea ni kuliletea taifa maafa makubwa.
Jamani hizi zote ni TETESI tu. Walioanzisha thread, watujuze kishindo ni kipi.