A
Anonymous
Guest
Uongozi Alsaedy High Class tatueni kero za abiria wenu, mtapoteza wateja.
Mimi ni abiria ambaye napenda kutumia usafiri wa bus la Alsaedy high class kwa safari zangu za Dar-Iringa, Iringa-Dar. Mnamo tarehe 9/6/2026 nilisafiri na familia yangu kutoka Dar es salaam na bus la Alsaedy linalotoka Mbezi Magufuli saa tatu na nusu asubuhi na tulifika Iringa mjini mida ya saa tatu usiku.
nilikua na mizigo mingi kidogo na kwa bahati mbaya begi langu moja sikuliona. Nilivomuuliza kondakta alisema kwamba kwenye buti ambamo begi hilo liliwekwa halikufunguliwa kwenye vituo vya njiani isipokua kwenye hicho kituo chao cha mwisho kilichopo kwenye ofisi zao zilizopo Gangilonga, Iringa mjini. Aliniomba nifike ofisini hapo kesho yake ili kuona kama kuna abiria yoyote aliyechanganya begi amefika kurudisha.
Nilienda kesho yake tarehe 10 na hakukuwa kuna taarifa yoyote ya abiria kurudisha begi. Kwa bahati nzuri niliona eneo lile kuna Camera kubwa kwahiyo niliongea na meneja wao kuomba kuangalia Camera ili tuone aliyechukua begi na ingekua rahisi kufatilia kwasababu huwa wana list ya abiria na namba zao za simu.
Meneja aliongea na kondakta afatilie issue ya kuangalia camera kwenye ofisi zao kuu zilizopo Morogoro kwasababu alisema yeye hana access ya camera hadi Morogoro hivo ni rahisi kwa kondakta kufatilia kwasababu anapita hapo kila siku.
Chaajabu ni kwamba, hadi sasa ni zaidi ya wiki mbili sipata msaada wowote. Begi langu lina vitu vya thamani ambavyo ninavihitaji mno. Kondakta kila nikimuuliza hanipi majibu yakuekeweka na hadi sasa hajibu meseji zangu. Najiuliza inashindikana nini kuangalia kwenye camera au waliangalia hawataki kunipa jibu kwasababu kuna kitu wanaficha nisijue?
JamiiForums naomba mnipazie sauti kwa Uongozi wa Alsaedy morogoro mjini ili nipate msaada. Naamini kupitia jukwaa hili nitapata msaada kama wanavyopata wengine