Jiongezeni Wakuu wa Shule; ni kwamba achaneni na habari za mahafali mtapigwa mawe!

WhoWeBe

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
2,301
4,243
Nasikia wenzenu wamesimamishwa kwa sababu ya 'kuruhusu' wanafunzi kucheza wimbo usio na 'maadili' wa Honey. Saaawa.

Kusimamishwa kwao ni ujumbe kwenu mlio madarakani. achaneni na habari za muziki huko mashuleni kwenu.

Kuachana na muziki tafsiri yake futeni mahafali, hakuna mahafali ambayo wanafunzi na 'hata wazazi/walezi' wetu wa kileo watakubali yafanyike bila muziki. Tena muziki wenyewe ni huu unaotamba mitaani na sio huo wa kuomboleza au kuhamasisha sera ya vijiji vya ujamaa.

Nawaambia, mkikubali kufanyika mahafali halafu muwalazimishe wacheze muziki wa gospel na qaswida, mtapigwa mawe na wanafunzi hawa mchana kweupeee! Nimemaliza.
 
Nimewaza kwenye mahafali yetu wimbo wa kuchukulia vyeti ulikuwa ule "tulikaa kinyonge sana....tajiri"
Zile video zikienda hewani mkanda atachukua hatua gani!
 
Nasikia wenzenu wamesimamishwa kwa sababu ya 'kuruhusu' wanafunzi kucheza wimbo usio na 'maadili' wa Honey. Saaawa.

Kusimamishwa kwao ni ujumbe kwenu mlio madarakani....
Mbona kuna nyimbo nyingi tu zenye maudhui mazuri kwa kila rika?

Huo wimbo hata mi sipendi kabisa kuusikiliza! Hauna maadili ya kitanzania!
 
Nimewaza kwenye mahafali yetu wimbo wa kuchukulia vyeti ulikuwa ule "tulikaa kinyonge sana....tajiri"
Zile video zikienda hewani mkanda atachukua hatua gani!
😆Tatizo vijana wa sasa wavivu sana.

Sisi enzi zetu tukiupenda wimbo tunatumia tune yake kutunga mistari yetu kuendana na muktadha!

Sasa leo hii watoto wadogo wanasikizishwa mambo ya honey akinuna namkatia viuno! Loh! Hii haikubaliki!
 
Nasikia wenzenu wamesimamishwa kwa sababu ya 'kuruhusu' wanafunzi kucheza wimbo usio na 'maadili' wa Honey. Saaawa.

Kusimamishwa kwao ni ujumbe kwenu mlio madarakani......achaneni na habari za muziki huko mashuleni kwenu.

Kuachana na muziki tafsiri yake futeni mahafali......hakuna mahafali ambayo wanafunzi na 'hata wazazi/walezi' wetu wa kileo watakubali yafanyike bila muziki. Tena muziki wenyewe ni huu unaotamba mitaani na sio huo wa kuomboleza au kuhamasisha sera ya vijiji vya ujamaa.

Nawaambia, mkikubali kufanyika mahafali halafu muwalazimishe wacheze muziki wa gospel na qaswida, mtapigwa mawe na wanafunzi hawa mchana kweupeee! Nimemaliza......
Pengine wanatakiwa kuimba nyimbo za CCM! Nashangaa nyimbo za yule Msanii anayeimba matusi zinaruhusiwa kwenye Mikutano Yao
 
Nasikia wenzenu wamesimamishwa kwa sababu ya 'kuruhusu' wanafunzi kucheza wimbo usio na 'maadili' wa Honey. Saaawa.

Kusimamishwa kwao ni ujumbe kwenu mlio madarakani......achaneni na habari za muziki huko mashuleni kwenu.

Kuachana na muziki tafsiri yake futeni mahafali......hakuna mahafali ambayo wanafunzi na 'hata wazazi/walezi' wetu wa kileo watakubali yafanyike bila muziki. Tena muziki wenyewe ni huu unaotamba mitaani na sio huo wa kuomboleza au kuhamasisha sera ya vijiji vya ujamaa.

Nawaambia, mkikubali kufanyika mahafali halafu muwalazimishe wacheze muziki wa gospel na qaswida, mtapigwa mawe na wanafunzi hawa mchana kweupeee! Nimemaliza......
Eti kuomboleza

Watu wanavibe la kumaliza shule,uwawekee mambo ya ujamaa
 
Tatizo vijana wa sasa wavivu sana.

Sisi enzi zetu tukiupenda wimbo tunatumia tune yake kutunga mistari yetu kuendana na muktadha!

Sasa leo hii watoto wadogo wanasikizishwa mambo ya honey akinuna namkatia viuno! Loh! Hii haikubaliki!
Vijana wa zamani tulisikiliza nyimbo mbaya zaidi kuliko Sasa Bora Sasa wanafichaficha maana
Zamani "khuma inauma ooh khuma inauma belooo belooo kizera wayaye man kizelewaaa"
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Yaani utumwa umeaathiri jamii za kitanzania ,yaani mwanasiasa akishiba kande anatoa matamko ,sheria za kusimamishwa kazi mtumishi hazifuatwi ,watanzania hili ni kosa Kwa mkenda kufanya huo ujinga ili wajinga wamshingilie mitaani Sisi tumenyamaza huku tukitekenywa kama mazuzu .Naanza kuamini Afrika mashariki nchi zilizobaki na wajinga ,manyani ni TANZANIA NA UGANDA yaani hatujali mtu anabakwa tumetulia,mikataba mibovu tumenyamaza .Aisee Nyerere uliifanyanye hii nchi??Yaani uzwazwaaaaa
 
Back
Top Bottom